Jumamosi, 3 Mei 2014

HISTORIA YA KANISA .I



MADA YA TATU
KANISA LA SMIRNA. (KANISA LA MATESO)
A. UTANGULIZI.
Simrna ni mji ambo ulikuwa  umbali wa Km 65 Kaskazini mwa Efeso na ulijulikana kama bandari ya salamakwa wakati ule ukliokuwa katikati ya njia kuu kutoka rumi kwenda India na Persia(Irani)
Katika moja ya mitaa yake kulikuwa na hekalu la mungu wa kigiriki alywejulikana kwa jina la zeus Munugu mkuu na katika upande mwingine wa mji kulikuwa na hekalu la Cybele {mama wa mungu}.
Mji wa Smirna pia ulikuwa ni kituo cha ibada ya kumwabudu kaisari. Kulikuwa na hekalu ya mfalme wa Rumi Teberio Kaisari
B. historia ya kipindi cha smirna inaaminika kwamba siku kumi za mateso yaliyotakiwa kuja juu ya smirna huhusisha vipindi maalum kumi vya mateso chini ya watawala mbalimbali wa kirumi  pia na wao watawala wangekuwa kumi.
Majina ya wafia dini mbalimali katika kipindi hiki cha  Smirna chini ya wafalme mbalimbali wa Rumi yanaorodheshwa hapa.
1.Klaudi  Nero (64-68 AD). Petro alisulubiwa katika kipindi cha utawala wa Nero. Paulo alikatwa kichwa katika kipindi hiki.
2.Domitiani (90-95 AD) aAlijaribu kumuua mtume yohana akashindwa na baadae akaamua kumpeleka uhamishoni katika kisiwa cha Patmo.
3.Trajani(104-117 AD)Simoni ndugu wa Yesu aliuawa katika kipindi hiki mwaka wa 107.  Askofu wa Ignatious  wa Antiokia  aliuawa pia katika utawala wamfame huyu mwaka 110.Watu wngine waliouawa katika kipindi hiki ni Polikap mwanafunzi wa Mtume Yohana(155),
4.  Marcus Aurelius.(161-180 AD). Yustini  aliuawa katika utawala huu katika mwaka 165 AD. Pia alifanya mauaji ya wakristo wengine  wengi pia.
5.Septimus  Severio.(200-211 AD) alimuua Leonidus baba wa Origeni mwanatheolojia mkuu., Pia aliwaua na Perpetua na Felistas na ireneos mwaka 202.AD.
6. Thraker Maximus (235-237 AD).alifanya mauaji lakini hatuna majina ya watu aliowaua.
7.Desiusi .(250-253 AD.)  katika kipndi cha utawala wake matso yaliibuka tena juu ya kanisa na kwa bahati nzuri utawala wake ulidumu kwa muda mfupi sana nabaada ya kuanguka kwa utawala wake kipindi kifupi cha amani kilikuja juu ya kanisa.
8. Vareliani   (257-260 AD.) Alipanga mauaji lakini hayakufanyika katika utawala wake.
(270-275 .AD.)Askofu Spriani wa Kathegi na askofu Sextus wa Rumi waliuawa

C.Mateso ya kitaifa. Tabia za msingi katika historia ya kanisa katika karne zote mbili yaani karne ya  pili naya tatu ni kanisa au wakristo kuteswa na wafalme wa kirumi. Mateso haya hayakuwa endelevu lakini yalitegemea mtazamo  aliokuwa nao mfalme aliyekuwa akitawala katika kipindi hicho.Mateso ambayo yalikuwa yakijirudia katika kipindi hiki yalidumu kwa karibu miaka 200 mpaka mfalme kostantino alipookoka.na kutangaza tamko la amani.(Edict of costantine) katika mwaka wa 313 AD.
D. Sababu za kanisa kuteswa.
Imani juu ya Mungu mmoja. Warumi walikuwa na miungu mbalimbali ambayo walikuwa wakiiabudu pamoja na sanamu zao. Wakristo walitangaza kwamba kuna Mungu mmoja tu Mfalme wa rumi alijenga hekalu ambalo lilipaswa kutumiwa na watu wote kuabudu miungu yao na akawapa wakristo nafasi na ya kushiriki kumwabudu Mungu wao katika hekalu hilo.  Wakristo walikataa fursa hiyo na kusababisha wao kuonekana kwamba wako tofauti na wananchi wengine. Hivyo mateso yalianza dhidi yao.
2.kukataa kumwabudu kaisari. Kama ilivyokwisha elezwa katika sura iliyopita kwamba makaisari wa kirumin walijitangaza kwamba wao ni miungu na wakadai waabudiwe na wananchi au raia wao. Hivyo raia wote wa dola ya Rumi walilazimika kushiriki ibada ya kumwabudu kaisari. Mahekalu ya ibada za kaisari yalijengwa kila mahali na sanamu za makaisari zikawekwa na watu wakalazimishwa kumwabudu kaisari na kutoa dhabihu mbele ya  sanamu za kaisari.  Hii ilikuwa mojawapo ya ibada za kitaifa katika dola ya Rumi.
Wakristo walipinga vikali  iabada hizona hawakuwa tayari kushiriki ibada hizo wala kutoa dhabihu mbele ya sanamu za kaisari. Kutokana na asababu hiyo wakristo waihesabiwa kuwa wasdaliti wa kaisari na dola kwa umjla na hivyo walipaswa kuhukumiwa kifo. Wakristo walianza kuteswa na dola ya Rumi kwa sababu ya kukataa kumwabudu kaisari na kumwita Yesu Mfalme(Kurious).
3.Kutojihusisha kwenye ibada za sanamu. Ibada hizi za sanamu zilikuwa sehemu ya maisha ya kila siku katika dola ya rumi. Sanamu hizo zilisimamishwa katika kila nyumbba na ziliabudiwa katika kila sherehe. Dhabihu za vinywaji  zilitolewa kwa  sanamu hizo. Hivyo wakristo walikataa kujihusisha katika shughuliza kilasiku za kijamii zilizohusha ibada za sanamu(mfano sherehe mbalimbali). Wakristo walipokataa kujihusisha na hayo mambo walionekana wako kinyume na jamii nzima.Kwa sababu hiyo jamii iliwahesabu kama maadui.
4.kutambuliwa rasmi kwa dini ya kiyahudi: Dini ya kiyahudi ilitambuliwa rasmi na dola ya Rumi kama dini ya kitaifa. Mwanzoni kanisa wakati linaanza lilitambuliwa kama kikundi tu ndani ya dini ya kiyahudi chenye msimamo mkali na hivyo  kanisa lilipata upendeleo wea serikali kwa namna fulani. Lakini mara baada ya kuanguka wa Yerusalemu na na kubomolewa kwa hekalu katika mwaka wa 70 AD, kanisa au ukristo ulisimama peke yake na dini ya kiyahudi walikuwa tayari kushirikiana na serikali   kulitesa kanisa.
Kanisa kufanya mikutano ya faragha. Kuokana na mateso kanisalilianza kukutana katika maeneo ya siri na hasa wakati wa usiku. Hii ilipelekea kanisa kuhisiwa vibaya na selrikali kwamba lilikuwa linafanya njama ya kupindua serikali au kufanya maasi kwa sababu serikali ya rumi ilipiga marufuku mikutano yote isiyo harali pia mikutano ya usiku ilipigwa marufuku. Kwa kuogopa kwamba mikutano yote iliyokuwa haina kibali cha serikali na iliyofanyika vifichoni haikuwa na nia njema kwa dola ya Rumi. Kwa sababu hiyo wakristo walitazamwa na dola kama waasi. Watu wanopanga njama na maadui kuleta vurugu na maasi ndani ya dola na hivyo dola ilianzisha mateso juu ya kanisa.

Usawa katika kanisa. Kanisa liliwaona watu wote kuwa sawa. Hakukuwa na matabaka katika kanisa. Waliwaona watu wote kuwa sawa a hawakumwogopa mtu yeote na wala hawakuogopa cheo cha mtu. Kuokana na sabu hiyo kanisa lilionekana kuwa na dharau, lisilo na heshima na hivyo kanisalilifanyika adui wa dola.
Kuharibu biashara za sanamu.: Kulikuwa na biashara  iliyokuwa inafanywa ndani ya dola ya Rumi.biasharahiyo ilikuwa ni ya uuzaji wa sanamu. Watu wengi  walijipatia faida kutokana na biashara hiyo.Mitume walipohubiri  Injili watu waliokoka na kuachana na ibada za sanamu . Mitume walifundishwa kwamba sanamu si kitu na hazipaswi kuabudiwa anaepaswakuabudiwa ni Mungu muumba Mbingu na nchi  pekee. Watu wengi waliacha kununua sanamu hizo . Kitendo hicho kilisababisha biashara hiyo ya uuzaji sanamu kudolola.  Watengenezaji na wauzaji wa sanmu  hizo walipata hasara na wakaamua kuanzisha  kuja juu  na
Kuanzisha ghasia dhidi ya kanisa kwani walipoteza wateja wao.


E.Hatua za mateso. Kuna mwingiliano kati ya kipindi cha efeso na Smirna. Kipindi cha Efeso kiliisha na kifo cha mtume Yohana mwaka 100 AD. Wakati kipindi cha Smirna kilianza wakati wa mateso ya kitaifa.(dola) wakati mfalme nero alipouchoma mji wa Rumi mwaka 64AD
VIPINDI KUMI VYA MATESO YA KITAIFA.
MATESO YA KWANZA Chini ya Kaisari Nero.(54-68 AD.)
Klaudi Nero alikuwa na umri wa miaka 16 alipoingia katika utawala (ufalme) katika mwaka 54 AD. Alikuwa mjukuu mkubwa wa Agustus aiyetoa amri ya watu wote kuhesabiwa sensa (Lk 2). Nero alikuwa mfalme wa kwanza katka wafalme kumi kuanzisha mateso   dhidi ya kanisa.Alichoma mji wa rumi mwaka 64 AD.Theruthi mbili ya mji wa Rumi iliteketea. Mfalme nero aliwasingizia wakristo kwamba ndiyo waliohusika na uharibifu huo. Hivyo kaina lililazimika kuingia kwenye mateso makali. Katika kipindi hiki  mtume Petro alisulibiwa miguu juu kichwa chini mnamo mwaka 67 AD.Pia mtume Paulo alikamatwa na kufungwa Rumi  ambapo alihukumiwa kifo na kisha akauawa kwa  kukatwa kichwa mwaka 68 AD. Mjini Rumi.



Mfalme Nero alikuwa katkili kuliko makaisari wote wa dola ya rumi waliomtangulia na waliomfuata. Kwani hajatokea kaisari katikadola ya Rumi aliyefanya mauaji kama Nero. Mwaka 59 AD.  mfalme Nero alimuua mama yake . pia alimuua mke wake wa kwanza(Octavia)na kisha mkewe wa pili(Pompea) na baadae alimuua kaka yake na  rafiki yake  mwalimu Seneka.
Mpaka mwaka wa 64 AD. Rumi ilikuwa katika ghasia kuu. Mfalme nero alituhumiwa kwamba yeye ndiye aliyehusika na kuuchoma moto mji wa Rumi. Lakini yeye alikanusha na kuwashutumu wakristo kuwa ndiyo waliohusika  na tukio hilo.Kutokana na hilo kanisa liliingia katika kipindi cha mateso makali. Maelfu ya wakristo waliuawa baadhi yao walitupiwa kwenye hifadhi za wanyama ili waliwe na wanyama wakali na baadhi yao walichomwa moto na mfalme akaendesha gari lake juu yao katika bustani yake. Bustani ya mfalme ambako tukio hili lilifanyika  leo ni eneo la  la jiji la Vatikani  makao makuu ya papa na kania la  MT. Petro.Kaisari Nero alijiua mwenyewe mwaka68. AD.
KIPINDI CHA PILI CHA MATESO CHINI YA DOMITIAN. (90-96 AD).
Baada ya nero kujiua mwaka wa 68 ADkatisa lilipata amani mpaka alipoinuka mtawala mwingine ambaye ni Domitiani. Wakristo wengi waliuawa . Mtume Yohana alipelekwa uhamishoni kwenye kisiwa cha Patmo ambapo ndipo mahali alipopokeas ufunuo amao sasa ni kitabu cha Ufunuo wa Yohana.
KIPINDI CHA TATU CHA MATESO CHINI YA TRAJANI 104-107 AD.
Trajani husemekana kuwa mtu muimusana miongoni mwa watawala wa Rumi. Alikuwa mtawala mzuri kwa nchi yake lakini aaliwaua wakristo. Mmoja wa mahakimu wake aliyeitwa  Plin the younger. Gavana wa behtania alichunguza maisha ya wakristo na mafundisho yao na kugundua kwamba  mafundisho hayo hayakuwa na chochote chenye kuleta uasi kwa serikali ya Rumi. Alileta ripoti yake mbele ya mfalme Trajani lakini mfalme alijibu “ Kama watu hawa walioletwa mbele yako wamepatikana na hatia kwa sababu ya kuwa wakristo na wauawe lakini ikiwa wataikana imani yao ya kikristo na na ikathibitika kwamba wanaabudu miungu yetu na waachiwe huru. Katika kipindi hiki waliuawa wakristo mbalimbali kama ifuatavyo.
Simoni mdogo wa Bwana Yesu. Alisulubiwa katika mwaka wa 107 AD.akiwa na umri wa miaka 110. Alisulubiwa kwa amri ya mfalme wa Rumi {Trajani}.
Askofu Ignatious wa Antiokia ambaye aliandika nyaraka mbalimbali kwa makanisa mbalimbali ambazo baadhi yake zinapatikana katika kitabu kiitwacho “Mababa wa Kitume”{Apostolic fathers}.  Alikuwa tayari kuuawa kwaajili ya Bwana Yesu. Aliandika barua za kuwafariji wakristo akiwa njiani kuelekea Rumi ambapo  alitumwa katika hifadhi ya wanyama wakali  na akaliwa na wanyama wakali mnamo mwaka 110.AD
PORIKAP. {69-155 AD} Alikuwa mwanafunzi wa mwaanfunzi wa mtume Yohana na rafiki wa trajani na mwalimu wa Irenius. Inadhaniwa kuwa Polikap aliteuliwa na mtume yohana kuwa askofu wa makanisa saba ya Asia. Alipoamriwa kumkana bwana Yesu Kristo ili kuepukana na kuuawa yeye alijibu:
“Miaka 86 nimemtumikia Bwana wangu na hajatenda Jambo lolote baya kwangu, nawezaje kunena vibaya juu ya Bwana wangu aliyeniokoa? Alichomwa kwenye moto na akafa kifo cha kishujaa kwaajili ya Imani yake juu ya Yesu Kristo. Aliuawa chini ya utawala wa mfalme Antonius Pius mwaka 155 A.D.
KIPINDI CHA NNE CHA NNE CHA MATESO CHINI  MARCUS
 AURELIUS 161-180 A.D.
           Marcus alikuwa alijulikana kam mfalme borawa nchi yake na mwandishi mwenye maadili. Japokuwa alikuwa mtumzuri kwa taifa lake alikuwa mtesi wa kanisa. Alifikiri kurejesha  maisha ya zamani ya kirumi na dini za zamani. Kwa wakati huo ukristo ulikuwa na mashiko zaidi.Waamini wengi walikuwa tayari kufa kwa ajili ya imani yao na wala hawakuogopa kifo. Walikikabili kifo kwa shangwe na ushindi mkuu. katika kipindi  hiki waaminni wengi waliuawa na wengine walitupwa  katika hifadhi za wanyama wakali  na wakaliwa na wanyama .
YUSTINI (Justine)Marty 100-165 A.D alizaliwa na alielimishwa vizuri mpaka kuwa mwanafalsafa na aliendelea kufundisha hata baada ya kuwa mkristo. Alirejerea kwa manabii wa zamani wa Kiebrania. Aliandika maneno yafuatayo dhidi ya ukatili na mauaji yaliyokuwa yanaendelea  dhidi  ya wakristo. “wanatushitaki, wanatusulubisha kwenye misalaba na kutupa kwenye hifadhi za wanyama  wakali na kwenye moto. Lakini wanapofanya mabaya zaidi juu yetu ndivyo idadi ya wakristo inaongezeka na kuwa kubwa zaidi. Mnamo mwaka 165 A.D .alikamatwa na mfalme wa Rumi  Marcus Aureliusi na kuuawa.
KIPINDI CHA TANO CHA MATESO CHINI YA SEPTIMUS. 202-211. A.D.
Baada ya kifo cha Marcus Aurelius kanisa lilipata amani mpaka alipoinuka mtawala mwingine aliyejulikana kwa jina la Septimus Severus. Mtawala huyu alimuua Leonides baba wa Origeni mwanatheologia mkuu. Katika mji wa kathegi Perpetua na mtumwa wake Felistas walitumwa katika hifadhi ya wanyama poli wakali na wakauawa.
 Mfalme Karakala alitoa uraia uraia kwa kila mtu katika dola yake. Huu ulikuwaq ni uhuru mkubwa kwa wakristo. Watumwa pekee ndio ambao wangeweza kusulubiwa au kutupwa kwenye  hifadhi za wayama poli wakali.

KIPINDI CHA SITA CHA MATESO CHINI YA THRAKA MAXIMUS
 235-237. A.D.  Baada ya kipindi cha amani Thraka alikalia kiti cha enzi cha Rumi. Alikua mpiganaji na alikusudia kuonyesha huruma zake kwa dini za kipagani kwa kuwatesa wakristo. Utawala wake ulikuwa mfupi kwa sababu ya kutawala kwake kwa njia ya udikteta. Maadui zake walitengeneza kikundi ambacho kilifanikiwa kumuua.

KIPINDI CHA SABA CHA MATESO.CHINI YA  DECIUS 250-253 A.D.
Katika kipindicha utawala wake mateso makali yaliibuka tena na kwa bahati nzuri kipindi chake cha utawala kilikuwa kifupi na kanisa lilipata raha kwa kipinda raha na amani kwa miaka 40.
KIPINDI CHA NANE CHA MATESO CHINI YA VARELIANI. 257-260. A.D.
Askofu Sipriani wa Kathegi aliuawa pia askofu wa Rumi Sextus aliuawa.
KIPINDI CHA  TISA  CHA MATESO. CHINI YA AURELIUS. 270-275. A.D
Mfalme Aurelius alikuwa mwabudu jua japokuwa hakulitesa kanisa moja kwa moja mwanzoni lakini hakuwapa uhuru  wakristo. Hatimae aliamuru kwamba wakristo wateswa. Kwa bahati nzuri amri yake haikutekelezwa Kutokana na kifo chake cha ghafla.
KIPINDI CHA KUMI CHA MATESO CHINI YA DEOCLETIAN 303 3010. A.D
Mfalme Deocletiani na wasaidizi wake waliwafunga wakristo gerezani. Baadae sehemu ya jingo hili lilibadilishwa na kuwa Kathedro ya Mtakatifu Petro. Deocletiani aliagiza kuchomwa moto kwa kila nakala Biblia, makanisa kubomolewa na wakristo wenye msimamo mkali kunyang’anywa uraia. Akiwa na umri wamiaka 80 deocletiani aliondoka kwenye kiti cha utawala, lakini wafuasi wake Galarius na Kostantinusi waliendeleza mateso mpka mfalme Kostantino mototo wa Kostantinus alipotoa tamko la amani kwa kanisa mwaka 313 A. Tamko hili la amani lilisitisha mateso kwa kanisa kwa kipindi cha karne mbili
Siku kumi za kujaribiwa zilizotajwa katika Ufuno wa yohana 2:10 zilifikia mwisho. Baadae mfalme Deocletiani alipotambua kwamba yuko karib na kufa alitubu dhambi zake mbele ya askofu wa mji.. Mwka 337 A.D alibatizwa. Mtu aliyeamini kwamba angeweza kuufuta ukristo alijikuta yeye mwenyewe anakuwa  mkristo.
UONGOZI KATIKA KANISA  KATIKA KIPINDI HIKI.
Wakati mitume wakiwa hai uongozi ulionekana ni utumishi yaani kutumikia au kuwajibika. Wakati Luka alipoandika kitabu cha matendo naPaulo alipoandika nyaraka zake tuna kuta maneno askofu na wazee yakiwa na maana sawa yaani yakimaanisha ofisi moja. Lakini katika miaka ya 125’s tunakuta maaskofu wamekuwa watawala katika maeneo yao. Katika baraza la yerusalemu mwaka 48 A,D {Mdo 15}  mitume wote na wazee walihusika. Lakini katika baraza la mwaka 150 A.D waliohusika ni maaskofu pekee. Hii inadhihirisha kwamba kanisa liliondoka taratibu kwenye mafundisho halisi ya mitume. Huduma ya mitume ilizimwa na ikachukuliwa na maaskofu . Maaskofu walijifanya watawala wa kanisa. Hii ndio sababu inayosababisha baadhi ya wataalam kuamini kwamba kipindi cha mitume kiliishia na kifo cha mtume Yohan, jambo ambalo si kweli. Huduma za mitume, manabii, waalimu wachungaji na wainjilisti kama zinavyoelezwa katika waefeso 4:11 ziliendelea kuwapo katika kipindicha mitume na vi[pindi vingine vyote vya kanisa, japokuwa zimekuwa  zikikataliwa na katika vipindi fulani ilionekana kama zimetoweka lakini  kwa uhakika zimekuwapo  na bado zimekuwa  zikifanya kazi katika kanisa hata sasa.
SHULE ZA THEOLOGIA.
Shule ya Alexndria. Ilianzishwa mwaka 180. A.D  na Pantaenusi ambaye alikuwani mwanafalsafa wa kigiriki na baadae akwa mkristo. Kisha alikwenda India, irani na Saudi Arabia katika huduma. Alikufa mwaka 200.A.D .
Klementi wav Alexandria. Alikkuwa mwanafunzi wa Pantaenus  na alimsaidia katika uendeshaji wa shule. Alikuwa ni mkuu wa shule hadi alipoondolewa kwenye wadhifa huo katika kipindi cha mateso cha septimus Severusi mwaka 2002. A.D. Baadhi ya vitabu vyake mpka sasa vipo.
Origeni(185-254 A.D). Alikuwa ni mwanatheologia mkuu. Baba yake  Alikuwa ni motto wa Leonidas. Baba yake aliuawa kutokana na imani yake katika Kristo chini ya utawala wa mfalme Severus katika mwaka wa 2002 A.D. Wakati huo Origeni alikuwa na umri wa miaka 17. Origeni aliisdaidia familia yake kwa kufundisha falsafa ya kigiriki pamoja na fasihi. Aliianzisha kwa upya shule ya Biblia iliyokuwa imefungwa kutokana na kuondoka kwa Klementi. Baadae alikuwa ni mwandishi wa vitabu vya dogma na thiologia. Baadae alikwenda Kaisaria na alianzisha shule nyingine ya Biblia ambapo alikuwa ni kiongozi wa shule hiyo kwa karibu zaidi ya miaka 20.  Alifungwa jela chini ya mateso Deciani na alikufa kutokana na kutendewa kinyama akiwa gerezani.alikufa akiwa na umri wa miaka 69 mnamo mwaka 254. A.D.
Shule ya Asia ndogo. Shule hii haikuwa katikamji wowote ilikuwa ni shule ya masafa (mobile Bible School). Ilihusisha waalimu wa thiolojia na waandishi. Baadhi yao ni Ireneus(130-202A.D) aliyezaliwa Smirna. Alipata elimu yake ya awali ya Biblia chini ya Porkap. Kansa la Asia ndogo lilimpeleka Ufaransa kama mmisionari. Aliuawa wakati wa mateso ya Severusi mwaka wa 202 A.D.
Shule ya kathegi: Shule hii ilikuwa kaskazini mwa Afrika na ilifanya vizuri kuliko shule zingine kubadili imani ya Kithiologia katika Ulaya. Watu wakuu katika katika shule hii walikuwa ni Tetullani  na Sipriani. Tetullani (160-200 A.D) Alikuwa ni mteteaji shujaa wa imani ya kikristo dhidi ya dini ya kiyahudi na mafundisho potofu  alijiunga na umontano na alitumia kalamu na mahubiri kuthibitisha kile alichofikiri ni mambo ya kidunia na  mabishano katika kanisisa.
Sipriani Askofu wa Kathegi (195-258 A.D) Alikuwa ni motto wa afisa wangazi ya juu wadola ya Kirumi. Alikuwa mkristo wakati wa ujana wake. Mambo matatu yaliyomjutia mpaka kuwa mkristo ni Maandiko ya tetullani, mafundisho ya Cellius toka Rumi na Maandiko matakatifu (Biblia).
Mwaka mmoja baada ya kuwa mkristo alikuwa askofu na kiongozi mkuuwa makanisa ya Afrika Kaskazini mwaka 248 A. D.  Mnamo Mwaka 257 A.D. Mfalme Valentine alimfungia kufanya huduma mwaka   na mwaka 258 aliuawa.

Kanisa la karne ya pili lilipambana na mambo makuu mawili ambayo ni  Mateso na uzushi(Heresy) yaani mafundisho potofu. Mtume Pulo alitabiri ya kwamba:
“ Najua mimi yakuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali wataingia kwenu wasilihurumie kundi. Tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao”
Baadhi ya makundi ya uzushi………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
HALI YA KANISA KATIKA KIPINDI CHA  MWISHO WA KARNE YA PILI:
Kanisa lililotakasika. Mateso yaliwaondolea mbali wale ambao hawakuwa waaminifu katika imani yao. Wale ambao hawakuwa na imani kamilifu na waliojiunga na kanisa kwa masilahi yao binafsi.
Mafundisho yenye mfumo mmoja. Japokuwa kanisa lilihusisha watu wa tamaduni , rangi na jamii mbalimbali bado lilikuwa na umoja wa imani wa ajabu katika kanisa lote. Walifuata mafundisho ya mtume Paulo, Petro na wengine. Mdo 2:42.
Kanisa lenye muundo: kazi iliyofanya na Paulo ya kuweka viongozi wa Kanisa katika kila mji ilileta ufanisi. Viongozi hao walikutana katika mikutano   na kujadili  mambo mbalimbali muhimu kuhusu kanisa. Hii ilisababisha kutokea kwa ushirikiano imara wa kimataifa.(International Fellowship) ambao umekuwepo mpaka  sasa.
Kanisa lenye kusitawi{kukua}. Licha ya mateso yaliyolikumba kanisa, kanisa liliendelea kukyua kwa kasi. Kanisa lilikumbana na mateso makali chini ya watawala mbalimbali wa Kirumi, lakini kanisaliliendelea kukabiliana na mateso hayo na likawa tayari kuwapelekea watesi hao Injili ya uzima.
Hakika Malango ya kuzimu hayakulishinda kanisa
Kuandikwa kwa agano jipya. Hatuwezi kueleza kwa udhahiri au kikamilifu  kwamba ni lini hili lilifanyika. Baadhi ya vitabu  kama  vile nyaraka za Paulo zilikubaliwa kila mahali, wakati vingine kama vile Waebrania, Yakobo na Ufuno wa Yohana vilikubaliwa Mashariki peke yake na kukataliwa Magharibi.
Kanisa la mashariki lilikubali baadhi ya vitabu  ambavyo havipo katika Biblia. Baadhi ya vitabu  hivyo  ni  Warakawa Balnaba, Mafundisho ya mitume kumi na wawali  na Ufunuo wa mtume  Petro. Mabaraza yalikutana mara kwa mara ili kutambua ni vitabu gani vilivyokuwa vimevuviwa  na  na vipi havikuvuviwa. Inadhaniwa kwambaAgano jipya halikutambuliwa rasmi mpka baada ya mwaka 300. A.D

Maoni 1 :