Alhamisi, 26 Desemba 2013
HISTORIA YA KANISA
Mada Ya Kwanza.
UTANGULIZI.
Somo hili linaanza na kupaa kwa Yesu Mbinguni katika mlima wa mizeituni kama mwaka wa 30 .AD na linaishias na kurudi kwa Yesu mara ya pili ya pili kupitia kwenye mlima wa mizeituni katika kipindi cha mwisho {ufu 19-16-26, Zek 14:1-9}
Waandishi wahistoria ya kanisa hawakubaliani katika namna ya ugawaji wa vipindi vya historia ya kanisa .Baadhi hugawa vipindi kulingana na matukio muhimu kuhusu watu Fulani maalufu, mfano kutawazwa kwa papa wa kwanza mnamo mwaka 590 AD, au wakati wa matengenezo ya Martini Luther, alipoandika maandiko{Thesis} yake 95 na kuyabandika katika mlango wa kanisa huko Witenberg Ujerumani mwaka 1517 . Baadhi pia hupenda kugawa vipindi katika historia ya kanisa kulingana na matukio mbali,bali yalioleta athari katika kanisa Mfano kuongoka kwa Kiongozi mkuu wa Dora y aRoma Mfalme Kostantino mwaka 313 AD .Au patano la amani la Westphalia mwaka wa 1646 .
Katika somo hili tutagawahipindi vya hisotria ya kanisa kwa kufuata mhutasari wa makanisa saba yanayopatikana katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana Sura ya pilina ya tatu ambapo vipindi mbalimbali vya kanisa vimeorodheshwa kwa njia ya kinabii.
Dhana ya historia.
Historia kama somo inafafanuliwa kwamba ni somo linalohusu matukio mbalimali katika vipindi mbalimbali vya maendeleo ya mwanadam u.
Baadhi ya wataalamu wanafafanua kwamba historia rekodi za shughuliza binadamu katika vipindi viliyopita.
Kwahiyo historia huhusika na kuainisha matukio mbalimbali muhimu yaliotokea katika vipindi mbalimbali katika jamii ya mwanadamu.
Maana ya hisoria ya kanisa
Ni taaluma inayoelezea vipindi mbalimbali ambavyo kanisa limepitia tangu kuanzishwa kwake mpaka Yesu kristo atakapokuja kulichukua kwenda mbinguni .
Sababu za kujifunza historia ya kanisa
Kuna sababu nyingi ambazo zinatufanya tujifunze historia ya kanisa na kuifanya kuwa mojawapo ya somo linalotakiwa kufundishwa katika shule za biblia na vyuo vya thiolojia .Baadhi ya sababu hizo ni;
Historia ya kanisa inatusaidia kutambua jinsi kanisa lilivyoanza na jinsi lilivyokabiliana na changamoto mbalimbali.
Inatusaidia kujifunza misimamo ya kiimani ya mababa wa kwanza wa kanisa na kututia moyo sisi kuitetea imani kama wao walivyoitetea.
Iatusaidia kujua changamoto mbalimbali kanisa lilizopitia tangu kuanziswa kwake mpaka sasa.mfano changamoto ya mateso wakati wa watawala mbalimbali wa Dora ya Roma waliyowapata kanisa la kwanza.kama vile kusulubiwa kwa mtume Petro, kunyongwa kwa Mtume Paulo, Kuchunwa ngozi na kutumbukizwa kwenye mafuta yanayochemka motoni Mtume Bathromeyo.
Inatusaidia kujua jinsi wakristo waliotutangulia walivyoitetea imani kwa kuwa tayari kufa bila kuisariti imani mfano John Huss Martini Luther, Porykap, Klement Origen, Urlich Zwingri. N.k
MAKANISA SABA YA ASIA NDOGO
Mfalme Domitiani alipeleka mtume Yohana uhamishoni katika kisiwa cha Patmo kwa sababu ya imani. Aikwa katika kisiwa hiki mtume Yohana alipokea jumbe toka kwa Bwana Yesu Kristo kwa ajili ya makanisa basda yaliyokuwa katika asia ndogo.Jumbec hizo baadae ziliingizwa kwenye orodya ya kanuni ya maandiko nas sasa ni kitabu cha Ufunuo wa Yohana .Mtume yohana alipokea jumbe hizi akiwa na umri wa miaka 90.Jumbe hizi zilikuwa na matuimizi ya aina nne ambayo ni
1. Zilikuwa ni jumbe maaalum kwaaiili ya makanisa ya katika wakatiwa mwandishi.
2. Zilidhihirisha na kufunua hai ya kiroho ya kila kanisa lililoandikiwa jinsi ilivokuwa .
3. Zilikuwa ni jumbe kwa waamini wote wa zama zote za kanisa
4. zilikuwa ni muhtasari wa kinabii wa historia ya kanisa
MUHTASARI WA MPANGILIO WA MAKANISA SABA YA ASIA NDOGO.UFUNUO 1
JINA LA KANISA KIPINDI CHA KANISA MAELEZO MIAKA
EFESO KANISA LA MITUME Tangu kupaa mbinguni kwa yesu Kristo
Mpaka kufa kwa mtume yohana 30 AD-100 AD
SMINA KANISA LA MATESO. Tangu kuungua kwa Mji wa Roma
Mpaka kuongoka kwa mfalme
kostanitno 64 AD-313 AD
PERGAMO KANISA LA KIFAHALI Tangu kuongoka kwa mfalme Kostantino.
Mpaka kuanguka kwa dora ya Roma 313 AD-474 AD
THIATHIRA KANISA LA KIPAPA {MEDIAVAL} Tangu kuanguka kwa dora ya Roma
mpaka kunguka kwa kostantinopale 474 AD-1453
SARDI KANISA LA MATENGENEZO Tangu kuanguka kwa Kostantinopale
mpaka patano la Westphalia 1453-1648
FILADELFIA KANISA LA UMESHENARI Tangu patano la Westphalia mpaka vita ya kwanza ya dunia 1648-1914
LAODEKIA KANISA LA SIKU ZA MWISHO. Tangu vita ya kwanza ya dunia 1914-MILLENIA MPYA
MADA YA PILI.
KANISA LA EFESO.{ KINDI CHA MITUME}
Kanisa la waefeso Ufu 2:1-7.
MUDA; Tangu kupaa kwa Yesu Kristo kama mwaka 30.AD.Mpaka kifo cha mtume Yohana kama mwaka wa 100. AD.
KRISTO: Anafunuliwa kama mtu anaeshika nyota {yaaani watumishi wake} katika mikono yake.
ONYO. SIKILIZA YALE AMBAYO Roho ayaambia makanisa .onyo hili lilitolewa kwa kila kipindi cha kanisa.
SIFA. Kanisa hili lilikuwa na sifa zifuatazo, matendo mema, uvumilivu, kupinga uovu, , lilikuwa limewajairibu watu waliokuwa wanajiita mitume na kugundua kuwa hawakuwa mitume wa kweli.
AHADI ; Utakula kutoka mtti wa uzima .
CHANGAMOTO;Kumbuka mahali ulipoanguka ukatubu.
ONYO: Usipotubu nitakiondoa kinara chako cha taa.
Utangulizi.
Efeso ulikuwa mji muhimu katika pwani ya asia ndogo na ulipewa jina la heshima heshima la Nuru ya Asia.waefeso waliabudu miungu ya kiasia ambayo ni Artemi, amba pia aliitwa Diana. Hekalu la artemi lilihezsabiwa kuwa mojawapo ya maajabu ya dunoia ya wakati ule. Mahali pengine walipoabudia paliitwa Augusteum. Mahali ha[po walitumia kumwabudu mfalme . kiwango cha kiburdani za kidunia zilikuwa nyingi na inakadiriweqwa kuwa Ukumbi wa Efeso u8likuwa na uwezo wa kucukua watu 25000.
Kipndi hiki kinaitwa kipindi cha mitume kwa sababu mitume wote12 wam wanakondoo {YEsu} waliishi katika kipndi hiki. Na kipndi hiki kilishia na kifo cha Mtume cYohana ambae alikufa kifo cha kawaida akiwa mzee mwenye umri wa kama miaka 100.
Tabia zxa kanisa la Efeso ni muhimu sana katika kipindi hiki . Kunma walimu wa theologia wanao fundisha kwamba mitme na manabii waliishia katka kipindi hiki. Jambo ambalo si kweli kabisa kwani huduma hizi zimekuwepo katika vipindi vyote vya kanisa japokuwa katika vipindi Fulani zilififia.Lakini zimekuwepo katika zama zote za kanisa.
B.Ulimwengu wa wakati wa mitume .
1. Wayahudi, wayahudi walikuwa ni adui nambas moja wa kanisa .walilivamia kanisa wakati lingali changa kwa kushirikiana na mfalme wa kirumi walimsulibisha Yesu Kristo.
a. masafarisayo.
Hawa walianza katika kipindi cha Ezra na Nehemia . waliporudi toka uhamishoni Babeli. Wakati ukuhani mpya ulipoanzishwa .Waliamini ufufuo wa wafu, ahabu ya wenye dhambi , kutokufa kwa nafsi,uwepo wa malaika na huduma zao na kwamba kila kitu kina mtegemea Mungu. Mtazamo wao wa kisiasa ulikuwa ni wa kiyahudi. Na waliogopa kushirikiana na waqtu wasiokuwa mafarisayo. Mfabno wasamaria, na wamataifa na kwa namna zote walizishika sheria za Musa na walifanya tohara.
b.Msadukayo,
Hwa jnia Lao lilitoka kwa Sadoki kuhani mkuu wa wakati wa Daudi toka uzao wa Haruni Kuhani Mkuu. Hivyo walikuwa ni uzao wa kikuhani.wao hawakuamini ufufuowa wafu wala uwepo wa malaika.
2. Dora ya Kirumi,.
Mwaka 63 mfalme wa Runmi Julius Kaizari aliivamia nakuishinda Parestina na akaanzisha utawala wa kirumi katika nchi ya parestina . Huu ulikuwa ni ufalme wan ne uliokuwa umeishina na kuitwala Israeli kulingana na unabii wa danieli . Israeli ilikuwa chini ya utawala wa dora y Roma Yesu Kriso alipozaliwa na katika kipindi cha maisha yake hapa duniani.
A. Heathenism , hii ilikuwa ni dini ambayo mianzo yake ni mtwala Nimrodi katika mnara wa babeli na > Dini hii ilibaadae ilisambaa katika maeneo mbalimbali yaliyoizunguka babeli mpaka misri, Ugiriki na Rumi.Waliabudu miungu ya kigeni {Yer 2:25}. Ilikuwa ni miungu ya zamani sana ya Kibabeli.ilikuwa na majina mbalimbali katika nchi mbalimbali. Mfano artemi ,Diana, Osiris, jupita appos Zeus. N.K
B.ibada ya mfalme. .Hii ilikuwani moja wapo ya tamaduni za dora ya kirumi. Baadhi ya wafalme wakirumi walijitangaza kwamba wao ni miungu na wakadai kwamba wana nchi wao wanatakiwa kuwaabudu.hivyo Ibada ya kuwaadudu wafalme {makaisari} ilianzishwa. Kukataa kumwabudu kaisari kungepelekea mtu kuhukumiwa adhabu ya kifo.Ibada ya kumwabudi mfalme ilikuwa imerithiwa toka kipindi cha babeli.
C.wanafasalsafa wa kigiriki.
Kulizuka falsafa za kigiriki ambazo zilikuwa zinasisitiza kwamba lengo la maisha ni furaha na anasa. Walisisitiza kwamba maarifa yanaweza kupatikana kwa njia ya kufikiri{Logic}.Waiegeme katika vitu vinavyoonekana tu .Falsafa hizi ndizo ambazo zilikuwa zimeshikiriwa na na watu mbalimbali katika kipindi hiki. Falsafa hizi zilisisitiza kwamba maisha ni kura na kunywa kwa sababu baada ya kufa mwanadamu alikuwa anaoza na kwamba hakukuwa na maisha baada ya kufa.
C. KUANZA KWA KANISA.
Kanisa lilianza Yerusalemu siku aliposhuka Roho mtakatifu katika chumba cha juu katika hekalu la Yerusalem.Baada ya Yesu Kristo kupaa Mbinguni wanafunzi walirudi toka mlima wamizeituni mpaka hekaluni na kukaa katika chumba cha juu. Waliomba na kusubiri kuvikwa nguvu.baada ya vsiku kumi Roho Mtakatifuv alishuka na wote waliokuwemo kwenye chumba cha juu walijazwa na Roho Mtakatifu na kuanza kumwazimisha Mungu kwa Lugha zingine. Kazi ya uinjilisti ilianza papo hapo mtume Petro alihubiri na watu 3000 wakaokolewa na kubatizwa. Hii inahesabiwa kwamba ndio mwanzo wa kanisa la agano jipya.hivyo
Sifa za kanisa la kwanza.
1.Utii.lilikuwa na utii kwa sehemu
2. utendaji. Lilikuwa na hali ya utendaji
3. utendaji likwanautendaji
MATOKEO Y KUJAZWA ROHOMTKAIFU WANA LAKWAZA.
1. Kutiwa nuru. Waamini kwa kwanza walitiwa nuru. Katika akili na fahamu zao na wakapata kuyaelewa maandiko matakatifu,
Kutiwa nguvu na ujasiri, wamini hawa walitiwa nguvu na ujasiri na na kuwezeshw Kulihubiri Neno la Mungu kwa ujasiri.
3. Kutenda ishara na maajabu. Mitume waliwezeshwaq kutenda miujiza sawasawa na ahadi ya Yesu Kristo Mk 16:15-20.
WANACHAMA KTIK A KANISA.
Wanachama katika kanisa la mwanzo walikuwa ni wayahudi {proselytes} ambao twaeza kuwagawanya katika makundi manne. Mabayo ni ;
1 Waebrania . hawa walikuwa ni wayahudi ambao baba zao walikaa Parestina na walikuwa ni Uzao wac Kiebrani .
2. Hellenists, walikuwa ni wayahudi waliokuwa wanakaa katika nchi zingine wengi wao walikaa parestina.
3. Proselyles.walikuwa niwatu wamataifa waliokuwa wamefanyika kuwa raia wa kiyahudi, walifuata sheria za kiyahudi na walijiunga na dini ya kiyahuni. Pia walitahiriwa kama wayahudi. Mfano Nikolasi {Mdo 6:5}
UONGOZI NA UTAWALA WA KANISA .
Kanisa la kwanza halikuwa na Mfumo wa uongozi wa kiutawala . Kama ilivo sasa .Kila kanisa la mahali pamoja lilikuwa na uongozi wake uliojitegemea .Hakukuwa uonozi uliokuwa unasimamia makanisa yote. Mitume walikuwa ni waangalizi wa kanisa na hawakujiweka kuwa watawala wa kanisa . Bali watumishi wa kanisa.
MAFUNDISHO YA KANISA LA KWANZA .
Mafundisho ya kanisa la kwanza yalikuwa rahisi ,agano jipya lilikua halijaandikwa.ujumbe wao ulikuwa na maeneo machache ambayo ni ;
Uungu wa Yesu Kristo. Yesu kristo wa nazareti ni mwana wa Mungu na ni nafsi hai .Maelezo yaha yalisababisha mateso katika kanisa .
Ufufuo wa Yesu Kristo. Ufufuo wa Yesu kristo ulikuwa ni kiini cha mahubiri au ujumbe wa kanisa la kwanza.
Kurudi kwa Yesu Kristo mara ya pili. Walihubiri kwamba yesu Kristo atarudi tena {Mdo 3:20-21, 1The 4;15-17}Hili lilikuwa ni tumaini la Baraka kwa waamini wote.
KUSHINDWA KWA KANISA LA KWANZA ..
Kanisa la kwana lilishindwa kufikia kusudi kwa sababu zifuatazo.
Kukosa maono ya umisheni . mungu aliliagiza kanisa kwenda kuhubiri Inlili ulimwnguni kote Mt20:28, Mk 16:16} lakini kanisa la kwanza hawakufanya hivyo bali walijihusisha na umisheni katika yerusalemu tu. Kujihusisha na shughuli za kijamii
Mitume walianza na kujihusisha na mambo ya kijamii {kiutawala} kwani shughuli zoe za kanisa za kila siku zilifanywa na wao.Tunaona Petro aliyekuwa mhubiri anaanza kujihusiha na mabo ya kiutwala . Mitume walifika mahali wakagundua tatizo hilo na waakachagua wahudumu saba waliotakiwa kushughulikia mabo ya kiutawala ili wao wadumu katika kulihubiri Neno na Kuomba.
Bwana alilionya kanisa lake “Tubu na ukafanye mabo ya kwanza la sivyo nitakiopndoa kinara chako mahli pake.Mungu alitimiza Neno lake kama Tutakavyo ona hapo baadae.
KUENEA KWA KANISA LA KWANZA.
Kupanuka kwa kanisa tangu mahubiri ya Stephano {mwaka 35. AD} hadi mkutano wa Yerusalemu {mwka 48. AD}.Mambo ya msingi katika kipindi hiki yalikuwa ni upandaji wa makanisa . Kipindi hiki kifupi kilikuwa na umuhimu mkubwa kwa kanisa .Japokuwa kanisa mwanzo lilikuwa Yerusalemu Tu sasa lilipandwa katika,a maeneo mengine kama vile Siria na Asia ndogo na kuelekea Ulaya. Waamini wa kwanza walikuwa ni wa yahudi lakini baada ya kipindi hiki kifupi waamini wengi walikuwa ni wamataifa .
Mwanzoni Injili ilihubiriwa kwa kiebrani na kwa kiaramu lakini baadae iligundulika kwamba ulimwengu mzima ungefikiwa na injili kupitia lugha ya Kigiriki kwa sababu kigiriki wakati huo kilikuwa ni lugha ya mawasiliano ya kimataifa kama ilivi kiingereza kwa dunia nzima ya sasa.
KUTESWA KWA KANISA NA VIONGOZI WA KIYAHUDI..
Yesu aliwaagiza mitume kwenda kuhubiri Injili duniani kote lakini wao walipenda kukaa Yerusalemu .Mungu alikasirika na kaamua kuruhusu mateso katika kanisa .{Mdo 9}
1. Mahubiri ya Stefano{.Mdo 6:1-4, 7} Kwa sababu ya imani yake kwa Neno la Mungu Stefano alihukumiwa kuuawa na kuwa mfia dini wa kwanza katika imani ya kikristo.Kijana mmoja mfalisayo wa tarso Sauli alishuhudia mauaji ya Stefano na Baadae kijana huyo akawa kiongozi mkuu wa mauwaji ya wakristo katika taifa la wayahudi.kutokana na tukio hili waamini wote walikimbia yerusaelimu isipokuwea mitume {Mdo 8:1-4}.Waamini hao walisambaa maeneo mbalimbali na kila mahali walipokwena walilihubiri Neno . Kwa njia hii kwamuda mfupi Injili ilipata kuenea kwa haraka katika maeneo yote yaliyoizunguka Yerusalemu.
2. Kanisa Linakwenda Samaria,{ Mdo 8}.wasamaria walikuwa ni chotera ambao asili yao ilikuwa ni Babeli anbo walihamishiwa katika eneo la Kaskazini mwa Israeli.Pale waisraeli walipochukuliwa kwenda utumwani Ashuru {Siria}. Mchanganyiko wa wageni hao na mabaki ya waisraeli ambao hawakwenda utumwani ashuru yaliunda kabira la Ashuru kutokana na kuona . watoto waliozaliwa walikuwa chotara.Walikuwa na hekalu lao katika mlima Gelzimu na walivitumia vitabu vitano vya Musa pekee kama Biblia yao.Kwa hiyo waayahudi hawakuchangamana nao.
Roho Mtakatifu alimwambia Shemasi Filipo kwenda kuhubiri Neno Samaria Mungu alimtumia kufanya ishara na maajabu kwa jina la Yesu huko Samaria.Uamsho mkuu ulitokea huka Samaria .Watu wa huko Samaria waliokoka na kubatizwa .Mitume walipopata habari hii walikuja kuwaombea ujazo wa Roho Mtakatifu.Baadaya maobi hayo wasamaria walijazwa Roho mtakatifu.
Angalizo. Wasamaria waiokolewa na kubatizwa katika maji chini ya huduma ya Filipo.lakini walikuwa bado hawajabatizwa kwa Roho Mtakatifu . Ubatizo wa Roho matatifu ni upako mzaaalumu ambao kupitia huo tunapokea nguvu toka kwa Mungu
3. Injili inakwenda Afrika {Mdo 8 }. Roho mtakatifu alimtuma mwinjilisti Filipo kwendfa kumhubiri neon Towashi wa Kushi {Wazri wa fedha wa Ethiopia}.Filipo alimwonoza towashi huyu kwa Bwana na kishaAkambatiza . Ina aminika kwamba towashi huyu alipeleka injili Afrika . Kwa sabau alikuwa ni mkza wa Barala Afrika katika nchi ya Ethiopia .
MTESI WA KANISA ABADILI UPANGA {Mdo 9 }
Sauli wa tarso ambae ndiye aliekuwa mtesi mkuu wa kanisa kwa kipindi hiki aliokoka baada ya kukutana na Yesu Kristo alipokuwa safariki kuelekea Dameski kuwakamata na kuwaua waamini {Mdo 9:20 }Mara baada ya kuokoka alianza kuihubiri injili {Kumhubiri Kristo Yesu}. Paulo aliweka chini upanga wake wa mauaji na kuchukua upanga wa Neno la mungu Ambao hakuuacha mpka kifo chake.{ 2Tim 4:7}
Paulo alikwenda katika jangwa la Arabia kwa miaka Mitatu ambapo alipata mafuo zaidi toka kwa Mungu.Baada ya hapo alirudi Yerusalemu kuonana na mitume. Baada ya sauli kukutana na Ndugu alirudi tena Tarso. Kanisa lilipata raha baada ya kuokoka kwa Sauri wa Taso.{Gal 1:16-18, Mdo 9:20-31}.
5.Injili inakwenda kwa watu wa mataifa{Mdo 10 }.
Mtume Petro alitumwa kwenda kumhubiri Kornelio mtu wa Mataif a Injili . Mtume petro ndiye aliyefungu lmango wa Inili kwa wayahudi na kwa Watu wa mataifa .petro alihubiri injili kwenye nyumba wote waliokuwa wamekusanyika wakimsikiliza walishukiwa na Roho mtakatifu na na wakaanza kunena kwa Lugha Mpya kasha Petro akawabatiza .Huu ulikuwa ni mwanzo wa
Injili au kanisa kuwafikia watu wa mataifa.
6.Injili inakwenda Asia Ndogo {Mdo 13 }
Katika surahii tunaona wito wa wamishenari wawili kwenda kuhubiri katika nchi ya kigeni . Wito huu na kutumwa huku kulifanyika Antiokia.mahali ambapo wanafunzi walipewa jina na kuitwa wakristo kwa mara ya kwanza {Mdo 11:26}. Balnaba alikuwa ni mchungaji wakati Paulo alpokuja kutoka Dameski. Wanafunzi wote walimwogopa. Balnaba alimpokea na kumtambulishwa kwa kanisa {mitume Yerusalemu} Mdo 9;26-29.Japokuwa mitume walimtuma balnaba antiokia mahali ambapo kanisa lilikuwa na uamsho mkubwa aliamua kufunga safari kutembea zaidi ya KM 150 kwa meli ili kwenda kutafuta Sauli wa Tarso .Ailmpata na kasha akamchukua na kuja nae Antiokia bila kujua kwamba miaka ya Mbele sauti ya Bwana ingemwita kupia jia ya unabii ‘Nitengeeni Balnaba na Sauli kwa kazi niliowaitia.{Mdo 13:1-5 }. Balnaba na Paulo waliombwa na kanisa na kisha kwenda kwenye umisheni wao kuelekea asia ndogo.Mahali ambapo walianzisha makanisa mengi. Kama inavyoainishwa katika Matendo ya Mitume 13 na 14. Baadae walirudi antiokia mahali ambapo palikuwa ni kituo chao cha umisheni.
KUTENGANA KWA WAMISHENARI .
Wakati mitume hao {Paulo naBalnaba} walipokuwa wanajiandaa kwaajiliya safari yao ya pili yaumisheni walipishana. Kulitokea kutokuelewana katika jambo moja.Balnaba alitaka kumchua Marko{ ambae aliwaacha katika safari ya kwanza ya umishenari na kurudi Yerusalemu}waende nae katika safari ya pili ya umisheni lakini Paulo alikataa kuambatana nae.hivyo kukatokea mgongano kati yao na kisha wakaamua kutengana.
Hapa tuna ona moyo wa kichungaji wa Balnaba japokuwa Marko alishindwa katika safari ya kwanza ya umishenari aiamua kumpa nafasi nyingine . tuna mwona Paulo akiwa mtu wa kushikiria kanuni kuliko kupendeza mtu yeyote. Mtu ambae yuko tayari kuvunja mahusiano na Balnaba kuliko kukubaliana nae. Miaka ilipita na Mtume Paulo akakomaa kiimani.Mtume Paulo ambae aisema katika uchanga wake : mimi si duni kuliko hao mitume wakubwa {2Kor 11:5}. Baadae alisema ‘Mimi ni wa kwanza kwa wenye dhambi {1Tim 1:16}. Paulo alfika mahali pa kujitambua, kujisifu kulibadilishwa na kujishusha na upendo ulichukua nafasi mahali pa chuki na kanuni. Katika waraka wake wa pili kwa Wakorintho alisisitiza sana upendo na msamaha. Baadae tunamwona Mtume Paulo akiwa katika upweke gerezani akisubiri kunyongwa. Alimwagiza Timotheo jkulmeta Marko. Marko huyu huyu ndiye aliye mkataa wakati wanafanya huduma na Balnaba. Kutokana na hili tunajifunza ya kwamba tusi mkatae mtu kutokana na makosa aliyoyafanya kwa sababu twaweza kumuhitaji tena baadae.
7.Mkutano wa Yerusalemu. {48. AD}.
Tatizo lliitokana na kuokoka kwa wamataifa na kujiunga na kujiunga na kanisa. Wakristo wakiyahudi walikuwa na mitazamo tofauti tofauti juu ya hili .walikuwa na mitazamo ifuatayo:
1. Kundi lenye msimamo. mkali liliamini ya kwamba hakuna wokovu nje ya Israeli . Kwa hiyo ingawa wamataifa wamempokea Yesu Kristo kama masihi wao kwahiyo walipaswa kutahiriwa na kushika Torati ya Musa {Sheria za Kiyahudi}Ili waweze kuokolewa Bila kufanya hivyo wokovu wao ungekuwa ni batili.
Kundi la wenye mabadiliko.Hawa waliamini kwamba wokovu ni kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.Bila ya kushika sheria za kiyaudi. Wao waliamini kwamba sheria za kiyahudi haziwahusu watu wa mataifa. Paulo na balnaba walikuwa mojawapo wa watu wenye mtazamo huu.
Mkutano uliitishwa Yerusalemu ili kushughulikia jambo hili muhimu la mafundisho kutokana na watu wa mataifa kumpokea Yesu Kristo kama bwana na mwokozi wao. Baada ya majadiliano marefu Mitume na Wazee walifikia hitimisho ambalo lilithibitishwa na Roho mtakatifu kwamba Wamataifa hawakuwa chini ya Sheria za kiyahudi na kwamba walichotakiwa kufanya ni kujiepusha na Ibada ya sanamu, kula nyama iliyosongolewa na damu, kujiepusha na uasherati na uzinzi. Barua iliandikwa na mitume na ikapelekwa kwa kanisa la mataifa kwa mikono ya Paulo, Balnaba Yuda na Sila. Walipofika antikoa walilikusanya kanisa na kuwapa ujumbe wa kikao cha mitume na wazee kilichofanyika Yerusalemu kuhusu tatizo lao. Waamini hawa walifurahi sana kupata ujumbe wenye kuwatia moyo {Mdo 15:30-31}
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni