Jumamosi, 28 Desemba 2013
.
PHILADELPHIA SCHOOL OF MISSION
PHISOM-KLPT IWALA PARISH.
MWONGOZO WA CHUO CHA MAFUNZO YA HUDUMA.
Maelezo ya chuo.
Uhitaji wa watendakazi walioandaliwa vema katika kuyafikia mataifa kwa injili kulipelekea kuanzishwa kwa chuo hiki. Chuo hiki kimeanzishwa na Mchungaji Gwamaka Mwang’onda wa Kanisa la Pentekoste Tanzania Parishi ya Iwala .
Mahali chuo kilipo;
Chuo hiki kipo katika kijiji cha Iwala nje kidogo ya mji wa mbalizi. Kwa sasa chuo kinatumia majengo ya kanisa la Pentekoste Tanzania parishi ya Iwala.Chuo kina maono ya kutafuta eneo kubwa la kutosha litakalowezesha kujenga majengo mbalimbali ya Chuo ,kama vile madarasa, ofisi za waalimu, ofisi za utawala.mabweni, ukumbi wa chakula , ukumbi wa mikutano, ukumbi wa kanisa la Chuo na majengo mengine muhimu uhitaji utakapotokea.
Aina ya chuo.
Chuo hiki si cha kidhehebu.wala hakitoi mafunzo na masomo yake kwa misingi ya dhehebu Fulani.Chuo hiki kinatoa mafunzo yake kwa kuzingatia misingi ya ki-Biblia, na kinapokea wanafunzi toka madhehebu mbalimbali bila kujali itikadi za kimadhehebu. Kwa sasa chuo hiki ni cha kutwa na ni cha mchanganyiko . Kinapokea wanafunzi wa kike na wa kiume.
Wakufunzi.
Chuo hiki kina waalimu au Wakufunzi wenye elimu na uzoefu wa kutosha katika fani ya Huduma za Kanisa ,Biblia na Thiolojia.wakufunzi hawa wamepitia katika vyuo vya thiolojia na huduma zakanisa.Chuo kina wakufunzi wa kudumu na wa muda .
Uongozi wa chuo;
Chuo kina uongozi ambao ndio unaoendesha na kuongoza chuo.Uongozi wa chuo umegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni sehemu ya udhamini na sehemu ya utawala/utendaji. Kwa pamoja sehemu hizi mbili zinakamilisha uongozi wa chuo.
Orodha ya viongozi waliopo kwa sasa
JINA LA KIONGOZI WADHFA
Rev.Dr. Erick Mponzi MKUU WA CHUO
Rev.GWAMAKA MWANG’ONDA MSHAURI WA WANACHUO
PENDO SHABAN.[MRS] MHASIBU
Gharama za masomo.
Chuo kinatoa masmo kwa gharama ndogo sana isiyo ya kibiashara ili kuwezesha watu wote waweze kusom malipo haya yanawezesha kukabiliana na gharama za uendeshaji wa chuo.Hivyo basi kuna gharama ambazo mwanafunzi anatakiwa kuchangia katika masomo yake, gharama hizo ni ,
Ada ya usajiri……………………………5000.
Kitambulisho……………………………5000.
Taaluma………………………….50000
Tahadhari………………………….5000
Mitihani ………………………..5000
Ada ya masomo kila muhula………..50000
Jumla ya malipo yote ya muhula wa kwanza ni 750000/=
Muda wa mafunzo.
Mafunzo katika chuo hiki huchukua mwaka mmoja kwa masomo ya cheti na miaka miwili kwa masomo ya stashahada. Ili mwanafunzi aweze kutunukiwa cheti ni lazima atomize muda wake wote wa mafunzo kutegemeana na ngazi ya mafunzo anayosoma.
Maono ya chuo.
Kuwa chombo bora cha kuwatayarisha watenda kazi kwaajili ya mavuno ya nyakati za mwisho ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika kazi ya kutekeleza Agizo kuu.
Aina ya mafunzo
Mafunzo yanayotolewa ni mafunzo ya Biblia na huduma za kanisa .masomo yaha yamegawanyika katika idara mbalimbali ambazo kwa pamoja zinakamilisha mafuzo haya , idara hizo ni,
• Idara ya masomo ya huduma za kanisa
• Idara ya masomo ya Biblia.
• Idara ya masomo ya theolojia.
• Idara ya masomo ya historia ya kanisa.
• Idara ya masomo ya uongozi ,na
• Idara ya masomo ya sanaa
Ngazi ya masomo,
Masomo yanayotolewa ni ya ngazi ya Cheti na Stashahada.Mafunzo ya ngazi ya cheti yanatolewa kwa mwaka mmoja na ni ya mihula mitatu ya masomo.Masomo ya ngazi ya stashahada yanatolewa kwa miaka miwili na ni ya mihula sita ya masomo.Mwanafunzi akimaliza masomo ya cheti anaweza kwendelea na masomo ya stashahada.
Mfumo wa ufundishaji.
Masomo katika chuo hiki yanafundishwa kwa njia ya ana kwa ana na baadhi ya kozi zinafundishwa kwa njia ya DVDs. Masomo haya yameandaliwa na Waalimu wa kimataifa toka sehemu mbalimbalimbali ulimwenguni.
Mtaala wa masomo.
Mtaala wa masomo umeandaliwa na uongozi wa chuo kwa kushirikiana na Shule ya Huduma ya Kimataifa iliyoko Amerika. Mtaala huu umefanyiwa utafiti na majaribio katika mataifa mbalimbali ulimwenguni na kuthibitika kwamba unafaa kutumika katika kuwaandaa watendakazi kwa ajili ya mavuno ya nyakati za mwisho.
Sifa za mwombaji.
Chuo kinapokea wanafunzi toka madhehebu mbalimbali wenye wito wa huduma. Hivyo mtu yeyote mwenye uhitaji wa kuandaliwa kihuduma anakaribiswa katika Chuo hiki. Hata hivyo mwanafunzi atapokelewa kwa kuwa na sifa zifuatazo.
• Awe ameokoka.
• Awe mshirika wa kanisa la mahali pamoja .
• Awe amethibitishwa na uongozi wa kanisa analotokea.
• Awe na wito wa kumtumika mungu katika hali zozote.
MTAALA WA MASOMO.
MASOMO YA MUHULA WA KWANZA.
KODI YA KOZI JINA LA KOZI KREDITI
PBS 102 PITIO LA AGANO JIPYA 3
PBS 101 PITIO LA AGANO LA KALE 3
PTS 101 MISINGI YA IMANI. 3
PTS 102 KUTUNGA HOTUBA 3
PTS 103 KANUNI ZA KUFASIRI MAANDIKO. 3
PAS 101 STADI ZA MAWASILIANO. 3
PMS 101 SIFA NA IBADA. 3
PBS 103 UANAFUNZI 3
PMS 102 UTANGULIZI WA KINABII. 3
MASOMO YA MUHULA WA PILI.
KODI YA KOZI JINA LA KOZI KREDITI
PTS 201 THIOLOJIA YA BIBLIA .I 3
PTS 202 SAIKOLOJIA YA BIBLIA. 3
PMS 201 USHAURI WA KICHUNGAJI .I 3
PMS 201 UINJILISTI. 3
PMS 202 KUPANDA MAKANISA .I 3
PMS 203 MAFUNDISHO POTOFU. 3
PTS 203 UTANGULIZI KWA KINBII 3
PHS 201 HISTORIA YA KANISA .I 3
MASOMO YA MUHULA WA TATU.
KODI YA KOZI JINA LA KOZI 3
PHS 301 HISTORIA YA KANISA .II 3
PTS 301 MAADILI YA KIKRISTO. 3
PTS 302 THIOLOJIA LINGANISHI. 3
PTS 303 THIOLOJIA YA KICHUNGAJI. I 3
PMS 301 KUPANDA MAKANISA .II 3
PTS 302 KANISA. 3
PLS 301 FEDHA,MIPANGO NA UTAWALA WA KANISA. 3
PMS 302 UPONYAJI. 3
PMS 303 MAZOEZI KWA VITENDO.I 3
MASOMO YA MUHULA WA NNE
KODI YA KOZI JINA LA KOZI KREDITI
PTS 401 KIINI CHA INJILI 3
PLS 401 UONGOZI WA KIROHO. I 3
PTS 402 NDOA NA FAMILIA 3
PAS 401 MBINU ZA UFUNDISHAJI. 3
PAS 402 URAIA. 3
PHS 401 HISTORIYA YA KANISA .III 3
PTS 403 KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU. 3
PMS 401 UKOMBOZI. 3
PMS 402 MAZOEZI KWA VITENDO.II 3
MASOMO YA MUHULA WA TANO.
KODI YA KOZI JINA LA KOZI 3
PMS 501 HUDUMA ZA MASAIDIANO. 3
PTS 501 THIOLOJIYA KICHUNGAJI.II 3
PBS 401 WAEBRANIA 3
PBS 502 DANIELI NA UFUNUO 3
PBS 503 NYARAKA ZA KICHUNGAJI. 3
PMS 502 MAOMBI. 3
PTS 502 UTAFITI WA KIBIBLIA. 3
PLS 501 UONGOZI WA KIROHO .II 3
MASOMO YA MUHULA WA SITA.
KODI YA KOZI JINA LA KOZI KREDITI
PMS 601 THIOLOJIA YA MATENDO. 3
PTS 601 THIOLOJI YA BIBLIA .II 3
PAS 601 UJASIRIAMALI. 3
PAS 602 TEKNOLOJIA NA KANISA. 3
PTS 601 IBRAHIMU. 3
PTS 602 ISRAELI KATIKA UNABII. 3
PMS 602 VITA YA KIROHO. 3
PBS602 WAGARATIA. 3
PBS 601. NYARAKA ZA YOHANA. 3
SHERIA NA KANUNI ZA CHUO
Ili kuwa na jumuia iliyo sawa na isiyo na migogoro kutakuwepo na sheria na kanuni mbalimbali ambazo wanafunzi watatakiwa kuzifuata.Hivyo kila mwanafunzi anatakiwa kuzielewa kanuni hizi na kuzifuata. Kuvunja mojawapo ya kanuni hizi kwaweza kupelekea kusimamishwa masomo kwa muda ua kufukuzwa chuo.
• Mwanafunzi anatakiwa kuwa mtii kwa waalimu na watumishi wengine wa chuo.
• Mwanafunzi anatakiwa kuhudhuria vipindi vyote vya masomo ndani na nje ya darasa kwa wakati .
• Mwanafunzi anatakiwa kufanya kazi zote anazopewa na waalimu.
• Mwanafunzi anatakiwa kulipa ada na michango mingine kwa wakati ,kabla ya kuanza muhula wowote wa masomo.
• Mwanafunzi anatakiwa kufaulu masomo yote ili kuweza kuhitimu.somo alilofeli atalirudia kulisoma au kufanya mtihani.
• Mwanafunzi anatakiwa kuomba ruhusa ikiwa kuna sababu ya msingi inayosababisha asihudhurie darasani.
• Mwanafunzi anatakiwa kuzima simu awapo darasani.au katika ofisi za waalimu.
• Mwanafunzi anatakiwa kununua vitabu atakavyo ambiwa na mwalimu wa somo husika.
• Mwanafunzi antakiwa kuhudhuria ibada za chuo.
• Mwanafunzi anatakiwa kuwa na lugha nzuri azungumzapo na wanafunzi wengine.
• Mwanafunzi hataruhusiwa kufanya mtihani wa mwisho wa muhula ikiwa hakukamilisha mazoezi na majaribio yote.
Makosa madogoma yatashughulikiwa na mlezi wa wanachuo na kamati ya nidhamuzi , makosa makubwa yatashugulikiwa na mkuu wa chuo. Uamuzi wowote uakaotolewa na mkuu wa chuo ndio utako kuwa uamuzi wa mwisho.
……………………………………………
Rev.Dr.Erick Mponzi.[D.D]
MKUU WA CHUO.
A PHILADELPHIA SCHOOL OF MISSION
KLPT PARISHI YA IWALA.P.O.Box 4606 MBALIZI MBEYA.
FOMU YA MAOMBI YA KUJIUNGA NA CHUO.
JINA LA MWOMBAJI……………………………………………………………………………………………………………………
ANWANI YA MWOMBAJI………………………………………………………………………………………………………………
UMRI WA MWOMBAJI…………………………..JINSI……………………………HADHI YA NDOA ……………………
ELIMU YAMWOMBAJI………………………………………………………………………………………………………………….
Eleza kwa nini unataka kujiunga na chuo hiki cha mafunzo ya huduma.
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
Mapendekezo ya mdhamini.
Mimi………………………………………………………napendekeza ndgugu……………………………….....................
Apewe nafasi ya kujiunga na chuo hiki cha mafunzo ya huduma ninamfahamu kwa muda mrefu na kwamba ana tabia nzuri.
Sahihi ya mdhamini ……………………………………………. Tarehe …………………………………………………….
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni