Mada ya Kwanza.
Utangulizi wa Pitio la Agano la Kale.
Malengo ya mada.
Baada ya kumaliza mada hii
mwanafunzi ataweza:
·
Kueleza maana ya
Agano.
·
Kueleza
maana ya Biblia
·
Kueleza
maana ya Agano la Kale
·
Kueleza
maana ya Pitio la Agano la Kale.
·
Kutambua
mpangilio wa vitabu katika Biblia ya kiebrania (Agano la kale).
·
Kutambua
muundo wa Agano la Kale katika Biblia yetu ya Kiswahili na Kiingereza.
·
Kueleza
kwanini wakristo wanasoma Agano la Kale.
·
Kueleza
Sababu za kujifunza Kozi ya Pitio la Agano la kale.
·
Kulinganisha
na kulinganua kati ya Agano la Kale na agano Jipya.
I. Utangulizi .
Somo
hili linachunguza Agano la kale kwa ujumla
tu. Halilengi kujifunza kila kitu kinachotajwa katika Agsno la Kale,
bali ninafanya mapitio tu na kutoa mtazamo wa jumla wa kila kitabu na mtazamo wa jumla wa Agano la kale.
Lengo
la kozi hii ni kutoa mwanga na msingi
kwa mwanafunzi juu ya Agano la Kale na kumjengea mwanafunzi uwezo na
msingi mzuri wa kulielewa Agano la Kale na kutambua uhusiano uliopo kati ya Agano la
Kale na Agano Jipya.
Katika
kozi hii mwanafunzi atajifunza kila kitabu cha agano la kale kwa muhtasdasri tu
kwa kutazama muuundo wa kitabu, mtindo, mafundisho makuu, matukio makuu na, mwandishi, mwaka wa
kuandikwa,watu mashuhuri, mitajo ya
Kristo na mistari ya kiini cha kila
kitabu.
Kozi
hii imegawanya katika sehemu tatu ili
kurahisisha ujifunzaji na ufundishaji. Lakini kimsingi ni kozi moja.
Kila
sehemu ya kozi hii itafundishwa kwa wiki moja.
II. Umuhimu wa kujifunza pitio la Agano la kale.
1. Linatupa
ufahamu juu ya historia ya mwanadamu tangu uumbaji mpaka sasa.
2. Linatupa
ujasili wa kusimama na kuitetea imani bila kuteteleka kama walivyofany
watakatifu wa Agano la Kale.
3. Kupitia
Kozi hii tunatambua kwamba Mungu wa Agano la Kale ndiye yeye Yule wa Agano Jipya.
4. Tunajengewa
msingi mzuri wa kuifahamu thiolojia ya Agano la Kale.
5. Tunatambu
ya kwamba wokovu kwa neema kwa njia ya
imani umekuwa daima ndiyo njia ya pekee ya kuwa na mahusiano na ushirika na Mungu.
6. Tunatambua ya kwamba kutembea kwa imani
kumekuwa daima ndiyo njia pekee ya kumpendeza Mungu.
III. Ufafanuzi wa Istilahi.
Katika
kipengele hiki tutafafanua baadhi ya Istilahi
mbalimbali kama zitakavyotumika katika kozi hii ya Pitio la Agano la Kale na
kama zilivyotumika katika Biblia na elimu ya thiolojia kwa ujmla.
Biblia. Ni
neno la Mungu lililo katika maandishi. Bibblia pia ni kitabu cha mawazo na
matendo ya Mungu.Biblia pia inaweza kufafanuliwa kama mkusanyiko wa maandiko
matakatifu yaliyoandikwa katika vipindi mbalimbali vya historia ya mwanadamu na
watu walioongozwa na Roho mtakatifu kuandika.2Pet 1:19-21. 2Tim 2:15-17.
Neno
la Mungu pia hujulikana kama maandiko. Neno
maandiko ni neno la kilatini ambalo humaanisha maandishi. Wakati neno
maandiko linapokuwa limetumika na kuwa na helufi kubwa mwanzoni mara nyingi
humaanisha maandiko matakatifu yaani Biblia.
Maana ya Agano. Neno
agano linatokana na neno la kiebrania Berith
lenye maana ya mapatano, makubaliano au mkataba unaofanywa baina ya pande
mbili.
Neno
hili Agano kwa Kiyunani ni Diatheke lenye
maana ya urithi au wosia.
Kwa hiyo tunaweza kusema agano ni mapatano
maalumu yanayounganisha watu wa pande mbili pamoja.
Neno Agano
la Kale Hulenga hasa kwenye Agano la Musa ambalo Mungu alifanya na wana wa
Israeli katika mlima Sinai Baada ya kutoka Misri lakini kabla ya kuingia kwenye nchi ya
ahadi. Kut 20-24. Kum 28-30, Yer31:32 Gal 3:6-26, Ebr 9:15-22.
Vitabu 39 vya
kwanza katika Bibli vinaitwa Agano La Kale.
AGANO maana yake
ni mapatano au makubaliano kati ya watu. Sehemu ya kwanza ya Biblia inaitwa
"AGANO LA KALE" kwa sababu inaeleza habari ya agano (mapatano)
kati ya Mungu na wanadamu wa kale.
Pia
Agano la Kale ni maelezo ya Kikristo ya
vitabu vilivyotolewa na Mungu kwa watu wa kiyahudi na ambayo yanahusika na
Agano la kale ambalo Mungu aliwapa Waisraeli
kwa kupitia kwa Musa kwenye mlima Sinai.
Agano
la kale ni zaidi ya sheria, hutoac taarifa na historia ya elimu ya kithiolojia
yaw a agano la Mungu kulingana na mpango
wake wa wokovusi kwa wayahudi pekee bali pia na kwa watu wa mataifa.
Hivyo
twaweza kuhitimisha kwa kusema kwamba
Agano la kale humaanisha vitabu vyote vilivyo katika Biblia vilivyoandikwa
kabla ya kuzaliwa Bwana wetu Yesu Kristo. Au ni maandiko matakatifu
yaliyoandikwa kabla ya kuzaliwa kwa Masihi
yaani Bwana wetu Yesu Kristo.
IV. Muhtasari.
1. Agano
la kale liliandikwa kwa muda wa kama miaka1000. Hivi.
2. Liliandikwa
kama na waandishi kama 30 chini ya uongozi wa Roho mtakatifu kama
mwandishi mkuu.
3. Lina
jumla ya vitabu 39.
4. Agano
la kale liliandikwa hasa kwa kiebrania na sehemu chache sana ziliandikwa kwa
kiaramu.
5. Maandiko
matakatifu ya asili yalinakiliwa kwa
uangalifu na kwa ustadi sana kwa mkono na waandishi wa kiyahudi na kisha
yakapokelewa toka kizazi hata kizazi.
6. Wakati
Bwana Yesu alipokuja ulimwenguni alikuta
Agano la kale limekkwisha kukamilika na kuwa
kitabu kimoja chenye vitabu 24 kwa kiyahudi, tulivyonavyo leo ambavyo ni sawa na vitabu 39
katika Biblia yetu vya Agano la Kale.
7. Tafsriri
ya kwanza ya Agano la kale ya kiyahudi
ilikuwa kwa lugha ya kiyunani ambayo
iliitwa Septuaginta (LXX). Iliitwa hivyo kwa sababu tafsiri hiyo ilifanywa na watu sabini.
Na tafsriri hiyo ilikamilika mnano mwaka 250 K.K.
8. Tafsri
ya pili ambayo ilikuwa muhimu ni ile ya kilatini iliyojulikana kama “ Latin vulgate “ (383-450
BK). Biblia hii ndiyo iliyokuwa Biblia ya Kikristo iliyotambuliwa kwa muda wa
miaka elfu moja.
9. Tafsiri
ya kwanza kwa lugha ya Kiingereza ilifanywa mnamo mwaka 1384 na John Wicliff, na
kufuatiwa na lie iliyoruhusiwa na mfame James manamo mwaka 1611. Tafsiri hii
ndiyo tafsiri ya mwanzo kabisa ya karibu
tafsiri zetu zote za kisasa.
10.
Nakala zilizopatikana kule Kumlani pwani
ya Bahari mfu (Dead sea.) mnamo mwaka 1947 zilithibitisha usahihi na muunganisho wa vitabu vyote pamoja vya Agano
la Kale kama tulivyo na kitabu hicho hivi leo.
11.
Kitabu cha Agano la Kale kimelindwa na
kuhifadhiwa kiajabu na Mungu baba kwa muda wa zaidi ya miaka elfu tatu.
V. Mpangilio
wa vitabu katika Biblia ya Kiebrania.
SHERIA
|
MANABII
|
MAANDIKO.
|
Mwanzo
Kutoka
Mambo ya walawi
Hesabu
Kumbukumbu la torati.
|
Wa kwanza
Yoshua
Waamuzi
Samweli (vitabu 2)
Wafalme(vitabu 2)
Waliofuata.
Isaya
Yeremia
Ezekieli
Manabii wadogo 12.
|
Ushairi.
Zaburi
Mithali
Ayubu.
Magombo
matano.
Wimbo
wa Solomoni (Ulio bora).
Ruthu
Maombolezo
Mhubiri
Esta.
Historia.
Danieli
Ezra-Nehemia.
Mambo ya nyakati
(vitabu 2)
|
·
Utaratibu
huu wa mapangilio wa vitabu wa kiebrania ndio Yesu
Alioutumia.
Luka 24”27.
“Kisha akawaambia, haya ndiyo maneno
yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali
pamoja nanyi, yakwamba nilazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati
ya Musa, , na katika Manabii, na
katika Zaburi”
Wayahudi wakati wa Yesu walikuwa na vitabu vyote tunavyoviita sasa
Agano la kale. Hiyo ndiyo Biblia ya Kiyahudi. Lakini wanapoviweka vitabu hivi
katika utaratibu wao na mpanglio, waliviweka katika makundi matatu.
Kundi la kwanza liliitwa Sheria au Torati, ambapo pia liliitwa vitabu
vitano vya Musa. Mwanzo hadi Kumbukumbu la torati.
Kundi la pili liliitwa.Manabii. Kundi hili waliligawanya
katika sehemu mbili ambazo ni:
1.
Manabii wa mwanzo (Yoshua hadi Wafalme)
2.
Manabii wa baadae. (Isaya hadi Malaki isipokuwa Danieli)
Kundi hili lilihusisha vitabu vya Yoshua hadi wafalme na Isaya hadi Malaki
isipokuwa Danieli.
Kundi la tatu liliitwa Maandiko. Ambayo ni Ayubu
hadi Mithali na Magombo matano(Wimbo uliobora, Ruth, Maombolezo, Mhubiri,
Esta.). Ndipo ilifuatiwa na Danieli, Ezra- Nehemia na Mambo ya nyakati.
Nukuu za Agano jipya zinatoka sehemu
zote tatu, 94 kutoka katika vitabu
vya sheria, 99 kutoka Manabii na 85 kutoka katika maandiko.
“Tangu
damu ya Habili hata damu ya Zekaria….( Luka 11:51 ).
·
Kifo cha Habili, hii inawakilisha
kitabu cha kwanza katika Biblia ya kiebrania ( Mwanzo
4:8 ) Ambacho ni Mwanzo.
·
Kifo cha Zekaria hii huwakilisha kitabu
cha mwisho katika Biblia ya kiebrania (Nya 24:20) ambacho ni Mambo ya nyakati.
Hivyo basi Yesu Kristo Bwana wetu
alilitambua Agano la Kale lote kama Neno la Mungu.
VI.Muundo wa Agano la kale katika Biblia yetu.
I.
Sheria.
|
II.
Historia.
|
Iii.Ushairi.
|
IV.
Manabii.
|
1. Mwanzo
2. Kutoka
3.Mambo ya walawi
4. Hesabu
5. Kummbukumbu la torati.
Jumla vitabu 5
|
1. Yoshua
2. Waamuzi
3 .Ruthu
4 . 1 Samweli
5. 2.Samweli
6. 1Wafalme
7. 2Wafalme wa pili
8. 1 Mambo ya nyakati
9. 2 mambo ya nyakati
10. Ezra
11. Nehemia
12
Esta
Jumla
vitabu 12.
|
1. Ayubu
2. Zaburi
3. Mithali
4. Mhubiri
5. Wimbo uliobora.
|
1.
Isaya
2. Yeremia
3.Maombolezo
4.ezekieli
5. Danieli
6. Hosea
7. Yoeli
8. Amosi
9.Obadia
10. Yona
11. Mika
12.Nahumu
13. Habakuki
14. Sefania
Hagai.
Zekaria
Malaki
Jumla vitabu 17
|
Jambo
la kukumbuka hapa ni kwamba mpangilio wa vitabu
katika Biblia yetu na ile ya kiebrania
ni tofauti na hakuna athali zozote juu ya neno la Mungu kutokana na
kutofautiana huko kwa mpangilio.
VII.
Sababu za kusoma Agano la Kale.
1. Agano jipya limefichwa ndani ya Agano
la Kale.
2. Agano la Kale limefunuliwa ndani ya
Agano Jipya.
3. Kile tulichonacho leo ni matokeo ya
kile kilichotokea jana.
4. Kile tunachofanya leo
kinatengeneza hali ya kesho.
5. Hatuwezi kulielewa agano jipya bila
kujifunza Agano la Kale.
6. Liliandikwa kwaajili yetu pia.
VIII.
Nukuu za Agano la Kale katika Agano jipya.
1. Agano jipya lina karibu rejea tofauti
295 toka kwenye Agano la Kale.
2. Imetumiwa mara 224 kwa njia kama
“Imeandikwa au Mungu akasema” na ina jumuisha karibu mistari tofauti 278 kutoka Agano la Kale.
3. Karibu mara 56 waandishi wa Agano la
Jipya wanarejea Mungu kama mwanzilishi wa Agano la Kale.
4. Kuna nafsi 41 ambazo kwa njia ya
utangulizi iko katika wakati uliopo kama
“ Asema” sio kama wakati uliopita kama “alisema”
IX. Tofauti
iliyopo kati ya agano la kale na agano jipya.
Kuna
tofauti kati ya Agano la Kale na Agano Jipya, tofauti hizo sio zenye kupingana
bali ni zenye kujengana, kutegemeana na kuathiliana, hivyo ni tofauti zenye
maana.
A.
Agano la Kale.
Agano la kale lina sura ya tofauti na
Agano jipya katika maeno mbalimbali na tofauti tofauti. Kama ifuatavyo:
1.
Sheria ya nje
2.
Uhusiano na Mungu pekee kupitia kwa
kuhani.
3.
Malipo ya dhambi kwa muda
4.
Kumjua Mungu kupitia kwa wale
wafundishao.
5.
Utiifu huonesha imani.
6.
Kuhusu watu wote.
7.
Kutokuwezeshwa.
8.
Wakati wa Agano la kale ulimalizika na
kifo cha Bwana Yesu.
9.
Umepangwa ili kuonesha mpango wa
utakatifu wa Mungu na hali ya dhambi ya mwanadamu.
B.
Agano jipya.
1. Sheria
ya ndani.
2.
Uhusiano wa karibu sana na Mungu
kibinafsi.
3.
Malipo ya dhambi milele.
4.
Kumjua Mungu kupitia Roho mtakatifu aishie
ndani yetu na Neno la Mungu.
5.
Imani huoneshwa kwa utiifu.
6.
Huhusu mtu mmojammoja.
7.
Ushindi kwa nguvu za Roho mtakatifu.
8.
Wakati wa Agano Jipya ulianza na kifo
cha Bwana Yesu pale Msalabani.
9.
Umepangwa ili kuokoa,huonesha utakatifu
wa Mungu katika Kristo.
X. Uhusiano uliopo kati ya Agano la Kale na Agano
jipya.
Agano
la kale lina husiana sana na agano jipya kwani vyote vina ujumbe mmoja
ambao ni ukumbozi na kiini kimoja ambacho ni Yesu Kristo mwokozi wa ulimwengu.
Maagano hayo yote mawili yanapatana
katika mambo yafuatayo.
Agano
la kale Agano
Jipya.
Huanzisha Ufunuo wa Mungu Humalizia ufunuo wa Mungu.
Hutabiri
kuwa Yesu ndiye masihi Humwonesha Bwana Yesu
kuwa ndiye Masihi.
Huhitaji
imani kwaajili ya wokovu Huhitaji imani kwaajili ya wokovu.
Huhitaji kuishi kwa imani Huhitaji kuishi
kwa imani.
Hutoa
ufahamu kuhusu Mungu na njia zake Hutoa ufahamu kuhusu Mungu na njia
zake
Agano
jipya limefichwa ndani ya Agano la Kale Agano la Kale limefichuliwa ndani ya
Jipya.
Agano
la Kale si kamili bila Agano jipya Agano Jipya haliwezi kueleweka bila Agano
la Kale.
Hivyo basi twaweza kuhitimisha kwa kusema kwamba Agano la kale si kamili bila ya Agano
jipya,hutarajia utimizo wake na kumalizikia katika Agano Jipya.
Zoezi.
Katika
makundi ya watu watano watano jadili
maswali yafuatayo.
1. Nakala
za kale zilizogunduliwa kule Kumlani mnamo mwaka 1947 hazina umuhimu wowote
katika ukristo na taaluma ya thiolojia kwa ujumla . Jadili kauli hii kwa hoja
madhubuti.
2. Utofauti
wa mpangilio wa vitabu katika Biblia ya Kiswahili na kiebrania unadhihirisha
dhahili kwamba Biblia yetu imepotoshwa sana. Jadili usemi huu kwa hoja kuntu.
3. Jadali
kauli inayosema kwamba bila Agano la
kale hakuna Agano Jipya.
4. Eleza
umuhimu wa kujifunza Kozi hii ya Pitio la Agsno la Kale.
5. Si
lazima wakristo kusoma na kufuata mafudisho ya Agano la kale kwa sabbu Agano la Kale ni
mahususi kwa wayahudi tu na si watu wote. Pinga kauli hii kwa hoja madhubuti.
6. Agano
la Kale limefafanuliwa ndani ya Agano jipya. Kubali usemib huu kwa hoja
madhubuti.
MADA YA PILI: PENTATUKI.
Malengo ya mada.
Baada
ya kumalza mada hii mwanafun zi ataweza:
·
Kueleza maana ya Pentatuki.
·
Kueleza maana ya torati.
·
Kufafanua maana ya kila jina la vitabu
vitano vya Musa.
·
Kutaja watu mashuhuri katika kila kitabu
·
Kueleza matukio makuu katika kila kitabu
·
Kutaja mitajo ya Kristo katika kila
kitabu
·
Kutaja baadhi ya mafundisho makuu katika
kila kitabu
·
Kutaja mistari ya Msingi katika kila
kitabu N.k
I. Utangulizi.
Katika mada hii tutatazama vitabu vyote
vya Musa kwa muhtasari
Tutachunguza mwandishi, matukio makuu,
watu mashuhuri, muundo, mtindo,mafundhisho makuu, mitajo ya Kristo na mistari
ya msingi au kiini cha kila kitabu.
Vitabu vitano vya kwaza vya Biblia hujulikana kama vitabu vya
Musa. Pia huitwa Sheria au Torati. Vitabu hivi hufanya katiba ya thiolojia kwaajili ya taifa la Israeli na pia vina
misingi ya kweli iliyodhihirishwa na Mungu
ambapo juu yake ukristo husimama. Vitabu hivi vitano vinatoa taarifa
tangu mwanzo wa uumbaji hadi wakati wa matayarisho ya kuingia nchi ya ahadi
yaani Kaanani.
Pia vitabu vitano vya kwanza vya Biblia
hujulikana kama Pentatuki ambalo ni
neno la kiyunani lililotokana na maneno mawili ya kiyunani ambayo ni Penta
maana yake tano na Teuchos maana yake kitabu.
Hapo awali vitabu vyote hivi vitano
vilikuwa kitabu kimoja tu, lakini viligawanywa kuwa vitabu vitano li
kurahishisha kuvitunza katika magombo matano.
Wayahudi
walikitaja kitabu cha Pentatuki kuwa sheria tu.(2Nya 17:9, Neh 8:1-3,18, Mt 5:17, Luk 24:44).
Kimsingi
haiwezekani kuzifahamu vizuri sehemu zingine za Biblia bila ya kuvifahamu
vitabu hivi vitano vya kwanza.
Vitabu
hivi vitano ni muhimu sana kwa kwa
sababu vinatusaidia katika kuelewa:
Mungu
mwenyewe
Mwanzo
wa ulimwengu na mwanadamu.
Msingi
wa mawazo ya kithiolojia kama vile
-Dhambi
-Wokovu
-Utakaso
-Imani. N.k.
Mwandishi
wa Pentetuki. Katika mapokeo ya Kiebrania na ya
Kikristo tangu zamani Musa anatambuliwa kuwa ndiye mwandishi wa Pentatuki.(Neh
8:1, 13:1, Dan 9:11, Mk 12:26.
Pentatuki yeenyewe haielezi kwamba Musa ndiye mwandishi wake
isipokuwa inaonesha kazi za uandishi ambayo Musa aliifanya. Aliandika sheria
ambayo Mungu aliwapa wana wa Israeli Kut 24:4,
34:27, Kum 31:9,24, Kut 17:14,
Hes 33:2. N.k.
Ufunguo katika usomaji wa Agano la kale:
1.
Kuchunguza
yale yaliyotokea kwa watu wa Munguwa kale. (Taifa la
Israeli na watu wa Agano la kale.)
Matukio
yaliyoandikwa katika Agano la kale ni halisi yalitukia kama Agano la kale
linavyoeleza.
2.
Kutazama
unabii kuhusu Yesu Kristo. Bwana Yesu Kristo ameoneshwa
katika kila kitabu cha Agano la Kale. (Mt 5:17-18, Yn 5:39).
3.
Kutazama
utimizo binafsi.
Kuangalia kile Agano la Kale linachomaanisha kwetu sasa.
II.
KITABU CHA MWANZO.
A.Utangulizi
Katika vitabu vitano vya Pentatuki kitabu cha
kwanza kinaitwa mwanzo. Kitabu hiki
kinaelezea kuhusu mianzo ya kila kitu isipokuwa Mungu ambaye hana mwanzo wala
mwisho.
Watafsiri wa septuaginta ndio waliotoa
jina hili la “Mwanzo” (Genesis) kwa
kitabu cha kwanza cha Biblia kwani Waebrania wa
kale walikiita kutokana na maneno yake ya kwanza yaani “ Hapo Mwanzo”.
Jina la kitabu hili lina asili katika
Kiyunani na humaanisha mwanzo wa kila kitu.
B.Kuhusu
mwandishi. Kulingana na mapokeo mwandishi wa kitabu hiki ni Musa. Musa alikuwa
mtaalamu wa kutunga mashairi na
Historia. Maisha yake yalikuwa na mahusiano mazuri na Mung.u.(Kum 34:10).
C.Muundo. Kitabu hiki kina sura hamsini na migawanyo mikuuu miwili
1.
Mgwanyo
wakwanza, sura ya kwanza
hadi ya kumi na moja (1-11).
2.
Mgawanyo
wa pili, sura ya kumi na mbili hadi sura ya hamsini.(12-50).
Mpangilio wa visa na matukio ni wa moja
kwa moja kwa kiasi kikubwa.
D.
Mtindo wa kiuandishi. Kitabu hiki kimetumia mtindo wa monolojia kwa kiasi kikubwa na daiyolojia kwa kiasi fulani. Majibizano yanajitokeza
wakati wahusika wanajibizana na kutenda katika kitabu.
Mwandishi ametumia Lugha ya kawaida yenye uwezo wa kueleweka kwa watu wote.Lugha
ya kishairi imetumika katika uandishi wa nyimbo na tenzi zinazojitokeza katika
kitabu.Mfano sura ya 49.
E.
Ujumbe wa kitabu ni Mwanzo wa kia kitu.
F.
Mstari wa msingi: Mwanzo 3:15.
Sura kumi na moja za kwanza za kitabu cha Mwanzo ndio msingi wa Biblia nzima.
Katika sura hizo kuna matukio yafuatayo:
1. Uumbaji (sura ya 1 & 2).
2. Anguko (sura ya 3).
3. ahadi ya kwanza ya mwokozi(3:15).
4. Mauaji ya kwanza (4:1-15).
5. Kuliitia jina la Bwana kwa mara ya
kwanza- wana wa Sethi (4:25-26).
6. Mwanzo wa familia ( 4:1-15).
7. Mwanzo wa ustaarabu wa mwanadamu (4:16- 22).
8.
Mtu wa kwanza Mwenye imani kuu-Nuhu (6:8-22)
9. Gharika ya kwanza (sura ya 6-8).
10. Upinde wa mvua Ahadi ya Mungu na
ishara ya Agano. (9:8-17).
11. Mwanzo wa mataifa. (sura ya 10).
12. Kutokea kwa lugha mbalimbali.
(11:1-9)
13. Kutawanyika kwa wana wa Nuhu
(11:8-32). Wana wa Nuhu walitawanyika na kwenda sehemu zifuatazo:
1.
Uzao
wa Yafethi: Walielekea magharibi kuelekea Uhispania (10:2-5).
2.
Uzao
wa Shemu:. Waliishi katika eneo la Kaskazini mwa Ghuba ya
Uajemi(10:21:31)
3.
Uzao
wa Hamu: Walielekea Kusini mpaka Afrika (10:6-14).
G.
Sehemu ya pili
Sehemu ya Pili ya kitabu cha mwanzo
ambayo inaanza na sura ya 12 hadi sura ya 50 inazungumzia mwito wa Mungu kwa Ibrahimu
na kumfanya taifa kubwa. Mungu alianzisha taifa kupitia Ibrahimu, Isaka na
Yakobo. Yakobo alizaa watoto kumi na mbili wa kiume ambao ndio waliofanya makabila kumi na mbili ambayo
ndiyo taifa la Israeli.
Katika sehemu hii tunajifunza mambo mbalimbali
namna Mungu alivyowaita watu na watu walivyoitikia wito huo.
Matuikio hayo ya kitabu cha Mwanzo ndiyo
yanayojenga msingi wa mtu kumjua Mungu alivyo na mpango wake mahususi wa kumkomboa
mwanadamu kutoka dhambini.
F. Watu
mashuhuri.
1.
Habili
2.
Sethi
3.
Henoko
4.
Nuhu
5.
Ibrahimu
6.
Isaka
7.
Melkizedeki
8.
Nimrodi
9.
Yusufu.N.k,
G.
Mitajo ya Kristo.
1. Isaka.
2. Melkizedeki
3. Yusufu.
H.
Baadhi ya mafundisho makuu ya kitabu cha Mwanzo.
1.
Mungu ndiye muumba mtawala na mwenye
nguvu za kushikilia dunia.
2.
Mungu alimuumba binadamukwa mfano wake
wa kiroho ili awe na ushirika nae.
3.
Mungu alimuumba mwanadamu akiwa na utashi yaani uhuru wa kuchagua.
4.
Mungu daima ni mwaminifu kwa ahadi zake.
5.
Mungu ana mpango wenye makusudi ya
ukombozi ambamo yumo katika
hatua
za kuutimiza.
6.
Mungu hupenda wanawe watembee kwa imani.
7.
Tabia ya Mungu haibadiliki.
8.
Mungu huwaacha wanadamu kwa hiari yao
wachague kumfuata yeye.
9.
Mapenzi ya Mungu ni kwamba watu wake wawe na uvumilivu wakisubiri atimize
ahadi zake kadri apendavyo yeye na si wao.
10.
Kutaka kutimiza mpango wa Mungu katka
maisha yetu bila yeye Mungu kuhusika ni dalili ya kiburi na kukosa uvumilivu.
11.
Daima Mungu huamua kumtumia mdogo badala
ya mkubwa na dhaifu badala ya mwenye
nguvu.
12.
Mungu hutazamia ibada toka kwa watu
wake.
13.
Sadaka hugusa moyo wa Mungu.
14.
Imani huonesha jinsi mtu anavyomjua
Mungu.
15.
Mungu huwatuza watu wanaomheshimu.
III. KUTOKA.
A.Utangulizi
Kitabu cha Kutoka ni kitabu cha pili
katika pentatuki.
Jina la kitabu cha Kutok(Exodus)a lina
asili ya kiyunani na maana yake halisi ni kutoka au kuondoka au njia ya
kuondoka au njia ya kutoka.
B.
Mwandishi. Kulingana na mapokeo mwandishi wa kitabu cha Kutoka
ni Musa na inadhaniwa kuwa kitabu hiki kiliandikwa mwaka 1550 au 1500 K.K
C.
Muundo. Kitabu kina sura arobaini na kimegawanyika katika
sehemu kuu tatu ambazo ni
Sehemu
ya kwanza. Utumwa (Sura 1-11).
1. Waebrania
wakiwa nchini Misri.
2. Taifa
kuongezeka
3. Mwito
wa Musa.
4. Mapigo
kumi
5. Nguvu
za Mungu.
Sehemu
ya pili. Ukombozi toka Misri. (Sura
12- 18).
1. Malaika
wa kifo
2. Pasaka
3. Kuondoka
Misri
4. Kuvuka
Bahari ya Shamu
5. Wingu
na Nguzo ya moto.
6. Mana
Sehemu
ya tatu. Ufunuo wa Mungu (Sura 20-40).
1. Agano
la Israeli
2. Sheria ya Musa
3. Sabato
4. Amri
kumi
5. Maskani
Ndama wa dhahabu
6.
Utukufu wa Mungu.
D.
Mtindo wa kiuandishi. Kitabu kimeandikwa kwa kutumia mtindo
wa monolojia (Masimulizi) na dayolojia kwa kiasi fulani. Pia kitabu kimetumia
mtindo wa kiushairi hasa katka nyimbo na Sara
mfano Kut 15:1-21.
Lugha iliyotumika ni rahisi na yenye
kueleweka kwa wasomaji wote . Kitabu hakina tamathali za semi zenye kiwango cha
kumchanganya msomaji
E.Ujumbe wa kitabu . Mungu ni Mkombozi.
Musa aliandika katika kitabu hiki cha Kutoka ukombozi wa ajabu wa Mungu kwa watu wake,
Israeli kutoka katika kifungo cha utumwa na dhambi na ufunuo wake yeye mwenyewe
na uadilifu wake kwao ili awaoneshe kwamba Mungu ndiye Mwokozi na mkombozi.
Katikati
ya mwazo na kutoka Familia ya
Mungu ilikua kwa kasi na kuwawa ni taifa
kubwa . Wana wa Israeli waliingia Misri wakiwa watu 70 yaani mzee Yakobo,
watoto wake, wake za watoto wake na watoto wao, jumla yao wakiwa sabini.
Baada ya miaka mianne (400)
familia hii ya watu sabini ilikuwa na kuongezeka kwa kasi sana na kufikia karibu milioni tatu na kuwa taifa kubwa na
hodari.
Tukio muhimu sana katika Agano la kale
limeorodheshwa katika sura ya kumi na mbili mpaka kumi na nne. Sura hii inahusu
ukombozi wa kila mwisraeli kupitia damu ya mwanakondoo wa pasaka na nguvu ya
Mungu walipovuka bahari ya shamu.
Tukio la kutoka kwa wana wa Israeli
Misri ni muhimu sana na linatazamwa kama kivuli cha waamini wote kuokolewa kutoka katika utumwa
wa dhambi na nguvu ya dhambi.
Waisraeli waliokolewa kwa damu ya
mwanakondo wa pasaka sisi tunaokolewa kwa damu ya mwanakondoo wa Mungu Yesu
Kristo. Yn 1:29.
Katika kitabu hiki kuna taashira mbalimbali au
mitajo mbalimbali inayosimama badala ya kitu kingine.Baadhi ya taashira hizo
ni:
1.
Musa anamwakilisha Bwana Yesu Kristo.
2.
Farao
anamwakilisha shetani
3.
Misri inawakilisha ulimwengu wa dhambi.
4.
Wana wa Israeli watu walio dhambini
wanaohitaji kuokolewa.
F.
Mitajo ya Kristo.
1. Musa.
Mkomobzi
2. Haruni-
Kuhani mkuu
3. Mwanakondoo
wa pasaka.
4. Damu
ya mwanakondoo wa pasaka.
5. Mana
G.
Matukio Makuu.
6. Mateso
katika nchi ya ugeni
7. Mauaji
ya Musa
8. Wito
wa Musa
9. Mapigo
kumi ya wamisri
10.
Kuondoka Misri
11.
Kuvuka bahari ya Shamu
12.
Muujiza wa Maana jangwani
13.
Kutolewa kwa sheria katika mlima Sinai
14.
Ndama wa dhahabu.
15.
Maagizo ya ya ujenzi wa Hema ya kukutania.
16.
Agano la Mungu na Isareli kupitia
mtumishi wake Musa.
F. Watu
mashuhuri.
1.
Farao
2.
Musa
3.
Haruni
4.
Miriamu
5.
Yethro
G.Mapigo
Kumi Ya Wamisri.
1.
Pigo laMaji kuwa damu.
2.
Pigo la Vyura.
3.
Pigo la Chawa
4.
Pigo la Nzi
5.
Pigo la majipu.
6.
Pigo la Tauni
7.
Pigo la Mua ya mawe
8.
Pigo la Nzige
9.
Pigo la Giza
10.
Pigo kuu lakifo cha mzaliwa wa kwanza wa
kila kitu katika jami ya wamisri..
Jambo
la msingi na kukumbuka hapa ni kwamba Mungu aliwalinda watu wake Israeli. Mapigo
yote haya yaliwapata wamisri lakini wana wa Israeli walikaa salama katika Eneo la Gosheni walililopewa na Farao kuwa
makazi yao .Halikuwapata pigo lolote kwani Bwanaa alikuwa upande wao.
H. Mafundisho makuu ya kitabu. Yafuatayo
ni baadhi ya mafundisho makuu yanayopatikana katika kitabu hiki cha Kutoka:
Mungu
pekee ndiye anaestahilikuabudiwa
1.
Mungu ni mwaminifu kwa ahadi zake
2.
Mungu anapomwita mtu kwaajili ya huduma
humpa upako wa kumwezesha kufanya huduma hiyo.
3.
Hakuna sababbu zinazokubalika kukataa
mwito wa Mungu.
4.
Mungu huchukua jukumu la kuwaumba watu
vile walivyo kwaajili ya utukufu wake.
5.
Ibada hukamilika kwa dhabihu.
6.
Ibada hufanya kwa maelekezo ya Mungu
mwenyewe.
7.
Uwezo wa Mungu ni mkuu kabisa kuliko ule
wa miungu.
8.
Mungu huheshimu mgawanyo wa majukumu na
utoaji wa mamlaka kwa wale watu wawezao, wacha Mungu na waaminifu.
9.
Mungu anahitaji watu wawe na masuhiano
safi na yeye na wao kwa wao
10.
Sheria za Mungu ni
takatifu na zilitolewa ili zifuatwe.
11.
Mungu hupenda kukaa miongoni mwa watu
wake na kushirikiana nao.
IV.
MAMBO YA WALAWI.
A.
Utangulizi.
Jina la kitabu hiki liatokana na neno la
kilatini “Leviticus”. Lenye maana ya walawi.Mambo ya kitabu hiki ni ya wakati wana
wa Israeli wakiwa chini ya mlima Sinai wakiwa safarini kueleka nchi ya ahadi.Kufuatana
na ahadi yake Mungu kwa Ibrahimu aliwatoa waisraeli kutoka utumwani Misri na
kuwaweka katika njia kuelekea Kaanani. Baada
ya miezi mitatu walifika katika mlima Sinai au Horebu, mahali walipokaa karibu
mwaka mzima. Katika muda ule walijiandaa kwa maisha mapya yaliyokuwa
yanawakabili.Kut 19:1, Hes 10:11.
Kabla ya kuelekea katika nchi ya ahadi
Mungu aliwaelekeza Waisraeli kwa kirefu
sana Jinsi walivyotakiwa kumwabudu yeye
na kufuata utaratibu wa matoleo yaliyo ambatana na dhabihu za wanyama kwenye
maskani ya ibada.
Mungu alitaka watu wake wawe watakatifu
kama yeye alivyo mtakatifu. Law 15:13, !8:1-5.
Katika sura ya kwanza hadi ya tano Mungu
alitoa aina tano za matoleo. Aina tatu za
kwanza zilikuwa za hiari na ziliwekwa ili kuhakikisha kujitoa binafsi na
kujiweka mikononi mwa Mungu.
Sadaka za aina mbili za mwisho zilikuwa
za dhambi, hatia na msamaha wa dhambi. Hizi zilikuwa ni sadaka za lazima na
ziliitwa sadaka za dhambi na hatia. Sadaka
za aina hii zilihusika na kuleta msamaha wa dhambi, mtu alizotenda.
Katika sura ya kumi vifo vya wana wawili
wa Haruni Nadabu na Abihu vilionesha jinsi Mungu asivyo na mchezo kuhusu mtu
kuwa mtakatifu.
B.
Kuhusu mwandishi wa kitabu. Kwa mujibu wa mapokeo mwandishi
wa Kitabu cha Mambo ya walawi ni Musa.Inadhaniwa kuwa imeandikwa katikati ya
miaka ya 1550 na 1530. K.K
C.
Muundo wa kitabu. Kitabu cha Mambo ya Walawi kina sura
ishirini na saba (27) na kimegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni.
1. Sehmu ya
kwanza.
Dhabihu(sura 1-10).
·
Kumwabudu
Mungu.
·
Matoleo
matano ya dhabihu.
·
Dhabihu
za wanyama
·
Ukuhani
wa Haruni
2. Sehemu ya
pili:Utakaso
(sura 11-27)
Kutembea
na Mungu.
·
Sheria
za usafi na unajisi.
·
Siku
ya upatanisho.
·
Dhabihu
za damu
·
Maisha
ya utakatifu
·
Sikukuu
saba za Israeli.
D.Mtinbdo wa kiuandishi.Mwandishi
ametumia mtindo wa monolojia tangu mwanzo hadi mwisho wa kitabu.
Lugha
iliyotumika ni ya kawaida yenye kueleweka karibu na wasomaji wote wa kawaida
.
E.Msitari wa
msingi
ni Law 17:11.
D. Ujumbe wa
kitabu: ni Utakatifu.
E. Ufafanuzi wa
sadaka mbalimbali.
1. Sadaka za
kuteketezwa
Sadaka
hii ilikuwa ni kwa kila mtu kwani ilikuwa ni kwaajili ya kufunika dhambi. ya
mtu mmoja mmoja.
Alitolewa
mnyama asiye na kasoro yoyote.(mfano kondoo, ng’ombe au njiwa kulingana na
uwezo wa mtu).
2. Sadaka ya
chakula.
Walitoa
unga au nafaka.
Sadaka
hii iliwakilisha shukrani kwa Mungu na kujiweka wakfu kwake.
3.Sadaka ya
amani.
Hii
ilikuwa ni sadaka ya hiari iliyokuwa inaonesha upendo wao kwa Mungu.
Mnyama
asiye na kasoro alitumika katika ibada hii.
Sehemu
chache kadhaa za nyanma mtoaji alichukua ili kufurahia cha kula chake na marafiki zake kama ishara ya ushirika na walipaswakula mbele za Bwana.
4. Sadaka ya
dhambi.
Hii
ilihusika na utakaso wa eneo fulani lililohusika. Mtoaji alihusika kama vile
kuitakasa hema ya kukutania na madhabahu yake.(Law 9:8-11).
Ilikuwa sehemu ya malipizi iliyokuwa ikifanywa
mara moja kila mwaka.(16:11-14).
Sadaka ya hatia.
Ilihusika kuleta utakaso kwa mtu binafsi
kama amechukua kitu ambcho kilikuwa ni mali ya Mungu, au mali ya mwingine. Mfano
fungu la kumi au kitu cha ndugu yake. Sheria iliagiza mtu alete kondoo dume
asiye na kasoro yoyote.
Jambo la kukumbuka na kuzingatia hapa ni
kwamba sadaka zote hapo juu zilimwakilisha Yesu na Huduma yake kama Kuhani mkuu
wetu.
Sadaka hizo zinaelezea pia utakatifu wa
Mungu wetu na kutudai kuwa na mwenendo wa kiuadilifu.(Ebr 6)
F.
Watu mashuhuri.
1.
Musa
2.
Haruni(Kuhani mkuu)
3.
Makuhani
4. Walawi.
G.
Mafundisho makuu.
1.
Mungu ni mtkatifu hivyo anadai watu wake
kuwa watakatifu kama yeye.
2.
Utakatifu huhusisha usafi, kujitenga na
kuwa tofauti kabisa.
3.
Msamaha wa dhambi hupatikana kwa njia ya
dhabihu ya kafara mbadala.
4.
Dhaibu hutolewa kwa kadri ya maelekezo
ya Mungu mwenyewe.
5.
Utakatifu ni mwenendo wa maisha ya kila
siku.
H.
Mitajo ya Kristo.
Katika kitabu hiki cha kutoka sadaka
zote zinazotajwa ni kiwakilishi cha Yesu Kristo. N.k
Tunaweza kuhitimisha kwa kusema kwamba
kitabu cha Mambo ya walawi ni katiba ya ibada ya Wana wa Israeli. Mungu aliwapa
mwongozo wa namna wanavyopaswa kuishi katika nchi ya ahadi alikokuwa
anawapeleka. Aliwapa sheria, kanuni na taratibu. Jumla ya sheria zote zilikuwa
613 ambazo Mungu aliwapa wana wa Isreli. Zikiwa zimegawanyika katika makundi
kadhaa. Mfano sheria za kiraia, sheria za kidini n.k. sheria zote hizo
zinapatikana katika pentatuki yote.
V.
HESABU.
A. Utangulizi
Kitabu hiki cha Hesabu ni kitabu cha nne
katika pentatuki. Jina la kitabu hiki linatokana na sensa ambayo Musa aliifanya
kabla ya kuondoka katika mlima Sinai. Biblia ya kiebrania inatumia jina la jangwani na kwa kweli jina hili lina
sadifu yale yaliyomo ndani ya kitabu kwa sababu kitabu hiki kinaelezea habari
ya safari ya waisraeli toka mlima Sinai hadi mpakani mwa nchi ya Kaanani. Na
sehemu kubwa ya safari hiyo ilikuwa ni jangwani.
B.
Kuhusu mwandishi wa kitabu. Kwa mujibu wa mapokeo kitabu hiki
kiliandikwa na Musa.Tarehe yake ya kuandikwa
haitofautiani na ile ya Warawi na kutoka.
C.
Muundo wa kitabu. Kitabu hiki kina sura therathini na sita(36)
na kinagawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni:
Sehemu
ya kwanza.Maagizo(sura 1-10)
Sehemu
ya pili. Kujaribiwa
(sura 11-21)
Sehemu
ya tatu.Maagizo.(sura 22-36)
D.
Mtindo wa kiuandishi. Kitabu hiki kimetumia mitndo wa
Monolojia kwa kiasi kikubwa na daiolojia kwa kiasi kidogo. Pia kimetumia lugha
ya kishairi hususani katika sura ya 21 hadi 24.
Lugha iliyotumika ni nyepesi yenye
kueleweka karibuni na wasomaji wote wa kawaida.
E.
Ujumbe wa kitabu. Kutangatanga jangwani.
Mungu hutaka watu wake watembee kwa
imani na wanaposhinwa kufanya hivyo
Hukosa Baraka muhimu za Mungu na kusababisha Mungu awaadhibu.
F. Mstari wa msingi Hes 14:20-24.
G.
Matukio muhimu.
1.
Safari ya wana wa Israeli toka Sinai
hadi kadeshi miaka miwili.
2.
Kuzunguka Kadeshi Barnea miaka therathini na nane.
3.
Wapelelezi kumi na wawili kupeleleza
nchi ya ahadi.
4.
Kuadhimishwa kwa pasaka ya kwanza.
5.
Nyoka wa moto na nyoka wa shaba.
6.
Sensa ya wana wa Israeli.
7.
Kifo cha Haruni.
8.
Kifo cha Koran na wenzake.
H. Watu mashuhuri.
1.
Musa
2.
Haruni.
3.
Miriamu
4.
Yoshua
5.
Karebu
6.
Kora
7.
Finehasi
8.
Eleazari
9.
Baalamu.
I. Baadhi ya mafundisho makuu.
1.
Mungu anatarajia moyo wa utIi na
shukrani toka kwa watu wake.
2.
Mungu anahitaji watu wake wawe wavumilivu.
3.
Mungu anataka watu wake waishi kwa imani
4.
Mungu anataka watu wake waheshimu
mamlaka aliyoiweka.
5.
Dhambi huleta madhara katika roho na
katika mwili.
6.
Kunung’unika ni hatari sana.
7.
Kutokuwa na imani ni dhambi.
8.
Tunaposhindwa kumwamini Mungu hupelekea
kukosa Baraka zake.
9.
Mgwanyo wa majukumu ni muhimu sana ili
kuweza kuleta ufanisi katika uongozi.
10.
Mungu ni mwaminifu kwa ahadi zake zote
yaani katika kubariki na katika kuadhibu.
J.
Mitajo ya Kristo.
1. Nyoka
wa shaba.
2. Mwamba
uliotoa maji.
3. Mana.
4. Miji
ya makimbilio
5. Nguzo
ya wingu na ya moto.
Jambo la kukumbuka hapa ni kwamba kitabu
hik cha Hesabu kinaelezea safari ya wana wa Israeli toka mlima Sinai paka
mpakani mwa nchi ya Kaanani. Ni kitabu cha safari. Kinaeleza changamoto
mbalimbali walizokutana nazo wana wa Israeli katika safari yao na namna
walivyoitikia changamoto hizo na matokeo yake.
Kitabu hiki kinatoa picha ya safari yetu
ya kwenda Mbinguni kwamba kuna changamoto mbalimbali ambazo tutakutana nazo.
Namna tunavyoitikia changamoto hizo itaamua
na kuathili safari yetu. Hivyo ni lazima kuwa wavumilivu na
wanyenyekevu. Kwa sababu Mungu ni Mwaminifu kwa ahadi zake atatimiza kila kitu
alichokisema kwa wakati wake. Tusiwe wepesi kukata tamaa, kulalamika na kunung’unika
kwani hii huonesha kukosa imani na kusababisha tushindwe kupata baraka alizotuandalia Mungu wetu.Tutembe kwa imani na
kwa ushujaa mkuu.
V.KUMBUKUMBU LA TORATI.
A. utangulizi
Jina
la kitabu hiki linatokana na neno la kiyunani “Deuteronomium” lenye maana ya sheria ya mara ya pili. Jina hili
lilitolewa na watafsiri 70 waliotafsiri Biblia kwa mara ya kwanza katika lugha
ya Kiyunani. Jina hilo linatokana n muungano
wa maneno mawili ambayo ni deuteros
likimaanisha pili na nomos likimaanisha sheria.
Katika kitabu hiki Musa anakifundisha
kizazi kipya hatima ya kumiliki nchi ya ahadi na njia mpya ya kuishi.
Kitabu hiki kiliandikwa katika uwanda wa
Moabu, wana wa Israeli walipokuwa karibu kuvuka mto Yordani na kuingia kuimiliki nchi ya ahadi.
Mua aliwaonya kuhusu hatari ya kurudia
makosa kama walivyofanya baba zao hapo awali.
Kwa hiyo tene na tena Musa alisema “ Kumbuka”
kuwu waangalifu, msisahau, sikilizeni
kwa umakini. Msirudie makosa tena
kama walivyotenda baba zenu.1Kor 10:1-11.
Taifa hili lilikuwa limefika mahali
palepale walipokuwa wamefika miaka 38 iliyopita. Wakati huu sasa wanapaswa
kumtii Mungu na kuwa waaminifu kwake ili waingie katika nchi ya ahadi.
Mungu alikuwa anataka kuwaingiza wana wa
Israeli katika nchi ya ahadi, wao walichokuwa wanapaswa ni kuwa waaminifu na
watiifu kwake.
Katika kitabu hiki Musa anarudia kufundisha kwa upya sheria ya Mungu kwa kuwa
kizazi hiki si kile cha wakongwe kilichotoka Misri bali ni watoto wao ambao
walipaswa kukumbushwa yale ambayo Mungu
alisema na baba zao. Ndiyo maana inaitwa sheria ya mara ya pili.
B. Kuhusu mwandishi.Kulingana
na mapokeo mwandishi wa kitabu hiki ni Musa. Inadhainwa kuwa sura ya mwisho ya
kitabu hiki iliandikwa na Yoshua.
C.Muundo
wa kitabu. Kitabu hiki kina sura therathini na nne(34) na
chaweza kugawanywa katika sehemu tatu ambazo ni kama hotuba, Musa akihutubia
kizazi kipya. Sehmu hizo ni :
Sehmu
ya kwanza. Kutazama
nyuma.(Historia ya Israeli) sura ya kwanza mpkaa ya tatu.(1-3)
Sehemu
ya pili. Kutazama ndani.
(sura ya nne hadi sura ya ishirini na sita ,4-26). Kulitambua Agano la Mungu wao. Wao ni taifa teule kwa hiyo wanapaswa kutii sheria ya Mungu wao.
Sehemu
ya tatu . Kutazama mbele.(Maandalizi ya safari) sura ya ishirini na saba hadi therathini na
nne. (27-34). Maagizo ya mambo ambayo walipaswa kufanya baada ya kuingia katika
nchi ya ahadi.
D.Lengo
la Mungu.
Alitutoa nje ili atuingize ndani
Wokovu si mwisho bali ni mwanzo wa
maisha mapya.
E.
Hatari ya mafanikio.
Musa aliwaonya kuhusu mafanikio
aliwaambia kwamba waangalie sana kwa sababu mafanikio yaweza:
1.
Kuwafanya wamsahau Mungu wao.
2.
Kuwapa majivuno kwamba ni kwa nguvu zao
wenyewe wamefanikiwa.
F.
Laana na Baraka.
Musa aliwaeleza na kuwafundisha umuhimu wa
kulitunza Agano la Mungu na Baraka
zilizoambatana na laana iliyoambatana kutokana na kulivunja Agano la Mungu.
1.
Tabia ambazo hazipendezwi na Mungu Kum
27:14-26.
2.
Baraka kwa utii Kum 28.1-14.
3.
Laana kwa kutotii a uasi Kum 28:15-48.
G.Agano la nchi ya
ahadi. Kum 29:10-14.
Ahadi
ya kutunza Agano ni kubaki katika nchi ya ahadi na alama ya agano itakuwa ni
kuwahi au kuchelewa kwa mvua Kum
11:13-14.
H.Maagizo kwa Yoshua.
Kum 31:6-8.
I.
Kubarikiwa kwa makabira kumi na mbili ya wana wa Israeli (Sura 32-33).
J.Kifo
cha Musa na Yoshua kuchukua uongozi. Kum 34:5-9.
K.
Baadhi ya mafundisho makuu ya kitabu.
1.
Mungu hutaka utii kamili.
2.
Kila itikio la mwanadamu ju ya agano la Mungu lina matokeo yake
3.
Mungu hututaka sisi kuwafundisha watu
wengine Neno lake kwa usahihi.
4.
Ni raishi kumsahau Mungu wakati wa
Mafanikio.
5.
Mungu anaheshimu uchaguzi wa mtu.
6.
Amri za Mungu ni kamilifu kabisa.
L.Watu
mashuhuri.
1. Musa
2. Yoshua.
3. Makuhani.
M.
Mitajo ya Kristo.
·
Musa.
·
Yoshua.
N. Matukio muhimu.
Matukio muhimu katika kitabu hiki ni kurudiwa kwa mafunzo ya sheria kwa kizazi
kipya cha wana wa Israeli na kifo cha Musa mtumishi wa Bwana.
Zoezi.
Katika
makundi ya watu watano watano jadili maswali yafuatayo.
1.
Taja majina ya watoto kumi na mbili wa Yakobo wapange kulinana na mama zao.
2.Chora
mti wa familia tangu Adam hadi makabila kumi na mbili ya Israeli.
3.
Chora mti wa ukoo/familia ukionesha
orodha ya vizazi tang Ibrahimu hadi taifa la Israeli.
4.
Changanua family ya Yakobo iliyoingia
Misri kwa kutaja uzao wa kila mtoto.
5.
Jadili mwanzo wa ustaarabu duniani na athali zake.
6.
Toa sababu za Farao kuanza kuwatesa wana wa Israeli.
7.
Jadili sababu za Mungu kuufanya moyo wa Farao kuwa mgumu.
8.
Jadili athali za kutii nusunusu mwito wa
Mungu.
9.Jadili
umuhimu wa kujifunza Pitio la Agano la kale.
10.
Jadili mapigo kumi Mungu aliyowapiga wamisri.
11.
Vitabu vitano vya Musa asili yake ni kitabu kimoja kilichoitwa Pentatuki.
Jadili kauli hii.
12.Jadili
mambo ambayo wana wa Israeli waliagizwa kuyafanya mara tu baada ya kuingia nchi
ya ahadi .
13.
Changanua vipimo na vitu mbalimbali vilivyohitajika katika ujenzi wa hema ya
kukutania (maskani)kule jangwani.
14.
Eleza sababu za msingi za kugawanya kitabu kimoja na kutokea kwa vitabu vitano
vya Musa badala yakuwa kitabu kimoja.
\
Uchunguzi wa agano la kale
JibuFutaNashukuru sana kwa mafundisho MUNGU awajaze hekima tele. Je mafundisho haya tutayapata je kwenye kitabu ao bronshua?
JibuFutaSOMO NI ZURI ILA NINAOMBA MWENDELEZO WA UCHAMBUZI WA BIBLIA NZIMA
JibuFutaUbarikiwe mwalimu kwa mafundisho mazuri ya pitio ya Agano la kale Mimi nimebarikiwa sana
JibuFuta