Ijumaa, 18 Oktoba 2013
THIOLOJIA YA BIBLIA
BIBLIOLOGY THE STUDY OF DOCTRINE OF BIBLE
BIBLIA: neno Biblia linatokana na neno la kiyunani Biblosi ambalo lina maanisha Kitabu ambalo kwa kingereza rimetafsiriwa kama Bible. na kwa Kiswahili Biblia. Hivyo tunaweza kusema kuwa Biblia ni kitabu cha vitabu kwa sababu ndani ya Biblia kuna vitabu 66 Agano la kale 39 na Agano jipya 27.Pia Biblia ni maktaba ya Mungu kwa mwanadanmu.Mungu amefunua mawazo yake kwa mwanadamu kupitia Biblia.Hivyo tunaweza kusema kuwa Biblia ni kitabu cha mawazo ya Mungu.Ndani ya Biblia kuna mawazo ya Mungu na matendo ya Mungu.
I. ASILI YA BIBLIA
Asili ya Biblia ni Mungu mwenyewe. Mungu ndiye chimbuko la Biblia kwani ndiye aliyetoa ufunuo wa kuandika Biblia. Aliwatuma watu mbalimbali walioishi nyakati mbalimbali na historia na tamaduni tofauti tofauti kuandika Biblia. watu hao wengine hawakujuana kabisa lakini tunashangaa jinsi mawazo yao yanavyopatana katika maandiko matakatifu.
“Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko
Upaswao kufasiriwa kama apendendavyo mtu fulani tu. Maana unabii
Haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu bali wanadamu
Walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho mtakatifu.2Pet 2;19
Mstari huu unathibitisha kuwa asili ya Biblia ni Mungu mwenyewe na kwamba aliwatuma wanadamu kama vyombo katika kuandika Biblia takatifu.
Nigel Day Leulis anasema “Biblia ni kitabu kilichoandikwa na watu waliovuviwa na Mungu chenye kumbukumbu zisizo na mapungufu au makosa, kumbukumbu zenye ufunuo wote wa mungu kwa mwanadamu na kwa hiyo Biblia inayo mamlaka ya mwisho kwetu katika mambo yote yahusuyo maisha na mafundisho.
Biblia ina kila kitu tunachohitaji kujua juu ya wokovu na hakuna chochote kinachohitajika kuondolewa ndani yake au kuongezwa juu yake.
II. BIBLIA NA MAANDISHI
Mungu Roho mtakatifu aliwatumia waandishi kama 40 katika kuandika Biblia na waliandika kwa muda wa miaka kama 1600. Biblia iliandikwa na waandishi wengi kama ilivyoelezwa hapo juu baadhi yao walikuwa wafalme kama Daudi na Sulemani na wengine walikuwa waganga na wataalamu kama Isaya na Luka. Wengine walimu wa dini kama Ezra na Paulo wengine maafisa wakubwa wa Serikali kama Musa, Danieli na Nehemia, wengine wakulima na mafundi Amosi na Yohana , wengine wavuvi kama Petro , wengine watunga muziki kama Asafu na watoto wa Kora wengine manabii kama Ezekiel, Yoeli na kadharika. Wengine kati ya waandishi hawakujuana kabisa, waliishi katika nchi tofauti tofauti wengine palestina (baadhi ya manabii) wengine Babeli kama Danieli na Ezekieli na wengine wakisafiri katika Nchi za mbali Paulo na Mitume wengine na mmoja wapo aliandika akiwa kifungoni katika kisiwa cha Patmo.{Yohana}
Kwa kweli Biblia iliandikwa kwa njia ya pekee kuliko vitabu vingine vyote. Ingawa Biblia iliandikwa kwa muda wa miaka 1600 na maandishi mengi tunaiona mbele yetu kama kitu kimoja jambo hili laweza kuelezwa kwa njia moja tu. Ingawa Biblia inawaandishi wengi ni moja tu aliyeitunga nae ni Roho mtakatifu. Habari yake tunaanza kuipata katika ukurasa wa kwanza wa Biblia (Mwa: 1: 2) Nae anasema nasi mpaka ukurasa wake wa mwisho (Ufu 22:17)
III. LUGHA ZA BIBLIA
Agano la kale: Agano la kale liliandikwa hasa katika Kiebrania kuna sehemu ndogo zilizoandikwa katika lugha ya kiaramu jina la kiaram linaonekana katika Danieli 2:4 sehemu zilizoandikwa katika kiaramu ni hizi:
Ezra 4:8 – 6:18:7:12 – 26
Danaeli 2:4 – 7:28
Yeremia 10:11.
Agano Jipya: Maneno yote ya agano jipya yaliandikwa kwa kiyunani kwa kuwa ilikuwa lugha iliyojulikana kwa karibu na watu wote ingawa katika nchi hiyo ya Israel kiaramu kilikuwa ni lugha ya nyumbani zamani za Bwana Yesu kristo.
IV. UMOJA WA BIBLIA
Sehemu za Biblia zinaonesha tofauti lakini ni tofauti zenye maana kwa kuwa sehemu zote zinapata na kuwa na umoja. Nikama sehemu za nyumba jinsi zinavyopata mlango haufanani na paa ila vinapatana katika nyumba moja. Dirisha halilingani na mlango bali vinapatana vivyohivyo na sehemu zote za vitabu vyote vya Biblia ndivyo zinavyopatana katika maneno yafuatayo
• Tabia ya mungu
• Hali ya mwanadamu
• Ukombozi
• Kuja kwa masihi mara ya pili
UJUMBE WA BIBLIA
Ujumbe wa Biblia nzima ni Ukombozi tangu mwanzo hadi Ufunuo yote inahusu ukombozi. Agano la kale linaonyesha watu kuwa wanaugonjwa usio kuwa na tiba wala nafuu isipokuwa Mungu alikuwa akiwaambia kuwa kuokoka kutaonekana kwa njia ya ukombozi tu. Aliwafundisha hivyo kupitia mifano na unabii dhima kuu katika unabii ni Isaya 53. Katika hii kuna mistari 12 tu.Katika Agano jipya tunaona kuwa Masihi alikuja kuwa mkombozi tunasoma maneno yake matendo yake hata kufa kwake alipojitoa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi ili achukue adhabu za wanadamu. Hivyo Biblia nzima ina ujumbe mkuyu mmoja tu nao ni ukombozi.na kiini chake ni kimoja tu nacho ni Yes
u Kristo Mwokozi wa ulimwengu
MUUNDO WA BIBLIA
Biblia ni maktaba yenye vitabu 66 ambavyo mpangilio wake haufuati vipindi vitabu vilipoandikwa (kama ambavyo tungetarajia) lakini mara nyingine vimepangiliwa kwa kufuata mitindi ya kiuandishi. Vitabu vyenye muundo mmoja wa kiandishi vimewekwa katika fungu moja mfano vitabu vya torati, Historia, Ushahiri na unabii.
CHATI YA MPANGILIO WA BIBLIA
MPANGILIO WA VITABU VYA AGANO LA KALE
Mtindo wa kiuandishi Majina ya vitabu Jumla
Sheria Mwanzo – kumbukumbu la torati 5
Historia Yoshua – Esta 12
Mashairi Ayubu – Wimbo uliobora 5
Kinabii / manabii Isaya - malaki 17
Jumla ya vitabu vy agano la kale 39
Mtindo kiuandishi Majina ya vitabu Jumla
Injili Mathayo – Luka 4
Historia Matendo ya Mitume 1
Barua Warumi – Yuda 21
Unabii Ufunuo wa Yohana 1
Jumla ya vitabu agano jipya 27
UANDISHI WA BIBLIA LA KALE
Wanadamu walianza kuandika kama mwaka 3200k.k. Kuandikwa kwa kwanza kulifanywa katika mabamba ya towe nyororo katika mawe na katika ngozi waliziunganisha ngozi na kuandika ngozi hizo ziliitwa “Parchment” kisha ngozi hizo baada ya kuziandika walizivingisha na kuitwa magombo “Scrolls’.
Katika Biblia neno kuandika lilitajwa kwanza katika Kutoka 17:14 Mungu alipomwambia Musa kuandika mambo ya ushindi wa Israeli juu ya waamaleki kama mwaka 1440k.k
BIBLIA NA MIAKA
Zamani za kale watu hawakuandika tarehe na miaka kama tufanyavyo sasa hivi walikuwa wakitaja nyakati za wafalme wa zama zao wenyewe tu. Mfano katika Isaya 6:1 katika mwaka aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi kilicho juu sana na kuinuliwa na pindo la vazi lake vikalijaza hekalu.” Luka 3:1 – 2 “Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake kaisari Teberio Pontio Pilato alipoalipokuwa liwali wa Uyahudi na Herode Mfalme wa Galilaya na Filipo ndugu yake Mfalme wa Itulea na nchi ya Trakoniti Lisania Mfalme wa Abilene wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa.Neno la Mungu lilimjia Yohana mwana wa Zakaria jangwani.”
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika nchi zote na nyakati zote za zamani hawakutaja miaka kama tunavyotaja sasa. Lakini iliandikwa hivi katika mwaka Fulani wa kutwala kwake Mfalme Sulemani. Hivyo wataalamu wa Biblia hufanya kazi ya kuchunguza na kuunganisha miaka na nyakati ya wafalme wanchi mbalimbali. Hii ni kutokana kwamba kila nchi ina hesabu yake yenyewe ya miaka. Hivyo wataalamu wa Biblia na Theologia hawakubaliani katika mambo yote kuhusu miaka, hivyo katika kutaja miaka tunatumia neno “Kama” kwa sababu hakuna anaejua mwaka kamili ila tunafanya makisio baada ya kufanya utafiti kwa kina.
Kalenda tunayotumia sasa iligunduliwa na mtaalamu mmoja mtawa anaeitwa Dionysius Exiguus. Warumi walihesabu miaka tangu kujengwa kwa Rumi. Miaka kabla ya kuzaliwa kwa Kikristo huhesabiwa kwa kurudi nyuma toka kwa Yesu Kristo kurudi nyuma na inaitwa K.K / BC na baada ya kuzaliwa kwa Yesu huhesabiwa toka kwa Yesu kwenda mbele na inajulikana kama BK/AD.
TAFSIRI ZA BIBLIA ZA ZAMANI SANA
Kutokana na kufifia kwa lugha ya kiebrania mpaka kufikia mwaka 200 K.K na lugha hii kusahaulika na wengi na kutotumiwa na wengi ndipo ilibidi Agano la kale litafsiriwe katika lugha za mataifa mengi kama vile Kiaramu, Kisuria, Kigiriki, Kiarabu, Kimisri n.k.
SEPTUAGINTI YA KIGIRIKI
Mwaka 300 – 200 K.K. Agano la kale lilitafsiriwa kama lugha ya Kigiriki iliitwa Septuaginti. kwa sababu inasemekana ilitafsiriwa na watu 70. Septuagintu haiwezi kufaa kutumika kama asili ya kutafsiri Biblia tena katika lugha zingine kwa sababu tafsiri yake inajichanganya kunasehemu imetafsiriwa neno kwa neno na kupoteza mantiki{ maana} halisi na sehemu zingine hazifahaamiki vema. Ila inasaidia wataalamu wa Biblia na Theolojia kujua maana ya maneno ya kiebrania cha zamani zile. Septuaginti ilikuwa Biblia ya wakristo wa kwanza na ilisomwa siku za Bwana Yesu ilisaidia sana watu wengi kulielewa Neno la Mungu wale ambao hawakuweza kusoma kiebrania.
TARGUMU ZA KIARAMU
Ni Agano la kale ambalo lilitafsiriwa kwa kiaramu baada ya lugha ya kiebrania kupoteza mashiko na kufifia watu walianza kutafsiri maneno yake katika masinagogi ya wayahudi walisoma kwa kiebrania na mtumwingine alitafsiri kwa kiaramu. Baadae tafsiri hizo ndipo zilipoandikwa na kusomwa na zilipewa jina la Targumu lenye maana ya tafsiri kama Kiaramu.
KISHAMU (KISURIA)
ni tafsiri za Biblia ambazo zilitafsiriwa kwa lugha ya kishamu. Wakristo walipoongezeka katika nchi ya Shamu walihitaji kuwa na Biblia katika lugha yao ya kishamu na hivyo Biblia ilitafsiriwa kwa Kishamu.
VULGALE ZA KITATIRI
Ni Biblia iliyokuwa imetafsiriwa kwa kilatini. Mwaka 329 alizaliwa mtu mmoja aliyeitwa Jerome alikuwa ni mtaalamu alitafsiri Biblia nzima kwa lugha ya kirumi ambay o ni kilatini tafsiri hiyo iliitwa Vulgate. Vulgate ni tafsiri nzuri na imefwatwa na watu wengi katika kutafsiri maandiko.
KASORO NDOGO NDOGO ZA KIUANDISHI
Kabla ya kuangalia kasoro ndogo ndogo za kiuandishi zilizopo katika Biblia tuna budi kutambua namna ya uandishi uliotumika katika kuandika Biblia zamani za kale na hata vitabu vinginevyo vya kawaida.
Ni vyema kutambua kwamba mashine za kuchapia vitabu hazikuwepo wakati wa kale mpaka mwaka wa 1450 BK ndipo zilipogunduliwa kwa hiyo kwa muda wa miaka 2730 watu walikuwa wakiandika kwa mkono katika mawe, ngozi, miti n.k. Hivyo kitabu kikichakaa ilipaswa kinakiliwe tena kwa herufi zote. Hivyo makosa machache yaliweza kujitokeza kutokana na zoezi la kunakiri toka kizazi hadi kizazi. Mfano no (i) 2 FAL 8:26 na 2 NYA 22:2 suruhisho 2FAL 8:17 Maandiko katika Biblia yalipangwa kwa sura kama mwaka wa 1250 BK na kardinali. Hugo na mistari iligawanywa kama 1550 BK na Sir Robert Stevens makosa hayo ni madogo na hayaleti kupingana kwa mantiki ya Maandiko Matakatifu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Theologia ya biblia ni nini?na bibilia ya zamani ilikuwa na milango mingapi ya kitabu cha ZABURI?pia naomba tofauti ya bibilia ya zamani na ya sasa
JibuFutaishmail
FutaJe ?nini ishara ya siku za mwisho?Je zimetimia ?au zinakaribia?
JibuFutaAsante somo imeeleweka vzr
JibuFutaNilikuwa na maswali mengi kuhusu chimbuko la Biblia na kutaka kujua kuwa ilitoka wapi lakini kwa mchango wenu huu nimefanikiwa kutatua na kufafanua swala hili kwa undani zaidi.MUNGU aendelee kuwapa mafunuo zaidi
JibuFutaHujaeleza Kwanini wengine Wana vitabu 66 na wengine 73??
JibuFuta