Ijumaa, 14 Machi 2014

SAYANSI NA SANAA YA MAHUBIRI

KUANDAA MAHUBIRI.(SANAA NA SAYANSI YA MAHUBIRI. MADA YA KWANZA. MAHUBIRI. Malengo ya mada. Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi aweze.  Kueleza maana yamahubiri.  Kueleza maana ya kuhubiri.  Kueleza wito wa kuhubiri ulivyo.  Kueleza umuhimu wa kujifunza homiletics. A. UTANGULIZI Katika kozi hii tutashughulikia mojawapo ya kazi kuu ya kanisa. Mojawapo ya wajibu mkuu ambao umewekwa mikononi mwa kanisa ni kuhubiri ujumbe wa Mungu yaani Injili. 1Kor 1:21 a) Ni amri iliyo wazi toka kwa Bwana Yesu kwa wafuasi wake. Mk 16:15. “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe”. b) Kuhubiri ni mojawapo ya kazi ya thamani sana ambayo Mungu ametupa. Kuwa msemaji wa Mungu, yaani Mjumbe wa Kristo. 2Kor 5:20. c) Kuhubiri ni wajibu mkuu. Rumi 10:14-15. d) K wa njia ya mahubiri Mungu alichagua kujidhihirisha mwenyewe kwa mwanadamu. B. MAANA YA MAHUBIRI. Neno mahubiri linatokana na maneno mawili ya kigiriki ambayo ni homileo na homilia yenye maana ya ‘kuwa pamoja na, kuongea na kuwasiliana. a) Homily pia humaanisha ujumbe au hotuba. b) Elimu inayohusu namna ya kuhubiri huitwa Homileticts. c) Homiletics ni ustadi wa kuhutubia au kuhubiri. d) Mtaalamu wa elimu ya kuhubiri huitwa Homilist e) Homiletics huhusisha kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri au kutunga hotuba. f) Mahubiri huhusu kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri masomo ya Biblia. g) Mahubiri ni ujuzi wa kuhubiri. h) Ni elimu au taaluma inayohusu kuhubiri Neno la Mungu. i) Ni elimu inayohusu namna ya kuhubiri.{ somo juu ya kila kitu kinachohusiana na kuhubiri}. j) Kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu. Mungu hutumia watu wake aliowachagua kuhubiri ujumbe wake. k) Ujumbe unapaswa kuwa ujumbe wa Mungu Kitu kingine chochote si mahubiri ila ni maoni na falsafa za kibinadamu tu. l) Kuhubiri ni lazima kuwe ni kutangaza binafsi na si kusoma au kuandika Dr. Martyn Lolyoyd Jones alisema “ Wahubiri huzaliwa na hawafanywi kamwe. Kamwe hutamfundisha mtu kuwa mhubiri kama yeye si muhubiri. Lakini mhubiri wa kuzaliwa unaweza kumsaidia na kumwendeleza akawa mhubiri bora kwa njia ya mafunzo” 1. -Mhubiri si chanzo cha ujumbe.Mungu ndiye chanzo cha ujumbe na mhubiri ni bomba au mfereji ambako Mungu hupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu aliowakusudia. Ujumbe wa Mugu hutiririka kupitia utu wa mhubiri. 2. -Ujumbe unapaswa kutiririka kwa uhuru toka kwenye chanzo chake (Mungu) kwenda kwa wakusudiwa yaani hadhira au wasikilizaji. 3. Mahubiri ni zao la mambo mawili ambayo ni Mungu na mhubiri. Mahubiri mazuri huzaliwa kutokana na ushirikiano mzuri (umoja) na ushirika mzuri kati ya Mungu na mhubiri. Hivyo kuna vipengele viwili vya wazi katika mahubiri cha kwanza ni kile cha ki Mungu na cha pili ni kile cha kibinadamu. Kwa sababu ya wito wake mkuu mhubiri anapaswa kuwa mwaminifu na awe na ufahamu wa kutosha juu ya Neno la Mungu. 4. Biblia ndiyo asili ya ujumbe. • Ujumbe wowote unaohubiri nilazima utokane na Biblia nje ya Biblia si mahubiri bali ni masimulizi tu. • Kwa nini Biblia peke yake? Kwanini si kitu kingine toka vitabu vizuri vya kikristoau toka magazeti au maelezo na masimulizi ya mtu maarufu na aliye mkuu. • Biblia ni maoni ya Mungu kwa kila jambo lolote lililotolewa. Mhubiri aliye kuwa amekosolewa kwaajili ya hotuba yake alisema “hata mimi sikuipenda pia lakini haikuwa maneno yangu na nilikuwa sitoi mawazo yangu bali kile Mungu amesema katika Neno lake. Kwahiyo nilitoa mawazo ya Mungu na si yangu. • Kuhubiri hotuba ya ki-Biblia humpa mhubiri ujasiri mkubwa. Kutangaza kwa nguvu; Biblia inasema …………………. Mungu anasema………………… • Neno la Mungu lina nguvu. Wab 4:12. • Neno la Mungu ni kama mbegu.sBiblia hukutana na kila hitajila mwanadamuna matatizo yake yote yanayomkabili. • Inampendeza Mungu- Neno lake lililovuviwa amri yake ilikuwa wazi • “Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi na muwafundishe kuyashika yote niliyowaamuru” • Roho mtakatifu hulithibitisha Neno la Mungu. C. MAANA YA KUHUBIRI. Mahubiri yana lengo mahususi katika mpango wa Mungu. Ni njia ambayo kwayo Mungu ameamua kuwafikia waliopotea dhambini na kuwaimarisha waamini.Kkwa sababu mahubiri ni njia ya Mungu kuwafikia wanadamu, tutatazama maana ya kuhubiri kwa mitazamo mbalimbali kama ilivyo ainishwa na wataalamu wa masomo ya homiletics. 1.Kuhubiri ni kuielezea imani. Mojawapo ya malengo ya mahubiri ni kuelezea au kutangaza kweli za maandiko matakatifu. Kila hotuba au ujumbe wapaswa kuwasilisha kweli za maandiko kwa njia itakayowezesha hadhira kupata uelewa zaidi juu ya maandiko matakatifu. Kuhubiri husababisha imani kuumbika kwa wasikilizaji wako. Hubiri kwa kukuza imani na kuielezea imani katika mwana wa Mungu Yesu Kristo. II. Kuhubiri ni kuitetea imani. Haitoshi kuelezea ukweli wa Mungu bali tunapaswa kuutetea. Shetani, ulimwengu na maadui wa imani huvamia na kupotosha kweli za neno la Mungu. Hivyo ni lazima kwa mhubiri yoyote kuwa tayari kuitete imani ya kweli kwa njia ya kuhubiri kweli za ki-Biblia. Kuna wahubiri wengi wa uongo ambao kazi yao ni kuposha kweli za maandiko matakatifi. Ni jukumu la kila mhubiri wa kweli kuhakikisha anasimama imara katika kuitetea imani ya kweli. III.Kuhubiri ni kuinjilisha. Wajibu mkubwa wa Mhubiri ni kuitangaza injili kwa watu waliopotea dhambini. Ni lazima watu wote waliopotea wapelekewe injili ili wapte kutambua hali yao ya kupotea na kuongozwa kwenye wokovu wa Yesu Kristo.Kila mhubiri ahakikishe anatimiza Agizo kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Ahakikishe anawafikia watu wote wasiofikiwa na injili na kuwaleta kwa Bwana Yesu. IV. Kuhubiri ni kukemea dhambi. Kama ukichunguza hotuba za agano jipya utagundua kwamba hakuna mhubiri hata mmoja aliyesita kukemea dhambi.mfano Yesu, Yohana, Paulo, Petro n.k wote walikemea dhambi kwa nguvu zo katika kila mahubiri. Mhubiri nilazima akemee dhambi kila mara kwani Mhubiri ni kinywa cha Mungu. Kemea dhambi bila kuogopa chochote .Mhubiri ni lazima afunue ubaya wa dhambi na kuwahamasisha waamini kuishi maisha matakatifu yenye kumpendeza Bwana Yesu na kujiepusha na uovu. V. Kuhubiri ni kuhamasisha waamini Mahubiri hutakiwa kuwasaidia wakristo kukua katika neema ya Mungu. Pamoja na kuonya na kukemea dhambi mahubiri hutakiwa kuwahamasisha na kuwawezesha waaamini kukua kiroho na kufikia kimo cha Kristo. Hili ni moja wapo wa lengo kuu la mhubiri. Hatuhubiri ili kupisha muda au kwa sababu ya mazoea bali kwa sababu Mungu anakitu anataka tukipeleke kwa watu wake. Lengo la mahubiri ni kuwabadilisha waamini kuwakuza na kuwawezesha kufikia kimo cha Kristo Yesu., Tunapohubiri tunaumba sura ya Kristo ndani ya wale tunaowahubiri. Hakikisha wale unaowahubiri wanakua kiroho na kufanana na kristo VI. Kuhubiri ni kufikia mahitaji ya hadhira. Mahubiri yatakuwa yameafanikiwa kama yatakuwa yamepokelewa na kukutana na mahitaji ya wasikilizaji. Mhubiri kwa uangalifu anatakiwa kujiweka katika daraja sawa na wasikilizaji. Anatakiwa kujitahidi kuhakikisha anapokelewa na makutano na kukutana na mahitaji yao. Mhubiri anapaswa kuhubiri kwa mguso. Hakikisha unagusa mahitaji ya watu unapohubiri. Mahubiri ni uhai hivyo ni lazima yalete majawabu kwa wale tunaowahubiri. Gusa mahitaji halisi ya watu ambayo Mungu anakusukuma kuyashughulikia. Hubiri kwa ufanisi na kwa mguso. VII.Kuhubiri ni kudhihirisha uweza wa Mungu. • Bwana Yesu aliahidi kuwa na wahubiri kwa kulithibitisha neno kwa ishara na maajabu. Popote injili inapohubiriwa ni sharti Bwana awepo akiithibitisha kwa isharaMk 16:15,20. 1Kor 2:4. Hakikisha nguvu ya Mungu iko juu yako unapohubiri. Unapaswa kupakwa mafuta kikamilifu a Roho mtakatifu unapokwenda kwenye huduma ya kuhubiri kwa sababu kuhubiri ni vita. Omba Mungu Roho mtakatifu afanye uthibitisho kwa kila utakachohubiri. Ishara na maajabu ziambatane nawe kokote unakohubiri. -Ikiwa kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu mhubiri anapaswa kwenda mahali Mungu alipoongea mara nyingi na waziwazi yaani “Biblia” • Kwa njia nyingine kuhubiri ni kuipa Biblia sauti.ni kuacha Mungu aongee mwenye toka kwa Neno l D. WITO WA KUHUBIRI Sehemu ya muhimu sana katika kuhubiri ni wito. Kimsingi wito ni wa mtu binafsi Mungu huwaita watu katika huduma na watu hupokea hilo rohoni mwao kisha huja uthibitisho wa nje kupitia kanisa au watumishi mbalimbali na fursa mbalimbali. Mungu Huwaita watu wake katika nafasi na huduma mbalimbali. Wengine kuwa wachungaji, wamishenari, wazee wa kanisani, wainjilisti, au huduma nyinginezo. Kazi ya kuhubiri si ajira ambayo mtu anakwenda chuoni kusoma kwa lengo la kupata baada ya kuhitimu masomo yake, bali ni mwito mtakatifu ambao mtu huitwa na Mungu mwenyewe kuwa muhubiri. Mtu huenda chuoni ili kupata maarifa yatakayomwezesha na kumsaidia katika kutimiza mwito wa Mungu uliondani yake. Haendi chuoni kupata mwito bali wito husababisha mtu kwenda chuoni kama sehemu ya maandalio. Hivyo wito usichanganywe na ajira na maslahi binafsi ya mtu. Ni lazima wito uheshimiwe na kuogopwa. Waamini hawapaswi kujihusisha na huduma kwa lengo la kujinufaisha na kujipatia mali kwa njia za ujanja ujanja. Kimsingi kila mwamini ni muhubiri kwani agizo kuu linamhusu kila mwamini. Kila mwamini anapaswa kujihusisha na kupeleka injili kwa watu waliopotea dhambini hili ni agazo la jumla. Lakini kuna watu maalumu ambao Bwana ameweka wito wa muda wote(Full time commitement) ndani yao. Amewachagua kwa kusudi hili katika maisha yao na muda wao wote. Hawa wanasimama katika zile huduma tano za uongozi katika kanisa, ambao ni mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu. Hawa ndio Bwana amewaweka kusimama katika kazi ya kuhubiri ya muda wote, Wao hawapaswi kujihusisha na shughuli zingine bali kazi yao ni kulihudumia Neno na kuomba yaani Kuhubiri. Bwana ameweka mwito mtakatifu ndani yao ambao ni wajibu mkuu na wa kuogofyapia{.Mdo6:2,4} hili ni agizo mahususi. Wito huu haupatikani kwa njia ya kusoma au kwa njia ya ulaghai bali kwa kuitwa na Mungu mwenyewe kuwa msemaji wake. Kuna baadhi ya makanisa ambayo yameufanya wito wa Mungu kuwa ni ajira. Kwani wao huwapeleka watu kwenda chuoni kusomea huduma fulani mfano uinjilisti, uchungaji nakadharika kwao wito si jambo la msingi kwao ila elimu ndiyo yenye kupewa kipaumbele. Wao humpa mtu kushika nafasi ya huduma baada ya kuhitimu mafunzo ya chuo cha Biblia bila kujali kama ana wito au la. Matokeo yake ni kwamba makanisa yamekuwa yakiongozwa na kuhudumiwa na watu wasio na wito wenye kutegemea elimu ya darasani tu, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo na uhai wa kanisa. Elimu ni jambo la zuri sana lakini elimu haiwezi kuchukua nafasi ya wito katika kanisa la Mungu ikiwa tunataka kufikia kusudi la Mungu la mwito mtakatifu na kusimama kiuaminifu mbele zake kupata ushindi mkuu. Usiwe mtumwa wa elimu. Elimu hii unayopata ikusaidie katika kumtumikia Mungu na kufanya huduma lakini isichukue nafasi ya Roho mtakatifu katika maisha yako na huduma yako. Wala haipaswi kuwa badala ya Roho mtakatifu. E. MAANDALIO KWAJILI YA HUDUMA. Ni muhimu mara mtu atambuapo kwamba Mungu anamwita katika huduma kufanya mambo kadhaa. Mojawapo ni kuanza kumngojea Bwana kwa njia ya maombi, Kujihusisha na huduma mbalimbali zinazojitokeza kanisani au sehemu nyingine yeyote . Pia ni muhimu kwenda shule kwajili ya mafunzo zaidi ya maandalio ya huduma. Kuwa na mlezi. Ni lazima kuwa na mlezi wa huduma ambae atakusaidia katika kutimiza mwito ulio ndani yako. Mlezi wa kwanza wa huduma na wito wako ni mchungaji wako. Mweleze mchungaji kuhusu wito ulio ndani yako na mwombe akusaidie katika kuulea wito huo. Kuwa mtii na mnyenyekevu kwa mcungaji wako. Shirikiana na watu wenye wito kama wako ili uweze kujifunza zaidi. Fanya kazi na huduma mbalimbali unazopewa na mchungaji au viongozi wa kanisa. Jifunze kwa watu wenye wito kama wako walifanikiwa katika utumishi wao. Kupata mafunzo zaidi. Ni vizuri mara unapogudua kwamba Mungu amekuita katika utumishi au mojawapo ya zile huduma tano kwenda chuo cha Biblia kwaajili ya mafunzo na matayarisho kwaajili ya huduma Mungu anayokuitia. Namna ya kuchagua Chuo cha Biblia 1. Omba Uongozi wa Mungu juu ya jambo hili. 2. Angalia chuo kitakachokidhi mahitaji yako ya kuandaliwa. 3. Angalia maswala ya usajili wa chuo.(Vyuo vingi vya Biblia havina usajili wa serikali kwani haviko kitaaluma zaidi bali kihuduma). 4. Chunguza misingi ya imani ya chuo. 5. Tathmini uwezekano wa kuingizwa katika huduma baada ya mafunzo. 1. Mambo ya kuzingatia unapokuwa katika Chuo cha Biblia. 2. Jikite katika masomo kabisa kwa miguu yako yote miwili. 3. Jihusishe kikamilifu na ratiba nzima ya Chuo. 4. Tia bidii katika masomo. 5. Tumia muda kuwa na waalimu na wanafunzi wenzako na jifunze vitu vyema toka kwao. 6. Epuka kuwa mjuaji (arogant). 7. Kuwa mtumishi. 8. Jitahidi kuonekana na si kusikika. 9. Shirikisha baadhi ya watu maono na wito ulio ndani yako. 10. Baki kuwa mwanafunzi daima hata baada ya kuhutimu mafunzo. 11. Kwa mtii kwa amri, shria, kanuni na taratibu za Chuo. • Usiongozwe na elimu bali ongozwa na Roho mtkatifu. • Usihubiri kwa maneno yenye hekima pekee kwa lengo la kushawishi akili za watu bali hubiri Kwa dalili za Roho mtakatifu na nguvu. 1Kor 2:4. • Hakikisha unautumikia wito ambao Mungu ameweka ndani yako kwa gharama yoyte ile bila kujali mazingira au kitu kingine chochote. • Kwa hiyo wito wa kuhubiri hautoki kwa mwanadamu yoyote Yule bali toka kwa Mungu mwenyewe. Mungu huwafanya watu wake kuwa wahubiri. • Jiulize wewe ni mhubiri wa kufanywa na nani ? F. Kweli kuu kuhusu wito wa kuwa mhubiri. 1. Roho mtakatifu huweka wito ndani ya mtu. Wito wa Mungu huja juu ya mtu kupitia Roho mtakatifu. Katika akili ya kawida ni kazi kubwa kuhubiri au kutumika. Wito huja kwa watu wa aina zote na umri wote wowote. Baahi ya watu husikia wito na kujitoa wangali wadogo lakini wengine katika umri mkubwa n.k 2. Shauku ya kutimiza wito. Watu wanaoitwa kuwa wahubiri waliumbwa na Mungu kwa kusudi hiloYer1:4-10 Hawawezi kupata utoshelevu kwa kufanya kitu kingine chochote. Hawawezi kupinga kujihusisha katika huduma au kuchukua fursa za kuhubiri. Hata kama hakuna nafasi za kutumika moja kwa moja bado watatafuta nafasi katika huduma yoyote inayojitokeza. 3. Mungu huwaandaa wale anaowaita kwajili ya huduma. Mungu hawaiti watu ambao hwana uwezo wa kutimiza mwito wake. Wahubiri wengi wanakipaji cha kuongea. Watu wenye wito juu ya watoto Mungu huwaandaa kwa kuwapa uwezo kwa kufanya huduma na watoto n na wanaoitwa kuwa wacghungaji huwezeshwa kuwa wachungaji. Kwa namna yoyte Mungu huwaandaa na kutoa nguvu ya uwezesho juuv yao. 4. Wito wa Mungu wapaswakuwa wazi. Wito wa Mungu usifichwe. Wito wa Mungu ulioju yako wapaswa kuwa wazi kwa watu wangine lakini haupaswi kukimbilia kwenye wito huo mara moja. Hutakuwa na furaha na mafanikio na wito huo mpaka utakopokuwa umejisalimisha kwa mapenzi sahihi ya Mungu juu yako.Wito ambao Mungu amekuita kuutimiza unapaswa kuuweka wazi. Shirikisha watu ambo watafanyika msaada katiki kuulea wito wako. Fanya kazi na watu. Tumika na watu wenye wito kama wako. Kaa chini ya mtu mwenye neema kama ya wito ulionao ili uweze kujifunza zaidi. 5. Wito wa Mungu ni wito wa matayarisho. Kuna wajibu mwingi na mkubwa ambao huja pamoja na wito wa kuhubiri. Mungu akisha mwita mtu humuandaa kwanza kabla ya kumtuma na kumwachilia kwnye huduma aliyomuitia. Mhubiri anapaswa kujiimalisha kiroho na kimwenendo.Anatakiwa ajiandae kiakili kwa kusoma na kupata mafunzo. Pia anapaswa kujiandaa kimatendo kwa kunoa vipawa vilivyo ndani yake na kuyatisha maisha yake yote kulingana na wito ulio ndani ya yake. Mungu akisha weka wito wake ndani ya mtu huanza kumwandaa kwajili ya wito huo. Humpitisha katika majaribu mbalimbali yanayoendana na wito wake, humpeleka kwenye shule yake ijulikanayo kama shule ya moto na baada ya kufuzu huko Mungu humwachilia mtu katika huduma. Musa aliandaliwa kwa zaidi ya miaka arobaini, Yusufu kwa muda wa zaidi ya miaka kumi, Paulo kwa muda wa miaka kadhaa.Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba Mungu huwa hana haraka. Ukipata wito wa Mungu ndani yako usifanye haraka kuutimiza Bwana anatenda kwa wakati. Unapaswa kusubiri wakati wa Bwana na ufanye kwa wakati wake na si nje ya wakati wa Mungu. G. Mawazo mawili potofu kuhusu mahubiri. Kuna dhana mbili potofu ambazo zinajitokeza katika uwanja na taaluma ya mahubiri mawazo hayo ni: a. Maaandalizi si lazima. Wazo la kwanzalenye makosa ni kwamba maandalizi si lazima na huonesha kukosa imani kwa mhubiri. Watu wenye kushikilia msimamo huu hufikili kwamba imani ya kweli hutupilia mbali jitihada yoyote inayojaribu kuandaa akili na hiyvo husimama mimbarini wakiamini kwamba Mungu atawapa maneno ya kusema.husimamia maawazo haya: i. Roho mtakatifu atakupa unachohitaji kuhubiri. Unapopanda mimbarini. _- Zab 81:10 “ Fumbua sana kinywa chako name nitakijaza”(Hutumia andiko hili kutetea msimamo wao.). Pia husema kwamba Yesu alisema kwamba “Msifikirifikiri nini cha kusema maana mtapewa kinywa cha usemi saa ili ilie mnapotakiwa kusema” Unapoyachunguza kwa umakini maandiko hayo utagundua kwamba maandiko hayo wanayafasili nje na mkutadha wake na na kulazimioshwa yaseme kile ambacho hayamaanishi. *Mahubiri ni kamana jengola kiroho ambalo linatakiwa kusanifiwa na kuandaliwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Roho mtakatifu ndiye mhandisi mkuu wa mahubiri. b. Uwezo wa mtu unatosha. Kuweka mkazo katika matayarisho na kutegemea uwezo wa kibidanu tu. Wahubri wanaoshikilia msimamo huu hudai kwamba maandalizi peke yake yanatosha na huweka mkazo kwenye matayarisho pekee.Kumtegemea Roho mtakatifu huwa ni kudogo sana au hakuna kabisa, bali tumaini la mtu binafsi ambalo ni matokeo ya kujifunza na kuendeleza uwezo wa asili. Ujumbe wa namna hii waweza kuwa mzuri kabisa lakini hauwezi kuleta matokeo yatakikanayo daima. Kwani ni Roho mtakatifu pekee ndiye anaeweza kuleta badiliko katika maisha ya waikilizaji wako. Bila yeye mahubiri huwa ni maiti na haiwezi kuleta uhai kwa sababu ni uhai wenye uwezo wa kuzaa uhai. *Roho mtakatifu huuhuishaujumbe na kuletaq matokeo yaliyokusudiwa na Mbingu katika maisha ya wasikilizaji. Ili mhubiri aweze kuhubiri sawasawa anapaswa kuwa na maansdalizi ya kutosha katika kuuandaa ujumbe wake kwa kusoma, kutafakari na kuchambua kweli zote zilizomo katika ujumbe wake. Lakini hayo yotec anapaswa kuyafanya akiwa katika hali ya maombi. Mhubiri anapaswa kumsikiliza Roho mtakatifu klwa kina na kupata uongozi kwake na kutaka Roho mtakatifu amshirikishe kile anachotaka kusema na watu wake na kukifanyia uchambuziyakinifu katika hali ya maombi ili aweze kukiwasilisha kwa ufanisi. • Mhubiri anapaswa kutambua kwamba yeye hana watu wala si Chanzo cha ujumbe. Kwasababu hiyo anatakiwa kumsikiliza mwenye watu na aliye chanzo cha huo ujumbe na kusimama katikati kwa uaminifu kuwafikishia watu kwa usahihi kile mwenye watu anachotaka kiwafikie watu wake. • Mhuibiri anapaswa kutambua kwamba kazi ya kuhubiri ni takatifusana na ni kazi nyeti ambayo yapaswa kufanywa kwa umakini, uaminifu na unyeyekevu mkuu. • Mhubiri mwenye kutegemea juhudi zake na uwezo wake wa asili atakuwa ni muhubiri kilema na halikadharika mhibiri mweye kutegemea kupewa ujumbe akiwa mimbarini atakuwa ni kilema. • Vyote viwili vyapaswa kwenda pamoja, maombi na matayarisho.Kwa sababu mahubiri ni matokeo ya mawasiliano na ushirika mzuri kati ya Roho mtakatifu na mhubiri. H. Umhuhimu wa kujifunza homiletics. a) Linatusaidia kujua mbinu mbalimbali za kuhubiri. b) Linatusaidia jinsi ya kuhubiri bila kuwachosha watu. c) Linatufanya kuwa na ujasiri tunapohubiri. d) Linatusaidia kuhubiri kwa usahhi. e) Linatusaidia kutambua mahubiri ya uongo. f) Linatusaidia kujua na kuheshimu wito tulio nao. g) Linatusaidia kujua kusudi la Mungu la mahubiri. h) Linatusaidia katika kuheshimu wito wa watu wengine. Zoezi. Jibu maswali fafuatayo. Wanafunzi waweza kujibu katika makundi au mmoja mmoja kama kazi ya nyumbani kwa kadri mwalimu atakavyoona inafaa. 1. eleza maana ya mahubiri kwa mitazamo mbalimbali. 2. Eleza vile mahubiri yasivyo. 3. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri na kuhubiri. 4. Taja faida tano za kujifunza somo la kuandaa mahubiri. 5. Tathmini misukumo mbalimbali inayosababisha watu waingie katika huduma tano za uongozi wa kanisa. na hali hawana wito. 6. Eleza namna gani mtu aweza kujua kwamba Mungu anamwita kuingia katika huduma. 7. Eleza umuhimu wa kipindi cha maandalizi na matayarisho kabla ya mtu kuingia katika huduma ambayo Mungu anamwita kuifanya. MADA YA PILI: MBINU ZA UTAYARISHAJI WA MAHUBIRI Utangulizi Katika mada hii tutajadili aina mbalimbali za utayarishaji wa mahubiri, maeno ya mahubiri na sehumu za mahubiri au hotuba. Tutapitia kwa undani kila kimojawapo ya vipengele hivi ili kujifunza jinsi vipengele hivyo vinavyohusiana na mahubiri na tunavyoweza kuvitumia katika huduma ya kuhubiri na kuandaa mahubiri. Malengo ya mada. Baada ya kumaliza kujifunza mada hii mwanafunzi ataweza. • Kutaja na kueleza mbinu mbalimbali zinazotumika katika utayarishaji wa mahubiri au hotuba. • Kutathmini kila mbinu kwa kueleza ubora na udhaifu wake. • Kuandaa jumbe za mahubiri kwa kutumia mbinu mbalimbali. • Kutambua maeneo muhimu katika mahubiri. • Kutambua sehemu muhimu katika jumbe na hotuba. • Kutayarisha jumbe na hotuba za ki-Biblia kwa kuzingatia sehemu muhumi katika • jumbe na hotuba. A. Mbinu za Utayarishaji wa jumbe na hotuba. Kuna aina nyingi za utayarishaji wa somo au hotuba, na kila mojawapo ina umuhimu wake. Lakini katika mada hii tutajifunza aina tatu za utayarishaji wa somo au hotuba. Kila mwanafunzi anatakiwa kuelewa aina zote tatu na anapaswa kujizoeza kutumia njia hizi zote ili aweze kufaidika zaidi. Mbinu hizi za utayarishaji wa somo pia zaweza kutumika kama mbinu za kuhubri. Kwa hiyo tutakapokuwa tunajadili zitaangaliwa katika maeneo haya mawili. ( Kama mbinu za utayarishaji na kuhubiri.) 1. Somo Lililoandikwa. Katika aina hii mhubiri hupaswa kuandika kila kitu anachokusudia kukihubiri. Wakati mwingine somo lote huandikwa. Kila eneo la somo huchambuliwa kwa undani na kuwekwa katika maandishi. Ujumbe au somo lote huandikwa kikamilifu kabla ya kuhubiri. Mhubiri huelezea kwa undani somo lake anapohubiri likiwa katika maandishi. Mhubiri anapohubiri mara nyingi hupitia kila kitu alichokiweka katika maandishi. Faida za aina mbinu hii. a) Ujumbe wote huandaliwa kwa uangalifu mkubwa. b) Ujumbe huwasilishwa kwa umakini na uhalisia. c) Ujumbe huwa ni wa kitaalam. d) Mhubiri hujikita katika somo. Hasara ya mbinu hii. a) Somo huwa haliwavutii wasikilizaji. b) Utoaji wa ujumbe wa namna hii unaweza kuwa wa kuchosha usipofanywa kwa uangalifu c) Utayarishaji wake huhitaji muda mwingi. ZOEZI. 1. Eleza maana ya somo lililoandikwa. 2. Taja vitu muhimu vilivyo katika somo lililoandikwa. 3. Taja ubora na udhaifu wa njia hii licha ya zilizotolewa katika kitabu hiki. 4. .Andaa ujumbe kwa kutumia mbinu ya somo lililoandikwa na kisha huburi kwa dakika kumi. 2.Somo Lisiloandikwa. Hii ni mbinu ya utayarishaji wa somo bila kuliandika. Mhubiri husoma vifungu vya maandiko na kivitafakari kwa kina kisha hukariri vitu vya msingi vilivyo katika ujumbe wake na maandiko yanayohusika. Aina hii mara nyingi hutumika katika kutayarisha na kuhubiri ujumbe wenye uvuvio zaidi. Njia hii ni nzuri sana katika kuhubiri ujumbe wa kiinjilisti. Ujumbe hutiririka toka rohoni na huwa wa kuvutia mno. Faidaza mbinu hii. a) Ni rahisi kutumia. b) Haihitaji muda mwingi wa matayarisho. c) Mhubiri huwa huru kutoa kila kinachokuja ndani yake maadam kinaendana na ujumbe wa somo. d) Huwasisimua wasikilizaji na kuwavutia. Udhaifu wa mbinu hii. a) Mhubiri kutoka nje ya ujumbe wake hasa ikifanywa na mhubiri asiye na uzoefu. b) Wasikilizaji waweza kulielewa somo vibaya. (waweza kuelewa vile somo lisicho maanisha). c) Somo kutowajenga wasikilizaji na kuishia kusisimua tu akili zao. d) Somo kutokuwa na maana halisi na hivyo kutowajenga wasikilizaji. ZOEZI. 1.Eleza maana ya somo lisiloandikwa. 2. Taja mabo matano ya kuzingatia katika utayarishaji wa ujumbe kwa kutumia njia ya somo sililoandikwa. 3.Toa tofauti iliyopo kati ya somo lililoandikwa na somo lisiloandikwa. 4. Andaa ujumbe kwa kutumia mbinu ya somo lisiloandikwa na kisha hubiri kwa dakika kumi 3.Mbinu Ya Skeletoni. Njia hii huhusisha kuandika maelezo ya somo au ujumbe kwa kifupi kwa lengo la kufanikisha utunzaji wa kumbukumbu sahihi juu ya ujumbe au somo. Kwa maana nyingine ni kwamba mhubiri hutayarisha muhtasari wa ujumbe au somo.Mhutasari huo huwa kama skeletoni ya somo, Skeletoni maana yake ni fuvu. Mfano wa fuvu la binadamu. . Mhubiri huhubiri kwa kutumia skeleton hiyo. Kazi yake hasa ni kuweka nyama katika skeletoni hiyo kwa njia ya mahubiri. Hivyo anapohubiri huweka nyama katika mahubiri yake ili yawze kuwa kitu kamili . Mhutasari wa somo huwa kama mifupa ya ujumbe. Ndiyo mifupa ambayo huleta sura na mategemeo kwa kile mhubiri anachotamani kusema. Anavyosema anaweka nyama katika mifupa na kuufanya mwili wa somo lake. Hupanua mawazo yake ambayo maelezo yake mafupi yamekuza. Faida za mbinu hii. a) Mbinu hii humpa mhubiri uhuru zaidi. b) Utoaji wa somo huwa wa kuvutia sana. c) Somo huwajenga wasikilizaji bila kuwachosha. d) Mhubiri huweza kutoa somo kwa mtiririko mzuri na sahihi. Zoezi 1. Eleza maana ya skeletoni. 2. Eleza maana ya mbinu ya skeletoni. 3. Linganua kati ya minu ya somo lisiloandikwa na mbinu ya skeleton. 4. Eleza kati ya mbinu tatu ulizosoma, ipi ni bora kuliko zote na toa sababu ya jibu lako B. Maeneo ya Mahubiri. Kuna maeneo makuu manne ambyo mahubiri huhusisha. Mhubiri yoyote ni lazima azingatie maeneo hayo ili aweze kufanikisha mahubiri yake. I.Wazo . Hii huhusu namna ya kupokea kichwa cha somo au ujmbe. Ni ujuzi unaohusu namna ya kupokea ujumbe toka kwa Mungu. Huhusu namna ya kupata wazo la awali na kichwa cha somo. Mungu hupanda mbegu ya wazo kuhusu somo au ujumbe siku kadhaa kabla ya mahubiri. Mbegu hiyo hukua kwa njia ya kuitafakari na maombi zaidi. Kutokana na ujuzi mhubiri aweza kuujenga uwezo wa kutambua mstari unaohusika. Mhubiri hupaswa kuliendeleza na kulikuza wazo lililopandwa ndani yake kwa njia ya maombi, kutafakari na kuchunguza zaidi juu ya wazo hilo ili aweze kutayarisha ujumbe. Pata muda wa utulivu utulie uweponi na omba nuru zaidi ya ufunuo huo. Kuna tofauti kubwa kati ya hotuba na ujumbe.mtu anaweza kujifunza jinsi ya kuandaa hotuba kupitia masomo ya Homiletics lakini Mtu anapaswa kuwa na ushirika na Mungu ili aweze kupata ujumbe. Kupata ujumbe ni jambo la kiroho zaidi kuliko taaluma. Wale wanaofanikiwa kupokea ujmbe wa kuhubiri toka kwa Mungu ndio wanaoweza kufanikisha lengo la kuhubiri. Mambo ya kusaidia kupata ujumbe. Tambua mahitaji ya watu.(Mahitaji ya kiroho na kimwili). Kujazwa na Neno la Mungu. Kujiweka katika viatu vya wengine (Soma Hotuba na sikiliza mahubiri ya watu wengine. Kutokana na uzoefu wa mhubiri. Kutambua kalenda ya Kikristo. Kutokana na mafundisho ya msingi ya Biblia. Kutokana na matukio mbalimbali. II.Muundo. Muundo huhusisha uchambuzi wa wazo ili kuweza kugundua kweli zilizomo katika wazo hilo.Baada ya kupokea Wazo toka kwa Mungu unapaswa uanze kulichambua ili kutambua vitu ambavyo wazo hilo linavyo. Katika hatua hii unapaswa kuorodhesha kwa urahisi kila kitu kilichomo kwenye wazo hilo.Mara nyingi unapokuwa katka hatua hii unahitaji kuandika kwa haraka ili kupata kwa kifupi mtiririko wa uvuvio unaokuja. Hakikisha kwamba unaandika kila kitu ili uweze kuchambua baadae. III. Ujenzi. Huhusisha kukusanya na kuyaweka mawazo yako uliyoyachambua katika kipengele cha uchambuzi katika mpango mzuri. Kuweka kila kitu katika mpangilio mzuri kutakusaidia na kukurahisishia katika utoaji wa somo lako. Kuwasislisha mawazo yaliyoendelezwa hufanyika msaada sana kwa wasikilizaji wako katika kuelewa na kufuata mpango wako wa kufikiri. Somo likiwalimechanganywa itawawia vigumu wasikilizaji wako katika kulielewa somo hilo.Ujenzi wa somo hulenga kulifanya somo rahisi kiasi cha kueleweka vizuri na wasikilizaji. Ni muhimu sana kwa mhubiri kuliweka somo katika namna itakayofanya lieleweke kwa urahisi. IV. Mawasiliano. Hii huhusu namana mhubiri anavyowasilisha somo au ujumbe kwa hadhira. Mhubiri anatakiwa kuliwasilisha somo lake kwa njia rahisi na nyepesi kueleweka na wasikilizaji wake. Anatakiwa: a) Kuwasilisha ukweli uliowazi na wenye kueleweka. b) Kutoa ujumbe kwa njia ya kuteka akili za hadhira. c) Kuendeleza mawazo yake katika mpango ambao hadhira wataweza kuyafuata kwa urahisi. d) Kuwahamasisha hadhira kulitendea kazi somo. Yak 1:22. C.Sehemu Kuu za ujumbe na Hotuba. Kwa kawaida mahubiri au hotuba yoyote ile ni lazima iwe na sehemtu tatu ambazo kwa pamoja huunda hotuba au mahubiri hayo. Sehemu tatu hizo ni utangulizi, kiini na hitimisho.Kila sehemu ni muhimusana na inatakiwa kupewa uzito wake. Sehemu mojawapo ikipuzwa yaweza kuvuruga au kuharibu kabisa ujumbe au hotuba yako. I.Utangulizi. I. Hii ni sehemu ya kwanza ya hotuba. Utangulizi hutambulisha hotuba au somo zima na kutoa picha jinsi somo litakavyokuwa. Utangulizi ni sehemu muhimu ya ujumbe na kama hadhira hawajakusikiliza kwa umakini katika kipindi hiki cha awali yawezekana kutokuuelewa ujumbe wako au kutokukusikiliza vizuri katika sehemu zinazobaki za hotuba yako. Mara nygingi utangulizi huwa kama muhtasari wa ujumbe.Katika utangulizi mhubiri huwaeleza hadhira kwa kifupi juu ya kile ulichopanga kuongelea au kuhubiri. Utangulizi ni kama mlango wa nyumba katika ujumbe na hotuba.Uangulizi huwa na lengo mahususi la kuwajulisha hadhira ujumbe ambao unawasislishwa kwao. Waamni wengi huja kanisani wakiwa na matatizo mbalimbali ya kifamilia , kikazi N.k .Utangulizi unatakiwa kuwavuta ili waweze kujikita kwenye ujumbe na kuwasahaulisha matatizo waliokuja nayo. Uangulizi ni silaha ya kuwateka wasikilizaji. Kuna namna mbalimbali za kuanza utangulizi. Mhubiri anapaswa kujifunza namna mbalimbali za kuanza utangulizi na ajizoeze kuanza utangulizi wa mahubiri yake kwa njia tofauti tofauti. Baadhi ya njia za kuanza utagulizi zimeorodheshwa hapa chini. II.Namana ya kuanza Utangulizi 1. Kuanza kwa kuuliza swali. 2. Kuanza na maelezo ya kuchanganya(Yenye kuhamasisha watu kusikia kw2a makini swehemu ya ujumbe inayobaki ). 3. Anza kwa andiko 4. Anza kwa mkutadha 5. Anza na habari au kielelezo. 6. Anza na tukio la sasa. 7. Anza na nukuu III. Mambo ya msingi katika utangulizi. Kuteka usikivu. utangulizi wako unapaswa utawale hamu na mawazo ya wasikilizaji. Kujenga masikilizano. Lazima ujenge mawasiliano kati yako na wasikilizaji. Kuleta kukubalika. Ni lazima utangulizi kwako ukujengee kukubalika kwa wasikilizaji. Unapaswa kupata usikivu wao, matumaini na heshima. Kujulisha. Utangulizi wako unapaswa kuwaeleza wasikilizaji kwamba somo lako lina husu nini hasa, na jinsi utakavyoliwasilisha. Kusadikisha. Ni lazima utangulizi uwasadikishe wasilizaji juu ya umuhimu wa ujumbe na kupata usikivu mzuri wa sehemu iliyobaki ya hotuba yako. Usitoe utangulizi kwa kuomba msamaha. Usiseme “Bahati mbaya sikujiandaa vizuri” Kufanya hivyo kutapoteza usikivu wa wasikilizaji wako na kukufanya usiaminike kwao. Sifa za utangulizi mzuri. 1.Sio wa kishindo mno. Utangulizi uwe wa kiasi usiweke hatua ambayo huwezi kuifikia. 2.Sio mrefu mno. Kumbuka kwamba utangulizi si ujumbe wote bali ni sehemu tu hivyo unapaswa kuwa mfupi. 3.Utangulizi uendane na ujumbe. Utangulizi ni sharti ulenge kichwa cha somo. Waweza kuwa muhtasari wa somo au kisa ambacho kinaonesha ukweli wa kile ulichokusudia kuongelea. 4.Unapaswa kuandaliwa kwa uangalifu. Kwa sababu utangulizi wako ni kitu muhimu katika kuvuta usikivu wa hadhira unapaswa kuandaliwa kwa umakini sana. 5.Tayarisha utangulizi wako kwa kujiuliza maswali yafuatayo a.“ Ningekuwa ni msikilizaji wa ujumbe huu nini kingenivuta zaidi ili kuleta usikivu katika yote niliyokusudia kuyasema? 1. “ Ni jambo gani hasa ambalo lingekamata usikivu wangu? b.Majibu yake unayoyapata ndiyo waweza kuyatumia katika sehemu ya utangulizi wa ujumbe wako. 6. Utoe nafasi ya kupitia kwenye kiini cha ujumbe. Utangulizi unapaswa kutoa njia ya kupitia kwenda kwenye kiini cha ujumbe. Kusiwe na pengo kati ya utangulizi na kiini cha ujumbe. II. Kiini. Hii ni sehemu kuu ya somo au ujumbe ambayo imebeba ukweli wote wa somo. Hatua ya kwaza kwenye kiini ni kutoa skeletoni ya kiini na kisha hatua ya pili ni kuweka nyama katika skeletoni yako.Waweza kuweka nyama katika sekeletoni yako kwa kufanya yafuatayo: Kufafanua msamiati mbalimbali inayojitokeza kwenye kiini na kutoa maelezo ya dondoo ulizoziandaa. Tumia kamusi au itifaki ya Biblia katika kupata maana ya maneno hayo. Kiini. Kiini cha ujumbe ni lazima kieleze, kisimulie, kijadili na kutoa kweli yote inayokusudiwa kuwasilishwa. Ni lazima kueleza maana ya andiko au habari. Ni lazima kutoa ushahidi wa kweli inayohubiriwa. Neno la Mungu linajieleza lenyewe. Jambo lingine la kutumia kuthibitisha ni ushuhuda binafsi. Mfano kama unahubiri uponyaji toa uthibitisho kwa kutumia wewe binafsi jinsi Mungu alivyokuponya au alivyowaponya watu wengine. Unapounda kiini unapaswa kujiuliza maswali kadhaa 1. NIini nataka kusema ? 2. Kwanini ninataka kusema hiki ? 3. Ni vipi nitakisema ? 4. Ninachotaka kukisema kitafanikisha nini ? Unaposhughulikia andiko au mada ni lazima kujiuliza kwanini? Namna gani ?, Lini?, Wapi ?, Nini kilitokea kabla na baada ?, Mazingira yalikuwaje?, Matokeo yake yalikuwa nini ?, Nani walikuwa pale ?, na kwanini walikuwepo pale? Walifanya nini?, Hii huhusikaje leo ? na inamaanisha nini leo ?. Kujua majibu ya maswali haya kutakusaidia kutengeneza mhutasari wa somo au andiko. Mfano Luka 16:19 Matumizi ya vielelezo. Moja wapo ya vipengele muhimu katika ujmube au kiini ni vielelezo.Vielelezo ni mifano mbalimbali inayotumika kufafanua na kuelezea ujumbe au somo. Watu wengi huweza kukumbuka vielelezo kuliko ujumbe na hivyo basi vielelezo husadia watu kukumbuka ujumbe. Bwana Yesu amekuwa kielelzo na mwalimu wa vielelezo. Watu hufurahia kusikia vielelezo. Wahubiri wenye ujuzi wa kutumia vielelezo katika jmube na hotuba zao hufanikiwaq kuvuta usikivu wa wasikilizaji wao. Vielelezo ni sawa na madirisha katika nyumba. Vielelzo ni madirisha ya jumbe na hotuba. Jumbe nyingi zinazohubiriwa na wahubiri wengi ni kama nyumba zisizo na madirisha. Nhyumba hizo zaweza kuwa na msingi imara na kuta imara lakini zitashindwa kuingiza mwanga na hewa ya Oksijeni ambayo ni muhimu kwa mwanadamu ili aweze kuishi. Vielelezo hutimiza lengo la kuleta nuru na hewa ya oksijeni ya ki-Biblia katika ujumbe. Vielelezo havipaswi kuwa mwisho vyenyewe lakini vyapaswa kufafanua kweli zinazoawsislishwa. Lengo la vielelezo. Kuleta nuru kwenye somo. Kuvuta usikivu. Kuelezea na kufafanua ujumbe. Kuthibitsha kweli (dondoo). Kanuni za kutumia vielelezo. Kuna kanuni kadha ambazo ni muhimu kuzizingatia wakati wa kutumia vielelezo . Baadhi ya kanuni hizo zimejadiliwa hapa chini. 1. Urahisi. Vielelezo vinapaswa kuwa rahisi kiasi cha kueleweka na kila msikilizaji. Havipaswi kuwa vigumu kiasi cha kuwachanganya wasikilizaji na kuhitaji vielelezo zaidi ili kufafanua vielelezo. Kuna baadhi ya vielelezo ambavyo huhitaji vielelzo vingine . Epuka kutumia vielelezo vya namna hiyo. Yesu alipotumia vielelezo vilikuwa rahisi na wazi Mifano aliyotoa ilkuwa wazi na rahis kueleweka na waikilizaji wa aina zot. Wasomi(mafarisayo na masadukayo) na wasio wasomi (wakulima na wavuvi). Kumbuka kwamba watu wengi utakaokuwa unawahubiria watakuwa ni wenye elimu ya kawaida au wasio na elimu. 2.Ukweli. Hadithi na vilelelzovinavyotumiaka katika amhubiri view wazi. Kama ni hadhi za kutunga usiwaambie watu kwamba ni matukio halisi yaliyotokea. Usilazimishe mfano na kuelelzo kuwa kitu halisi. 3.Kiasi. Vielelzo visizidi na wala visigeuke kuwa ujumbe. Kuna baadhi ya wahjubiri ambao ni mabigwa wa kutoa vielelezona watu huvutiwa sana na vielelezo hivyo. Wanatumia muda mwingi kusimulia vielelzo badala ya kuhubiri. Jambo hili ni hatari sana. Vielelezo vinatakiwa kutumika kuelezea kweli za kiroho na na visigeuke kuwa jumbe.Yesu hakututuma kusimulia hadithi na vielelzo alitutuma kuhubiri. Kwa kawaida kila dondoo kuu inapaswa kuwa na kielelezo kimoja na si vinginevyo. 4. Lengo. Unapaswa kukumbuka kwamba lengo la vielelezo ni kuelezea na kufafanua ujumbe wako. Kweli zipo kumsaidia mhubiri kufikia lengo lake la mahubiri. Lengo la mhubiri linapaswa kubaki kuwa ujumbe na si vielelezo. 5. Uhalisia. Vielelezo viendane na dondoo unayoielezea. Kama hakuna uhusiano hakuna umhuhiu wa kutumia kielelezo hicho. Hakikisha vinahusiana na kwendana. Vyanzo vya vielelezo. Bwana wetu Yesu Kristo alitmia vielelezo na mifano kutoka katika mazingira ya kawaida yaliyomzunguka. Alitumia mifano rahisi kama vile nuru, chumvi mbegu. Mzabibu, kondoo. N.k. Alitumia mifano iliyokuwaikitumika katika maisha ya kawaida. Alizielezea na kuzifafanuana kuzifundisha kweli za kiroho kwa kutumia vielelezo vilivyokuwa katika ulimwengu uliomzunguka. Hivyo basi kila mhubiri anatakiwa kujifunza kutumia vitu mbalimbali vilivyo katka mazingira yake kama vielelezo. Soma vitabu, magazeti ,vijarida na vipeperushi. Sikiliza natutzama vyombo vya habari. Katika mabo yote hayo kua vielelezo vingi ambavyo waweza kuvipata na kuvitumia. Kabla ya kuanza kuitumia kielelezo hakikisha unatihafamu vizuri. Kielelezo kiwasaidie watu kujisikia, kusikia na kuona kile unachokielezea. Ni lazima wewe mwenyewe uguswe na kuvutiwa na kielelezo hicho. Kama hakikuvuti wewe bila shaka hata watu wengine hakita wavutia. Jifunze kwa mwalimu mkuu Yesu Kristo. Vichekesho. . Vichekesho ni muhimu katika mahubiri kutegemeana na ujumbe unaohubriwa. Vichekesho vyapaswa kuendana na somo au ujumbe. Tumia vichekesho kuamsha akili za watu na kuvuta usikivu wao. Vichekesho havipaswi kuzidi kiasi cha kupunguza uzito wa somo. Pia Ujumbe usitawaliwa na vichekesho. Kumbuka kwamba mahubiri si vichekezo ni kitu muhimu na nyeti sana. Usifanye mahubiri kuwa komedi. Wala usiwe mwanakomedi. III. Hitimisho. Hii ni sehemu ya mwisho ya hotuba au ujmbe lakini kipengele cha muhumi sana . Kipengele hiki kisipozingatiwa maana na malengo yote ya kuhubiri huvurugika na kutokuwa na maana. Hivyo ni lazima kipewe uzito unaostahili. Mambo ya kuzingatia. Tunia muda kidogo kwa kuuelezea ujumbe kwa kifupi. Kazia maeneo ya msingi unayofikiri kwamba hayakueleweka vizuri kwa hadhira wakati ukihubiri na yale yanayotakiwa kupewa uzito maalumu. Pia waweza kurudia kuzitamka kwa sauti dondoo za ujumbe wako kila moja. Usiwachushe (bore) kwa kuanza kurudia kuhubiri ujumbe wako wote. Mwaliko. Mwaliko ni kipengele muhimu sana katika hitimisho. Kwa sababu mahubiri ni tofauti na aina nyingine za hotuba hivyo mwaliko huwa ni muhimu sana kwa kuwa mahubiri huhusu kuchukua maamuzi au hatua juu ya kile kilichohubiriwa. Mahubiri bila mwaliko huwa hayajafikia lengo la kuhubiri. Mwaliko ni lazima katika mahubiri ya aina yoyote ile. Mwaliko huwa ni wakati wa kuitikia Kile Mungu amesema kupitia mahubiri. Ni wakati wa kutendea kazi kile kilichofundishwa au kuhubiriwa. Mhubiri anapaswa kuufanya mwaliko kuwa wazi kwa wasikilizaji wote. Lengo la mwaliko si kuwaita watu madhabahuni tu bali ni kuwahamasisha watu kuweka ujumbe katika matendo. Pia Mhubiri hutakiwa kuuweka ujumbe wake katika matendo. • Ukihubiri uponyaji waite watu madhabahuni na waombee uponyaji. • Ukihubiri kutembea katika mamlaka unatakiwa udhihishe mamlaka hiyo. • Ukihubiri utoaji waite watu kumtolea Mungu. • Ukihibiri toba unapaswa kuwaongoza hadhira kwenye maombi ya toba na kuwaita madhabahuni wale wanohitaji kutengeneza kwa upya mwenendo na mahusiano na Mungu na kuomba nao. • Wapeleke watu kwenye matendo na matumizi Mt 21:23. Yak 2:22. • Unatakiwa kuwaongoza hadhira kuomba kwaajili ya ujumbe au somo kwa kadri ya maongozi ya Mungu na kwa kadri Mungu alivyosema na kila mmoja. • Unaweza kuwaongoza watu waimbe wimbo unaoendana na ujumbe uili kuwaogoza uweponi na kuwapa hamasa. • Toa mwaliko kwa watu ambao wanataka kuokoka na kama wapo omba nao. Baada ya hapo maliza na mkabiribishe anaehusika na ratiba inayofuata. Kwa kuhitimisha juu ya sehemu tatu za ujumbe au hotuba twaweza kuvifupisha vipenele vyote hivyo vitatu kwa sentensi tatu ambazo ni: 1. Waambie hadhira kile unachotaka kuhubiri.(Utangulizi.) 2. Hubiri kile ulichowaambia (Kiini), kisha: 3. Waambie kile ulichohubiri.(Hitimisho). ZOEZI. Katika makundi ya watu watatu watatu jadilini maswali yafuatayo: 1. Jadili umuhimu wa vipengele vinne vya maeneo ya mahubiri kila kimoja. 2. Nini kitatokea kama mhubiri atatayarisha ujumbe wa mahubiri bila kuzingatia maeneo hayo. 3. Eleza umuhimu wa sehemu tatu za ujumbe wa mahubiri. 4. Mhubiri bora ni lazima azingatie sehemu tatu za ujumbe. Jadili kauli hii kwa mifano dhahiri. Kuhubiri si kazi rahisi. Kubali usemi huu kwa hoja kumi madhubuti. MADA YA TATU: AINA MBALIMBALI ZA MAHUBIRI. Kuna aina mbalimbali za mahubiri na kila aina ya mahubiri ina nafasi yake katika kuujenga na kuimarisha mwili wa Kristo na kuwaleta waliopotea dhambini. Mhubiri analazimika kufahamu aina mbalimbali za mahubiri ili aweze kuwa na ujuzi mwingi wa kuhubiri na ili aweze kuhubiri kwa kuyafanya mahubiri kuwa mapya kila ahubiripo. Kuhubiri kwa kutumia aina mbalimbali za mahubiri huwajenga wasikiliza kwa namna mbalimbali ambapo aina mojaya mahubiri isingeweza kufanya hivyo. Pia husaidia washirika na waamini kuwa na msingi mzuri wa uelewa wa Neno la Mungu. I. Mahubiri ya kifungu. Aina hii ya mahubiri hujengwa juu ya kifungu kimoja kidogo cha maandiko tu. Huhusisha kuchagua maelezo fulani maalum ya maandiko na kuyachunguza, kuchambua na kugundua kweli zote zilizomo ndani yake na kuziwasilisha kwa wasikilizaji kwa mtindo rahisi na wenye kueleweka. A. Faida za mahubiri ya Kifungu. a) Huvutia. b) Huzuia kutoka nje ya somo. c) Hufanya mahubiri kuwa ya ki- Biblia. d) Humwongezea mhubiri ujasiri. e) Husaidia wasikilizaji kulikumbuka somo. B. Jinsi ya kuandaa mahubiri ya kifungu. Kuna mambo kadhaa ambayo mhubiri anapaswa kuyazingatia wakati wa kuandaa mahubiri ya aya, badhi ya mambo hayo yamejadiliwa hapa chini. 1.Soma Biblia mara kwa mara. Unapaswa kusoma Biblia mara kwa mara ikiwa unataka kuwa mhubiri mwenye mafanikio katika huduma yako. -Tenga muda wa kusoma Biblia kila siku. Beba Biblia ndogo kila mahali unapokwenda ili upatapo muda uweze kuisoma. 2. Jifunze Biblia. Kujifunza ni zaidi ya kusoma.Kujifunza kuna husisha kusoma Biblia kwa undani kwa kuchunguza kikamilifu kila kitu kilicho katika maandiko unayosoma na kutafakari kwa kina,.Yos1:8. Unapaswa kutafakari kwa uangalifu vitu unavyosoma. Viweke kwenye akili yako na kuvifikiri tena na tena. Unapaswa kujizoesha kuchambua kile ulichojifunza. Baada ya kukichambua kwa umakini unapaswa kukiweka tena akilini. 2. Kuwa na Daftari la kuandikia. Kila usomapo Biblia yako jitahidi kuwa na kalamu na daftari la kuandika mambo muhimu unayojifunza. Jenga mazoea ya kuandika kwa ufupi kila ufunuo unaoupata. 3. Dumisha hali ya maombi. Unapaswa kuwa katika hali ya maombi kila usomapo Biblia .Omba Mungu akufunulie upate kulielewa Neno lake.Pia unapaswa kumwomba Mungu akupe usikivu juu ya kweli anazokufunulia katika Neno lake. 4. Jenga usikivu.Unapaswa kuwa katika hali ya utulivu na usikivu katika Nyanja zote yaani kimwili, kiroho na kisaikolojia. Mungu hutoa ufunuo wake kwa sauti ya kimya ndani ya roho ya mhubiri. Kama hunautulivu na usikivu wa kutosha ni vigumu kugundua maarifa hayo.. - C.Sifa za aya ya mahubiri Kifungu cha mahubiri au aya yapasa kuwa : a. Yenye mamlaka ya ki-Biblia. Mafundisho unayokusudia kuhubiri toka kifungu au aya fualani ya maandiko yapasa ikubaliane na kile Biblia nzima inachofundisha. Katika mahubiri ya kifungu kuna uwezekano wa kuchukua kimakosa mstari nje ya maana yake na kuutumia kufundishia kitu ambacho Biblia haikubaliani nacho. Ni Muhimu sana kwa ,mhubiri kujua jinsi mstari anaoshughulikia jinsi unavyokubaliana na kusudi la sura yote na kitabu chote. Daima mhubiri anapaswa kujitahidi kufasili aya yake katika nuru ya yale ambayo Biblia nzima inafundisha. b.Kamili. Aya yapaswa kuwa katika maandisha ya ukweli ulio kamilika. Baadhi ya wahubiri huchukua kifungu cha maneno katika mstari na kukitumia bila kujali maneno yaliyotangulia au yanayofuata. Jambo hili si zuri na huzaa mafundsho ya uongo. Na huku huitwa. “Kulichanganya neno la Mungu na uongo……..2Kor 4:2. Ni lazima uepuke jambo hili kwani litaleta kutokuaminika na maelezo yasiyo ya ki- Biblia na hatimae utawapotosha wasikilizaji wako. c. Fupi kiasi. Kifungu cha mahubiri chapaswa kitolewe kwenye maelezo ya maandiko ambayo ni mafupi na ya kulizisha. c. Ya kueleweka. Aya yapaswa kueleweka na iwe muhtasari wa kutosha wa kile unachotaka kukishirikisha. *Unapaswa ubaki katika mipaka ya kile ambacho aya yako inaelezea. D. Namna ya kuandaa mahibiri ya aya. a. Elewa maneno yake vema. Kipitie kifungu kwa kukisoma mara kadhaa, kitafakari na kujenga kumbukumbu juu yake na kiseme mwenyewe kwako. Hakikisha unakielewa vizuri. b. Elewa lugha yake.Tamabua lugha yake kama ina maana halisi au kama ni lugha ya mifano tu. Jiulize kama mwandishi alikuwa na maana hasa ya kile alichokiandika au maneno yake yachukuliwe kama mfano wa mahubiri? c. Changanua ujumbe wake.Chambua ujumbe unaoupata na kuutenga katika sehemu kadhaa zenye kulandana ili uweze kuuwasilisha kwa mtiririko mzuri. d. Chunguza maneno yake. Jitahidi kugundua kile maneno hayo yalikusudia kuwasilisha hapo awali. Ikiwa una kamusi ya kigiriki au Kiebrania unapaswa kulitazama neno hilo. Jaribu kubaini kama kuna maana maalumu ndani ya neno unalolishughulikia. Kufanya hivyo kutakusaidia kugundua maana yoyote maalumu ambayo mwandishi alikusudia kuiwasilisha. e. Tathmni mwendelezo wake. Baini kweli zile mwandishi alitaka kuzielezea. Tambua jinsi alivyo kamilisha katika kuziwasilisha kweli hizo. Jaribu kufuata mwongozo wake na kuuendeleza katika mtindo huo. f. Mkutadha wa kifungu.. i. Maneno ya mbele na ya nyuma ya kifungu. Angalia jinsi mistari iliyotangulia na inayofuata inachosema. Chunguza aya kuhusiana na sura nzima ambayo umetoka. Chunguza kifungu hicho katika nuru ya kitabu kizima ambamo kinapatikana. Jifunze kiini na mazingira yote ya kitabu. ii. Hali ya mila. Je mila za wakati ule ziliathiri kile kilichoandikwa? Je watu walioandikiwa kifungu hicho awali wangekuwa na wazo la kile kilichoandikwa tofauti na ambalo tungepata katika hali yetu? Kama ndivyo nini ingekuwa maana inayolingana na sasa? ii. Hali ya kihistoria. Je jambo hili liliandikwa lini? je wakati huo ulishawishi kile kilichoandikwa? Je matukio ya wakati ule yaliyokuwa yakijulikana wakati ule wa uandishi yalikuwa na maana maalum juu ya kile kilichosemwa? iv. Hali ya kijiografia. Mwandishi alikuwa wapi wakati anaandika maneno hayo? je Watu walioandikiwa walikuwa wapi?Je mazingira yao yana uhusiano wa chochote katika kile kilichosemwa? v. Biblia kwa ujumla. Kila sehemu ya maandiko ifasiliwe kwa uaminifu na kwa umakini ili ikubaliane na maandiko yote. Andiko lolote lisifasiliwe nje ya mkutadha wake. Maandiko ni lazima yafasiri maandiko. E.Kupanga Maelezo. Mpanglio mzuri wa maelezo na kazi kwa ujumla ni wa maana sana kwa mhubiri. Hakikisha unapanga maelezo yako kimaantiki. Mpangilio mzuri wa kazi na mawazo humwezesha mhubiri kulielewa vizuri somo na kulishughulikia somo kikamilifu. Pia huwawezesha wasikilizaji kulielwa somo na kulikumbuka somo . 1. Ujumbe uwe katika mpangilio.Panga ujumbe wako katika mtiririko mzuri ili uweze kuufuata kwa urahisi wakati wa kuhubiri. 2. Weka ujumbe wako katika hali ya kueleweka. Jitahidi kukamilisha vipengele vyote unavyohitaji kuviongelea katika mahubiri yako. Kabla ya kupanda mimbarini. 3. Kazia katika mawazo. Unapaswa kuyaweka mawazo yako katika sentensi fupi. Jifunze namna ya kuyaimarisha mawazo yako kwa pamoja na kuyaelezea katika sentensi fupi zinazoeleweka kwa urahisi.Jizoeze kupunguza na kulielezea wazo kwa sentensi moja. 4. Tayarisha maelezo mafupi.Kumbuka kwamba maelezo yako ili kusaidia kumbukumbu yako.unapaswa kuwa na vidokezo vitakavyosaidia kulikumbuka somo lako au ujumbe wako. 5. Ufanye rahisi kuusoma. Ni vizuri kupiga chapa mahubiri yako ili uweze kusoma kwa urahisi wakati wa kuhubiri. Pia waweza kutoa vipeperushi na vijarida kwa wasikilizaji wako ili waweze kufuatilia zaidi ujmbe au somo lako. Zoezi. 1. Eleza maana ya mahubiri ya aya. 2.Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya aya. 3.Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya aya au kifungu licha ya yaliyotajwa katika kitabu hiki. 4. Andaa hotuba ya mahubiri ya aya na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako. II. MAHUBIRI YA KUFAFANUA. Mahubiri ya kufafanua ni aina ya mahubiri ambayo huhusisha kuchagua sehemu kubwa ya maandiko na kuichunguza kwa undani na kuifasiri na kugungua kweli zilizomo katika sehemu hiyo ya maandiko na kushirikisha mkutano au usharika wako. Mfano unaweza kuamua kupitia Injili yote ya Luka sura baada ya sura. Kuanzia sura ya kwanza, unatafuta kufasili na kuelezea maana na umuhimu wake mstari kwa mstari sura kwa sura mpaka umeimaliza yote. Waweza kushughulikia sura moja kila wiki, na baada ya wiki kadhaa utakuwa umemaliza kitabu chote. A.Faida ya mahubiri ya ufafanuzi. Hufanya mahubiri kuwa ya ki-Biblia. 1. Yesu alitumia aina hii ya mahubiri. Alichukua kifungu cha Agano la kale na kufasili maana yake kwa wasikilizaji wake. 2. Petro alitumia njia hii siku ya Pentekoste. 3. Stefano alitumia njia hii. Huwezesha waamini kuwa na msingi na uelewa mkubwa wa Biblia.Waamini huimalishwa na huwa na ufahamu mzuri na wa kina wa Neno la Mungu. Kwani kweli zote zilizomo katika kitabu kilichopitiwa tayari hufahamika vizuri kwa usharika wote. Huvuta kuimalishwa na Roho mtakatifu. Roho mtakatifu hulithibitisha neno lake kwa ishara na miujiza sawasawa na Kweli zote zilizofunuliwa katika kitabu husika. Humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia. Mahubiri ya kufafanua humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia kwani mhubiri huhubiri kile kilicho katika maandiko ya eneo husika. Mhubiri huwa anajikita katika mkutadha wa aya, sura na kitabu chote kwa ujumla. Hivyo kiini cha kitabu ndicho ambacho hubeba mahubiri yake yote. Mambo ya kuzingatia katika kutayarisha mahubiri ya kufafanua. I. Kwa umakini chagua kifungu cha maandiko kinachostahili. Hakikisha kwamba kifungu hicho kitahudumia uzima na uwezo wa wasikilizaji wako. 1. Usichague somo kwa sababu linakuvutia au kukupendeza. 2. Usichague somo ambalo litazaa machafuko, mgawanyiko na mashindano. 3. Jitahidi kufanyika njia ili Mungu akupitie ili aweze kuongea Neno lake kwa watu wake kwa kupitia wewe. 4. HIvyo basi unawajibika kutafuta kujua mawazo ya Mungu kuhusu watu wake ambao amekupa wajibu juu yao. 5. Huduma hii ni moja ya heshima kuu uliopewa lakini pia ni wajibu mkuu unaoogopesha sana. Hivyo basi unapaswa kuifanya kwa umakini wa hali ya juu. II.Tafuta ujumbe unaolingana na hali ya watu ya wakati ule. 1. Mungu kila mara huwa na ukweli wa sasa ambao hutaka kunena na watu wake. 2. Mungu hukusudia jambo maalum kwa kila kundi la waamini 3. Jifunze kujua kile Mungu anacho kwaajili ya kusanyiko kwa kila wakati. III. Jifunze sura ya kitabu kwa umakini. 1. Soma sura unayoshughulikia mara nyingi mpaka umeielewa vizuri. 2. Soma kwa uangalifu mstari hadi mstari. 3. Kila kunapokuwepo na uhusiano wa wazi kati ya kifungu hicho na kifungu kingine unapaswa kusoma kifungu hicho ili uweze kupata maana zaidi. Maandiko hufasiri maandiko. 4. Jenga usikivu kwa sauti ya Roho mtakatifu ili kupokea ufunuo toka kwake. Tumia vitabu vya rejea ili kupata msaada zaidi. Mfano. Itifaki ya Biblia, Kamusi ya Biblia, Biblia ya Tafsiri nyingine.Nk IV. Kusanya taarifa muhimu. Waweza kupata vitu vingine muhimu vya kuhusisha kwenye somo lako kwa kutumia mbinu ya maswali na majibu kama ifuatavyo. 1. Nimewahi kusikia au kusoma nini juu ya somo hili? 2. Roho mtakatifu amewahi kunionesha nini juu ya somo hili? 3. Nimewahi kuona nini chenye uhusiano na somo hili ? 4. Nimewahi kuwa na mawazo gani juu ya somo hili ? 5. Naweza kupata habari zaidi ju ya somo hili kwa nani au wapi ? 5. V. Tambua kiini cha somo lako. 1. Daima tafuta kugundua kiini cha sura unayoshughulikia. 2. Tafuta kujua kile Roho mtakatifu alikusudia kuwasilisha alipoivuvia sura hiyo. 3. Gundua undani wa somo hilo. 4. Baini kile Mungu anataka kusema na watu wake kupitia sura hiyo. VI.Kuwa na Lengo kamili. Lengo lako daima lapaswa kuendana kikamilifu na lengo la Mungu. 1. Hakikisha kwamba Umegundua kile Mungu anataka kutoa kupitia maadiko hayo na kisha jizamishe katika kile Mungu anataka kufanya. 2. Unapaswa kuhisi kile Mungu anachohisi Mungu humshirikisha mhubiri moyo wake na akili yake ili waweze kufanya kazi pamoja. Unapaswa kuchangamka. 3. Fanyika chombo cha Mungu cha kupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu wake. 4. Kumbuka hukuitwa kushiriki mawazo yako na watu bali kuwashirikisha watu mawazo ya Mungu. VII. Zungumza kulingana na ujuzi wako mwenyewe. 1. Usitoe nadharia toa uhai. Hubiri kile ulicho na uzoefu nacho.kile ambacho umekifanyia kazi . wapaswa kuwa mtu kwa kwanza kula matunda ya kazi yako. 2. Umeitwa kuwa barua Sio tu kwamba unataakiwa kuuhubiri ukweli bali pia unatakiwa kuufanyia mazoezi na kuuonesha kwa matendo. 3. Unapaswa kuwa mfano hai wa yote unayoyahubiri. VIII. Upe maana ujumbe wako. 1. Unawajibika kwa uwezo wako wote, kuhakikisha kwamba maana ya kweli na umuhimu wa maandiko unakuwa wazi na wakueleweka kwa wasikilizaji. 2. Daima jitahidi kuufanya ujumbe wako kuwa rahisi. 3. Hivi ndivyo Yesu alivyofanya Hii ilisababisha huduma yake kuwa na nguvu na mafanikio. 4. Alichukua mambo yaliyokuwa mafumbo na akayaweka rahisi sana. 5. Wahubiri wengine huyachukua masomo rahisi sana na kuyafanya mafumbo magumu sana kiasi cha kutoeleweka kwa wasikilizaji wake au kuelewa kidogo. IX.Fanya ujumbe wenye kutekelezeka. 1. Daima unapohubiri jitahidi kuonesha wazi wasikilizaji wako jinsi wanavyoweza kuutendea kazi ujumbe wako. 2. Jitahidi kutoa ushauri wa kimatendo kuhusu watu wanavyotakiwa kumwitikia Mungu kwa namna ya kufaa. 3. Husianisha mahubiri yako na maazimio yako kimatendo ambayo yaweza kuwafanya watu kuwa watendaji wa Neno na si wasikilizaji tu. Zoezi 1.Eleza maana ya mahubiri ya kufafanua. 2. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya kufafanua. 3. Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya kufafanua. 4. Chagua sura mojawapo ya injili ya Yohana na kisha andaa mahubiri ya kufafanua kutokana na sura hiyo na kisha hubiri kwa dakika kumi. III. MAHUBIRI JUU YA MAISHA YA WATU. A.Utangulizi Hii huhusu hadithi ya maisha ya watu. Kwa hiyo njia hii huhusisha mafunzo juu ya maisha ya watu mbalimbali tunaosoma habari zao katika Biblia. Kila hadithi ya mtu iliyoandikwa katika Biblia ina umuhimu kwetu. Maisha ya kila mhusika aliye kwenye Biblia yana mafunzo kadhaa ambayo twaweza kujifunza. Kila habari iliyoandikwa kwenye Biblia ipo kutufundisha kitu fulani ambacho ni cha thamani sana. 1Kor 10:1-11. Mhubiri huchagua mhusika mmojawapo wa wahusika walio katika Biblia na kujifunza kwa kina kila kitu kilichotoke katika maisha ya mhusika huyo, tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Pia mhubiri hutakiwa kujifunza kuhusu nasaba na mbari ya mhusika huyo ili aweze kufahamu vizuri vitu vilivyomjenga na kumkuza mhusika, kisha hutayarisha mahubiri juu ya mhusika huyo na kuhubri katika kusanyiko lake. Mafundisho ya wahusika wa Biblia ni ya kushangaza na ya kuvutia. Katkia aina hii ya mahubiri, mhubiri hupaswa kuchagua mhusika mmoja na kusoma habari zake zote zilizo kwenye Biblia na kisha huandikia kila wazo analolipata. Hapa mhubiri anapaswa kusoma kumbukumbuzote za mhusika katika Biblia. Baada ya kusoma kumbukumbumbu hizo unapaswa kuanza kuweka pamoja mawazo yote unayoyapata katika utaratibu wa miaka yaani jinsi matukio yalivyotokea ya mhusika huyo. B. Faida za mahubiri juu ya maisha ya watu. I.Hufunua ukweli wa maisha. Biblia imeeleza wazi maisha ya wahusika kama yalivyokuwa bila kuficha chochote. Imeeleza mafanikio yao na madhaifu yao. Ukweli wa maisha ya wahusika umewekwa wazi na kwa uhalisia. Wengi wa mashujaa wa Biblia wanahitilafu zao za kibinadamu.Twajua kuwa walikuwa wanadamu kama sisi na walikutana na majaribu kama sisi. Katika visa vyote vya historia kuna mtu mmoja tu mkamirifu ambae ni Yesu kristo pekee. Hata mashujaa wakubwa wa imani walikuwa na hitilafu zao. Hii inatupa kujua kwamba wao si tofauti na sisi. Ni mifano ya kujifunzia. Ni mifano na msada kwetu. Tunaweza kujifunza kutokana nayo kuliko ujuzi wetu wa uchungu. C. Mambo ya kuzingatia a) Jifunze kuzaliwa kwa huyo mtu. b) Tafakali hali na mazingira aliyolelewa. c) Angalia uhusiano wake na Mungu katika maisha yake. d) Angalia jinsi alivyo wajibika kuhusu uhusiano wake na Mungu. e) Baini vitu alivyojifunza kutokana na mahusiano yake na Mungu. f) Tathimini mafanikio yake. Jifunze vitu vilivyomfanya afanikiwe. g) Tazama maeneo aliyokosea kama yapo. Na jifunze vitu vilivyomfanya akosee. h) Toa hitimisho kile tunachoweza kujifunza kutokana na maisha ya mtu huyo. Mambo hayo yote yanavutia na ni yenye vitu vingi vya Kutufundisha ambayo twaweza kujifunza kutokana na watu hao. Tunaosoma habari za maisha yao katika Biblia. D. Hatua za kufuata katika kuandaa mahubiri juu ya maisha ya watu. I. Chagua mtu au msusika toka kwenye Biblia. Unapaswa kuanza na watu mashuhuri katika Biblia ambao habari zao ziko wazi kabisa, kama vile Ibrahimu,Musa,Samweli, Daudi, Yusufu, Debora, Miriamu, Mariamu, Dorkasi, Paulo, Petro. N.k. Hawa ni baadhi ya watu ambao matendo yao yamefanyika kuwa nuru katika historia ya ushusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Kuna mambo mengi sana ambayo twaweza kujifunza kutokana na maisha yao. Aina hii ya mahubiri ni nzuri sana, kujifunza toka kwa wacha Mungu wenzetu waliotutangulia katiki wito na huduma hii ni jambo la msingi sana. 1Kor 10.1-11. II. Chunguza maisha yake. Anza kwa kusoma hadithi inayoelezea kuzaliwa kwa mtu huyo. Tafuta maana ya jina lake. Kwani jina lina maana sana ki-Biblia. Angalia kwa umakini kusudi la Mungu katka maisha yake. Ili uweze kuvumbua vitu vingi unapaswa kujiuliza maswali yafuatayo: 1. Mungu alitaka kutekeleza nini kupitia mtu huyu ? 2. Je Mungu alifanya nini ili kusudi lake lijulikane kwa mtu huyu? 3. Mtu huyu aliitikia vipi Mungu alipomjulisha kusudi lake? 4. Tunaweza kujifunza nini kutokana na Mungu kuhusika katika maisha yake ? 5. Kuna tahadhari zozote ambazo tunapaswa kuzichukua ? 6. Je siri ya mafanikio yake ilikuwa nini ? 7. Je mwisho wa maisha yake ulikuwaje ? III. Chambua somo na kisha hubiri. Baada ya kujiuliza maswali hayo na kupata majibu utakuwa umepata vitu vingi ambavyo waweza kuvichambua kwa umakini na kuandaa somo kisha na kulihubiri somo hilo katika mpangilio na mtiririko Mzuri wa mawazo. Mwombe Roho mtakatifu akupe ufunuo zaidi unapokuwa ukihubiri somo lako na lifanye somo lako kuwa na uhalisia katika maisha ya sasa ya wasikilizaji. Zoezi 1.Eleza maana ya mahubiri ya wahusika au maisha ya watu. 2. Tengeneza orodha ya watu mashuhuri walio katika Biblia. Orodha hiyo ihusishe wanawake na wanaume. 3. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya wahusika. 4. Chagua mhusika mmoja wa kike au wa kiume na kisha andaa mahubiri kwa kumtumia mhusika huyo na kisha hubiri kwa dakika kumi. IV. MAHUBIRI YA MIFANO HALISI NA VIVULI. Huu ni ujuzi unaohusu kuweka wazi au kuchimbua na kuwasilisha ukweli uliojificha wa mifano mbalimbali katika Biblia. Mfano ni kitu, mtu au tukio ambalo kinabii ni ishara ya kitu au mtu fulani atakaetokea baadae. Inafanana au ni mfano wa Yule mtu au tukio. Katika matumizi ya Biblia ina maana ya mtu wa Bibli au tukio litakaloonesha kitu fulani kitakachotokea. Mfano mwanakondoo katika kitabu cha Kutoka ni mfano wa Bwana Yesu. Kila kitu kuhusu kondoo wa pasaka kiunabii kilikuwa na maana ya ukombozi wa wajibu ambao Bwana Yesu Kristo angetimiza.Yn 1:29. Mifano ya Biblia mara nyingi inaonekana kama kivuli(type) cha mambo yanayokuja baadae. Ebr 8:5,10:1. Siku takatifu pia katika agano la kale zilikuwa vivuli juu ya mambo ambayo yalikuwa yanakuja. Kol 2:17. Hizo siku takatifu hazikukamilika zenyewe sehemu ya kusudi la kutimizwa kwake ilikuwa ni kutanguliza sura ya kinabii ya vitu ambavyo vilikuwa bado vinakuja. Kanuni za kutumia. a. Unapojaribu kwa mara ya kwanza kufundisha kwa kutumia mifano ya kwenye Biblia, zingatia misingi ifuatayo. I. Tumia mifano rahisi zaidi. Anza na mifano rahisi ambayo maana yake iko wazi. II.Endelea na tafsiri ya wazi. Usijaribu kufasiri kila kitu.Elezea ukweli wote kama ulivyo na wala si kutafuta kila kipengele chake na kukielezea kwa undani. III. Usitumie maneno makavu. Usitumie mifano ya kufundishia kama kanuni. IV.Sisitiza ukweli wa msingi. Usitumie nafai uliyonayo kwa kutoa mifano ya kufundishia. Mifano itumike kusisitiza mafundisho na si kutumia kama chanzo cha ukweli. V. Uwe tayari kusahihishwa. Uwe tayari kusahihishwa na kukosolewa na wale waliokomaa kuliko wewe ili uweze kujifunza zaidi. 4. Kuelezea kusudi. Ni njia ambayo kwayo mhubiri hupanua maana ya ukweli ulio katika kifungu maalum cha maandiko. Unatafuta namana ya kuuweka wazi ukweli ambao umejificha ndani ya kifungu. Hii njia nzuri sana ya kufundishia kusudi lote la ki-Mungu. Mdo 20:27. Zoezi 1. Eleza maana ya vivuli na mifano.(Types). 2. Taja hatua za kufuata katika kutayarisha na kuhubiri mahubiri ya mifano na vivuli. 3. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya mifano na vivuli. 4. Tayarisha mahubiri ya mifano na vivuli na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako. V. MAHUBIRI YA MADA. Aina hii ya mahubiri hukusudia kutoa kiini maalum kwa hadhira.Mhubiri huchagua somo fulani kisha huchunguza kila kitu ambacho Biblia inasema juu ya somo hilo. Baada ya kuchunguza na kuchambua, kweli hizo huandikwa katika mapngilio wa somo. Mhubiri hupitia vifungu mbalimbali vya maandiko vinavyohusu somo hilo. Aina hii ya mahubiri huhitaji maandalizi ya muda mrefu na utulivu mwingi. Pia huwasilishwa katika mfululizo wa vipindi kadhaa na si kimoja, kwa sababu ni vigumu kupitia kweli zote zilizo katika somo kwa kipindi kimoja tu. Mfano wa mada za kuhubiri. 1. Upendo wa ki-Mungu 2. Ubatizo wa Roho mtakatifu 3. Maombi ya kufunga. 4. Nguvu ya usaidizi. 5. Vita vya kiroho. 6. Kutambua Ulimwengu wa roho. 7. Kutembea katika mamlaka. 8. Nguvu ya madhabahu. 9. Kushughulikia majira na nyakati. 10. Kutii mamlaka. Mambo ya kuzingatia katika mahubiri ya mada. 1. Uwe na ufahamu wa kutosha juu ya somo husika. 2. Fanya maandalizi ya mudamrefu na ya kina 3. Unapaswa kuwa na lengo mahususi la mahubiri yako. 4. Gawa somo katika vipengele vidogovidogo. 5. Kila kipengele lazima kiwe na maandiko yanayokithibitisha na kukielezea 6. Andiko liendane na dondoo unayoitoa. Zoezi. Somo hili lipo kimatendo zaidi. Kila mwanafunzi ashiriki katika kufanya mazoezi ya kuandaa mahubiri na ahubiri katika dakika zilizopendekezwa au mwalimu atakazopanga kulingana na muda uliopo. Mwalimu anatakiwa kusimamia na kusahihisha kazi za wanafunzi na kutoa marekebisho katika maeneo ambayo wanafunzi hawajafanya vizuri. 1.Andaa Ujumbe kwa kutumia aina ya mahubi ya mada na kisha hubiri mkutano kwa dakikika kumi. Chagua mada yoyote. 2.Taja ubora na udhaifu wa mahubiri ya mada. 3. Taja mambo mengine matano muhimu ya kuzingatia katika kuandaa mahubiri ya mada. 4. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri ya mada na mahubiri ya kufafanua. VI.MAHUBIRI YA MATUKIO. Mahubiri ya matukio ni kipengele katika mahubiri ya maada, lakini kutokana na umhuhimu wake tumekitenga na kukielezea peke yake. Mahubiri haya ni mahubiri ambayo huandaliwa kutokana na tukio lilipo au ambalo litafanyika katika kipndi fulani. Kiini cha mahubiri haya huwa ni tukio ambalo linafanyika katika ibada hiyo.Mfano wa matukio hayo ni Tukio la, 1. Kusimikwa kwa uongozi wa kanisa. 2. Ndoa au kumuaga bnti. 3. Kubariki watoto. 4. Ushirika mtakatifu 5. Ubatizo 6. Kuweka wakfu vitu mbalimbali. 7. Kuhitimu mafunzo.(graduation) 8. Msiba na mazishi. 9. Sikukuu mfano Pasaka, mwaka mpya, N.k Mambo ya kuzingatia 1. Mahubiri haya yanapaswa kuendana na tukio husika. 2. Mhubiri anatakiwa kufahamu ratiba nzima ya tukio hilo au shughuli hiyo. 3. Mhubiri ahubiri kulingana na tukio husika. 4. Mhubiri aepuke kutumia muda mwingi katika mahubiri. 5. Mhubiri ahubiri kwa lugha itakayoeleweka na kusanyiko lote na lugha yapaswa kuwa rahisi. 6. Mahubiri yapaswa kugusa kusanyiko lote. 7. Mhubiri anapaswa kuhubiri kwa upendo. 8. Mhubiri azingatie ratiba ya tukio. ZOEZI. 1. Chagua tukio mojawapo na kisha andaa mahubiri juu ya tukio hilo na hubiri kwa dakika 10 .2. Taja mabo mengine kumi ya kuzingatia katika mahubiri ya matukio. 3.Eleza ubora na udhaifu wa mahubiri ya matukio. MADA YA NNE MHUBIRI. Malengo ya mada. • Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi anataweza. • Kueleza maana ya mhubiri kwa mitazamo mbalimbali. • Kuelza wasifu wa mhubiri. • Kueleza vidokezo mbalimbali kuhusu mhubiri. A. Utangulizi. Mahubiri yana mwanzo wake katika Agano la kale. Wakati manabii walipotangaza neno la Mungu kwa watu wa kale. Manabii walikuwa wahubiri wa kwanza katika agano la kale. Mungu ameamua kuwachagua na kuwatumia watu wa kawaida kulitangaza Neno lake.Amewachagua wanawake na wanaume kuwa vyombo vya kulitangaza neno lake kupitia huduma ya kuhubiri. Ufafanuzi Neno mhubiri (kwa kigiriki kerux) limetumika mara kadhaa katika agano jipya ambapo humaanisha kutangaza. (Rumi 10:14, 1Tim 2:7, 2Tim 1:11, 2Pet 2:5. Unapolitazama neno hili (mhubiri) halijikiti na kuishia kwenye huduma moja au huduma fulani tu bali linahusisha zile huduma zote tano za uongozi wa kanisa. Ikijumuisha mitume, manabii waijilisti,wachungaji na waalimu. Pia linajumuisha kila mtu atangazae neno la Mungu. Hata kama hana mojawapo ya zile huduma tano za uongozi. Ingawa hudma zote hizi zinawasifu wake kila moja lakini zote zaangukia katika neno moja “Mhubiri”. Inavutia kutambua kwamba neno la Kigiriki lililotafsiriwa kama mhubiri linaelezea mtu anaeongea kwa mamlaka , anaewasilisha ujumbe bila kikwazo au kizuizi chochote. Hii hudhihirisha mamlaka iliyo juu ya mhubiri. Mhubiri ni mtu yeyote anayehubiri Injili. • Mhubiri ni mtu anayetumiwa na Roho mtakatifu katika kuwasilisha kweli za ki-Mungu kwa njia ya hotuba. • Mhubiri ni mtangaza ujumbe wa Mungu. • Yeye ni msemaji wa Mungu. Husimama katika nafasi ya Mungu na kuzungumza kwa niaba yake Mungu. Hivyo ni lazima mhubiri awa na sifa zinazostahili ambazo zitamfanya kuwa na mamlaka. B.Sifa za mhubiri. Mhubiri ni lazima awe na sifa stahilifu ambazo zitamfanya awe na mamlaka na thabiti katika wito na huduma yake. Badhi ya sifa hizo zimeorodheshwa hapa chini. 1. Awe ameokoka (Amezaliwa mara ya pili). 2. Awe amejazwa Roho mtakatifu. 3. Awe na wito halisi (Wito ulio wazi na wenye ushahidi). 4. Ajazwe na Neno la Kristo ndani yake Kol 3:16. 5. Awe mtu wa maombi. 6. Awe mwadilifu.( Mkweli na mchaji Mungu na mwenye kuchukia mapatato ya udhalimu ) 7. Awe na nidhamu. 8. Aishi kulingana na wito wake. 9. Asiwe mvivu. 10. Awe na baba wa kiroho. Kuna tofauti kubwa kati ya hotuba na ujumbe.mtu anaweza kujifunza jinsi ya kuandaa hotuba kupitia masomo ya Homiletics lakini Mtu anapaswa kuwa na ushirika na Mungu ili aweze C. Kujihusisha binafsi katika kuhubiri. 1. Unapaswa kuwa kawaida. Unatakiwa kutulia na kuwa vile ulivyo. Mugu hutaka kutumia utu wa kila Mhubiri katika kuwasilisha Neno lake. Unatakiwa kujikubali hivyohivyo ulivyo. Mungu anapendezwa nawe na ndiyo maana amekuita hivyo ulivyo. Usijichambue sana. 2. Kuwa wa kipekee. Unatakiwa kuutayarisha ujumbe wako na kuuwasilisha kwa njia ya kipekee ili uweze kuleta matokeo ya kipekee. Unapasa kutumia utu wako wa kipekee Mungu aliokupa na kumwacha Mungu atumie utu na maisha yako kwa njia maalum ya kipekee anayotaka yeye. 3. Kuwa rahisi. Unapokuwa ndiyo unaanza kuhubiri au kusimama mimbarini kwa mara ya kwanza unatakiwa usijaribu kutumia ufasaha au kuingia ndani mno katika kuhubiri. Huhitaji kuwavuta watu. Upo pale kwa lengo la kuwahudumia na si kuwapendeza. 4. Kuwa huru. Unatakiwa kuwa huru unapohubiri na ujifunze kujizoeza hali mbalimbali. Ufanye mtindo wako wa mawasiliano utiririke kawaida na kwa uhuru. Kila kusanyiko utakalo hubiri linatofautiana na lingine, hivyo unapaswa kujizoeza hali mbalimbali. Mungu huwa na lengo maalumu analotaka kufanikisha katika kila ibada na mhubiri ndiyo ufunguo muhimu katika kutekeleza hili. Kuwa huru na msikivu kwa Roho mtakatifu.Roho mtakatifu anaweza kufanya hali za jinsi mbalimbali katika kila ibada.Wasikilizaji wako wakati mwingine waweza kuwa wachangamfu na wakati mwingine wakimya na wanyenyekevu. 5. Tambua njia ambayo Mungu anapitia na utembee nae. 6. Dhihilisha mamlaka..Hakikisha Kuna madhihirisho ya nguvu za Mungu katika kila ibada unayohubiri. Hakikisha Bwana anakithibitisha kila unachokihubiri kwa ishara na maajabu. Hubiri kwa uthibitisho D. Zana za mhubiri. Kuna vitu kadhaa ambavyo ni muhimu kwa mhubiri yoyote . Bila vitu hivo kazi ya Kuhubiri itakuwa haijafanikiwa au kufika lengo kwani wasikilizaji watakuwa wameachwa njiani. Baadhi ya zana hizo ni: I. Maono. Kila mhubiri nilazima awe na maono katika huduma yake na wito wake. Wazo la kile ambacho huduma yako itafanikisha kwa Mungu. Maono ni picha au taswira juu ya kile unachohitaji kukifikia katika huduma yako. Kumbuka kwamba bila maono watu huangamia Mit 29:18. Ni maono pekee yatakayokuweka salama. Usipokuwa na ufahamu wa kuhusu kusudi la Mungu alilonalo kwaajili yako ,waweza kulemewa na kuishia n jiani na kushindwa kufikia lengo la –ki-Mungu ulilochaguliwa kwalo. II.Msamiati. Msmiati ni jumla ya maneno yaliyo katika lugha fulani. Msamiati wamhubiri hujumuisha maneno yote anayoyajua na kuyazoea kuyatamka. Maneno ni dhana ambayo mhubiri hutumia katika kutimiza wito wake. Muhubiri anatakiwa kuwa mahili wa lugha. Jifunze msamiati mbalimbali na matumizi yake.Silaha yetu kuu ni maneno katika kazi ya kuhubiri. Maneno huundwa na msamiati. Soma vitabu mbalimbali ili uweze kujitajirisha na msamiati. Unapokutana na neno usilolifahamu lichunguze na kutafutamaana yake na matumizi yake. Pia mhubiri anatakiwa afahamu kutumia msamiati mbalimbali katika kazi yake ya kuhubiri. Tambua matumizi ya Lugha kulingana na mahali. Jifunze misimu, Rejesta na misemo mbalimbali inayotumika katika Lugha husika. Hii itakusaidia unapohubiri uweze kuwagusa watu wote waliopo katika eneo hilo. Mhubiri ni lazima ajifunze namna ya kutamka maneno sahihi. Jifunze kutumia lafuzi vizuri na kuepuka athali za lugha mama katika Lugha unayotumia kuhubiri. Kuwa na lafuzi nzuri na kuongea lugha kwa ufasaha hukupa kukubalika kwa wasikilizaji wako na kupewa usikivu. Tumia Lugha inayoeleweka na wasililizaji wako, lakini lugha hiyo yapaswa kuwa sanifu au fasaha III. Sauti. Sauti ndiyo chombo kikuu mhubiri anachotumia katika kuhubiri. Ni lazima mhubiri kujifunza mitindo mbalimbali ya sauti na namna ya kuitumia sauti yake. Jifunze matumizi ya sauti katika mahubiri yako. Sauti yako inapaswa kusikika na wasikilizaji wako lakini haipaswi kuwa kubwa sana kiasi cha kuwaumiza. Fahamu mahali pa kutumia asuti kidogo na mahali pa kuongeza sauti. Hubiri kwa mitindo mbalimbali ya sauti. Zingatia kiimbo, toni na kidatu unapohubiri. E. Kanuni za Kuhubiri Katika kipengere hiki tutaajadili baadhi ya kanuni chache za kuzingaita katika mahubiri ya hadharani. Mhubiri anapswa kufuata na kuzingatia kanuni hizi ili aweze kufanikisha lengo la mahubiri 1. Kuvuta hewa. Kuvutahewa sahihi ni muhimu kwa mhubiri. • Vuta hewa nyingi kiasi cha kufika mapafuni. • Jizoeze kujaza hewa kifuani na kwenye mapafu. • Izuie na kisha itoe nje polepole.Dhibiti utoaji wa hewa. Iache hewa itoke chini ya mapafu kupitia sanduku la sauti na kugusa ukuta wa juu wa mdomo. • Jifunze jinsi ya kupumua ili usiishiwe pumzi wakati wa kuhubiri. 2. Utamkaji mzuri wa maneno. Jitahidi kutamka maneno vizuri na waziwazi. Hakikisha kila neno unalolitamka linasikika vizuri kwa wasikilizaji wako. Usilete kikwazo kwa wasikilizaji wako kwa kutosikika vizuri. 3. Ubadilishaji wa sauti. Hii inahusu kuifanya sauti kuwa nene au nyembamba. Sauti ya kila mwanadamu inahali mbalimbali. Jitahidi kutumia aina mbalimbali za sauti. Ukitumia aina moja ya sauti yaweza kuwachosha wasikilizaji wako. Tambua maeneo unayotakiwa kuongea kwa sauti ya chini na sauti ya juu. Endeleza viwango tofauti vya sauti yako. Ubadilishaji wa ukubwa wa sauti waweza kusisitiza kipengere fulani muhimu. Baadhi ya wahubiri huona ni muhimu sana kuhubiri kwa sauti kubwa sana kiasi chakuumiza masikio ya wasikilizaji . Jaribu kuepuka hili. Iwapo ujumbe wako wote utawasilishwa kwa sauti kubwa au ya juu itakuwa vigumu kusisitiza jambo maalum katika zile sehemu ambazo ni za maana zaidi. 4. Kasi ya kuongea. Kasi unayotumia kuongea ni muhimu sana katika mahubiri. Baadhi ya wahubiri huhubiri kwa kasi moja tu . hii si nzuri, pia yaweza kuwachosha wasikilizaji. Sehemu kubwa ya ujumbe wako yapaswa kuwasilishwa kwa mwendo na kasi ya kawaida ya mazungumzo. Katika maeneo mbalimbali ni lazima kuongeza au kupunguza mwendo ilikuleta tofauti na msisitizo zaidi katika mahubiri yako. 5. Kupumzika kidogo. Usiongee mfululizo bila kuwa na vituo. Kupumzika kidogo wakati wa kuongea au kuhubiri ni muhimu pia kwaweza kuongeza msisitizo kwenye maeneo ya muhimu. Kuongea mfululizo kwaweza kusababisha wasikilizaji washindwe kusharabu mambo ya muhimu katika akili zao. Usipitie ujumbe kwa kukimbia na kuongea kwa haraka bila kuvuta pumzi. Hadhira wanahitaji muda wa kufikiri na kuchambua kile ulichosema, Hii inasaidia sana kusharabu ukweli wa ujumbe wako. Unahitaji kuzifahamisha akili pamoja na kuzichangamsha hisia za hadhira. Kama ukihubiri kwa haraka tu bila kupumzika utawaacha hadhira wako nyuma. 6. Kurudia. Kurudia sehemu za msingi wakati unahubiri ni jambo la msingi sana. Inasaidia kusisitiza vipengere na kushindilia kwenye akili za wasikilizaji. Unatakiwa kukielezea kipengere kwa njia mbalimbali. Usisite kurudia eneo unalohisi wasikilizaji wako hawajakuelewa vizuri. F.Vidokezo muhimu kwa mhubiri. 1. Uwe vile ulivyo.Usijaribu kutokeza sura ambayo si ya kweli. Kuwa vile ulivyo ndiyo njia pekee inayoweza kukufanya utulie.usijaribu kumwiga mhubiri mwingine yeyote ukifanya hivi itakusababishia kutoaminika kwa hadhira wako.Jitahidi kuwa mhubiri bora na si kuwa mhubiri mkuu. 2. Usijenge sauti ya kidini. Baadhi ya wahubiri wamejiundia sauti za mimbarini ambazo ni tofauti na sauti zao za kawaida.Hii huleta kutokuaminika na kuonesha kana kwamba unamwiga mtu mwingine. Jizoeze kuhubiri kwa kutumia sauti ya kawaida na unayotumia katika mawasiliano katika maisha ya kila siku. Hii huonesha ukweli na uaminifu katika mahubiri. 3. Usiongee kwa sauti ndogo mno. Hakikisha kwamba kila mmoja katika mkutano wako anakusikiliza vema. Usifanye wachoke kwa sababu ya kutokukusikia vizuri. Ikibidi uliza je kila mmoja ananisikia vizuri ? Si vizuri kuendelea kuhubiri na hali kuna baadhi ya watu hawakusikilizi. 4. Usipige kelele. Jitahidi kuongea kwa sauti ya kawaida ya maongezi ambayo inaweza kuongezwa kiasi kufuatana na wingi wa makutano na kama huna au una vyombo vya kupazia sauti. Sauti iongezwa kulingana wingi wa hadhira. 5. Kumbuka kubadili kasi na upeo wa sauti ya mahubiri kukwepa kuchosha hadhira. 6. Ufanye mkutano ukukubali. Pata matumaini ya hadhira.Hakikisha mkutano wako unakukubali.. Kama mkutano wako hawakukubali nidhahiri kabisa kwamba hawataupokea ujumbe wako. 7. Vaa vizuri. Ni jambo la maana sana kwa mhubiri kuvaa mavazi ya heshima na safi. Namna ulivyo vaa yaweza kuharibu ujumbe wako.Hakikisha uvaaji wako hauvurugi ujumbe wako. Vaa kulingana na tamaduni za taifa husika. 8. Jifunze kusimama vizuri. Ni vizuri sana kusimama wakati unazungumza au kuhubiri. Simama vizuri kwa miguu yote miwili.. Simama wima ukitazamana na hadhira wako. Usipende kuegemea kitu chochote. Kama kuna mimbari itumie kuwekea Biblia na zana zako za kuhubiria. Kusimama wima kutakusadia katika kuvuta hewa. Watazame hadhira wako wakati wote unapohubiri. Hubiri kwa kumgusa kila mtu. Kila mtu ajione kwamba unaongea na yeye binafsi. 9. Jifunze kutembea wakati unahubiri. Usisimame mahali pamoja kana kwamba umefungwa.Jizoeze kutembeatembea wakati unahubiri. Mwili wako unaleta ujumbe sawaswa na sauti yako.Tumia ishara wakati unahubiri lakini epuka ishara sisizo na umuhimu. Kama unaeleza juu ya kitu fulani ni kawaida kuelezea jambo hilo kwa mikono yako. Ishara za namna hiyo zinapaswa kutokea zenyewe kiasili bila kuzilazimisha. 10. Endeleza uhuisano na hadhira. Macho ya mhubiri huelezea ujumbe pia. Usiangalie hewani au juu ya vichwa vya watu. Waangalie watu unaowahubiri moja kwa moja. Kila mmoja atambue kwamba unamwangalia yeye binafsi. 11. Jifunze kutawala mkutano. Hakikisha unatawala kusanyiko. Watu wote wako pale kukusikiliza wewe hakikisha kila mmoja anakusikia. Zungukia watu wako nakuwashitua wanao lala au kusinzia. Tafuta namna itakayosababisha watu wote kukusiliza kwa makini. 12. Omba upako wa Roho mtakatifu. Mwombe Mungu akupake mafuta daima. Hakikisha utendaji wa Roho mtakatifu upo katika mahubiri yako. F. Matumizi ya muda katika mahubiri. Ni lazima mhubiri ajifunze matumizi sahihi ya muda katika mahubiri. Jambo hili ni la muhimu sana na lisipozingatiwa huweza kuvuruga kazi nzima ya kuhubiri. Ni lazima kuamua muda utako tumia kuhubiri kabla ya kupanda mimbarini. Utafiti kule Marekani umeonesha kwamba watu huanza kupoteza usikivu wao baada ya dakika ishirini tu za mahubiri. Waweza usikubaliane na matokeo ya utafiti huo lakini unatakiwa kukumbuka kwamba akili ya mwanadamu inakiwango cha kuelwa na muda wa kuelewa. Muda ukizidi kila kinachoongelewa au kuhubiriwa huwa hakisharabiwi kwani akili hufikia upeo wa kuelewa na kushika mambo. Upako wa Roho Mtakatifu huhuisha akili za wasikilizaji kwa kiwango fulani lakini mhubiri aepuke kuwachosha wasikilizaji. Ni vizuri sana kumaliza ujumbe wako wakati watu wanatamani uendelee na ni vibaya sana kumaliza ujumbe wako wakati watu wanataka umalize. Jitahidi kuzingatia muda katika kazi yako ya kuhubiri. Kwa kawaida ujumbe unapaswa kutumia dakika arobaini na tano. Utangulizi uwe na dakika tatu hadi tano, Kiini kiwe na dakika ishirini na tanno hadi therathini. Hitimisho liwe na kakika tatu hadi tano. Ujumbe wote usizidi dakika arobaini Vinginevyo utawaacha wasikilizaji wako. Ukitaka kuhubiri kwa muda mrefu hakikisha ujumbe wako unauvuvio mwingi. Spurgeon alisema” tumia muda mwingi katika matayarisho ili uweze kutumia muda mchache katika kuhubiri” Kutumia muda mrefu katika kuhubiri hakukufanyi ueleweke zaidi wala hakufanikishi zaidi lengo la kuhubiri. Tambua cha kusema. Kiseme na kisha maliza. Unapokuwa umealikwa na mhubiri mwingine kuhubiri unapaswa kumuuliza muda ambao yeye hutumia katika kuhubiri na muda wa kumaliza mahubiri. Unapokuwa unahubiri zingati muda ulioelekezwa na mwenyeji wako na uwezo wa kuelewa wa wasikilizaji wako. Mgeni akija kanisani kwako kama hukumwandaa kuhubiri kabla si vizuri kumpa madhabahu ili ahubiri. Kwani kuhubiri ni kazi nyeti sana na inahitaji maandalizi ya kutosha. Maelezo haya hayazuii mwongozo na maelekezo ya Roho mtakatifu. Lakini ni vizuri kumwandaa mhubiri mapema ili awe na muda wa kuafanya maandalizi. Usiwashitukize watu kuhubiri. Ni lazima uwe na heshima kwa kazi hii kwani Mungu mwenyewe anaiheshimu sana. Usihubiri ujmube au somo ambalo mwenyeji wako hakubaliani nalo. Kama kuna ulazima fanya nae mazungumzo kabla ya kuhubiri au tafuta namna utakayotumia kuhubiri na kufanya akubaliane na kile unachohubiri. Jambo hili ni muhimu sana na linapaswa kuzingatiwa. Mahubiri na mazingira. Mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyopatikana na kuzunguka eneo fulani. Mazingira ni muhimu sana katika kufanikisha kazi ya kuhubiri. Ni lazima mazingira yawe safi hasa ikiwa mahubri yatafanywa katika eneo fulani maalum. Mfano kanisani, uanjani au eneo lolote rasmi. Kuna baadhi ya mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa. Baadhi ya mambo hayo yameorodheshwa hapa chini. 1. Watu wanaokuja kwa kuchelewa wakae katika viti vya nyuma. 2. Mimbari inapaswa kuwekwa mahali sahihi panapoonekana na watu wote bila shida. 3. Lango la kuingilia lapaswa kuwa mahali sahihi. 4. Akina mamawenye watoto wadogo wakae eno maalumu. 5. Watoto wanapaswakutengewa sehemu yao ya kukaa kama hakuna kanisa la watoto. 6. Mwanga na hewa ya kutosha ni kitu muhimu sana katka eneo lolote. G. Jaribu kuu la Mhubiri. Wahubiri wengi hujisulisha na kutafuta chakula kwajili ya watu wengine na kujisahau wenyewe. Huu ni mtego mkubwa katika kazi ya kuhubiri na ni moja ya hatari za huduma. Wakati mwingine mhubiri aweza kujishughulisha sana na kutafuta haki za kiroho za kundi lake na kwa masikitiko makubwa anasahau zile za kwake mwenyewe. Hii ni moja ya sababu kuu zinazomfanya mhubiri kushindwa. Sulemani anasema katika kitabu cha Wimbo ulio bora “”’ Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu bali shamba langu mwenyewe sikulilinda” Mhubiri ni lazima ajali kwanzai maisha yake mwenyewe ya kiroho. Mhubiri anapaswa kulipa neno la Mungu nafasi ya kuchipua ndani ya moyo na roho yake. Aliache likue kwa nguvu katika maisha na ujuzi wake. Halafu atakapohubiri atahudumu kutokana na ujuzi. Hataongea kamwe kama mwenye nadharia bali atashirikisha vitu ambavyo yeye mwenyewe anavielewa kikamilifu na ana ujuzi navyo. Paulo anasema hivi. “Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza kupata fungu la matunda”. ( 2Tim 2:6 ). Hii inatufundisha kwamba unachopanda na kuvuna ( kiroho) yapasa ule (ujuzi)- kabla ya kulisha wengine. Huwezi kulisha wengine kile ambacho wewe mweyewe hujakila kwanza. Huwezi kujaribu kuongoza wengine katika njia na mapito ambayo wewe mwenyewe hujapitia. Jinsi Neno la Mungu linavyokuwa dhahiri katika maneno yako ndivyo wewe unafanyika ujumbe toka kwa Mungu. Hutakuwa mtu anaye kariri somo tu bali mtu ambaye uhai wake binafsi na mtindo wake wa maisha huhudumia uhai, Baraka na nguvu kwa wale wanaomfahamu na kumsikia. I.Hitimisho. Mahubiri mazuri hayaji kirahisi wala hayatokei tu. Ni matokeo ya vitu vingi. Kama tulivyotazama huko nyuma kwamba mahubiri huanza na wito wa mhubiri na wasifu wake.Pia huhusisha maandalizi ya kutosha kwa kuomba na kusoma kwa bidii. Kilele cha mahubiri ni katika kuwasilisha ujumbe. Ujumbe hauwi ujumbe mpaka umewasilishwa. Ujumbe ulioandaliwa vema utakuwa ujumbe wa kiungu pale Roho mtakatifu atakpoupaka mafuta. Mahubi mazuri daima yataleta matokeo mazuri. Mahubiri mazuri dama yatamtukuza Mungu na si mhubiri au mtu mwingine yeyote. Yatawaongozawatu msalabani na kuwafanya kuwa wanafunzi. Angalizo.Mhubiri hapaswi kutwaa utukufu kwa namna yoyote ile katika kila inachotokea katika kazi yake ya kuhubiri. Daima anapaswa kumpa Mungu heshima na utukufu kwa kila kinachotokea. HOMILETICS. MADA YA KWANZA. MAHUBIRI. Malengo ya mada. Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi aweze.  Kueleza maana yamahubiri.  Kueleza maana ya kuhubiri.  Kueleza wito wa kuhubiri ulivyo.  Kueleza umuhimu wa kujifunza homiletics. A. UTANGULIZI Katika kozi hii tutashughulikia mojawapo ya kazi kuu ya kanisa. Mojawapo ya wajibu mkuu ambao umewekwa mikononi mwa kanisa ni kuhubiri ujumbe wa Mungu yaani Injili. 1Kor 1:21 a) Ni amri iliyo wazi toka kwa Bwana Yesu kwa wafuasi wake. Mk 16:15. “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe”. b) Kuhubiri ni mojawapo ya kazi ya thamani sana ambayo Mungu ametupa. Kuwa msemaji wa Mungu, yaani Mjumbe wa Kristo. 2Kor 5:20. c) Kuhubiri ni wajibu mkuu. Rumi 10:14-15. d) K wa njia ya mahubiri Mungu alichagua kujidhihirisha mwenyewe kwa mwanadamu. B. MAANA YA MAHUBIRI. Neno mahubiri linatokana na maneno mawili ya kigiriki ambayo ni homileo na homilia yenye maana ya ‘kuwa pamoja na, kuongea na kuwasiliana. a) Homily pia humaanisha ujumbe au hotuba. b) Elimu inayohusu namna ya kuhubiri huitwa Homileticts. c) Homiletics ni ustadi wa kuhutubia au kuhubiri. d) Mtaalamu wa elimu ya kuhubiri huitwa Homilist e) Homiletics huhusisha kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri au kutunga hotuba. f) Mahubiri huhusu kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri masomo ya Biblia. g) Mahubiri ni ujuzi wa kuhubiri. h) Ni elimu au taaluma inayohusu kuhubiri Neno la Mungu. i) Ni elimu inayohusu namna ya kuhubiri.{ somo juu ya kila kitu kinachohusiana na kuhubiri}. j) Kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu. Mungu hutumia watu wake aliowachagua kuhubiri ujumbe wake. k) Ujumbe unapaswa kuwa ujumbe wa Mungu Kitu kingine chochote si mahubiri ila ni maoni na falsafa za kibinadamu tu. l) Kuhubiri ni lazima kuwe ni kutangaza binafsi na si kusoma au kuandika Dr. Martyn Lolyoyd Jones alisema “ Wahubiri huzaliwa na hawafanywi kamwe. Kamwe hutamfundisha mtu kuwa mhubiri kama yeye si muhubiri. Lakini mhubiri wa kuzaliwa unaweza kumsaidia na kumwendeleza akawa mhubiri bora kwa njia ya mafunzo” 1. -Mhubiri si chanzo cha ujumbe.Mungu ndiye chanzo cha ujumbe na mhubiri ni bomba au mfereji ambako Mungu hupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu aliowakusudia. Ujumbe wa Mugu hutiririka kupitia utu wa mhubiri. 2. -Ujumbe unapaswa kutiririka kwa uhuru toka kwenye chanzo chake (Mungu) kwenda kwa wakusudiwa yaani hadhira au wasikilizaji. 3. Mahubiri ni zao la mambo mawili ambayo ni Mungu na mhubiri. Mahubiri mazuri huzaliwa kutokana na ushirikiano mzuri (umoja) na ushirika mzuri kati ya Mungu na mhubiri. Hivyo kuna vipengele viwili vya wazi katika mahubiri cha kwanza ni kile cha ki Mungu na cha pili ni kile cha kibinadamu. Kwa sababu ya wito wake mkuu mhubiri anapaswa kuwa mwaminifu na awe na ufahamu wa kutosha juu ya Neno la Mungu. 4. Biblia ndiyo asili ya ujumbe. • Ujumbe wowote unaohubiri nilazima utokane na Biblia nje ya Biblia si mahubiri bali ni masimulizi tu. • Kwa nini Biblia peke yake? Kwanini si kitu kingine toka vitabu vizuri vya kikristoau toka magazeti au maelezo na masimulizi ya mtu maarufu na aliye mkuu. • Biblia ni maoni ya Mungu kwa kila jambo lolote lililotolewa. Mhubiri aliye kuwa amekosolewa kwaajili ya hotuba yake alisema “hata mimi sikuipenda pia lakini haikuwa maneno yangu na nilikuwa sitoi mawazo yangu bali kile Mungu amesema katika Neno lake. Kwahiyo nilitoa mawazo ya Mungu na si yangu. • Kuhubiri hotuba ya ki-Biblia humpa mhubiri ujasiri mkubwa. Kutangaza kwa nguvu; Biblia inasema …………………. Mungu anasema………………… • Neno la Mungu lina nguvu. Wab 4:12. • Neno la Mungu ni kama mbegu.sBiblia hukutana na kila hitajila mwanadamuna matatizo yake yote yanayomkabili. • Inampendeza Mungu- Neno lake lililovuviwa amri yake ilikuwa wazi • “Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi na muwafundishe kuyashika yote niliyowaamuru” • Roho mtakatifu hulithibitisha Neno la Mungu. C. MAANA YA KUHUBIRI. Mahubiri yana lengo mahususi katika mpango wa Mungu. Ni njia ambayo kwayo Mungu ameamua kuwafikia waliopotea dhambini na kuwaimarisha waamini.Kkwa sababu mahubiri ni njia ya Mungu kuwafikia wanadamu, tutatazama maana ya kuhubiri kwa mitazamo mbalimbali kama ilivyo ainishwa na wataalamu wa masomo ya homiletics. 1.Kuhubiri ni kuielezea imani. Mojawapo ya malengo ya mahubiri ni kuelezea au kutangaza kweli za maandiko matakatifu. Kila hotuba au ujumbe wapaswa kuwasilisha kweli za maandiko kwa njia itakayowezesha hadhira kupata uelewa zaidi juu ya maandiko matakatifu. Kuhubiri husababisha imani kuumbika kwa wasikilizaji wako. Hubiri kwa kukuza imani na kuielezea imani katika mwana wa Mungu Yesu Kristo. II. Kuhubiri ni kuitetea imani. Haitoshi kuelezea ukweli wa Mungu bali tunapaswa kuutetea. Shetani, ulimwengu na maadui wa imani huvamia na kupotosha kweli za neno la Mungu. Hivyo ni lazima kwa mhubiri yoyote kuwa tayari kuitete imani ya kweli kwa njia ya kuhubiri kweli za ki-Biblia. Kuna wahubiri wengi wa uongo ambao kazi yao ni kuposha kweli za maandiko matakatifi. Ni jukumu la kila mhubiri wa kweli kuhakikisha anasimama imara katika kuitetea imani ya kweli. III.Kuhubiri ni kuinjilisha. Wajibu mkubwa wa Mhubiri ni kuitangaza injili kwa watu waliopotea dhambini. Ni lazima watu wote waliopotea wapelekewe injili ili wapte kutambua hali yao ya kupotea na kuongozwa kwenye wokovu wa Yesu Kristo.Kila mhubiri ahakikishe anatimiza Agizo kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Ahakikishe anawafikia watu wote wasiofikiwa na injili na kuwaleta kwa Bwana Yesu. IV. Kuhubiri ni kukemea dhambi. Kama ukichunguza hotuba za agano jipya utagundua kwamba hakuna mhubiri hata mmoja aliyesita kukemea dhambi.mfano Yesu, Yohana, Paulo, Petro n.k wote walikemea dhambi kwa nguvu zo katika kila mahubiri. Mhubiri nilazima akemee dhambi kila mara kwani Mhubiri ni kinywa cha Mungu. Kemea dhambi bila kuogopa chochote .Mhubiri ni lazima afunue ubaya wa dhambi na kuwahamasisha waamini kuishi maisha matakatifu yenye kumpendeza Bwana Yesu na kujiepusha na uovu. V. Kuhubiri ni kuhamasisha waamini Mahubiri hutakiwa kuwasaidia wakristo kukua katika neema ya Mungu. Pamoja na kuonya na kukemea dhambi mahubiri hutakiwa kuwahamasisha na kuwawezesha waaamini kukua kiroho na kufikia kimo cha Kristo. Hili ni moja wapo wa lengo kuu la mhubiri. Hatuhubiri ili kupisha muda au kwa sababu ya mazoea bali kwa sababu Mungu anakitu anataka tukipeleke kwa watu wake. Lengo la mahubiri ni kuwabadilisha waamini kuwakuza na kuwawezesha kufikia kimo cha Kristo Yesu., Tunapohubiri tunaumba sura ya Kristo ndani ya wale tunaowahubiri. Hakikisha wale unaowahubiri wanakua kiroho na kufanana na kristo VI. Kuhubiri ni kufikia mahitaji ya hadhira. Mahubiri yatakuwa yameafanikiwa kama yatakuwa yamepokelewa na kukutana na mahitaji ya wasikilizaji. Mhubiri kwa uangalifu anatakiwa kujiweka katika daraja sawa na wasikilizaji. Anatakiwa kujitahidi kuhakikisha anapokelewa na makutano na kukutana na mahitaji yao. Mhubiri anapaswa kuhubiri kwa mguso. Hakikisha unagusa mahitaji ya watu unapohubiri. Mahubiri ni uhai hivyo ni lazima yalete majawabu kwa wale tunaowahubiri. Gusa mahitaji halisi ya watu ambayo Mungu anakusukuma kuyashughulikia. Hubiri kwa ufanisi na kwa mguso. VII.Kuhubiri ni kudhihirisha uweza wa Mungu. • Bwana Yesu aliahidi kuwa na wahubiri kwa kulithibitisha neno kwa ishara na maajabu. Popote injili inapohubiriwa ni sharti Bwana awepo akiithibitisha kwa isharaMk 16:15,20. 1Kor 2:4. Hakikisha nguvu ya Mungu iko juu yako unapohubiri. Unapaswa kupakwa mafuta kikamilifu a Roho mtakatifu unapokwenda kwenye huduma ya kuhubiri kwa sababu kuhubiri ni vita. Omba Mungu Roho mtakatifu afanye uthibitisho kwa kila utakachohubiri. Ishara na maajabu ziambatane nawe kokote unakohubiri. -Ikiwa kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu mhubiri anapaswa kwenda mahali Mungu alipoongea mara nyingi na waziwazi yaani “Biblia” • Kwa njia nyingine kuhubiri ni kuipa Biblia sauti.ni kuacha Mungu aongee mwenye toka kwa Neno l D. WITO WA KUHUBIRI Sehemu ya muhimu sana katika kuhubiri ni wito. Kimsingi wito ni wa mtu binafsi Mungu huwaita watu katika huduma na watu hupokea hilo rohoni mwao kisha huja uthibitisho wa nje kupitia kanisa au watumishi mbalimbali na fursa mbalimbali. Mungu Huwaita watu wake katika nafasi na huduma mbalimbali. Wengine kuwa wachungaji, wamishenari, wazee wa kanisani, wainjilisti, au huduma nyinginezo. Kazi ya kuhubiri si ajira ambayo mtu anakwenda chuoni kusoma kwa lengo la kupata baada ya kuhitimu masomo yake, bali ni mwito mtakatifu ambao mtu huitwa na Mungu mwenyewe kuwa muhubiri. Mtu huenda chuoni ili kupata maarifa yatakayomwezesha na kumsaidia katika kutimiza mwito wa Mungu uliondani yake. Haendi chuoni kupata mwito bali wito husababisha mtu kwenda chuoni kama sehemu ya maandalio. Hivyo wito usichanganywe na ajira na maslahi binafsi ya mtu. Ni lazima wito uheshimiwe na kuogopwa. Waamini hawapaswi kujihusisha na huduma kwa lengo la kujinufaisha na kujipatia mali kwa njia za ujanja ujanja. Kimsingi kila mwamini ni muhubiri kwani agizo kuu linamhusu kila mwamini. Kila mwamini anapaswa kujihusisha na kupeleka injili kwa watu waliopotea dhambini hili ni agazo la jumla. Lakini kuna watu maalumu ambao Bwana ameweka wito wa muda wote(Full time commitement) ndani yao. Amewachagua kwa kusudi hili katika maisha yao na muda wao wote. Hawa wanasimama katika zile huduma tano za uongozi katika kanisa, ambao ni mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu. Hawa ndio Bwana amewaweka kusimama katika kazi ya kuhubiri ya muda wote, Wao hawapaswi kujihusisha na shughuli zingine bali kazi yao ni kulihudumia Neno na kuomba yaani Kuhubiri. Bwana ameweka mwito mtakatifu ndani yao ambao ni wajibu mkuu na wa kuogofyapia{.Mdo6:2,4} hili ni agizo mahususi. Wito huu haupatikani kwa njia ya kusoma au kwa njia ya ulaghai bali kwa kuitwa na Mungu mwenyewe kuwa msemaji wake. Kuna baadhi ya makanisa ambayo yameufanya wito wa Mungu kuwa ni ajira. Kwani wao huwapeleka watu kwenda chuoni kusomea huduma fulani mfano uinjilisti, uchungaji nakadharika kwao wito si jambo la msingi kwao ila elimu ndiyo yenye kupewa kipaumbele. Wao humpa mtu kushika nafasi ya huduma baada ya kuhitimu mafunzo ya chuo cha Biblia bila kujali kama ana wito au la. Matokeo yake ni kwamba makanisa yamekuwa yakiongozwa na kuhudumiwa na watu wasio na wito wenye kutegemea elimu ya darasani tu, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo na uhai wa kanisa. Elimu ni jambo la zuri sana lakini elimu haiwezi kuchukua nafasi ya wito katika kanisa la Mungu ikiwa tunataka kufikia kusudi la Mungu la mwito mtakatifu na kusimama kiuaminifu mbele zake kupata ushindi mkuu. Usiwe mtumwa wa elimu. Elimu hii unayopata ikusaidie katika kumtumikia Mungu na kufanya huduma lakini isichukue nafasi ya Roho mtakatifu katika maisha yako na huduma yako. Wala haipaswi kuwa badala ya Roho mtakatifu. E. MAANDALIO KWAJILI YA HUDUMA. Ni muhimu mara mtu atambuapo kwamba Mungu anamwita katika huduma kufanya mambo kadhaa. Mojawapo ni kuanza kumngojea Bwana kwa njia ya maombi, Kujihusisha na huduma mbalimbali zinazojitokeza kanisani au sehemu nyingine yeyote . Pia ni muhimu kwenda shule kwajili ya mafunzo zaidi ya maandalio ya huduma. Kuwa na mlezi. Ni lazima kuwa na mlezi wa huduma ambae atakusaidia katika kutimiza mwito ulio ndani yako. Mlezi wa kwanza wa huduma na wito wako ni mchungaji wako. Mweleze mchungaji kuhusu wito ulio ndani yako na mwombe akusaidie katika kuulea wito huo. Kuwa mtii na mnyenyekevu kwa mcungaji wako. Shirikiana na watu wenye wito kama wako ili uweze kujifunza zaidi. Fanya kazi na huduma mbalimbali unazopewa na mchungaji au viongozi wa kanisa. Jifunze kwa watu wenye wito kama wako walifanikiwa katika utumishi wao. Kupata mafunzo zaidi. Ni vizuri mara unapogudua kwamba Mungu amekuita katika utumishi au mojawapo ya zile huduma tano kwenda chuo cha Biblia kwaajili ya mafunzo na matayarisho kwaajili ya huduma Mungu anayokuitia. Namna ya kuchagua Chuo cha Biblia 1. Omba Uongozi wa Mungu juu ya jambo hili. 2. Angalia chuo kitakachokidhi mahitaji yako ya kuandaliwa. 3. Angalia maswala ya usajili wa chuo.(Vyuo vingi vya Biblia havina usajili wa serikali kwani haviko kitaaluma zaidi bali kihuduma). 4. Chunguza misingi ya imani ya chuo. 5. Tathmini uwezekano wa kuingizwa katika huduma baada ya mafunzo. 1. Mambo ya kuzingatia unapokuwa katika Chuo cha Biblia. 2. Jikite katika masomo kabisa kwa miguu yako yote miwili. 3. Jihusishe kikamilifu na ratiba nzima ya Chuo. 4. Tia bidii katika masomo. 5. Tumia muda kuwa na waalimu na wanafunzi wenzako na jifunze vitu vyema toka kwao. 6. Epuka kuwa mjuaji (arogant). 7. Kuwa mtumishi. 8. Jitahidi kuonekana na si kusikika. 9. Shirikisha baadhi ya watu maono na wito ulio ndani yako. 10. Baki kuwa mwanafunzi daima hata baada ya kuhutimu mafunzo. 11. Kwa mtii kwa amri, shria, kanuni na taratibu za Chuo. • Usiongozwe na elimu bali ongozwa na Roho mtkatifu. • Usihubiri kwa maneno yenye hekima pekee kwa lengo la kushawishi akili za watu bali hubiri Kwa dalili za Roho mtakatifu na nguvu. 1Kor 2:4. • Hakikisha unautumikia wito ambao Mungu ameweka ndani yako kwa gharama yoyte ile bila kujali mazingira au kitu kingine chochote. • Kwa hiyo wito wa kuhubiri hautoki kwa mwanadamu yoyote Yule bali toka kwa Mungu mwenyewe. Mungu huwafanya watu wake kuwa wahubiri. • Jiulize wewe ni mhubiri wa kufanywa na nani ? F. Kweli kuu kuhusu wito wa kuwa mhubiri. 1. Roho mtakatifu huweka wito ndani ya mtu. Wito wa Mungu huja juu ya mtu kupitia Roho mtakatifu. Katika akili ya kawida ni kazi kubwa kuhubiri au kutumika. Wito huja kwa watu wa aina zote na umri wote wowote. Baahi ya watu husikia wito na kujitoa wangali wadogo lakini wengine katika umri mkubwa n.k 2. Shauku ya kutimiza wito. Watu wanaoitwa kuwa wahubiri waliumbwa na Mungu kwa kusudi hiloYer1:4-10 Hawawezi kupata utoshelevu kwa kufanya kitu kingine chochote. Hawawezi kupinga kujihusisha katika huduma au kuchukua fursa za kuhubiri. Hata kama hakuna nafasi za kutumika moja kwa moja bado watatafuta nafasi katika huduma yoyote inayojitokeza. 3. Mungu huwaandaa wale anaowaita kwajili ya huduma. Mungu hawaiti watu ambao hwana uwezo wa kutimiza mwito wake. Wahubiri wengi wanakipaji cha kuongea. Watu wenye wito juu ya watoto Mungu huwaandaa kwa kuwapa uwezo kwa kufanya huduma na watoto n na wanaoitwa kuwa wacghungaji huwezeshwa kuwa wachungaji. Kwa namna yoyte Mungu huwaandaa na kutoa nguvu ya uwezesho juuv yao. 4. Wito wa Mungu wapaswakuwa wazi. Wito wa Mungu usifichwe. Wito wa Mungu ulioju yako wapaswa kuwa wazi kwa watu wangine lakini haupaswi kukimbilia kwenye wito huo mara moja. Hutakuwa na furaha na mafanikio na wito huo mpaka utakopokuwa umejisalimisha kwa mapenzi sahihi ya Mungu juu yako.Wito ambao Mungu amekuita kuutimiza unapaswa kuuweka wazi. Shirikisha watu ambo watafanyika msaada katiki kuulea wito wako. Fanya kazi na watu. Tumika na watu wenye wito kama wako. Kaa chini ya mtu mwenye neema kama ya wito ulionao ili uweze kujifunza zaidi. 5. Wito wa Mungu ni wito wa matayarisho. Kuna wajibu mwingi na mkubwa ambao huja pamoja na wito wa kuhubiri. Mungu akisha mwita mtu humuandaa kwanza kabla ya kumtuma na kumwachilia kwnye huduma aliyomuitia. Mhubiri anapaswa kujiimalisha kiroho na kimwenendo.Anatakiwa ajiandae kiakili kwa kusoma na kupata mafunzo. Pia anapaswa kujiandaa kimatendo kwa kunoa vipawa vilivyo ndani yake na kuyatisha maisha yake yote kulingana na wito ulio ndani ya yake. Mungu akisha weka wito wake ndani ya mtu huanza kumwandaa kwajili ya wito huo. Humpitisha katika majaribu mbalimbali yanayoendana na wito wake, humpeleka kwenye shule yake ijulikanayo kama shule ya moto na baada ya kufuzu huko Mungu humwachilia mtu katika huduma. Musa aliandaliwa kwa zaidi ya miaka arobaini, Yusufu kwa muda wa zaidi ya miaka kumi, Paulo kwa muda wa miaka kadhaa.Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba Mungu huwa hana haraka. Ukipata wito wa Mungu ndani yako usifanye haraka kuutimiza Bwana anatenda kwa wakati. Unapaswa kusubiri wakati wa Bwana na ufanye kwa wakati wake na si nje ya wakati wa Mungu. G. Mawazo mawili potofu kuhusu mahubiri. Kuna dhana mbili potofu ambazo zinajitokeza katika uwanja na taaluma ya mahubiri mawazo hayo ni: a. Maaandalizi si lazima. Wazo la kwanzalenye makosa ni kwamba maandalizi si lazima na huonesha kukosa imani kwa mhubiri. Watu wenye kushikilia msimamo huu hufikili kwamba imani ya kweli hutupilia mbali jitihada yoyote inayojaribu kuandaa akili na hiyvo husimama mimbarini wakiamini kwamba Mungu atawapa maneno ya kusema.husimamia maawazo haya: i. Roho mtakatifu atakupa unachohitaji kuhubiri. Unapopanda mimbarini. _- Zab 81:10 “ Fumbua sana kinywa chako name nitakijaza”(Hutumia andiko hili kutetea msimamo wao.). Pia husema kwamba Yesu alisema kwamba “Msifikirifikiri nini cha kusema maana mtapewa kinywa cha usemi saa ili ilie mnapotakiwa kusema” Unapoyachunguza kwa umakini maandiko hayo utagundua kwamba maandiko hayo wanayafasili nje na mkutadha wake na na kulazimioshwa yaseme kile ambacho hayamaanishi. *Mahubiri ni kamana jengola kiroho ambalo linatakiwa kusanifiwa na kuandaliwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Roho mtakatifu ndiye mhandisi mkuu wa mahubiri. b. Uwezo wa mtu unatosha. Kuweka mkazo katika matayarisho na kutegemea uwezo wa kibidanu tu. Wahubri wanaoshikilia msimamo huu hudai kwamba maandalizi peke yake yanatosha na huweka mkazo kwenye matayarisho pekee.Kumtegemea Roho mtakatifu huwa ni kudogo sana au hakuna kabisa, bali tumaini la mtu binafsi ambalo ni matokeo ya kujifunza na kuendeleza uwezo wa asili. Ujumbe wa namna hii waweza kuwa mzuri kabisa lakini hauwezi kuleta matokeo yatakikanayo daima. Kwani ni Roho mtakatifu pekee ndiye anaeweza kuleta badiliko katika maisha ya waikilizaji wako. Bila yeye mahubiri huwa ni maiti na haiwezi kuleta uhai kwa sababu ni uhai wenye uwezo wa kuzaa uhai. *Roho mtakatifu huuhuishaujumbe na kuletaq matokeo yaliyokusudiwa na Mbingu katika maisha ya wasikilizaji. Ili mhubiri aweze kuhubiri sawasawa anapaswa kuwa na maansdalizi ya kutosha katika kuuandaa ujumbe wake kwa kusoma, kutafakari na kuchambua kweli zote zilizomo katika ujumbe wake. Lakini hayo yotec anapaswa kuyafanya akiwa katika hali ya maombi. Mhubiri anapaswa kumsikiliza Roho mtakatifu klwa kina na kupata uongozi kwake na kutaka Roho mtakatifu amshirikishe kile anachotaka kusema na watu wake na kukifanyia uchambuziyakinifu katika hali ya maombi ili aweze kukiwasilisha kwa ufanisi. • Mhubiri anapaswa kutambua kwamba yeye hana watu wala si Chanzo cha ujumbe. Kwasababu hiyo anatakiwa kumsikiliza mwenye watu na aliye chanzo cha huo ujumbe na kusimama katikati kwa uaminifu kuwafikishia watu kwa usahihi kile mwenye watu anachotaka kiwafikie watu wake. • Mhuibiri anapaswa kutambua kwamba kazi ya kuhubiri ni takatifusana na ni kazi nyeti ambayo yapaswa kufanywa kwa umakini, uaminifu na unyeyekevu mkuu. • Mhubiri mwenye kutegemea juhudi zake na uwezo wake wa asili atakuwa ni muhubiri kilema na halikadharika mhibiri mweye kutegemea kupewa ujumbe akiwa mimbarini atakuwa ni kilema. • Vyote viwili vyapaswa kwenda pamoja, maombi na matayarisho.Kwa sababu mahubiri ni matokeo ya mawasiliano na ushirika mzuri kati ya Roho mtakatifu na mhubiri. H. Umhuhimu wa kujifunza homiletics. a) Linatusaidia kujua mbinu mbalimbali za kuhubiri. b) Linatusaidia jinsi ya kuhubiri bila kuwachosha watu. c) Linatufanya kuwa na ujasiri tunapohubiri. d) Linatusaidia kuhubiri kwa usahhi. e) Linatusaidia kutambua mahubiri ya uongo. f) Linatusaidia kujua na kuheshimu wito tulio nao. g) Linatusaidia kujua kusudi la Mungu la mahubiri. h) Linatusaidia katika kuheshimu wito wa watu wengine. Zoezi. Jibu maswali fafuatayo. Wanafunzi waweza kujibu katika makundi au mmoja mmoja kama kazi ya nyumbani kwa kadri mwalimu atakavyoona inafaa. 1. eleza maana ya mahubiri kwa mitazamo mbalimbali. 2. Eleza vile mahubiri yasivyo. 3. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri na kuhubiri. 4. Taja faida tano za kujifunza somo la kuandaa mahubiri. 5. Tathmini misukumo mbalimbali inayosababisha watu waingie katika huduma tano za uongozi wa kanisa. na hali hawana wito. 6. Eleza namna gani mtu aweza kujua kwamba Mungu anamwita kuingia katika huduma. 7. Eleza umuhimu wa kipindi cha maandalizi na matayarisho kabla ya mtu kuingia katika huduma ambayo Mungu anamwita kuifanya. MADA YA PILI: MBINU ZA UTAYARISHAJI WA MAHUBIRI Utangulizi Katika mada hii tutajadili aina mbalimbali za utayarishaji wa mahubiri, maeno ya mahubiri na sehumu za mahubiri au hotuba. Tutapitia kwa undani kila kimojawapo ya vipengele hivi ili kujifunza jinsi vipengele hivyo vinavyohusiana na mahubiri na tunavyoweza kuvitumia katika huduma ya kuhubiri na kuandaa mahubiri. Malengo ya mada. Baada ya kumaliza kujifunza mada hii mwanafunzi ataweza. • Kutaja na kueleza mbinu mbalimbali zinazotumika katika utayarishaji wa mahubiri au hotuba. • Kutathmini kila mbinu kwa kueleza ubora na udhaifu wake. • Kuandaa jumbe za mahubiri kwa kutumia mbinu mbalimbali. • Kutambua maeneo muhimu katika mahubiri. • Kutambua sehemu muhimu katika jumbe na hotuba. • Kutayarisha jumbe na hotuba za ki-Biblia kwa kuzingatia sehemu muhumi katika • jumbe na hotuba. A. Mbinu za Utayarishaji wa jumbe na hotuba. Kuna aina nyingi za utayarishaji wa somo au hotuba, na kila mojawapo ina umuhimu wake. Lakini katika mada hii tutajifunza aina tatu za utayarishaji wa somo au hotuba. Kila mwanafunzi anatakiwa kuelewa aina zote tatu na anapaswa kujizoeza kutumia njia hizi zote ili aweze kufaidika zaidi. Mbinu hizi za utayarishaji wa somo pia zaweza kutumika kama mbinu za kuhubri. Kwa hiyo tutakapokuwa tunajadili zitaangaliwa katika maeneo haya mawili. ( Kama mbinu za utayarishaji na kuhubiri.) 1. Somo Lililoandikwa. Katika aina hii mhubiri hupaswa kuandika kila kitu anachokusudia kukihubiri. Wakati mwingine somo lote huandikwa. Kila eneo la somo huchambuliwa kwa undani na kuwekwa katika maandishi. Ujumbe au somo lote huandikwa kikamilifu kabla ya kuhubiri. Mhubiri huelezea kwa undani somo lake anapohubiri likiwa katika maandishi. Mhubiri anapohubiri mara nyingi hupitia kila kitu alichokiweka katika maandishi. Faida za aina mbinu hii. a) Ujumbe wote huandaliwa kwa uangalifu mkubwa. b) Ujumbe huwasilishwa kwa umakini na uhalisia. c) Ujumbe huwa ni wa kitaalam. d) Mhubiri hujikita katika somo. Hasara ya mbinu hii. a) Somo huwa haliwavutii wasikilizaji. b) Utoaji wa ujumbe wa namna hii unaweza kuwa wa kuchosha usipofanywa kwa uangalifu c) Utayarishaji wake huhitaji muda mwingi. ZOEZI. 1. Eleza maana ya somo lililoandikwa. 2. Taja vitu muhimu vilivyo katika somo lililoandikwa. 3. Taja ubora na udhaifu wa njia hii licha ya zilizotolewa katika kitabu hiki. 4. .Andaa ujumbe kwa kutumia mbinu ya somo lililoandikwa na kisha huburi kwa dakika kumi. 2.Somo Lisiloandikwa. Hii ni mbinu ya utayarishaji wa somo bila kuliandika. Mhubiri husoma vifungu vya maandiko na kivitafakari kwa kina kisha hukariri vitu vya msingi vilivyo katika ujumbe wake na maandiko yanayohusika. Aina hii mara nyingi hutumika katika kutayarisha na kuhubiri ujumbe wenye uvuvio zaidi. Njia hii ni nzuri sana katika kuhubiri ujumbe wa kiinjilisti. Ujumbe hutiririka toka rohoni na huwa wa kuvutia mno. Faidaza mbinu hii. a) Ni rahisi kutumia. b) Haihitaji muda mwingi wa matayarisho. c) Mhubiri huwa huru kutoa kila kinachokuja ndani yake maadam kinaendana na ujumbe wa somo. d) Huwasisimua wasikilizaji na kuwavutia. Udhaifu wa mbinu hii. a) Mhubiri kutoka nje ya ujumbe wake hasa ikifanywa na mhubiri asiye na uzoefu. b) Wasikilizaji waweza kulielewa somo vibaya. (waweza kuelewa vile somo lisicho maanisha). c) Somo kutowajenga wasikilizaji na kuishia kusisimua tu akili zao. d) Somo kutokuwa na maana halisi na hivyo kutowajenga wasikilizaji. ZOEZI. 1.Eleza maana ya somo lisiloandikwa. 2. Taja mabo matano ya kuzingatia katika utayarishaji wa ujumbe kwa kutumia njia ya somo sililoandikwa. 3.Toa tofauti iliyopo kati ya somo lililoandikwa na somo lisiloandikwa. 4. Andaa ujumbe kwa kutumia mbinu ya somo lisiloandikwa na kisha hubiri kwa dakika kumi 3.Mbinu Ya Skeletoni. Njia hii huhusisha kuandika maelezo ya somo au ujumbe kwa kifupi kwa lengo la kufanikisha utunzaji wa kumbukumbu sahihi juu ya ujumbe au somo. Kwa maana nyingine ni kwamba mhubiri hutayarisha muhtasari wa ujumbe au somo.Mhutasari huo huwa kama skeletoni ya somo, Skeletoni maana yake ni fuvu. Mfano wa fuvu la binadamu. . Mhubiri huhubiri kwa kutumia skeleton hiyo. Kazi yake hasa ni kuweka nyama katika skeletoni hiyo kwa njia ya mahubiri. Hivyo anapohubiri huweka nyama katika mahubiri yake ili yawze kuwa kitu kamili . Mhutasari wa somo huwa kama mifupa ya ujumbe. Ndiyo mifupa ambayo huleta sura na mategemeo kwa kile mhubiri anachotamani kusema. Anavyosema anaweka nyama katika mifupa na kuufanya mwili wa somo lake. Hupanua mawazo yake ambayo maelezo yake mafupi yamekuza. Faida za mbinu hii. a) Mbinu hii humpa mhubiri uhuru zaidi. b) Utoaji wa somo huwa wa kuvutia sana. c) Somo huwajenga wasikilizaji bila kuwachosha. d) Mhubiri huweza kutoa somo kwa mtiririko mzuri na sahihi. Zoezi 1. Eleza maana ya skeletoni. 2. Eleza maana ya mbinu ya skeletoni. 3. Linganua kati ya minu ya somo lisiloandikwa na mbinu ya skeleton. 4. Eleza kati ya mbinu tatu ulizosoma, ipi ni bora kuliko zote na toa sababu ya jibu lako B. Maeneo ya Mahubiri. Kuna maeneo makuu manne ambyo mahubiri huhusisha. Mhubiri yoyote ni lazima azingatie maeneo hayo ili aweze kufanikisha mahubiri yake. I.Wazo . Hii huhusu namna ya kupokea kichwa cha somo au ujmbe. Ni ujuzi unaohusu namna ya kupokea ujumbe toka kwa Mungu. Huhusu namna ya kupata wazo la awali na kichwa cha somo. Mungu hupanda mbegu ya wazo kuhusu somo au ujumbe siku kadhaa kabla ya mahubiri. Mbegu hiyo hukua kwa njia ya kuitafakari na maombi zaidi. Kutokana na ujuzi mhubiri aweza kuujenga uwezo wa kutambua mstari unaohusika. Mhubiri hupaswa kuliendeleza na kulikuza wazo lililopandwa ndani yake kwa njia ya maombi, kutafakari na kuchunguza zaidi juu ya wazo hilo ili aweze kutayarisha ujumbe. Pata muda wa utulivu utulie uweponi na omba nuru zaidi ya ufunuo huo. Kuna tofauti kubwa kati ya hotuba na ujumbe.mtu anaweza kujifunza jinsi ya kuandaa hotuba kupitia masomo ya Homiletics lakini Mtu anapaswa kuwa na ushirika na Mungu ili aweze kupata ujumbe. Kupata ujumbe ni jambo la kiroho zaidi kuliko taaluma. Wale wanaofanikiwa kupokea ujmbe wa kuhubiri toka kwa Mungu ndio wanaoweza kufanikisha lengo la kuhubiri. Mambo ya kusaidia kupata ujumbe. Tambua mahitaji ya watu.(Mahitaji ya kiroho na kimwili). Kujazwa na Neno la Mungu. Kujiweka katika viatu vya wengine (Soma Hotuba na sikiliza mahubiri ya watu wengine. Kutokana na uzoefu wa mhubiri. Kutambua kalenda ya Kikristo. Kutokana na mafundisho ya msingi ya Biblia. Kutokana na matukio mbalimbali. II.Muundo. Muundo huhusisha uchambuzi wa wazo ili kuweza kugundua kweli zilizomo katika wazo hilo.Baada ya kupokea Wazo toka kwa Mungu unapaswa uanze kulichambua ili kutambua vitu ambavyo wazo hilo linavyo. Katika hatua hii unapaswa kuorodhesha kwa urahisi kila kitu kilichomo kwenye wazo hilo.Mara nyingi unapokuwa katka hatua hii unahitaji kuandika kwa haraka ili kupata kwa kifupi mtiririko wa uvuvio unaokuja. Hakikisha kwamba unaandika kila kitu ili uweze kuchambua baadae. III. Ujenzi. Huhusisha kukusanya na kuyaweka mawazo yako uliyoyachambua katika kipengele cha uchambuzi katika mpango mzuri. Kuweka kila kitu katika mpangilio mzuri kutakusaidia na kukurahisishia katika utoaji wa somo lako. Kuwasislisha mawazo yaliyoendelezwa hufanyika msaada sana kwa wasikilizaji wako katika kuelewa na kufuata mpango wako wa kufikiri. Somo likiwalimechanganywa itawawia vigumu wasikilizaji wako katika kulielewa somo hilo.Ujenzi wa somo hulenga kulifanya somo rahisi kiasi cha kueleweka vizuri na wasikilizaji. Ni muhimu sana kwa mhubiri kuliweka somo katika namna itakayofanya lieleweke kwa urahisi. IV. Mawasiliano. Hii huhusu namana mhubiri anavyowasilisha somo au ujumbe kwa hadhira. Mhubiri anatakiwa kuliwasilisha somo lake kwa njia rahisi na nyepesi kueleweka na wasikilizaji wake. Anatakiwa: a) Kuwasilisha ukweli uliowazi na wenye kueleweka. b) Kutoa ujumbe kwa njia ya kuteka akili za hadhira. c) Kuendeleza mawazo yake katika mpango ambao hadhira wataweza kuyafuata kwa urahisi. d) Kuwahamasisha hadhira kulitendea kazi somo. Yak 1:22. C.Sehemu Kuu za ujumbe na Hotuba. Kwa kawaida mahubiri au hotuba yoyote ile ni lazima iwe na sehemtu tatu ambazo kwa pamoja huunda hotuba au mahubiri hayo. Sehemu tatu hizo ni utangulizi, kiini na hitimisho.Kila sehemu ni muhimusana na inatakiwa kupewa uzito wake. Sehemu mojawapo ikipuzwa yaweza kuvuruga au kuharibu kabisa ujumbe au hotuba yako. I.Utangulizi. I. Hii ni sehemu ya kwanza ya hotuba. Utangulizi hutambulisha hotuba au somo zima na kutoa picha jinsi somo litakavyokuwa. Utangulizi ni sehemu muhimu ya ujumbe na kama hadhira hawajakusikiliza kwa umakini katika kipindi hiki cha awali yawezekana kutokuuelewa ujumbe wako au kutokukusikiliza vizuri katika sehemu zinazobaki za hotuba yako. Mara nygingi utangulizi huwa kama muhtasari wa ujumbe.Katika utangulizi mhubiri huwaeleza hadhira kwa kifupi juu ya kile ulichopanga kuongelea au kuhubiri. Utangulizi ni kama mlango wa nyumba katika ujumbe na hotuba.Uangulizi huwa na lengo mahususi la kuwajulisha hadhira ujumbe ambao unawasislishwa kwao. Waamni wengi huja kanisani wakiwa na matatizo mbalimbali ya kifamilia , kikazi N.k .Utangulizi unatakiwa kuwavuta ili waweze kujikita kwenye ujumbe na kuwasahaulisha matatizo waliokuja nayo. Uangulizi ni silaha ya kuwateka wasikilizaji. Kuna namna mbalimbali za kuanza utangulizi. Mhubiri anapaswa kujifunza namna mbalimbali za kuanza utangulizi na ajizoeze kuanza utangulizi wa mahubiri yake kwa njia tofauti tofauti. Baadhi ya njia za kuanza utagulizi zimeorodheshwa hapa chini. II.Namana ya kuanza Utangulizi 1. Kuanza kwa kuuliza swali. 2. Kuanza na maelezo ya kuchanganya(Yenye kuhamasisha watu kusikia kw2a makini swehemu ya ujumbe inayobaki ). 3. Anza kwa andiko 4. Anza kwa mkutadha 5. Anza na habari au kielelezo. 6. Anza na tukio la sasa. 7. Anza na nukuu III. Mambo ya msingi katika utangulizi. Kuteka usikivu. utangulizi wako unapaswa utawale hamu na mawazo ya wasikilizaji. Kujenga masikilizano. Lazima ujenge mawasiliano kati yako na wasikilizaji. Kuleta kukubalika. Ni lazima utangulizi kwako ukujengee kukubalika kwa wasikilizaji. Unapaswa kupata usikivu wao, matumaini na heshima. Kujulisha. Utangulizi wako unapaswa kuwaeleza wasikilizaji kwamba somo lako lina husu nini hasa, na jinsi utakavyoliwasilisha. Kusadikisha. Ni lazima utangulizi uwasadikishe wasilizaji juu ya umuhimu wa ujumbe na kupata usikivu mzuri wa sehemu iliyobaki ya hotuba yako. Usitoe utangulizi kwa kuomba msamaha. Usiseme “Bahati mbaya sikujiandaa vizuri” Kufanya hivyo kutapoteza usikivu wa wasikilizaji wako na kukufanya usiaminike kwao. Sifa za utangulizi mzuri. 1.Sio wa kishindo mno. Utangulizi uwe wa kiasi usiweke hatua ambayo huwezi kuifikia. 2.Sio mrefu mno. Kumbuka kwamba utangulizi si ujumbe wote bali ni sehemu tu hivyo unapaswa kuwa mfupi. 3.Utangulizi uendane na ujumbe. Utangulizi ni sharti ulenge kichwa cha somo. Waweza kuwa muhtasari wa somo au kisa ambacho kinaonesha ukweli wa kile ulichokusudia kuongelea. 4.Unapaswa kuandaliwa kwa uangalifu. Kwa sababu utangulizi wako ni kitu muhimu katika kuvuta usikivu wa hadhira unapaswa kuandaliwa kwa umakini sana. 5.Tayarisha utangulizi wako kwa kujiuliza maswali yafuatayo a.“ Ningekuwa ni msikilizaji wa ujumbe huu nini kingenivuta zaidi ili kuleta usikivu katika yote niliyokusudia kuyasema? 1. “ Ni jambo gani hasa ambalo lingekamata usikivu wangu? b.Majibu yake unayoyapata ndiyo waweza kuyatumia katika sehemu ya utangulizi wa ujumbe wako. 6. Utoe nafasi ya kupitia kwenye kiini cha ujumbe. Utangulizi unapaswa kutoa njia ya kupitia kwenda kwenye kiini cha ujumbe. Kusiwe na pengo kati ya utangulizi na kiini cha ujumbe. II. Kiini. Hii ni sehemu kuu ya somo au ujumbe ambayo imebeba ukweli wote wa somo. Hatua ya kwaza kwenye kiini ni kutoa skeletoni ya kiini na kisha hatua ya pili ni kuweka nyama katika skeletoni yako.Waweza kuweka nyama katika sekeletoni yako kwa kufanya yafuatayo: Kufafanua msamiati mbalimbali inayojitokeza kwenye kiini na kutoa maelezo ya dondoo ulizoziandaa. Tumia kamusi au itifaki ya Biblia katika kupata maana ya maneno hayo. Kiini. Kiini cha ujumbe ni lazima kieleze, kisimulie, kijadili na kutoa kweli yote inayokusudiwa kuwasilishwa. Ni lazima kueleza maana ya andiko au habari. Ni lazima kutoa ushahidi wa kweli inayohubiriwa. Neno la Mungu linajieleza lenyewe. Jambo lingine la kutumia kuthibitisha ni ushuhuda binafsi. Mfano kama unahubiri uponyaji toa uthibitisho kwa kutumia wewe binafsi jinsi Mungu alivyokuponya au alivyowaponya watu wengine. Unapounda kiini unapaswa kujiuliza maswali kadhaa 1. NIini nataka kusema ? 2. Kwanini ninataka kusema hiki ? 3. Ni vipi nitakisema ? 4. Ninachotaka kukisema kitafanikisha nini ? Unaposhughulikia andiko au mada ni lazima kujiuliza kwanini? Namna gani ?, Lini?, Wapi ?, Nini kilitokea kabla na baada ?, Mazingira yalikuwaje?, Matokeo yake yalikuwa nini ?, Nani walikuwa pale ?, na kwanini walikuwepo pale? Walifanya nini?, Hii huhusikaje leo ? na inamaanisha nini leo ?. Kujua majibu ya maswali haya kutakusaidia kutengeneza mhutasari wa somo au andiko. Mfano Luka 16:19 Matumizi ya vielelezo. Moja wapo ya vipengele muhimu katika ujmube au kiini ni vielelezo.Vielelezo ni mifano mbalimbali inayotumika kufafanua na kuelezea ujumbe au somo. Watu wengi huweza kukumbuka vielelezo kuliko ujumbe na hivyo basi vielelezo husadia watu kukumbuka ujumbe. Bwana Yesu amekuwa kielelzo na mwalimu wa vielelezo. Watu hufurahia kusikia vielelezo. Wahubiri wenye ujuzi wa kutumia vielelezo katika jmube na hotuba zao hufanikiwaq kuvuta usikivu wa wasikilizaji wao. Vielelezo ni sawa na madirisha katika nyumba. Vielelzo ni madirisha ya jumbe na hotuba. Jumbe nyingi zinazohubiriwa na wahubiri wengi ni kama nyumba zisizo na madirisha. Nhyumba hizo zaweza kuwa na msingi imara na kuta imara lakini zitashindwa kuingiza mwanga na hewa ya Oksijeni ambayo ni muhimu kwa mwanadamu ili aweze kuishi. Vielelezo hutimiza lengo la kuleta nuru na hewa ya oksijeni ya ki-Biblia katika ujumbe. Vielelezo havipaswi kuwa mwisho vyenyewe lakini vyapaswa kufafanua kweli zinazoawsislishwa. Lengo la vielelezo. Kuleta nuru kwenye somo. Kuvuta usikivu. Kuelezea na kufafanua ujumbe. Kuthibitsha kweli (dondoo). Kanuni za kutumia vielelezo. Kuna kanuni kadha ambazo ni muhimu kuzizingatia wakati wa kutumia vielelezo . Baadhi ya kanuni hizo zimejadiliwa hapa chini. 1. Urahisi. Vielelezo vinapaswa kuwa rahisi kiasi cha kueleweka na kila msikilizaji. Havipaswi kuwa vigumu kiasi cha kuwachanganya wasikilizaji na kuhitaji vielelezo zaidi ili kufafanua vielelezo. Kuna baadhi ya vielelezo ambavyo huhitaji vielelzo vingine . Epuka kutumia vielelezo vya namna hiyo. Yesu alipotumia vielelezo vilikuwa rahisi na wazi Mifano aliyotoa ilkuwa wazi na rahis kueleweka na waikilizaji wa aina zot. Wasomi(mafarisayo na masadukayo) na wasio wasomi (wakulima na wavuvi). Kumbuka kwamba watu wengi utakaokuwa unawahubiria watakuwa ni wenye elimu ya kawaida au wasio na elimu. 2.Ukweli. Hadithi na vilelelzovinavyotumiaka katika amhubiri view wazi. Kama ni hadhi za kutunga usiwaambie watu kwamba ni matukio halisi yaliyotokea. Usilazimishe mfano na kuelelzo kuwa kitu halisi. 3.Kiasi. Vielelzo visizidi na wala visigeuke kuwa ujumbe. Kuna baadhi ya wahjubiri ambao ni mabigwa wa kutoa vielelezona watu huvutiwa sana na vielelezo hivyo. Wanatumia muda mwingi kusimulia vielelzo badala ya kuhubiri. Jambo hili ni hatari sana. Vielelezo vinatakiwa kutumika kuelezea kweli za kiroho na na visigeuke kuwa jumbe.Yesu hakututuma kusimulia hadithi na vielelzo alitutuma kuhubiri. Kwa kawaida kila dondoo kuu inapaswa kuwa na kielelezo kimoja na si vinginevyo. 4. Lengo. Unapaswa kukumbuka kwamba lengo la vielelezo ni kuelezea na kufafanua ujumbe wako. Kweli zipo kumsaidia mhubiri kufikia lengo lake la mahubiri. Lengo la mhubiri linapaswa kubaki kuwa ujumbe na si vielelezo. 5. Uhalisia. Vielelezo viendane na dondoo unayoielezea. Kama hakuna uhusiano hakuna umhuhiu wa kutumia kielelezo hicho. Hakikisha vinahusiana na kwendana. Vyanzo vya vielelezo. Bwana wetu Yesu Kristo alitmia vielelezo na mifano kutoka katika mazingira ya kawaida yaliyomzunguka. Alitumia mifano rahisi kama vile nuru, chumvi mbegu. Mzabibu, kondoo. N.k. Alitumia mifano iliyokuwaikitumika katika maisha ya kawaida. Alizielezea na kuzifafanuana kuzifundisha kweli za kiroho kwa kutumia vielelezo vilivyokuwa katika ulimwengu uliomzunguka. Hivyo basi kila mhubiri anatakiwa kujifunza kutumia vitu mbalimbali vilivyo katka mazingira yake kama vielelezo. Soma vitabu, magazeti ,vijarida na vipeperushi. Sikiliza natutzama vyombo vya habari. Katika mabo yote hayo kua vielelezo vingi ambavyo waweza kuvipata na kuvitumia. Kabla ya kuanza kuitumia kielelezo hakikisha unatihafamu vizuri. Kielelezo kiwasaidie watu kujisikia, kusikia na kuona kile unachokielezea. Ni lazima wewe mwenyewe uguswe na kuvutiwa na kielelezo hicho. Kama hakikuvuti wewe bila shaka hata watu wengine hakita wavutia. Jifunze kwa mwalimu mkuu Yesu Kristo. Vichekesho. . Vichekesho ni muhimu katika mahubiri kutegemeana na ujumbe unaohubriwa. Vichekesho vyapaswa kuendana na somo au ujumbe. Tumia vichekesho kuamsha akili za watu na kuvuta usikivu wao. Vichekesho havipaswi kuzidi kiasi cha kupunguza uzito wa somo. Pia Ujumbe usitawaliwa na vichekesho. Kumbuka kwamba mahubiri si vichekezo ni kitu muhimu na nyeti sana. Usifanye mahubiri kuwa komedi. Wala usiwe mwanakomedi. III. Hitimisho. Hii ni sehemu ya mwisho ya hotuba au ujmbe lakini kipengele cha muhumi sana . Kipengele hiki kisipozingatiwa maana na malengo yote ya kuhubiri huvurugika na kutokuwa na maana. Hivyo ni lazima kipewe uzito unaostahili. Mambo ya kuzingatia. Tunia muda kidogo kwa kuuelezea ujumbe kwa kifupi. Kazia maeneo ya msingi unayofikiri kwamba hayakueleweka vizuri kwa hadhira wakati ukihubiri na yale yanayotakiwa kupewa uzito maalumu. Pia waweza kurudia kuzitamka kwa sauti dondoo za ujumbe wako kila moja. Usiwachushe (bore) kwa kuanza kurudia kuhubiri ujumbe wako wote. Mwaliko. Mwaliko ni kipengele muhimu sana katika hitimisho. Kwa sababu mahubiri ni tofauti na aina nyingine za hotuba hivyo mwaliko huwa ni muhimu sana kwa kuwa mahubiri huhusu kuchukua maamuzi au hatua juu ya kile kilichohubiriwa. Mahubiri bila mwaliko huwa hayajafikia lengo la kuhubiri. Mwaliko ni lazima katika mahubiri ya aina yoyote ile. Mwaliko huwa ni wakati wa kuitikia Kile Mungu amesema kupitia mahubiri. Ni wakati wa kutendea kazi kile kilichofundishwa au kuhubiriwa. Mhubiri anapaswa kuufanya mwaliko kuwa wazi kwa wasikilizaji wote. Lengo la mwaliko si kuwaita watu madhabahuni tu bali ni kuwahamasisha watu kuweka ujumbe katika matendo. Pia Mhubiri hutakiwa kuuweka ujumbe wake katika matendo. • Ukihubiri uponyaji waite watu madhabahuni na waombee uponyaji. • Ukihubiri kutembea katika mamlaka unatakiwa udhihishe mamlaka hiyo. • Ukihubiri utoaji waite watu kumtolea Mungu. • Ukihibiri toba unapaswa kuwaongoza hadhira kwenye maombi ya toba na kuwaita madhabahuni wale wanohitaji kutengeneza kwa upya mwenendo na mahusiano na Mungu na kuomba nao. • Wapeleke watu kwenye matendo na matumizi Mt 21:23. Yak 2:22. • Unatakiwa kuwaongoza hadhira kuomba kwaajili ya ujumbe au somo kwa kadri ya maongozi ya Mungu na kwa kadri Mungu alivyosema na kila mmoja. • Unaweza kuwaongoza watu waimbe wimbo unaoendana na ujumbe uili kuwaogoza uweponi na kuwapa hamasa. • Toa mwaliko kwa watu ambao wanataka kuokoka na kama wapo omba nao. Baada ya hapo maliza na mkabiribishe anaehusika na ratiba inayofuata. Kwa kuhitimisha juu ya sehemu tatu za ujumbe au hotuba twaweza kuvifupisha vipenele vyote hivyo vitatu kwa sentensi tatu ambazo ni: 1. Waambie hadhira kile unachotaka kuhubiri.(Utangulizi.) 2. Hubiri kile ulichowaambia (Kiini), kisha: 3. Waambie kile ulichohubiri.(Hitimisho). ZOEZI. Katika makundi ya watu watatu watatu jadilini maswali yafuatayo: 1. Jadili umuhimu wa vipengele vinne vya maeneo ya mahubiri kila kimoja. 2. Nini kitatokea kama mhubiri atatayarisha ujumbe wa mahubiri bila kuzingatia maeneo hayo. 3. Eleza umuhimu wa sehemu tatu za ujumbe wa mahubiri. 4. Mhubiri bora ni lazima azingatie sehemu tatu za ujumbe. Jadili kauli hii kwa mifano dhahiri. Kuhubiri si kazi rahisi. Kubali usemi huu kwa hoja kumi madhubuti. MADA YA TATU: AINA MBALIMBALI ZA MAHUBIRI. Kuna aina mbalimbali za mahubiri na kila aina ya mahubiri ina nafasi yake katika kuujenga na kuimarisha mwili wa Kristo na kuwaleta waliopotea dhambini. Mhubiri analazimika kufahamu aina mbalimbali za mahubiri ili aweze kuwa na ujuzi mwingi wa kuhubiri na ili aweze kuhubiri kwa kuyafanya mahubiri kuwa mapya kila ahubiripo. Kuhubiri kwa kutumia aina mbalimbali za mahubiri huwajenga wasikiliza kwa namna mbalimbali ambapo aina mojaya mahubiri isingeweza kufanya hivyo. Pia husaidia washirika na waamini kuwa na msingi mzuri wa uelewa wa Neno la Mungu. I. Mahubiri ya kifungu. Aina hii ya mahubiri hujengwa juu ya kifungu kimoja kidogo cha maandiko tu. Huhusisha kuchagua maelezo fulani maalum ya maandiko na kuyachunguza, kuchambua na kugundua kweli zote zilizomo ndani yake na kuziwasilisha kwa wasikilizaji kwa mtindo rahisi na wenye kueleweka. A. Faida za mahubiri ya Kifungu. a) Huvutia. b) Huzuia kutoka nje ya somo. c) Hufanya mahubiri kuwa ya ki- Biblia. d) Humwongezea mhubiri ujasiri. e) Husaidia wasikilizaji kulikumbuka somo. B. Jinsi ya kuandaa mahubiri ya kifungu. Kuna mambo kadhaa ambayo mhubiri anapaswa kuyazingatia wakati wa kuandaa mahubiri ya aya, badhi ya mambo hayo yamejadiliwa hapa chini. 1.Soma Biblia mara kwa mara. Unapaswa kusoma Biblia mara kwa mara ikiwa unataka kuwa mhubiri mwenye mafanikio katika huduma yako. -Tenga muda wa kusoma Biblia kila siku. Beba Biblia ndogo kila mahali unapokwenda ili upatapo muda uweze kuisoma. 2. Jifunze Biblia. Kujifunza ni zaidi ya kusoma.Kujifunza kuna husisha kusoma Biblia kwa undani kwa kuchunguza kikamilifu kila kitu kilicho katika maandiko unayosoma na kutafakari kwa kina,.Yos1:8. Unapaswa kutafakari kwa uangalifu vitu unavyosoma. Viweke kwenye akili yako na kuvifikiri tena na tena. Unapaswa kujizoesha kuchambua kile ulichojifunza. Baada ya kukichambua kwa umakini unapaswa kukiweka tena akilini. 2. Kuwa na Daftari la kuandikia. Kila usomapo Biblia yako jitahidi kuwa na kalamu na daftari la kuandika mambo muhimu unayojifunza. Jenga mazoea ya kuandika kwa ufupi kila ufunuo unaoupata. 3. Dumisha hali ya maombi. Unapaswa kuwa katika hali ya maombi kila usomapo Biblia .Omba Mungu akufunulie upate kulielewa Neno lake.Pia unapaswa kumwomba Mungu akupe usikivu juu ya kweli anazokufunulia katika Neno lake. 4. Jenga usikivu.Unapaswa kuwa katika hali ya utulivu na usikivu katika Nyanja zote yaani kimwili, kiroho na kisaikolojia. Mungu hutoa ufunuo wake kwa sauti ya kimya ndani ya roho ya mhubiri. Kama hunautulivu na usikivu wa kutosha ni vigumu kugundua maarifa hayo.. - C.Sifa za aya ya mahubiri Kifungu cha mahubiri au aya yapasa kuwa : a. Yenye mamlaka ya ki-Biblia. Mafundisho unayokusudia kuhubiri toka kifungu au aya fualani ya maandiko yapasa ikubaliane na kile Biblia nzima inachofundisha. Katika mahubiri ya kifungu kuna uwezekano wa kuchukua kimakosa mstari nje ya maana yake na kuutumia kufundishia kitu ambacho Biblia haikubaliani nacho. Ni Muhimu sana kwa ,mhubiri kujua jinsi mstari anaoshughulikia jinsi unavyokubaliana na kusudi la sura yote na kitabu chote. Daima mhubiri anapaswa kujitahidi kufasili aya yake katika nuru ya yale ambayo Biblia nzima inafundisha. b.Kamili. Aya yapaswa kuwa katika maandisha ya ukweli ulio kamilika. Baadhi ya wahubiri huchukua kifungu cha maneno katika mstari na kukitumia bila kujali maneno yaliyotangulia au yanayofuata. Jambo hili si zuri na huzaa mafundsho ya uongo. Na huku huitwa. “Kulichanganya neno la Mungu na uongo……..2Kor 4:2. Ni lazima uepuke jambo hili kwani litaleta kutokuaminika na maelezo yasiyo ya ki- Biblia na hatimae utawapotosha wasikilizaji wako. c. Fupi kiasi. Kifungu cha mahubiri chapaswa kitolewe kwenye maelezo ya maandiko ambayo ni mafupi na ya kulizisha. c. Ya kueleweka. Aya yapaswa kueleweka na iwe muhtasari wa kutosha wa kile unachotaka kukishirikisha. *Unapaswa ubaki katika mipaka ya kile ambacho aya yako inaelezea. D. Namna ya kuandaa mahibiri ya aya. a. Elewa maneno yake vema. Kipitie kifungu kwa kukisoma mara kadhaa, kitafakari na kujenga kumbukumbu juu yake na kiseme mwenyewe kwako. Hakikisha unakielewa vizuri. b. Elewa lugha yake.Tamabua lugha yake kama ina maana halisi au kama ni lugha ya mifano tu. Jiulize kama mwandishi alikuwa na maana hasa ya kile alichokiandika au maneno yake yachukuliwe kama mfano wa mahubiri? c. Changanua ujumbe wake.Chambua ujumbe unaoupata na kuutenga katika sehemu kadhaa zenye kulandana ili uweze kuuwasilisha kwa mtiririko mzuri. d. Chunguza maneno yake. Jitahidi kugundua kile maneno hayo yalikusudia kuwasilisha hapo awali. Ikiwa una kamusi ya kigiriki au Kiebrania unapaswa kulitazama neno hilo. Jaribu kubaini kama kuna maana maalumu ndani ya neno unalolishughulikia. Kufanya hivyo kutakusaidia kugundua maana yoyote maalumu ambayo mwandishi alikusudia kuiwasilisha. e. Tathmni mwendelezo wake. Baini kweli zile mwandishi alitaka kuzielezea. Tambua jinsi alivyo kamilisha katika kuziwasilisha kweli hizo. Jaribu kufuata mwongozo wake na kuuendeleza katika mtindo huo. f. Mkutadha wa kifungu.. i. Maneno ya mbele na ya nyuma ya kifungu. Angalia jinsi mistari iliyotangulia na inayofuata inachosema. Chunguza aya kuhusiana na sura nzima ambayo umetoka. Chunguza kifungu hicho katika nuru ya kitabu kizima ambamo kinapatikana. Jifunze kiini na mazingira yote ya kitabu. ii. Hali ya mila. Je mila za wakati ule ziliathiri kile kilichoandikwa? Je watu walioandikiwa kifungu hicho awali wangekuwa na wazo la kile kilichoandikwa tofauti na ambalo tungepata katika hali yetu? Kama ndivyo nini ingekuwa maana inayolingana na sasa? ii. Hali ya kihistoria. Je jambo hili liliandikwa lini? je wakati huo ulishawishi kile kilichoandikwa? Je matukio ya wakati ule yaliyokuwa yakijulikana wakati ule wa uandishi yalikuwa na maana maalum juu ya kile kilichosemwa? iv. Hali ya kijiografia. Mwandishi alikuwa wapi wakati anaandika maneno hayo? je Watu walioandikiwa walikuwa wapi?Je mazingira yao yana uhusiano wa chochote katika kile kilichosemwa? v. Biblia kwa ujumla. Kila sehemu ya maandiko ifasiliwe kwa uaminifu na kwa umakini ili ikubaliane na maandiko yote. Andiko lolote lisifasiliwe nje ya mkutadha wake. Maandiko ni lazima yafasiri maandiko. E.Kupanga Maelezo. Mpanglio mzuri wa maelezo na kazi kwa ujumla ni wa maana sana kwa mhubiri. Hakikisha unapanga maelezo yako kimaantiki. Mpangilio mzuri wa kazi na mawazo humwezesha mhubiri kulielewa vizuri somo na kulishughulikia somo kikamilifu. Pia huwawezesha wasikilizaji kulielwa somo na kulikumbuka somo . 1. Ujumbe uwe katika mpangilio.Panga ujumbe wako katika mtiririko mzuri ili uweze kuufuata kwa urahisi wakati wa kuhubiri. 2. Weka ujumbe wako katika hali ya kueleweka. Jitahidi kukamilisha vipengele vyote unavyohitaji kuviongelea katika mahubiri yako. Kabla ya kupanda mimbarini. 3. Kazia katika mawazo. Unapaswa kuyaweka mawazo yako katika sentensi fupi. Jifunze namna ya kuyaimarisha mawazo yako kwa pamoja na kuyaelezea katika sentensi fupi zinazoeleweka kwa urahisi.Jizoeze kupunguza na kulielezea wazo kwa sentensi moja. 4. Tayarisha maelezo mafupi.Kumbuka kwamba maelezo yako ili kusaidia kumbukumbu yako.unapaswa kuwa na vidokezo vitakavyosaidia kulikumbuka somo lako au ujumbe wako. 5. Ufanye rahisi kuusoma. Ni vizuri kupiga chapa mahubiri yako ili uweze kusoma kwa urahisi wakati wa kuhubiri. Pia waweza kutoa vipeperushi na vijarida kwa wasikilizaji wako ili waweze kufuatilia zaidi ujmbe au somo lako. Zoezi. 1. Eleza maana ya mahubiri ya aya. 2.Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya aya. 3.Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya aya au kifungu licha ya yaliyotajwa katika kitabu hiki. 4. Andaa hotuba ya mahubiri ya aya na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako. II. MAHUBIRI YA KUFAFANUA. Mahubiri ya kufafanua ni aina ya mahubiri ambayo huhusisha kuchagua sehemu kubwa ya maandiko na kuichunguza kwa undani na kuifasiri na kugungua kweli zilizomo katika sehemu hiyo ya maandiko na kushirikisha mkutano au usharika wako. Mfano unaweza kuamua kupitia Injili yote ya Luka sura baada ya sura. Kuanzia sura ya kwanza, unatafuta kufasili na kuelezea maana na umuhimu wake mstari kwa mstari sura kwa sura mpaka umeimaliza yote. Waweza kushughulikia sura moja kila wiki, na baada ya wiki kadhaa utakuwa umemaliza kitabu chote. A.Faida ya mahubiri ya ufafanuzi. Hufanya mahubiri kuwa ya ki-Biblia. 1. Yesu alitumia aina hii ya mahubiri. Alichukua kifungu cha Agano la kale na kufasili maana yake kwa wasikilizaji wake. 2. Petro alitumia njia hii siku ya Pentekoste. 3. Stefano alitumia njia hii. Huwezesha waamini kuwa na msingi na uelewa mkubwa wa Biblia.Waamini huimalishwa na huwa na ufahamu mzuri na wa kina wa Neno la Mungu. Kwani kweli zote zilizomo katika kitabu kilichopitiwa tayari hufahamika vizuri kwa usharika wote. Huvuta kuimalishwa na Roho mtakatifu. Roho mtakatifu hulithibitisha neno lake kwa ishara na miujiza sawasawa na Kweli zote zilizofunuliwa katika kitabu husika. Humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia. Mahubiri ya kufafanua humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia kwani mhubiri huhubiri kile kilicho katika maandiko ya eneo husika. Mhubiri huwa anajikita katika mkutadha wa aya, sura na kitabu chote kwa ujumla. Hivyo kiini cha kitabu ndicho ambacho hubeba mahubiri yake yote. Mambo ya kuzingatia katika kutayarisha mahubiri ya kufafanua. I. Kwa umakini chagua kifungu cha maandiko kinachostahili. Hakikisha kwamba kifungu hicho kitahudumia uzima na uwezo wa wasikilizaji wako. 1. Usichague somo kwa sababu linakuvutia au kukupendeza. 2. Usichague somo ambalo litazaa machafuko, mgawanyiko na mashindano. 3. Jitahidi kufanyika njia ili Mungu akupitie ili aweze kuongea Neno lake kwa watu wake kwa kupitia wewe. 4. HIvyo basi unawajibika kutafuta kujua mawazo ya Mungu kuhusu watu wake ambao amekupa wajibu juu yao. 5. Huduma hii ni moja ya heshima kuu uliopewa lakini pia ni wajibu mkuu unaoogopesha sana. Hivyo basi unapaswa kuifanya kwa umakini wa hali ya juu. II.Tafuta ujumbe unaolingana na hali ya watu ya wakati ule. 1. Mungu kila mara huwa na ukweli wa sasa ambao hutaka kunena na watu wake. 2. Mungu hukusudia jambo maalum kwa kila kundi la waamini 3. Jifunze kujua kile Mungu anacho kwaajili ya kusanyiko kwa kila wakati. III. Jifunze sura ya kitabu kwa umakini. 1. Soma sura unayoshughulikia mara nyingi mpaka umeielewa vizuri. 2. Soma kwa uangalifu mstari hadi mstari. 3. Kila kunapokuwepo na uhusiano wa wazi kati ya kifungu hicho na kifungu kingine unapaswa kusoma kifungu hicho ili uweze kupata maana zaidi. Maandiko hufasiri maandiko. 4. Jenga usikivu kwa sauti ya Roho mtakatifu ili kupokea ufunuo toka kwake. Tumia vitabu vya rejea ili kupata msaada zaidi. Mfano. Itifaki ya Biblia, Kamusi ya Biblia, Biblia ya Tafsiri nyingine.Nk IV. Kusanya taarifa muhimu. Waweza kupata vitu vingine muhimu vya kuhusisha kwenye somo lako kwa kutumia mbinu ya maswali na majibu kama ifuatavyo. 1. Nimewahi kusikia au kusoma nini juu ya somo hili? 2. Roho mtakatifu amewahi kunionesha nini juu ya somo hili? 3. Nimewahi kuona nini chenye uhusiano na somo hili ? 4. Nimewahi kuwa na mawazo gani juu ya somo hili ? 5. Naweza kupata habari zaidi ju ya somo hili kwa nani au wapi ? 5. V. Tambua kiini cha somo lako. 1. Daima tafuta kugundua kiini cha sura unayoshughulikia. 2. Tafuta kujua kile Roho mtakatifu alikusudia kuwasilisha alipoivuvia sura hiyo. 3. Gundua undani wa somo hilo. 4. Baini kile Mungu anataka kusema na watu wake kupitia sura hiyo. VI.Kuwa na Lengo kamili. Lengo lako daima lapaswa kuendana kikamilifu na lengo la Mungu. 1. Hakikisha kwamba Umegundua kile Mungu anataka kutoa kupitia maadiko hayo na kisha jizamishe katika kile Mungu anataka kufanya. 2. Unapaswa kuhisi kile Mungu anachohisi Mungu humshirikisha mhubiri moyo wake na akili yake ili waweze kufanya kazi pamoja. Unapaswa kuchangamka. 3. Fanyika chombo cha Mungu cha kupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu wake. 4. Kumbuka hukuitwa kushiriki mawazo yako na watu bali kuwashirikisha watu mawazo ya Mungu. VII. Zungumza kulingana na ujuzi wako mwenyewe. 1. Usitoe nadharia toa uhai. Hubiri kile ulicho na uzoefu nacho.kile ambacho umekifanyia kazi . wapaswa kuwa mtu kwa kwanza kula matunda ya kazi yako. 2. Umeitwa kuwa barua Sio tu kwamba unataakiwa kuuhubiri ukweli bali pia unatakiwa kuufanyia mazoezi na kuuonesha kwa matendo. 3. Unapaswa kuwa mfano hai wa yote unayoyahubiri. VIII. Upe maana ujumbe wako. 1. Unawajibika kwa uwezo wako wote, kuhakikisha kwamba maana ya kweli na umuhimu wa maandiko unakuwa wazi na wakueleweka kwa wasikilizaji. 2. Daima jitahidi kuufanya ujumbe wako kuwa rahisi. 3. Hivi ndivyo Yesu alivyofanya Hii ilisababisha huduma yake kuwa na nguvu na mafanikio. 4. Alichukua mambo yaliyokuwa mafumbo na akayaweka rahisi sana. 5. Wahubiri wengine huyachukua masomo rahisi sana na kuyafanya mafumbo magumu sana kiasi cha kutoeleweka kwa wasikilizaji wake au kuelewa kidogo. IX.Fanya ujumbe wenye kutekelezeka. 1. Daima unapohubiri jitahidi kuonesha wazi wasikilizaji wako jinsi wanavyoweza kuutendea kazi ujumbe wako. 2. Jitahidi kutoa ushauri wa kimatendo kuhusu watu wanavyotakiwa kumwitikia Mungu kwa namna ya kufaa. 3. Husianisha mahubiri yako na maazimio yako kimatendo ambayo yaweza kuwafanya watu kuwa watendaji wa Neno na si wasikilizaji tu. Zoezi 1.Eleza maana ya mahubiri ya kufafanua. 2. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya kufafanua. 3. Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya kufafanua. 4. Chagua sura mojawapo ya injili ya Yohana na kisha andaa mahubiri ya kufafanua kutokana na sura hiyo na kisha hubiri kwa dakika kumi. III. MAHUBIRI JUU YA MAISHA YA WATU. A.Utangulizi Hii huhusu hadithi ya maisha ya watu. Kwa hiyo njia hii huhusisha mafunzo juu ya maisha ya watu mbalimbali tunaosoma habari zao katika Biblia. Kila hadithi ya mtu iliyoandikwa katika Biblia ina umuhimu kwetu. Maisha ya kila mhusika aliye kwenye Biblia yana mafunzo kadhaa ambayo twaweza kujifunza. Kila habari iliyoandikwa kwenye Biblia ipo kutufundisha kitu fulani ambacho ni cha thamani sana. 1Kor 10:1-11. Mhubiri huchagua mhusika mmojawapo wa wahusika walio katika Biblia na kujifunza kwa kina kila kitu kilichotoke katika maisha ya mhusika huyo, tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Pia mhubiri hutakiwa kujifunza kuhusu nasaba na mbari ya mhusika huyo ili aweze kufahamu vizuri vitu vilivyomjenga na kumkuza mhusika, kisha hutayarisha mahubiri juu ya mhusika huyo na kuhubri katika kusanyiko lake. Mafundisho ya wahusika wa Biblia ni ya kushangaza na ya kuvutia. Katkia aina hii ya mahubiri, mhubiri hupaswa kuchagua mhusika mmoja na kusoma habari zake zote zilizo kwenye Biblia na kisha huandikia kila wazo analolipata. Hapa mhubiri anapaswa kusoma kumbukumbuzote za mhusika katika Biblia. Baada ya kusoma kumbukumbumbu hizo unapaswa kuanza kuweka pamoja mawazo yote unayoyapata katika utaratibu wa miaka yaani jinsi matukio yalivyotokea ya mhusika huyo. B. Faida za mahubiri juu ya maisha ya watu. I.Hufunua ukweli wa maisha. Biblia imeeleza wazi maisha ya wahusika kama yalivyokuwa bila kuficha chochote. Imeeleza mafanikio yao na madhaifu yao. Ukweli wa maisha ya wahusika umewekwa wazi na kwa uhalisia. Wengi wa mashujaa wa Biblia wanahitilafu zao za kibinadamu.Twajua kuwa walikuwa wanadamu kama sisi na walikutana na majaribu kama sisi. Katika visa vyote vya historia kuna mtu mmoja tu mkamirifu ambae ni Yesu kristo pekee. Hata mashujaa wakubwa wa imani walikuwa na hitilafu zao. Hii inatupa kujua kwamba wao si tofauti na sisi. Ni mifano ya kujifunzia. Ni mifano na msada kwetu. Tunaweza kujifunza kutokana nayo kuliko ujuzi wetu wa uchungu. C. Mambo ya kuzingatia a) Jifunze kuzaliwa kwa huyo mtu. b) Tafakali hali na mazingira aliyolelewa. c) Angalia uhusiano wake na Mungu katika maisha yake. d) Angalia jinsi alivyo wajibika kuhusu uhusiano wake na Mungu. e) Baini vitu alivyojifunza kutokana na mahusiano yake na Mungu. f) Tathimini mafanikio yake. Jifunze vitu vilivyomfanya afanikiwe. g) Tazama maeneo aliyokosea kama yapo. Na jifunze vitu vilivyomfanya akosee. h) Toa hitimisho kile tunachoweza kujifunza kutokana na maisha ya mtu huyo. Mambo hayo yote yanavutia na ni yenye vitu vingi vya Kutufundisha ambayo twaweza kujifunza kutokana na watu hao. Tunaosoma habari za maisha yao katika Biblia. D. Hatua za kufuata katika kuandaa mahubiri juu ya maisha ya watu. I. Chagua mtu au msusika toka kwenye Biblia. Unapaswa kuanza na watu mashuhuri katika Biblia ambao habari zao ziko wazi kabisa, kama vile Ibrahimu,Musa,Samweli, Daudi, Yusufu, Debora, Miriamu, Mariamu, Dorkasi, Paulo, Petro. N.k. Hawa ni baadhi ya watu ambao matendo yao yamefanyika kuwa nuru katika historia ya ushusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Kuna mambo mengi sana ambayo twaweza kujifunza kutokana na maisha yao. Aina hii ya mahubiri ni nzuri sana, kujifunza toka kwa wacha Mungu wenzetu waliotutangulia katiki wito na huduma hii ni jambo la msingi sana. 1Kor 10.1-11. II. Chunguza maisha yake. Anza kwa kusoma hadithi inayoelezea kuzaliwa kwa mtu huyo. Tafuta maana ya jina lake. Kwani jina lina maana sana ki-Biblia. Angalia kwa umakini kusudi la Mungu katka maisha yake. Ili uweze kuvumbua vitu vingi unapaswa kujiuliza maswali yafuatayo: 1. Mungu alitaka kutekeleza nini kupitia mtu huyu ? 2. Je Mungu alifanya nini ili kusudi lake lijulikane kwa mtu huyu? 3. Mtu huyu aliitikia vipi Mungu alipomjulisha kusudi lake? 4. Tunaweza kujifunza nini kutokana na Mungu kuhusika katika maisha yake ? 5. Kuna tahadhari zozote ambazo tunapaswa kuzichukua ? 6. Je siri ya mafanikio yake ilikuwa nini ? 7. Je mwisho wa maisha yake ulikuwaje ? III. Chambua somo na kisha hubiri. Baada ya kujiuliza maswali hayo na kupata majibu utakuwa umepata vitu vingi ambavyo waweza kuvichambua kwa umakini na kuandaa somo kisha na kulihubiri somo hilo katika mpangilio na mtiririko Mzuri wa mawazo. Mwombe Roho mtakatifu akupe ufunuo zaidi unapokuwa ukihubiri somo lako na lifanye somo lako kuwa na uhalisia katika maisha ya sasa ya wasikilizaji. Zoezi 1.Eleza maana ya mahubiri ya wahusika au maisha ya watu. 2. Tengeneza orodha ya watu mashuhuri walio katika Biblia. Orodha hiyo ihusishe wanawake na wanaume. 3. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya wahusika. 4. Chagua mhusika mmoja wa kike au wa kiume na kisha andaa mahubiri kwa kumtumia mhusika huyo na kisha hubiri kwa dakika kumi. IV. MAHUBIRI YA MIFANO HALISI NA VIVULI. Huu ni ujuzi unaohusu kuweka wazi au kuchimbua na kuwasilisha ukweli uliojificha wa mifano mbalimbali katika Biblia. Mfano ni kitu, mtu au tukio ambalo kinabii ni ishara ya kitu au mtu fulani atakaetokea baadae. Inafanana au ni mfano wa Yule mtu au tukio. Katika matumizi ya Biblia ina maana ya mtu wa Bibli au tukio litakaloonesha kitu fulani kitakachotokea. Mfano mwanakondoo katika kitabu cha Kutoka ni mfano wa Bwana Yesu. Kila kitu kuhusu kondoo wa pasaka kiunabii kilikuwa na maana ya ukombozi wa wajibu ambao Bwana Yesu Kristo angetimiza.Yn 1:29. Mifano ya Biblia mara nyingi inaonekana kama kivuli(type) cha mambo yanayokuja baadae. Ebr 8:5,10:1. Siku takatifu pia katika agano la kale zilikuwa vivuli juu ya mambo ambayo yalikuwa yanakuja. Kol 2:17. Hizo siku takatifu hazikukamilika zenyewe sehemu ya kusudi la kutimizwa kwake ilikuwa ni kutanguliza sura ya kinabii ya vitu ambavyo vilikuwa bado vinakuja. Kanuni za kutumia. a. Unapojaribu kwa mara ya kwanza kufundisha kwa kutumia mifano ya kwenye Biblia, zingatia misingi ifuatayo. I. Tumia mifano rahisi zaidi. Anza na mifano rahisi ambayo maana yake iko wazi. II.Endelea na tafsiri ya wazi. Usijaribu kufasiri kila kitu.Elezea ukweli wote kama ulivyo na wala si kutafuta kila kipengele chake na kukielezea kwa undani. III. Usitumie maneno makavu. Usitumie mifano ya kufundishia kama kanuni. IV.Sisitiza ukweli wa msingi. Usitumie nafai uliyonayo kwa kutoa mifano ya kufundishia. Mifano itumike kusisitiza mafundisho na si kutumia kama chanzo cha ukweli. V. Uwe tayari kusahihishwa. Uwe tayari kusahihishwa na kukosolewa na wale waliokomaa kuliko wewe ili uweze kujifunza zaidi. 4. Kuelezea kusudi. Ni njia ambayo kwayo mhubiri hupanua maana ya ukweli ulio katika kifungu maalum cha maandiko. Unatafuta namana ya kuuweka wazi ukweli ambao umejificha ndani ya kifungu. Hii njia nzuri sana ya kufundishia kusudi lote la ki-Mungu. Mdo 20:27. Zoezi 1. Eleza maana ya vivuli na mifano.(Types). 2. Taja hatua za kufuata katika kutayarisha na kuhubiri mahubiri ya mifano na vivuli. 3. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya mifano na vivuli. 4. Tayarisha mahubiri ya mifano na vivuli na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako. V. MAHUBIRI YA MADA. Aina hii ya mahubiri hukusudia kutoa kiini maalum kwa hadhira.Mhubiri huchagua somo fulani kisha huchunguza kila kitu ambacho Biblia inasema juu ya somo hilo. Baada ya kuchunguza na kuchambua, kweli hizo huandikwa katika mapngilio wa somo. Mhubiri hupitia vifungu mbalimbali vya maandiko vinavyohusu somo hilo. Aina hii ya mahubiri huhitaji maandalizi ya muda mrefu na utulivu mwingi. Pia huwasilishwa katika mfululizo wa vipindi kadhaa na si kimoja, kwa sababu ni vigumu kupitia kweli zote zilizo katika somo kwa kipindi kimoja tu. Mfano wa mada za kuhubiri. 1. Upendo wa ki-Mungu 2. Ubatizo wa Roho mtakatifu 3. Maombi ya kufunga. 4. Nguvu ya usaidizi. 5. Vita vya kiroho. 6. Kutambua Ulimwengu wa roho. 7. Kutembea katika mamlaka. 8. Nguvu ya madhabahu. 9. Kushughulikia majira na nyakati. 10. Kutii mamlaka. Mambo ya kuzingatia katika mahubiri ya mada. 1. Uwe na ufahamu wa kutosha juu ya somo husika. 2. Fanya maandalizi ya mudamrefu na ya kina 3. Unapaswa kuwa na lengo mahususi la mahubiri yako. 4. Gawa somo katika vipengele vidogovidogo. 5. Kila kipengele lazima kiwe na maandiko yanayokithibitisha na kukielezea 6. Andiko liendane na dondoo unayoitoa. Zoezi. Somo hili lipo kimatendo zaidi. Kila mwanafunzi ashiriki katika kufanya mazoezi ya kuandaa mahubiri na ahubiri katika dakika zilizopendekezwa au mwalimu atakazopanga kulingana na muda uliopo. Mwalimu anatakiwa kusimamia na kusahihisha kazi za wanafunzi na kutoa marekebisho katika maeneo ambayo wanafunzi hawajafanya vizuri. 1.Andaa Ujumbe kwa kutumia aina ya mahubi ya mada na kisha hubiri mkutano kwa dakikika kumi. Chagua mada yoyote. 2.Taja ubora na udhaifu wa mahubiri ya mada. 3. Taja mambo mengine matano muhimu ya kuzingatia katika kuandaa mahubiri ya mada. 4. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri ya mada na mahubiri ya kufafanua. VI.MAHUBIRI YA MATUKIO. Mahubiri ya matukio ni kipengele katika mahubiri ya maada, lakini kutokana na umhuhimu wake tumekitenga na kukielezea peke yake. Mahubiri haya ni mahubiri ambayo huandaliwa kutokana na tukio lilipo au ambalo litafanyika katika kipndi fulani. Kiini cha mahubiri haya huwa ni tukio ambalo linafanyika katika ibada hiyo.Mfano wa matukio hayo ni Tukio la, 1. Kusimikwa kwa uongozi wa kanisa. 2. Ndoa au kumuaga bnti. 3. Kubariki watoto. 4. Ushirika mtakatifu 5. Ubatizo 6. Kuweka wakfu vitu mbalimbali. 7. Kuhitimu mafunzo.(graduation) 8. Msiba na mazishi. 9. Sikukuu mfano Pasaka, mwaka mpya, N.k Mambo ya kuzingatia 1. Mahubiri haya yanapaswa kuendana na tukio husika. 2. Mhubiri anatakiwa kufahamu ratiba nzima ya tukio hilo au shughuli hiyo. 3. Mhubiri ahubiri kulingana na tukio husika. 4. Mhubiri aepuke kutumia muda mwingi katika mahubiri. 5. Mhubiri ahubiri kwa lugha itakayoeleweka na kusanyiko lote na lugha yapaswa kuwa rahisi. 6. Mahubiri yapaswa kugusa kusanyiko lote. 7. Mhubiri anapaswa kuhubiri kwa upendo. 8. Mhubiri azingatie ratiba ya tukio. ZOEZI. 1. Chagua tukio mojawapo na kisha andaa mahubiri juu ya tukio hilo na hubiri kwa dakika 10 .2. Taja mabo mengine kumi ya kuzingatia katika mahubiri ya matukio. 3.Eleza ubora na udhaifu wa mahubiri ya matukio. MADA YA NNE MHUBIRI. Malengo ya mada. • Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi anataweza. • Kueleza maana ya mhubiri kwa mitazamo mbalimbali. • Kuelza wasifu wa mhubiri. • Kueleza vidokezo mbalimbali kuhusu mhubiri. A. Utangulizi. Mahubiri yana mwanzo wake katika Agano la kale. Wakati manabii walipotangaza neno la Mungu kwa watu wa kale. Manabii walikuwa wahubiri wa kwanza katika agano la kale. Mungu ameamua kuwachagua na kuwatumia watu wa kawaida kulitangaza Neno lake.Amewachagua wanawake na wanaume kuwa vyombo vya kulitangaza neno lake kupitia huduma ya kuhubiri. Ufafanuzi Neno mhubiri (kwa kigiriki kerux) limetumika mara kadhaa katika agano jipya ambapo humaanisha kutangaza. (Rumi 10:14, 1Tim 2:7, 2Tim 1:11, 2Pet 2:5. Unapolitazama neno hili (mhubiri) halijikiti na kuishia kwenye huduma moja au huduma fulani tu bali linahusisha zile huduma zote tano za uongozi wa kanisa. Ikijumuisha mitume, manabii waijilisti,wachungaji na waalimu. Pia linajumuisha kila mtu atangazae neno la Mungu. Hata kama hana mojawapo ya zile huduma tano za uongozi. Ingawa hudma zote hizi zinawasifu wake kila moja lakini zote zaangukia katika neno moja “Mhubiri”. Inavutia kutambua kwamba neno la Kigiriki lililotafsiriwa kama mhubiri linaelezea mtu anaeongea kwa mamlaka , anaewasilisha ujumbe bila kikwazo au kizuizi chochote. Hii hudhihirisha mamlaka iliyo juu ya mhubiri. Mhubiri ni mtu yeyote anayehubiri Injili. • Mhubiri ni mtu anayetumiwa na Roho mtakatifu katika kuwasilisha kweli za ki-Mungu kwa njia ya hotuba. • Mhubiri ni mtangaza ujumbe wa Mungu. • Yeye ni msemaji wa Mungu. Husimama katika nafasi ya Mungu na kuzungumza kwa niaba yake Mungu. Hivyo ni lazima mhubiri awa na sifa zinazostahili ambazo zitamfanya kuwa na mamlaka. B.Sifa za mhubiri. Mhubiri ni lazima awe na sifa stahilifu ambazo zitamfanya awe na mamlaka na thabiti katika wito na huduma yake. Badhi ya sifa hizo zimeorodheshwa hapa chini. 1. Awe ameokoka (Amezaliwa mara ya pili). 2. Awe amejazwa Roho mtakatifu. 3. Awe na wito halisi (Wito ulio wazi na wenye ushahidi). 4. Ajazwe na Neno la Kristo ndani yake Kol 3:16. 5. Awe mtu wa maombi. 6. Awe mwadilifu.( Mkweli na mchaji Mungu na mwenye kuchukia mapatato ya udhalimu ) 7. Awe na nidhamu. 8. Aishi kulingana na wito wake. 9. Asiwe mvivu. 10. Awe na baba wa kiroho. Kuna tofauti kubwa kati ya hotuba na ujumbe.mtu anaweza kujifunza jinsi ya kuandaa hotuba kupitia masomo ya Homiletics lakini Mtu anapaswa kuwa na ushirika na Mungu ili aweze C. Kujihusisha binafsi katika kuhubiri. 1. Unapaswa kuwa kawaida. Unatakiwa kutulia na kuwa vile ulivyo. Mugu hutaka kutumia utu wa kila Mhubiri katika kuwasilisha Neno lake. Unatakiwa kujikubali hivyohivyo ulivyo. Mungu anapendezwa nawe na ndiyo maana amekuita hivyo ulivyo. Usijichambue sana. 2. Kuwa wa kipekee. Unatakiwa kuutayarisha ujumbe wako na kuuwasilisha kwa njia ya kipekee ili uweze kuleta matokeo ya kipekee. Unapasa kutumia utu wako wa kipekee Mungu aliokupa na kumwacha Mungu atumie utu na maisha yako kwa njia maalum ya kipekee anayotaka yeye. 3. Kuwa rahisi. Unapokuwa ndiyo unaanza kuhubiri au kusimama mimbarini kwa mara ya kwanza unatakiwa usijaribu kutumia ufasaha au kuingia ndani mno katika kuhubiri. Huhitaji kuwavuta watu. Upo pale kwa lengo la kuwahudumia na si kuwapendeza. 4. Kuwa huru. Unatakiwa kuwa huru unapohubiri na ujifunze kujizoeza hali mbalimbali. Ufanye mtindo wako wa mawasiliano utiririke kawaida na kwa uhuru. Kila kusanyiko utakalo hubiri linatofautiana na lingine, hivyo unapaswa kujizoeza hali mbalimbali. Mungu huwa na lengo maalumu analotaka kufanikisha katika kila ibada na mhubiri ndiyo ufunguo muhimu katika kutekeleza hili. Kuwa huru na msikivu kwa Roho mtakatifu.Roho mtakatifu anaweza kufanya hali za jinsi mbalimbali katika kila ibada.Wasikilizaji wako wakati mwingine waweza kuwa wachangamfu na wakati mwingine wakimya na wanyenyekevu. 5. Tambua njia ambayo Mungu anapitia na utembee nae. 6. Dhihilisha mamlaka..Hakikisha Kuna madhihirisho ya nguvu za Mungu katika kila ibada unayohubiri. Hakikisha Bwana anakithibitisha kila unachokihubiri kwa ishara na maajabu. Hubiri kwa uthibitisho D. Zana za mhubiri. Kuna vitu kadhaa ambavyo ni muhimu kwa mhubiri yoyote . Bila vitu hivo kazi ya Kuhubiri itakuwa haijafanikiwa au kufika lengo kwani wasikilizaji watakuwa wameachwa njiani. Baadhi ya zana hizo ni: I. Maono. Kila mhubiri nilazima awe na maono katika huduma yake na wito wake. Wazo la kile ambacho huduma yako itafanikisha kwa Mungu. Maono ni picha au taswira juu ya kile unachohitaji kukifikia katika huduma yako. Kumbuka kwamba bila maono watu huangamia Mit 29:18. Ni maono pekee yatakayokuweka salama. Usipokuwa na ufahamu wa kuhusu kusudi la Mungu alilonalo kwaajili yako ,waweza kulemewa na kuishia n jiani na kushindwa kufikia lengo la –ki-Mungu ulilochaguliwa kwalo. II.Msamiati. Msmiati ni jumla ya maneno yaliyo katika lugha fulani. Msamiati wamhubiri hujumuisha maneno yote anayoyajua na kuyazoea kuyatamka. Maneno ni dhana ambayo mhubiri hutumia katika kutimiza wito wake. Muhubiri anatakiwa kuwa mahili wa lugha. Jifunze msamiati mbalimbali na matumizi yake.Silaha yetu kuu ni maneno katika kazi ya kuhubiri. Maneno huundwa na msamiati. Soma vitabu mbalimbali ili uweze kujitajirisha na msamiati. Unapokutana na neno usilolifahamu lichunguze na kutafutamaana yake na matumizi yake. Pia mhubiri anatakiwa afahamu kutumia msamiati mbalimbali katika kazi yake ya kuhubiri. Tambua matumizi ya Lugha kulingana na mahali. Jifunze misimu, Rejesta na misemo mbalimbali inayotumika katika Lugha husika. Hii itakusaidia unapohubiri uweze kuwagusa watu wote waliopo katika eneo hilo. Mhubiri ni lazima ajifunze namna ya kutamka maneno sahihi. Jifunze kutumia lafuzi vizuri na kuepuka athali za lugha mama katika Lugha unayotumia kuhubiri. Kuwa na lafuzi nzuri na kuongea lugha kwa ufasaha hukupa kukubalika kwa wasikilizaji wako na kupewa usikivu. Tumia Lugha inayoeleweka na wasililizaji wako, lakini lugha hiyo yapaswa kuwa sanifu au fasaha III. Sauti. Sauti ndiyo chombo kikuu mhubiri anachotumia katika kuhubiri. Ni lazima mhubiri kujifunza mitindo mbalimbali ya sauti na namna ya kuitumia sauti yake. Jifunze matumizi ya sauti katika mahubiri yako. Sauti yako inapaswa kusikika na wasikilizaji wako lakini haipaswi kuwa kubwa sana kiasi cha kuwaumiza. Fahamu mahali pa kutumia asuti kidogo na mahali pa kuongeza sauti. Hubiri kwa mitindo mbalimbali ya sauti. Zingatia kiimbo, toni na kidatu unapohubiri. E. Kanuni za Kuhubiri Katika kipengere hiki tutaajadili baadhi ya kanuni chache za kuzingaita katika mahubiri ya hadharani. Mhubiri anapswa kufuata na kuzingatia kanuni hizi ili aweze kufanikisha lengo la mahubiri 1. Kuvuta hewa. Kuvutahewa sahihi ni muhimu kwa mhubiri. • Vuta hewa nyingi kiasi cha kufika mapafuni. • Jizoeze kujaza hewa kifuani na kwenye mapafu. • Izuie na kisha itoe nje polepole.Dhibiti utoaji wa hewa. Iache hewa itoke chini ya mapafu kupitia sanduku la sauti na kugusa ukuta wa juu wa mdomo. • Jifunze jinsi ya kupumua ili usiishiwe pumzi wakati wa kuhubiri. 2. Utamkaji mzuri wa maneno. Jitahidi kutamka maneno vizuri na waziwazi. Hakikisha kila neno unalolitamka linasikika vizuri kwa wasikilizaji wako. Usilete kikwazo kwa wasikilizaji wako kwa kutosikika vizuri. 3. Ubadilishaji wa sauti. Hii inahusu kuifanya sauti kuwa nene au nyembamba. Sauti ya kila mwanadamu inahali mbalimbali. Jitahidi kutumia aina mbalimbali za sauti. Ukitumia aina moja ya sauti yaweza kuwachosha wasikilizaji wako. Tambua maeneo unayotakiwa kuongea kwa sauti ya chini na sauti ya juu. Endeleza viwango tofauti vya sauti yako. Ubadilishaji wa ukubwa wa sauti waweza kusisitiza kipengere fulani muhimu. Baadhi ya wahubiri huona ni muhimu sana kuhubiri kwa sauti kubwa sana kiasi chakuumiza masikio ya wasikilizaji . Jaribu kuepuka hili. Iwapo ujumbe wako wote utawasilishwa kwa sauti kubwa au ya juu itakuwa vigumu kusisitiza jambo maalum katika zile sehemu ambazo ni za maana zaidi. 4. Kasi ya kuongea. Kasi unayotumia kuongea ni muhimu sana katika mahubiri. Baadhi ya wahubiri huhubiri kwa kasi moja tu . hii si nzuri, pia yaweza kuwachosha wasikilizaji. Sehemu kubwa ya ujumbe wako yapaswa kuwasilishwa kwa mwendo na kasi ya kawaida ya mazungumzo. Katika maeneo mbalimbali ni lazima kuongeza au kupunguza mwendo ilikuleta tofauti na msisitizo zaidi katika mahubiri yako. 5. Kupumzika kidogo. Usiongee mfululizo bila kuwa na vituo. Kupumzika kidogo wakati wa kuongea au kuhubiri ni muhimu pia kwaweza kuongeza msisitizo kwenye maeneo ya muhimu. Kuongea mfululizo kwaweza kusababisha wasikilizaji washindwe kusharabu mambo ya muhimu katika akili zao. Usipitie ujumbe kwa kukimbia na kuongea kwa haraka bila kuvuta pumzi. Hadhira wanahitaji muda wa kufikiri na kuchambua kile ulichosema, Hii inasaidia sana kusharabu ukweli wa ujumbe wako. Unahitaji kuzifahamisha akili pamoja na kuzichangamsha hisia za hadhira. Kama ukihubiri kwa haraka tu bila kupumzika utawaacha hadhira wako nyuma. 6. Kurudia. Kurudia sehemu za msingi wakati unahubiri ni jambo la msingi sana. Inasaidia kusisitiza vipengere na kushindilia kwenye akili za wasikilizaji. Unatakiwa kukielezea kipengere kwa njia mbalimbali. Usisite kurudia eneo unalohisi wasikilizaji wako hawajakuelewa vizuri. F.Vidokezo muhimu kwa mhubiri. 1. Uwe vile ulivyo.Usijaribu kutokeza sura ambayo si ya kweli. Kuwa vile ulivyo ndiyo njia pekee inayoweza kukufanya utulie.usijaribu kumwiga mhubiri mwingine yeyote ukifanya hivi itakusababishia kutoaminika kwa hadhira wako.Jitahidi kuwa mhubiri bora na si kuwa mhubiri mkuu. 2. Usijenge sauti ya kidini. Baadhi ya wahubiri wamejiundia sauti za mimbarini ambazo ni tofauti na sauti zao za kawaida.Hii huleta kutokuaminika na kuonesha kana kwamba unamwiga mtu mwingine. Jizoeze kuhubiri kwa kutumia sauti ya kawaida na unayotumia katika mawasiliano katika maisha ya kila siku. Hii huonesha ukweli na uaminifu katika mahubiri. 3. Usiongee kwa sauti ndogo mno. Hakikisha kwamba kila mmoja katika mkutano wako anakusikiliza vema. Usifanye wachoke kwa sababu ya kutokukusikia vizuri. Ikibidi uliza je kila mmoja ananisikia vizuri ? Si vizuri kuendelea kuhubiri na hali kuna baadhi ya watu hawakusikilizi. 4. Usipige kelele. Jitahidi kuongea kwa sauti ya kawaida ya maongezi ambayo inaweza kuongezwa kiasi kufuatana na wingi wa makutano na kama huna au una vyombo vya kupazia sauti. Sauti iongezwa kulingana wingi wa hadhira. 5. Kumbuka kubadili kasi na upeo wa sauti ya mahubiri kukwepa kuchosha hadhira. 6. Ufanye mkutano ukukubali. Pata matumaini ya hadhira.Hakikisha mkutano wako unakukubali.. Kama mkutano wako hawakukubali nidhahiri kabisa kwamba hawataupokea ujumbe wako. 7. Vaa vizuri. Ni jambo la maana sana kwa mhubiri kuvaa mavazi ya heshima na safi. Namna ulivyo vaa yaweza kuharibu ujumbe wako.Hakikisha uvaaji wako hauvurugi ujumbe wako. Vaa kulingana na tamaduni za taifa husika. 8. Jifunze kusimama vizuri. Ni vizuri sana kusimama wakati unazungumza au kuhubiri. Simama vizuri kwa miguu yote miwili.. Simama wima ukitazamana na hadhira wako. Usipende kuegemea kitu chochote. Kama kuna mimbari itumie kuwekea Biblia na zana zako za kuhubiria. Kusimama wima kutakusadia katika kuvuta hewa. Watazame hadhira wako wakati wote unapohubiri. Hubiri kwa kumgusa kila mtu. Kila mtu ajione kwamba unaongea na yeye binafsi. 9. Jifunze kutembea wakati unahubiri. Usisimame mahali pamoja kana kwamba umefungwa.Jizoeze kutembeatembea wakati unahubiri. Mwili wako unaleta ujumbe sawaswa na sauti yako.Tumia ishara wakati unahubiri lakini epuka ishara sisizo na umuhimu. Kama unaeleza juu ya kitu fulani ni kawaida kuelezea jambo hilo kwa mikono yako. Ishara za namna hiyo zinapaswa kutokea zenyewe kiasili bila kuzilazimisha. 10. Endeleza uhuisano na hadhira. Macho ya mhubiri huelezea ujumbe pia. Usiangalie hewani au juu ya vichwa vya watu. Waangalie watu unaowahubiri moja kwa moja. Kila mmoja atambue kwamba unamwangalia yeye binafsi. 11. Jifunze kutawala mkutano. Hakikisha unatawala kusanyiko. Watu wote wako pale kukusikiliza wewe hakikisha kila mmoja anakusikia. Zungukia watu wako nakuwashitua wanao lala au kusinzia. Tafuta namna itakayosababisha watu wote kukusiliza kwa makini. 12. Omba upako wa Roho mtakatifu. Mwombe Mungu akupake mafuta daima. Hakikisha utendaji wa Roho mtakatifu upo katika mahubiri yako. F. Matumizi ya muda katika mahubiri. Ni lazima mhubiri ajifunze matumizi sahihi ya muda katika mahubiri. Jambo hili ni la muhimu sana na lisipozingatiwa huweza kuvuruga kazi nzima ya kuhubiri. Ni lazima kuamua muda utako tumia kuhubiri kabla ya kupanda mimbarini. Utafiti kule Marekani umeonesha kwamba watu huanza kupoteza usikivu wao baada ya dakika ishirini tu za mahubiri. Waweza usikubaliane na matokeo ya utafiti huo lakini unatakiwa kukumbuka kwamba akili ya mwanadamu inakiwango cha kuelwa na muda wa kuelewa. Muda ukizidi kila kinachoongelewa au kuhubiriwa huwa hakisharabiwi kwani akili hufikia upeo wa kuelewa na kushika mambo. Upako wa Roho Mtakatifu huhuisha akili za wasikilizaji kwa kiwango fulani lakini mhubiri aepuke kuwachosha wasikilizaji. Ni vizuri sana kumaliza ujumbe wako wakati watu wanatamani uendelee na ni vibaya sana kumaliza ujumbe wako wakati watu wanataka umalize. Jitahidi kuzingatia muda katika kazi yako ya kuhubiri. Kwa kawaida ujumbe unapaswa kutumia dakika arobaini na tano. Utangulizi uwe na dakika tatu hadi tano, Kiini kiwe na dakika ishirini na tanno hadi therathini. Hitimisho liwe na kakika tatu hadi tano. Ujumbe wote usizidi dakika arobaini Vinginevyo utawaacha wasikilizaji wako. Ukitaka kuhubiri kwa muda mrefu hakikisha ujumbe wako unauvuvio mwingi. Spurgeon alisema” tumia muda mwingi katika matayarisho ili uweze kutumia muda mchache katika kuhubiri” Kutumia muda mrefu katika kuhubiri hakukufanyi ueleweke zaidi wala hakufanikishi zaidi lengo la kuhubiri. Tambua cha kusema. Kiseme na kisha maliza. Unapokuwa umealikwa na mhubiri mwingine kuhubiri unapaswa kumuuliza muda ambao yeye hutumia katika kuhubiri na muda wa kumaliza mahubiri. Unapokuwa unahubiri zingati muda ulioelekezwa na mwenyeji wako na uwezo wa kuelewa wa wasikilizaji wako. Mgeni akija kanisani kwako kama hukumwandaa kuhubiri kabla si vizuri kumpa madhabahu ili ahubiri. Kwani kuhubiri ni kazi nyeti sana na inahitaji maandalizi ya kutosha. Maelezo haya hayazuii mwongozo na maelekezo ya Roho mtakatifu. Lakini ni vizuri kumwandaa mhubiri mapema ili awe na muda wa kuafanya maandalizi. Usiwashitukize watu kuhubiri. Ni lazima uwe na heshima kwa kazi hii kwani Mungu mwenyewe anaiheshimu sana. Usihubiri ujmube au somo ambalo mwenyeji wako hakubaliani nalo. Kama kuna ulazima fanya nae mazungumzo kabla ya kuhubiri au tafuta namna utakayotumia kuhubiri na kufanya akubaliane na kile unachohubiri. Jambo hili ni muhimu sana na linapaswa kuzingatiwa. Mahubiri na mazingira. Mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyopatikana na kuzunguka eneo fulani. Mazingira ni muhimu sana katika kufanikisha kazi ya kuhubiri. Ni lazima mazingira yawe safi hasa ikiwa mahubri yatafanywa katika eneo fulani maalum. Mfano kanisani, uanjani au eneo lolote rasmi. Kuna baadhi ya mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa. Baadhi ya mambo hayo yameorodheshwa hapa chini. 1. Watu wanaokuja kwa kuchelewa wakae katika viti vya nyuma. 2. Mimbari inapaswa kuwekwa mahali sahihi panapoonekana na watu wote bila shida. 3. Lango la kuingilia lapaswa kuwa mahali sahihi. 4. Akina mamawenye watoto wadogo wakae eno maalumu. 5. Watoto wanapaswakutengewa sehemu yao ya kukaa kama hakuna kanisa la watoto. 6. Mwanga na hewa ya kutosha ni kitu muhimu sana katka eneo lolote. G. Jaribu kuu la Mhubiri. Wahubiri wengi hujisulisha na kutafuta chakula kwajili ya watu wengine na kujisahau wenyewe. Huu ni mtego mkubwa katika kazi ya kuhubiri na ni moja ya hatari za huduma. Wakati mwingine mhubiri aweza kujishughulisha sana na kutafuta haki za kiroho za kundi lake na kwa masikitiko makubwa anasahau zile za kwake mwenyewe. Hii ni moja ya sababu kuu zinazomfanya mhubiri kushindwa. Sulemani anasema katika kitabu cha Wimbo ulio bora “”’ Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu bali shamba langu mwenyewe sikulilinda” Mhubiri ni lazima ajali kwanzai maisha yake mwenyewe ya kiroho. Mhubiri anapaswa kulipa neno la Mungu nafasi ya kuchipua ndani ya moyo na roho yake. Aliache likue kwa nguvu katika maisha na ujuzi wake. Halafu atakapohubiri atahudumu kutokana na ujuzi. Hataongea kamwe kama mwenye nadharia bali atashirikisha vitu ambavyo yeye mwenyewe anavielewa kikamilifu na ana ujuzi navyo. Paulo anasema hivi. “Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza kupata fungu la matunda”. ( 2Tim 2:6 ). Hii inatufundisha kwamba unachopanda na kuvuna ( kiroho) yapasa ule (ujuzi)- kabla ya kulisha wengine. Huwezi kulisha wengine kile ambacho wewe mweyewe hujakila kwanza. Huwezi kujaribu kuongoza wengine katika njia na mapito ambayo wewe mwenyewe hujapitia. Jinsi Neno la Mungu linavyokuwa dhahiri katika maneno yako ndivyo wewe unafanyika ujumbe toka kwa Mungu. Hutakuwa mtu anaye kariri somo tu bali mtu ambaye uhai wake binafsi na mtindo wake wa maisha huhudumia uhai, Baraka na nguvu kwa wale wanaomfahamu na kumsikia. I.Hitimisho. Mahubiri mazuri hayaji kirahisi wala hayatokei tu. Ni matokeo ya vitu vingi. Kama tulivyotazama huko nyuma kwamba mahubiri huanza na wito wa mhubiri na wasifu wake.Pia huhusisha maandalizi ya kutosha kwa kuomba na kusoma kwa bidii. Kilele cha mahubiri ni katika kuwasilisha ujumbe. Ujumbe hauwi ujumbe mpaka umewasilishwa. Ujumbe ulioandaliwa vema utakuwa ujumbe wa kiungu pale Roho mtakatifu atakpoupaka mafuta. Mahubi mazuri daima yataleta matokeo mazuri. Mahubiri mazuri dama yatamtukuza Mungu na si mhubiri au mtu mwingine yeyote. Yatawaongozawatu msalabani na kuwafanya kuwa wanafunzi. Angalizo.Mhubiri hapaswi kutwaa utukufu kwa namna yoyote ile katika kila inachotokea katika kazi yake ya kuhubiri. Daima anapaswa kumpa Mungu heshima na utukufu kwa kila kinachotokea. HOMILETICS. MADA YA KWANZA. MAHUBIRI. Malengo ya mada. Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi aweze.  Kueleza maana yamahubiri.  Kueleza maana ya kuhubiri.  Kueleza wito wa kuhubiri ulivyo.  Kueleza umuhimu wa kujifunza homiletics. A. UTANGULIZI Katika kozi hii tutashughulikia mojawapo ya kazi kuu ya kanisa. Mojawapo ya wajibu mkuu ambao umewekwa mikononi mwa kanisa ni kuhubiri ujumbe wa Mungu yaani Injili. 1Kor 1:21 a) Ni amri iliyo wazi toka kwa Bwana Yesu kwa wafuasi wake. Mk 16:15. “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe”. b) Kuhubiri ni mojawapo ya kazi ya thamani sana ambayo Mungu ametupa. Kuwa msemaji wa Mungu, yaani Mjumbe wa Kristo. 2Kor 5:20. c) Kuhubiri ni wajibu mkuu. Rumi 10:14-15. d) K wa njia ya mahubiri Mungu alichagua kujidhihirisha mwenyewe kwa mwanadamu. B. MAANA YA MAHUBIRI. Neno mahubiri linatokana na maneno mawili ya kigiriki ambayo ni homileo na homilia yenye maana ya ‘kuwa pamoja na, kuongea na kuwasiliana. a) Homily pia humaanisha ujumbe au hotuba. b) Elimu inayohusu namna ya kuhubiri huitwa Homileticts. c) Homiletics ni ustadi wa kuhutubia au kuhubiri. d) Mtaalamu wa elimu ya kuhubiri huitwa Homilist e) Homiletics huhusisha kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri au kutunga hotuba. f) Mahubiri huhusu kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri masomo ya Biblia. g) Mahubiri ni ujuzi wa kuhubiri. h) Ni elimu au taaluma inayohusu kuhubiri Neno la Mungu. i) Ni elimu inayohusu namna ya kuhubiri.{ somo juu ya kila kitu kinachohusiana na kuhubiri}. j) Kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu. Mungu hutumia watu wake aliowachagua kuhubiri ujumbe wake. k) Ujumbe unapaswa kuwa ujumbe wa Mungu Kitu kingine chochote si mahubiri ila ni maoni na falsafa za kibinadamu tu. l) Kuhubiri ni lazima kuwe ni kutangaza binafsi na si kusoma au kuandika Dr. Martyn Lolyoyd Jones alisema “ Wahubiri huzaliwa na hawafanywi kamwe. Kamwe hutamfundisha mtu kuwa mhubiri kama yeye si muhubiri. Lakini mhubiri wa kuzaliwa unaweza kumsaidia na kumwendeleza akawa mhubiri bora kwa njia ya mafunzo” 1. -Mhubiri si chanzo cha ujumbe.Mungu ndiye chanzo cha ujumbe na mhubiri ni bomba au mfereji ambako Mungu hupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu aliowakusudia. Ujumbe wa Mugu hutiririka kupitia utu wa mhubiri. 2. -Ujumbe unapaswa kutiririka kwa uhuru toka kwenye chanzo chake (Mungu) kwenda kwa wakusudiwa yaani hadhira au wasikilizaji. 3. Mahubiri ni zao la mambo mawili ambayo ni Mungu na mhubiri. Mahubiri mazuri huzaliwa kutokana na ushirikiano mzuri (umoja) na ushirika mzuri kati ya Mungu na mhubiri. Hivyo kuna vipengele viwili vya wazi katika mahubiri cha kwanza ni kile cha ki Mungu na cha pili ni kile cha kibinadamu. Kwa sababu ya wito wake mkuu mhubiri anapaswa kuwa mwaminifu na awe na ufahamu wa kutosha juu ya Neno la Mungu. 4. Biblia ndiyo asili ya ujumbe. • Ujumbe wowote unaohubiri nilazima utokane na Biblia nje ya Biblia si mahubiri bali ni masimulizi tu. • Kwa nini Biblia peke yake? Kwanini si kitu kingine toka vitabu vizuri vya kikristoau toka magazeti au maelezo na masimulizi ya mtu maarufu na aliye mkuu. • Biblia ni maoni ya Mungu kwa kila jambo lolote lililotolewa. Mhubiri aliye kuwa amekosolewa kwaajili ya hotuba yake alisema “hata mimi sikuipenda pia lakini haikuwa maneno yangu na nilikuwa sitoi mawazo yangu bali kile Mungu amesema katika Neno lake. Kwahiyo nilitoa mawazo ya Mungu na si yangu. • Kuhubiri hotuba ya ki-Biblia humpa mhubiri ujasiri mkubwa. Kutangaza kwa nguvu; Biblia inasema …………………. Mungu anasema………………… • Neno la Mungu lina nguvu. Wab 4:12. • Neno la Mungu ni kama mbegu.sBiblia hukutana na kila hitajila mwanadamuna matatizo yake yote yanayomkabili. • Inampendeza Mungu- Neno lake lililovuviwa amri yake ilikuwa wazi • “Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi na muwafundishe kuyashika yote niliyowaamuru” • Roho mtakatifu hulithibitisha Neno la Mungu. C. MAANA YA KUHUBIRI. Mahubiri yana lengo mahususi katika mpango wa Mungu. Ni njia ambayo kwayo Mungu ameamua kuwafikia waliopotea dhambini na kuwaimarisha waamini.Kkwa sababu mahubiri ni njia ya Mungu kuwafikia wanadamu, tutatazama maana ya kuhubiri kwa mitazamo mbalimbali kama ilivyo ainishwa na wataalamu wa masomo ya homiletics. 1.Kuhubiri ni kuielezea imani. Mojawapo ya malengo ya mahubiri ni kuelezea au kutangaza kweli za maandiko matakatifu. Kila hotuba au ujumbe wapaswa kuwasilisha kweli za maandiko kwa njia itakayowezesha hadhira kupata uelewa zaidi juu ya maandiko matakatifu. Kuhubiri husababisha imani kuumbika kwa wasikilizaji wako. Hubiri kwa kukuza imani na kuielezea imani katika mwana wa Mungu Yesu Kristo. II. Kuhubiri ni kuitetea imani. Haitoshi kuelezea ukweli wa Mungu bali tunapaswa kuutetea. Shetani, ulimwengu na maadui wa imani huvamia na kupotosha kweli za neno la Mungu. Hivyo ni lazima kwa mhubiri yoyote kuwa tayari kuitete imani ya kweli kwa njia ya kuhubiri kweli za ki-Biblia. Kuna wahubiri wengi wa uongo ambao kazi yao ni kuposha kweli za maandiko matakatifi. Ni jukumu la kila mhubiri wa kweli kuhakikisha anasimama imara katika kuitetea imani ya kweli. III.Kuhubiri ni kuinjilisha. Wajibu mkubwa wa Mhubiri ni kuitangaza injili kwa watu waliopotea dhambini. Ni lazima watu wote waliopotea wapelekewe injili ili wapte kutambua hali yao ya kupotea na kuongozwa kwenye wokovu wa Yesu Kristo.Kila mhubiri ahakikishe anatimiza Agizo kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Ahakikishe anawafikia watu wote wasiofikiwa na injili na kuwaleta kwa Bwana Yesu. IV. Kuhubiri ni kukemea dhambi. Kama ukichunguza hotuba za agano jipya utagundua kwamba hakuna mhubiri hata mmoja aliyesita kukemea dhambi.mfano Yesu, Yohana, Paulo, Petro n.k wote walikemea dhambi kwa nguvu zo katika kila mahubiri. Mhubiri nilazima akemee dhambi kila mara kwani Mhubiri ni kinywa cha Mungu. Kemea dhambi bila kuogopa chochote .Mhubiri ni lazima afunue ubaya wa dhambi na kuwahamasisha waamini kuishi maisha matakatifu yenye kumpendeza Bwana Yesu na kujiepusha na uovu. V. Kuhubiri ni kuhamasisha waamini Mahubiri hutakiwa kuwasaidia wakristo kukua katika neema ya Mungu. Pamoja na kuonya na kukemea dhambi mahubiri hutakiwa kuwahamasisha na kuwawezesha waaamini kukua kiroho na kufikia kimo cha Kristo. Hili ni moja wapo wa lengo kuu la mhubiri. Hatuhubiri ili kupisha muda au kwa sababu ya mazoea bali kwa sababu Mungu anakitu anataka tukipeleke kwa watu wake. Lengo la mahubiri ni kuwabadilisha waamini kuwakuza na kuwawezesha kufikia kimo cha Kristo Yesu., Tunapohubiri tunaumba sura ya Kristo ndani ya wale tunaowahubiri. Hakikisha wale unaowahubiri wanakua kiroho na kufanana na kristo VI. Kuhubiri ni kufikia mahitaji ya hadhira. Mahubiri yatakuwa yameafanikiwa kama yatakuwa yamepokelewa na kukutana na mahitaji ya wasikilizaji. Mhubiri kwa uangalifu anatakiwa kujiweka katika daraja sawa na wasikilizaji. Anatakiwa kujitahidi kuhakikisha anapokelewa na makutano na kukutana na mahitaji yao. Mhubiri anapaswa kuhubiri kwa mguso. Hakikisha unagusa mahitaji ya watu unapohubiri. Mahubiri ni uhai hivyo ni lazima yalete majawabu kwa wale tunaowahubiri. Gusa mahitaji halisi ya watu ambayo Mungu anakusukuma kuyashughulikia. Hubiri kwa ufanisi na kwa mguso. VII.Kuhubiri ni kudhihirisha uweza wa Mungu. • Bwana Yesu aliahidi kuwa na wahubiri kwa kulithibitisha neno kwa ishara na maajabu. Popote injili inapohubiriwa ni sharti Bwana awepo akiithibitisha kwa isharaMk 16:15,20. 1Kor 2:4. Hakikisha nguvu ya Mungu iko juu yako unapohubiri. Unapaswa kupakwa mafuta kikamilifu a Roho mtakatifu unapokwenda kwenye huduma ya kuhubiri kwa sababu kuhubiri ni vita. Omba Mungu Roho mtakatifu afanye uthibitisho kwa kila utakachohubiri. Ishara na maajabu ziambatane nawe kokote unakohubiri. -Ikiwa kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu mhubiri anapaswa kwenda mahali Mungu alipoongea mara nyingi na waziwazi yaani “Biblia” • Kwa njia nyingine kuhubiri ni kuipa Biblia sauti.ni kuacha Mungu aongee mwenye toka kwa Neno l D. WITO WA KUHUBIRI Sehemu ya muhimu sana katika kuhubiri ni wito. Kimsingi wito ni wa mtu binafsi Mungu huwaita watu katika huduma na watu hupokea hilo rohoni mwao kisha huja uthibitisho wa nje kupitia kanisa au watumishi mbalimbali na fursa mbalimbali. Mungu Huwaita watu wake katika nafasi na huduma mbalimbali. Wengine kuwa wachungaji, wamishenari, wazee wa kanisani, wainjilisti, au huduma nyinginezo. Kazi ya kuhubiri si ajira ambayo mtu anakwenda chuoni kusoma kwa lengo la kupata baada ya kuhitimu masomo yake, bali ni mwito mtakatifu ambao mtu huitwa na Mungu mwenyewe kuwa muhubiri. Mtu huenda chuoni ili kupata maarifa yatakayomwezesha na kumsaidia katika kutimiza mwito wa Mungu uliondani yake. Haendi chuoni kupata mwito bali wito husababisha mtu kwenda chuoni kama sehemu ya maandalio. Hivyo wito usichanganywe na ajira na maslahi binafsi ya mtu. Ni lazima wito uheshimiwe na kuogopwa. Waamini hawapaswi kujihusisha na huduma kwa lengo la kujinufaisha na kujipatia mali kwa njia za ujanja ujanja. Kimsingi kila mwamini ni muhubiri kwani agizo kuu linamhusu kila mwamini. Kila mwamini anapaswa kujihusisha na kupeleka injili kwa watu waliopotea dhambini hili ni agazo la jumla. Lakini kuna watu maalumu ambao Bwana ameweka wito wa muda wote(Full time commitement) ndani yao. Amewachagua kwa kusudi hili katika maisha yao na muda wao wote. Hawa wanasimama katika zile huduma tano za uongozi katika kanisa, ambao ni mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu. Hawa ndio Bwana amewaweka kusimama katika kazi ya kuhubiri ya muda wote, Wao hawapaswi kujihusisha na shughuli zingine bali kazi yao ni kulihudumia Neno na kuomba yaani Kuhubiri. Bwana ameweka mwito mtakatifu ndani yao ambao ni wajibu mkuu na wa kuogofyapia{.Mdo6:2,4} hili ni agizo mahususi. Wito huu haupatikani kwa njia ya kusoma au kwa njia ya ulaghai bali kwa kuitwa na Mungu mwenyewe kuwa msemaji wake. Kuna baadhi ya makanisa ambayo yameufanya wito wa Mungu kuwa ni ajira. Kwani wao huwapeleka watu kwenda chuoni kusomea huduma fulani mfano uinjilisti, uchungaji nakadharika kwao wito si jambo la msingi kwao ila elimu ndiyo yenye kupewa kipaumbele. Wao humpa mtu kushika nafasi ya huduma baada ya kuhitimu mafunzo ya chuo cha Biblia bila kujali kama ana wito au la. Matokeo yake ni kwamba makanisa yamekuwa yakiongozwa na kuhudumiwa na watu wasio na wito wenye kutegemea elimu ya darasani tu, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo na uhai wa kanisa. Elimu ni jambo la zuri sana lakini elimu haiwezi kuchukua nafasi ya wito katika kanisa la Mungu ikiwa tunataka kufikia kusudi la Mungu la mwito mtakatifu na kusimama kiuaminifu mbele zake kupata ushindi mkuu. Usiwe mtumwa wa elimu. Elimu hii unayopata ikusaidie katika kumtumikia Mungu na kufanya huduma lakini isichukue nafasi ya Roho mtakatifu katika maisha yako na huduma yako. Wala haipaswi kuwa badala ya Roho mtakatifu. E. MAANDALIO KWAJILI YA HUDUMA. Ni muhimu mara mtu atambuapo kwamba Mungu anamwita katika huduma kufanya mambo kadhaa. Mojawapo ni kuanza kumngojea Bwana kwa njia ya maombi, Kujihusisha na huduma mbalimbali zinazojitokeza kanisani au sehemu nyingine yeyote . Pia ni muhimu kwenda shule kwajili ya mafunzo zaidi ya maandalio ya huduma. Kuwa na mlezi. Ni lazima kuwa na mlezi wa huduma ambae atakusaidia katika kutimiza mwito ulio ndani yako. Mlezi wa kwanza wa huduma na wito wako ni mchungaji wako. Mweleze mchungaji kuhusu wito ulio ndani yako na mwombe akusaidie katika kuulea wito huo. Kuwa mtii na mnyenyekevu kwa mcungaji wako. Shirikiana na watu wenye wito kama wako ili uweze kujifunza zaidi. Fanya kazi na huduma mbalimbali unazopewa na mchungaji au viongozi wa kanisa. Jifunze kwa watu wenye wito kama wako walifanikiwa katika utumishi wao. Kupata mafunzo zaidi. Ni vizuri mara unapogudua kwamba Mungu amekuita katika utumishi au mojawapo ya zile huduma tano kwenda chuo cha Biblia kwaajili ya mafunzo na matayarisho kwaajili ya huduma Mungu anayokuitia. Namna ya kuchagua Chuo cha Biblia 1. Omba Uongozi wa Mungu juu ya jambo hili. 2. Angalia chuo kitakachokidhi mahitaji yako ya kuandaliwa. 3. Angalia maswala ya usajili wa chuo.(Vyuo vingi vya Biblia havina usajili wa serikali kwani haviko kitaaluma zaidi bali kihuduma). 4. Chunguza misingi ya imani ya chuo. 5. Tathmini uwezekano wa kuingizwa katika huduma baada ya mafunzo. 1. Mambo ya kuzingatia unapokuwa katika Chuo cha Biblia. 2. Jikite katika masomo kabisa kwa miguu yako yote miwili. 3. Jihusishe kikamilifu na ratiba nzima ya Chuo. 4. Tia bidii katika masomo. 5. Tumia muda kuwa na waalimu na wanafunzi wenzako na jifunze vitu vyema toka kwao. 6. Epuka kuwa mjuaji (arogant). 7. Kuwa mtumishi. 8. Jitahidi kuonekana na si kusikika. 9. Shirikisha baadhi ya watu maono na wito ulio ndani yako. 10. Baki kuwa mwanafunzi daima hata baada ya kuhutimu mafunzo. 11. Kwa mtii kwa amri, shria, kanuni na taratibu za Chuo. • Usiongozwe na elimu bali ongozwa na Roho mtkatifu. • Usihubiri kwa maneno yenye hekima pekee kwa lengo la kushawishi akili za watu bali hubiri Kwa dalili za Roho mtakatifu na nguvu. 1Kor 2:4. • Hakikisha unautumikia wito ambao Mungu ameweka ndani yako kwa gharama yoyte ile bila kujali mazingira au kitu kingine chochote. • Kwa hiyo wito wa kuhubiri hautoki kwa mwanadamu yoyote Yule bali toka kwa Mungu mwenyewe. Mungu huwafanya watu wake kuwa wahubiri. • Jiulize wewe ni mhubiri wa kufanywa na nani ? F. Kweli kuu kuhusu wito wa kuwa mhubiri. 1. Roho mtakatifu huweka wito ndani ya mtu. Wito wa Mungu huja juu ya mtu kupitia Roho mtakatifu. Katika akili ya kawida ni kazi kubwa kuhubiri au kutumika. Wito huja kwa watu wa aina zote na umri wote wowote. Baahi ya watu husikia wito na kujitoa wangali wadogo lakini wengine katika umri mkubwa n.k 2. Shauku ya kutimiza wito. Watu wanaoitwa kuwa wahubiri waliumbwa na Mungu kwa kusudi hiloYer1:4-10 Hawawezi kupata utoshelevu kwa kufanya kitu kingine chochote. Hawawezi kupinga kujihusisha katika huduma au kuchukua fursa za kuhubiri. Hata kama hakuna nafasi za kutumika moja kwa moja bado watatafuta nafasi katika huduma yoyote inayojitokeza. 3. Mungu huwaandaa wale anaowaita kwajili ya huduma. Mungu hawaiti watu ambao hwana uwezo wa kutimiza mwito wake. Wahubiri wengi wanakipaji cha kuongea. Watu wenye wito juu ya watoto Mungu huwaandaa kwa kuwapa uwezo kwa kufanya huduma na watoto n na wanaoitwa kuwa wacghungaji huwezeshwa kuwa wachungaji. Kwa namna yoyte Mungu huwaandaa na kutoa nguvu ya uwezesho juuv yao. 4. Wito wa Mungu wapaswakuwa wazi. Wito wa Mungu usifichwe. Wito wa Mungu ulioju yako wapaswa kuwa wazi kwa watu wangine lakini haupaswi kukimbilia kwenye wito huo mara moja. Hutakuwa na furaha na mafanikio na wito huo mpaka utakopokuwa umejisalimisha kwa mapenzi sahihi ya Mungu juu yako.Wito ambao Mungu amekuita kuutimiza unapaswa kuuweka wazi. Shirikisha watu ambo watafanyika msaada katiki kuulea wito wako. Fanya kazi na watu. Tumika na watu wenye wito kama wako. Kaa chini ya mtu mwenye neema kama ya wito ulionao ili uweze kujifunza zaidi. 5. Wito wa Mungu ni wito wa matayarisho. Kuna wajibu mwingi na mkubwa ambao huja pamoja na wito wa kuhubiri. Mungu akisha mwita mtu humuandaa kwanza kabla ya kumtuma na kumwachilia kwnye huduma aliyomuitia. Mhubiri anapaswa kujiimalisha kiroho na kimwenendo.Anatakiwa ajiandae kiakili kwa kusoma na kupata mafunzo. Pia anapaswa kujiandaa kimatendo kwa kunoa vipawa vilivyo ndani yake na kuyatisha maisha yake yote kulingana na wito ulio ndani ya yake. Mungu akisha weka wito wake ndani ya mtu huanza kumwandaa kwajili ya wito huo. Humpitisha katika majaribu mbalimbali yanayoendana na wito wake, humpeleka kwenye shule yake ijulikanayo kama shule ya moto na baada ya kufuzu huko Mungu humwachilia mtu katika huduma. Musa aliandaliwa kwa zaidi ya miaka arobaini, Yusufu kwa muda wa zaidi ya miaka kumi, Paulo kwa muda wa miaka kadhaa.Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba Mungu huwa hana haraka. Ukipata wito wa Mungu ndani yako usifanye haraka kuutimiza Bwana anatenda kwa wakati. Unapaswa kusubiri wakati wa Bwana na ufanye kwa wakati wake na si nje ya wakati wa Mungu. G. Mawazo mawili potofu kuhusu mahubiri. Kuna dhana mbili potofu ambazo zinajitokeza katika uwanja na taaluma ya mahubiri mawazo hayo ni: a. Maaandalizi si lazima. Wazo la kwanzalenye makosa ni kwamba maandalizi si lazima na huonesha kukosa imani kwa mhubiri. Watu wenye kushikilia msimamo huu hufikili kwamba imani ya kweli hutupilia mbali jitihada yoyote inayojaribu kuandaa akili na hiyvo husimama mimbarini wakiamini kwamba Mungu atawapa maneno ya kusema.husimamia maawazo haya: i. Roho mtakatifu atakupa unachohitaji kuhubiri. Unapopanda mimbarini. _- Zab 81:10 “ Fumbua sana kinywa chako name nitakijaza”(Hutumia andiko hili kutetea msimamo wao.). Pia husema kwamba Yesu alisema kwamba “Msifikirifikiri nini cha kusema maana mtapewa kinywa cha usemi saa ili ilie mnapotakiwa kusema” Unapoyachunguza kwa umakini maandiko hayo utagundua kwamba maandiko hayo wanayafasili nje na mkutadha wake na na kulazimioshwa yaseme kile ambacho hayamaanishi. *Mahubiri ni kamana jengola kiroho ambalo linatakiwa kusanifiwa na kuandaliwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Roho mtakatifu ndiye mhandisi mkuu wa mahubiri. b. Uwezo wa mtu unatosha. Kuweka mkazo katika matayarisho na kutegemea uwezo wa kibidanu tu. Wahubri wanaoshikilia msimamo huu hudai kwamba maandalizi peke yake yanatosha na huweka mkazo kwenye matayarisho pekee.Kumtegemea Roho mtakatifu huwa ni kudogo sana au hakuna kabisa, bali tumaini la mtu binafsi ambalo ni matokeo ya kujifunza na kuendeleza uwezo wa asili. Ujumbe wa namna hii waweza kuwa mzuri kabisa lakini hauwezi kuleta matokeo yatakikanayo daima. Kwani ni Roho mtakatifu pekee ndiye anaeweza kuleta badiliko katika maisha ya waikilizaji wako. Bila yeye mahubiri huwa ni maiti na haiwezi kuleta uhai kwa sababu ni uhai wenye uwezo wa kuzaa uhai. *Roho mtakatifu huuhuishaujumbe na kuletaq matokeo yaliyokusudiwa na Mbingu katika maisha ya wasikilizaji. Ili mhubiri aweze kuhubiri sawasawa anapaswa kuwa na maansdalizi ya kutosha katika kuuandaa ujumbe wake kwa kusoma, kutafakari na kuchambua kweli zote zilizomo katika ujumbe wake. Lakini hayo yotec anapaswa kuyafanya akiwa katika hali ya maombi. Mhubiri anapaswa kumsikiliza Roho mtakatifu klwa kina na kupata uongozi kwake na kutaka Roho mtakatifu amshirikishe kile anachotaka kusema na watu wake na kukifanyia uchambuziyakinifu katika hali ya maombi ili aweze kukiwasilisha kwa ufanisi. • Mhubiri anapaswa kutambua kwamba yeye hana watu wala si Chanzo cha ujumbe. Kwasababu hiyo anatakiwa kumsikiliza mwenye watu na aliye chanzo cha huo ujumbe na kusimama katikati kwa uaminifu kuwafikishia watu kwa usahihi kile mwenye watu anachotaka kiwafikie watu wake. • Mhuibiri anapaswa kutambua kwamba kazi ya kuhubiri ni takatifusana na ni kazi nyeti ambayo yapaswa kufanywa kwa umakini, uaminifu na unyeyekevu mkuu. • Mhubiri mwenye kutegemea juhudi zake na uwezo wake wa asili atakuwa ni muhubiri kilema na halikadharika mhibiri mweye kutegemea kupewa ujumbe akiwa mimbarini atakuwa ni kilema. • Vyote viwili vyapaswa kwenda pamoja, maombi na matayarisho.Kwa sababu mahubiri ni matokeo ya mawasiliano na ushirika mzuri kati ya Roho mtakatifu na mhubiri. H. Umhuhimu wa kujifunza homiletics. a) Linatusaidia kujua mbinu mbalimbali za kuhubiri. b) Linatusaidia jinsi ya kuhubiri bila kuwachosha watu. c) Linatufanya kuwa na ujasiri tunapohubiri. d) Linatusaidia kuhubiri kwa usahhi. e) Linatusaidia kutambua mahubiri ya uongo. f) Linatusaidia kujua na kuheshimu wito tulio nao. g) Linatusaidia kujua kusudi la Mungu la mahubiri. h) Linatusaidia katika kuheshimu wito wa watu wengine. Zoezi. Jibu maswali fafuatayo. Wanafunzi waweza kujibu katika makundi au mmoja mmoja kama kazi ya nyumbani kwa kadri mwalimu atakavyoona inafaa. 1. eleza maana ya mahubiri kwa mitazamo mbalimbali. 2. Eleza vile mahubiri yasivyo. 3. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri na kuhubiri. 4. Taja faida tano za kujifunza somo la kuandaa mahubiri. 5. Tathmini misukumo mbalimbali inayosababisha watu waingie katika huduma tano za uongozi wa kanisa. na hali hawana wito. 6. Eleza namna gani mtu aweza kujua kwamba Mungu anamwita kuingia katika huduma. 7. Eleza umuhimu wa kipindi cha maandalizi na matayarisho kabla ya mtu kuingia katika huduma ambayo Mungu anamwita kuifanya. MADA YA PILI: MBINU ZA UTAYARISHAJI WA MAHUBIRI Utangulizi Katika mada hii tutajadili aina mbalimbali za utayarishaji wa mahubiri, maeno ya mahubiri na sehumu za mahubiri au hotuba. Tutapitia kwa undani kila kimojawapo ya vipengele hivi ili kujifunza jinsi vipengele hivyo vinavyohusiana na mahubiri na tunavyoweza kuvitumia katika huduma ya kuhubiri na kuandaa mahubiri. Malengo ya mada. Baada ya kumaliza kujifunza mada hii mwanafunzi ataweza. • Kutaja na kueleza mbinu mbalimbali zinazotumika katika utayarishaji wa mahubiri au hotuba. • Kutathmini kila mbinu kwa kueleza ubora na udhaifu wake. • Kuandaa jumbe za mahubiri kwa kutumia mbinu mbalimbali. • Kutambua maeneo muhimu katika mahubiri. • Kutambua sehemu muhimu katika jumbe na hotuba. • Kutayarisha jumbe na hotuba za ki-Biblia kwa kuzingatia sehemu muhumi katika • jumbe na hotuba. A. Mbinu za Utayarishaji wa jumbe na hotuba. Kuna aina nyingi za utayarishaji wa somo au hotuba, na kila mojawapo ina umuhimu wake. Lakini katika mada hii tutajifunza aina tatu za utayarishaji wa somo au hotuba. Kila mwanafunzi anatakiwa kuelewa aina zote tatu na anapaswa kujizoeza kutumia njia hizi zote ili aweze kufaidika zaidi. Mbinu hizi za utayarishaji wa somo pia zaweza kutumika kama mbinu za kuhubri. Kwa hiyo tutakapokuwa tunajadili zitaangaliwa katika maeneo haya mawili. ( Kama mbinu za utayarishaji na kuhubiri.) 1. Somo Lililoandikwa. Katika aina hii mhubiri hupaswa kuandika kila kitu anachokusudia kukihubiri. Wakati mwingine somo lote huandikwa. Kila eneo la somo huchambuliwa kwa undani na kuwekwa katika maandishi. Ujumbe au somo lote huandikwa kikamilifu kabla ya kuhubiri. Mhubiri huelezea kwa undani somo lake anapohubiri likiwa katika maandishi. Mhubiri anapohubiri mara nyingi hupitia kila kitu alichokiweka katika maandishi. Faida za aina mbinu hii. a) Ujumbe wote huandaliwa kwa uangalifu mkubwa. b) Ujumbe huwasilishwa kwa umakini na uhalisia. c) Ujumbe huwa ni wa kitaalam. d) Mhubiri hujikita katika somo. Hasara ya mbinu hii. a) Somo huwa haliwavutii wasikilizaji. b) Utoaji wa ujumbe wa namna hii unaweza kuwa wa kuchosha usipofanywa kwa uangalifu c) Utayarishaji wake huhitaji muda mwingi. ZOEZI. 1. Eleza maana ya somo lililoandikwa. 2. Taja vitu muhimu vilivyo katika somo lililoandikwa. 3. Taja ubora na udhaifu wa njia hii licha ya zilizotolewa katika kitabu hiki. 4. .Andaa ujumbe kwa kutumia mbinu ya somo lililoandikwa na kisha huburi kwa dakika kumi. 2.Somo Lisiloandikwa. Hii ni mbinu ya utayarishaji wa somo bila kuliandika. Mhubiri husoma vifungu vya maandiko na kivitafakari kwa kina kisha hukariri vitu vya msingi vilivyo katika ujumbe wake na maandiko yanayohusika. Aina hii mara nyingi hutumika katika kutayarisha na kuhubiri ujumbe wenye uvuvio zaidi. Njia hii ni nzuri sana katika kuhubiri ujumbe wa kiinjilisti. Ujumbe hutiririka toka rohoni na huwa wa kuvutia mno. Faidaza mbinu hii. a) Ni rahisi kutumia. b) Haihitaji muda mwingi wa matayarisho. c) Mhubiri huwa huru kutoa kila kinachokuja ndani yake maadam kinaendana na ujumbe wa somo. d) Huwasisimua wasikilizaji na kuwavutia. Udhaifu wa mbinu hii. a) Mhubiri kutoka nje ya ujumbe wake hasa ikifanywa na mhubiri asiye na uzoefu. b) Wasikilizaji waweza kulielewa somo vibaya. (waweza kuelewa vile somo lisicho maanisha). c) Somo kutowajenga wasikilizaji na kuishia kusisimua tu akili zao. d) Somo kutokuwa na maana halisi na hivyo kutowajenga wasikilizaji. ZOEZI. 1.Eleza maana ya somo lisiloandikwa. 2. Taja mabo matano ya kuzingatia katika utayarishaji wa ujumbe kwa kutumia njia ya somo sililoandikwa. 3.Toa tofauti iliyopo kati ya somo lililoandikwa na somo lisiloandikwa. 4. Andaa ujumbe kwa kutumia mbinu ya somo lisiloandikwa na kisha hubiri kwa dakika kumi 3.Mbinu Ya Skeletoni. Njia hii huhusisha kuandika maelezo ya somo au ujumbe kwa kifupi kwa lengo la kufanikisha utunzaji wa kumbukumbu sahihi juu ya ujumbe au somo. Kwa maana nyingine ni kwamba mhubiri hutayarisha muhtasari wa ujumbe au somo.Mhutasari huo huwa kama skeletoni ya somo, Skeletoni maana yake ni fuvu. Mfano wa fuvu la binadamu. . Mhubiri huhubiri kwa kutumia skeleton hiyo. Kazi yake hasa ni kuweka nyama katika skeletoni hiyo kwa njia ya mahubiri. Hivyo anapohubiri huweka nyama katika mahubiri yake ili yawze kuwa kitu kamili . Mhutasari wa somo huwa kama mifupa ya ujumbe. Ndiyo mifupa ambayo huleta sura na mategemeo kwa kile mhubiri anachotamani kusema. Anavyosema anaweka nyama katika mifupa na kuufanya mwili wa somo lake. Hupanua mawazo yake ambayo maelezo yake mafupi yamekuza. Faida za mbinu hii. a) Mbinu hii humpa mhubiri uhuru zaidi. b) Utoaji wa somo huwa wa kuvutia sana. c) Somo huwajenga wasikilizaji bila kuwachosha. d) Mhubiri huweza kutoa somo kwa mtiririko mzuri na sahihi. Zoezi 1. Eleza maana ya skeletoni. 2. Eleza maana ya mbinu ya skeletoni. 3. Linganua kati ya minu ya somo lisiloandikwa na mbinu ya skeleton. 4. Eleza kati ya mbinu tatu ulizosoma, ipi ni bora kuliko zote na toa sababu ya jibu lako B. Maeneo ya Mahubiri. Kuna maeneo makuu manne ambyo mahubiri huhusisha. Mhubiri yoyote ni lazima azingatie maeneo hayo ili aweze kufanikisha mahubiri yake. I.Wazo . Hii huhusu namna ya kupokea kichwa cha somo au ujmbe. Ni ujuzi unaohusu namna ya kupokea ujumbe toka kwa Mungu. Huhusu namna ya kupata wazo la awali na kichwa cha somo. Mungu hupanda mbegu ya wazo kuhusu somo au ujumbe siku kadhaa kabla ya mahubiri. Mbegu hiyo hukua kwa njia ya kuitafakari na maombi zaidi. Kutokana na ujuzi mhubiri aweza kuujenga uwezo wa kutambua mstari unaohusika. Mhubiri hupaswa kuliendeleza na kulikuza wazo lililopandwa ndani yake kwa njia ya maombi, kutafakari na kuchunguza zaidi juu ya wazo hilo ili aweze kutayarisha ujumbe. Pata muda wa utulivu utulie uweponi na omba nuru zaidi ya ufunuo huo. Kuna tofauti kubwa kati ya hotuba na ujumbe.mtu anaweza kujifunza jinsi ya kuandaa hotuba kupitia masomo ya Homiletics lakini Mtu anapaswa kuwa na ushirika na Mungu ili aweze kupata ujumbe. Kupata ujumbe ni jambo la kiroho zaidi kuliko taaluma. Wale wanaofanikiwa kupokea ujmbe wa kuhubiri toka kwa Mungu ndio wanaoweza kufanikisha lengo la kuhubiri. Mambo ya kusaidia kupata ujumbe. Tambua mahitaji ya watu.(Mahitaji ya kiroho na kimwili). Kujazwa na Neno la Mungu. Kujiweka katika viatu vya wengine (Soma Hotuba na sikiliza mahubiri ya watu wengine. Kutokana na uzoefu wa mhubiri. Kutambua kalenda ya Kikristo. Kutokana na mafundisho ya msingi ya Biblia. Kutokana na matukio mbalimbali. II.Muundo. Muundo huhusisha uchambuzi wa wazo ili kuweza kugundua kweli zilizomo katika wazo hilo.Baada ya kupokea Wazo toka kwa Mungu unapaswa uanze kulichambua ili kutambua vitu ambavyo wazo hilo linavyo. Katika hatua hii unapaswa kuorodhesha kwa urahisi kila kitu kilichomo kwenye wazo hilo.Mara nyingi unapokuwa katka hatua hii unahitaji kuandika kwa haraka ili kupata kwa kifupi mtiririko wa uvuvio unaokuja. Hakikisha kwamba unaandika kila kitu ili uweze kuchambua baadae. III. Ujenzi. Huhusisha kukusanya na kuyaweka mawazo yako uliyoyachambua katika kipengele cha uchambuzi katika mpango mzuri. Kuweka kila kitu katika mpangilio mzuri kutakusaidia na kukurahisishia katika utoaji wa somo lako. Kuwasislisha mawazo yaliyoendelezwa hufanyika msaada sana kwa wasikilizaji wako katika kuelewa na kufuata mpango wako wa kufikiri. Somo likiwalimechanganywa itawawia vigumu wasikilizaji wako katika kulielewa somo hilo.Ujenzi wa somo hulenga kulifanya somo rahisi kiasi cha kueleweka vizuri na wasikilizaji. Ni muhimu sana kwa mhubiri kuliweka somo katika namna itakayofanya lieleweke kwa urahisi. IV. Mawasiliano. Hii huhusu namana mhubiri anavyowasilisha somo au ujumbe kwa hadhira. Mhubiri anatakiwa kuliwasilisha somo lake kwa njia rahisi na nyepesi kueleweka na wasikilizaji wake. Anatakiwa: a) Kuwasilisha ukweli uliowazi na wenye kueleweka. b) Kutoa ujumbe kwa njia ya kuteka akili za hadhira. c) Kuendeleza mawazo yake katika mpango ambao hadhira wataweza kuyafuata kwa urahisi. d) Kuwahamasisha hadhira kulitendea kazi somo. Yak 1:22. C.Sehemu Kuu za ujumbe na Hotuba. Kwa kawaida mahubiri au hotuba yoyote ile ni lazima iwe na sehemtu tatu ambazo kwa pamoja huunda hotuba au mahubiri hayo. Sehemu tatu hizo ni utangulizi, kiini na hitimisho.Kila sehemu ni muhimusana na inatakiwa kupewa uzito wake. Sehemu mojawapo ikipuzwa yaweza kuvuruga au kuharibu kabisa ujumbe au hotuba yako. I.Utangulizi. I. Hii ni sehemu ya kwanza ya hotuba. Utangulizi hutambulisha hotuba au somo zima na kutoa picha jinsi somo litakavyokuwa. Utangulizi ni sehemu muhimu ya ujumbe na kama hadhira hawajakusikiliza kwa umakini katika kipindi hiki cha awali yawezekana kutokuuelewa ujumbe wako au kutokukusikiliza vizuri katika sehemu zinazobaki za hotuba yako. Mara nygingi utangulizi huwa kama muhtasari wa ujumbe.Katika utangulizi mhubiri huwaeleza hadhira kwa kifupi juu ya kile ulichopanga kuongelea au kuhubiri. Utangulizi ni kama mlango wa nyumba katika ujumbe na hotuba.Uangulizi huwa na lengo mahususi la kuwajulisha hadhira ujumbe ambao unawasislishwa kwao. Waamni wengi huja kanisani wakiwa na matatizo mbalimbali ya kifamilia , kikazi N.k .Utangulizi unatakiwa kuwavuta ili waweze kujikita kwenye ujumbe na kuwasahaulisha matatizo waliokuja nayo. Uangulizi ni silaha ya kuwateka wasikilizaji. Kuna namna mbalimbali za kuanza utangulizi. Mhubiri anapaswa kujifunza namna mbalimbali za kuanza utangulizi na ajizoeze kuanza utangulizi wa mahubiri yake kwa njia tofauti tofauti. Baadhi ya njia za kuanza utagulizi zimeorodheshwa hapa chini. II.Namana ya kuanza Utangulizi 1. Kuanza kwa kuuliza swali. 2. Kuanza na maelezo ya kuchanganya(Yenye kuhamasisha watu kusikia kw2a makini swehemu ya ujumbe inayobaki ). 3. Anza kwa andiko 4. Anza kwa mkutadha 5. Anza na habari au kielelezo. 6. Anza na tukio la sasa. 7. Anza na nukuu III. Mambo ya msingi katika utangulizi. Kuteka usikivu. utangulizi wako unapaswa utawale hamu na mawazo ya wasikilizaji. Kujenga masikilizano. Lazima ujenge mawasiliano kati yako na wasikilizaji. Kuleta kukubalika. Ni lazima utangulizi kwako ukujengee kukubalika kwa wasikilizaji. Unapaswa kupata usikivu wao, matumaini na heshima. Kujulisha. Utangulizi wako unapaswa kuwaeleza wasikilizaji kwamba somo lako lina husu nini hasa, na jinsi utakavyoliwasilisha. Kusadikisha. Ni lazima utangulizi uwasadikishe wasilizaji juu ya umuhimu wa ujumbe na kupata usikivu mzuri wa sehemu iliyobaki ya hotuba yako. Usitoe utangulizi kwa kuomba msamaha. Usiseme “Bahati mbaya sikujiandaa vizuri” Kufanya hivyo kutapoteza usikivu wa wasikilizaji wako na kukufanya usiaminike kwao. Sifa za utangulizi mzuri. 1.Sio wa kishindo mno. Utangulizi uwe wa kiasi usiweke hatua ambayo huwezi kuifikia. 2.Sio mrefu mno. Kumbuka kwamba utangulizi si ujumbe wote bali ni sehemu tu hivyo unapaswa kuwa mfupi. 3.Utangulizi uendane na ujumbe. Utangulizi ni sharti ulenge kichwa cha somo. Waweza kuwa muhtasari wa somo au kisa ambacho kinaonesha ukweli wa kile ulichokusudia kuongelea. 4.Unapaswa kuandaliwa kwa uangalifu. Kwa sababu utangulizi wako ni kitu muhimu katika kuvuta usikivu wa hadhira unapaswa kuandaliwa kwa umakini sana. 5.Tayarisha utangulizi wako kwa kujiuliza maswali yafuatayo a.“ Ningekuwa ni msikilizaji wa ujumbe huu nini kingenivuta zaidi ili kuleta usikivu katika yote niliyokusudia kuyasema? 1. “ Ni jambo gani hasa ambalo lingekamata usikivu wangu? b.Majibu yake unayoyapata ndiyo waweza kuyatumia katika sehemu ya utangulizi wa ujumbe wako. 6. Utoe nafasi ya kupitia kwenye kiini cha ujumbe. Utangulizi unapaswa kutoa njia ya kupitia kwenda kwenye kiini cha ujumbe. Kusiwe na pengo kati ya utangulizi na kiini cha ujumbe. II. Kiini. Hii ni sehemu kuu ya somo au ujumbe ambayo imebeba ukweli wote wa somo. Hatua ya kwaza kwenye kiini ni kutoa skeletoni ya kiini na kisha hatua ya pili ni kuweka nyama katika skeletoni yako.Waweza kuweka nyama katika sekeletoni yako kwa kufanya yafuatayo: Kufafanua msamiati mbalimbali inayojitokeza kwenye kiini na kutoa maelezo ya dondoo ulizoziandaa. Tumia kamusi au itifaki ya Biblia katika kupata maana ya maneno hayo. Kiini. Kiini cha ujumbe ni lazima kieleze, kisimulie, kijadili na kutoa kweli yote inayokusudiwa kuwasilishwa. Ni lazima kueleza maana ya andiko au habari. Ni lazima kutoa ushahidi wa kweli inayohubiriwa. Neno la Mungu linajieleza lenyewe. Jambo lingine la kutumia kuthibitisha ni ushuhuda binafsi. Mfano kama unahubiri uponyaji toa uthibitisho kwa kutumia wewe binafsi jinsi Mungu alivyokuponya au alivyowaponya watu wengine. Unapounda kiini unapaswa kujiuliza maswali kadhaa 1. NIini nataka kusema ? 2. Kwanini ninataka kusema hiki ? 3. Ni vipi nitakisema ? 4. Ninachotaka kukisema kitafanikisha nini ? Unaposhughulikia andiko au mada ni lazima kujiuliza kwanini? Namna gani ?, Lini?, Wapi ?, Nini kilitokea kabla na baada ?, Mazingira yalikuwaje?, Matokeo yake yalikuwa nini ?, Nani walikuwa pale ?, na kwanini walikuwepo pale? Walifanya nini?, Hii huhusikaje leo ? na inamaanisha nini leo ?. Kujua majibu ya maswali haya kutakusaidia kutengeneza mhutasari wa somo au andiko. Mfano Luka 16:19 Matumizi ya vielelezo. Moja wapo ya vipengele muhimu katika ujmube au kiini ni vielelezo.Vielelezo ni mifano mbalimbali inayotumika kufafanua na kuelezea ujumbe au somo. Watu wengi huweza kukumbuka vielelezo kuliko ujumbe na hivyo basi vielelezo husadia watu kukumbuka ujumbe. Bwana Yesu amekuwa kielelzo na mwalimu wa vielelezo. Watu hufurahia kusikia vielelezo. Wahubiri wenye ujuzi wa kutumia vielelezo katika jmube na hotuba zao hufanikiwaq kuvuta usikivu wa wasikilizaji wao. Vielelezo ni sawa na madirisha katika nyumba. Vielelzo ni madirisha ya jumbe na hotuba. Jumbe nyingi zinazohubiriwa na wahubiri wengi ni kama nyumba zisizo na madirisha. Nhyumba hizo zaweza kuwa na msingi imara na kuta imara lakini zitashindwa kuingiza mwanga na hewa ya Oksijeni ambayo ni muhimu kwa mwanadamu ili aweze kuishi. Vielelezo hutimiza lengo la kuleta nuru na hewa ya oksijeni ya ki-Biblia katika ujumbe. Vielelezo havipaswi kuwa mwisho vyenyewe lakini vyapaswa kufafanua kweli zinazoawsislishwa. Lengo la vielelezo. Kuleta nuru kwenye somo. Kuvuta usikivu. Kuelezea na kufafanua ujumbe. Kuthibitsha kweli (dondoo). Kanuni za kutumia vielelezo. Kuna kanuni kadha ambazo ni muhimu kuzizingatia wakati wa kutumia vielelezo . Baadhi ya kanuni hizo zimejadiliwa hapa chini. 1. Urahisi. Vielelezo vinapaswa kuwa rahisi kiasi cha kueleweka na kila msikilizaji. Havipaswi kuwa vigumu kiasi cha kuwachanganya wasikilizaji na kuhitaji vielelezo zaidi ili kufafanua vielelezo. Kuna baadhi ya vielelezo ambavyo huhitaji vielelzo vingine . Epuka kutumia vielelezo vya namna hiyo. Yesu alipotumia vielelezo vilikuwa rahisi na wazi Mifano aliyotoa ilkuwa wazi na rahis kueleweka na waikilizaji wa aina zot. Wasomi(mafarisayo na masadukayo) na wasio wasomi (wakulima na wavuvi). Kumbuka kwamba watu wengi utakaokuwa unawahubiria watakuwa ni wenye elimu ya kawaida au wasio na elimu. 2.Ukweli. Hadithi na vilelelzovinavyotumiaka katika amhubiri view wazi. Kama ni hadhi za kutunga usiwaambie watu kwamba ni matukio halisi yaliyotokea. Usilazimishe mfano na kuelelzo kuwa kitu halisi. 3.Kiasi. Vielelzo visizidi na wala visigeuke kuwa ujumbe. Kuna baadhi ya wahjubiri ambao ni mabigwa wa kutoa vielelezona watu huvutiwa sana na vielelezo hivyo. Wanatumia muda mwingi kusimulia vielelzo badala ya kuhubiri. Jambo hili ni hatari sana. Vielelezo vinatakiwa kutumika kuelezea kweli za kiroho na na visigeuke kuwa jumbe.Yesu hakututuma kusimulia hadithi na vielelzo alitutuma kuhubiri. Kwa kawaida kila dondoo kuu inapaswa kuwa na kielelezo kimoja na si vinginevyo. 4. Lengo. Unapaswa kukumbuka kwamba lengo la vielelezo ni kuelezea na kufafanua ujumbe wako. Kweli zipo kumsaidia mhubiri kufikia lengo lake la mahubiri. Lengo la mhubiri linapaswa kubaki kuwa ujumbe na si vielelezo. 5. Uhalisia. Vielelezo viendane na dondoo unayoielezea. Kama hakuna uhusiano hakuna umhuhiu wa kutumia kielelezo hicho. Hakikisha vinahusiana na kwendana. Vyanzo vya vielelezo. Bwana wetu Yesu Kristo alitmia vielelezo na mifano kutoka katika mazingira ya kawaida yaliyomzunguka. Alitumia mifano rahisi kama vile nuru, chumvi mbegu. Mzabibu, kondoo. N.k. Alitumia mifano iliyokuwaikitumika katika maisha ya kawaida. Alizielezea na kuzifafanuana kuzifundisha kweli za kiroho kwa kutumia vielelezo vilivyokuwa katika ulimwengu uliomzunguka. Hivyo basi kila mhubiri anatakiwa kujifunza kutumia vitu mbalimbali vilivyo katka mazingira yake kama vielelezo. Soma vitabu, magazeti ,vijarida na vipeperushi. Sikiliza natutzama vyombo vya habari. Katika mabo yote hayo kua vielelezo vingi ambavyo waweza kuvipata na kuvitumia. Kabla ya kuanza kuitumia kielelezo hakikisha unatihafamu vizuri. Kielelezo kiwasaidie watu kujisikia, kusikia na kuona kile unachokielezea. Ni lazima wewe mwenyewe uguswe na kuvutiwa na kielelezo hicho. Kama hakikuvuti wewe bila shaka hata watu wengine hakita wavutia. Jifunze kwa mwalimu mkuu Yesu Kristo. Vichekesho. . Vichekesho ni muhimu katika mahubiri kutegemeana na ujumbe unaohubriwa. Vichekesho vyapaswa kuendana na somo au ujumbe. Tumia vichekesho kuamsha akili za watu na kuvuta usikivu wao. Vichekesho havipaswi kuzidi kiasi cha kupunguza uzito wa somo. Pia Ujumbe usitawaliwa na vichekesho. Kumbuka kwamba mahubiri si vichekezo ni kitu muhimu na nyeti sana. Usifanye mahubiri kuwa komedi. Wala usiwe mwanakomedi. III. Hitimisho. Hii ni sehemu ya mwisho ya hotuba au ujmbe lakini kipengele cha muhumi sana . Kipengele hiki kisipozingatiwa maana na malengo yote ya kuhubiri huvurugika na kutokuwa na maana. Hivyo ni lazima kipewe uzito unaostahili. Mambo ya kuzingatia. Tunia muda kidogo kwa kuuelezea ujumbe kwa kifupi. Kazia maeneo ya msingi unayofikiri kwamba hayakueleweka vizuri kwa hadhira wakati ukihubiri na yale yanayotakiwa kupewa uzito maalumu. Pia waweza kurudia kuzitamka kwa sauti dondoo za ujumbe wako kila moja. Usiwachushe (bore) kwa kuanza kurudia kuhubiri ujumbe wako wote. Mwaliko. Mwaliko ni kipengele muhimu sana katika hitimisho. Kwa sababu mahubiri ni tofauti na aina nyingine za hotuba hivyo mwaliko huwa ni muhimu sana kwa kuwa mahubiri huhusu kuchukua maamuzi au hatua juu ya kile kilichohubiriwa. Mahubiri bila mwaliko huwa hayajafikia lengo la kuhubiri. Mwaliko ni lazima katika mahubiri ya aina yoyote ile. Mwaliko huwa ni wakati wa kuitikia Kile Mungu amesema kupitia mahubiri. Ni wakati wa kutendea kazi kile kilichofundishwa au kuhubiriwa. Mhubiri anapaswa kuufanya mwaliko kuwa wazi kwa wasikilizaji wote. Lengo la mwaliko si kuwaita watu madhabahuni tu bali ni kuwahamasisha watu kuweka ujumbe katika matendo. Pia Mhubiri hutakiwa kuuweka ujumbe wake katika matendo. • Ukihubiri uponyaji waite watu madhabahuni na waombee uponyaji. • Ukihubiri kutembea katika mamlaka unatakiwa udhihishe mamlaka hiyo. • Ukihubiri utoaji waite watu kumtolea Mungu. • Ukihibiri toba unapaswa kuwaongoza hadhira kwenye maombi ya toba na kuwaita madhabahuni wale wanohitaji kutengeneza kwa upya mwenendo na mahusiano na Mungu na kuomba nao. • Wapeleke watu kwenye matendo na matumizi Mt 21:23. Yak 2:22. • Unatakiwa kuwaongoza hadhira kuomba kwaajili ya ujumbe au somo kwa kadri ya maongozi ya Mungu na kwa kadri Mungu alivyosema na kila mmoja. • Unaweza kuwaongoza watu waimbe wimbo unaoendana na ujumbe uili kuwaogoza uweponi na kuwapa hamasa. • Toa mwaliko kwa watu ambao wanataka kuokoka na kama wapo omba nao. Baada ya hapo maliza na mkabiribishe anaehusika na ratiba inayofuata. Kwa kuhitimisha juu ya sehemu tatu za ujumbe au hotuba twaweza kuvifupisha vipenele vyote hivyo vitatu kwa sentensi tatu ambazo ni: 1. Waambie hadhira kile unachotaka kuhubiri.(Utangulizi.) 2. Hubiri kile ulichowaambia (Kiini), kisha: 3. Waambie kile ulichohubiri.(Hitimisho). ZOEZI. Katika makundi ya watu watatu watatu jadilini maswali yafuatayo: 1. Jadili umuhimu wa vipengele vinne vya maeneo ya mahubiri kila kimoja. 2. Nini kitatokea kama mhubiri atatayarisha ujumbe wa mahubiri bila kuzingatia maeneo hayo. 3. Eleza umuhimu wa sehemu tatu za ujumbe wa mahubiri. 4. Mhubiri bora ni lazima azingatie sehemu tatu za ujumbe. Jadili kauli hii kwa mifano dhahiri. Kuhubiri si kazi rahisi. Kubali usemi huu kwa hoja kumi madhubuti. MADA YA TATU: AINA MBALIMBALI ZA MAHUBIRI. Kuna aina mbalimbali za mahubiri na kila aina ya mahubiri ina nafasi yake katika kuujenga na kuimarisha mwili wa Kristo na kuwaleta waliopotea dhambini. Mhubiri analazimika kufahamu aina mbalimbali za mahubiri ili aweze kuwa na ujuzi mwingi wa kuhubiri na ili aweze kuhubiri kwa kuyafanya mahubiri kuwa mapya kila ahubiripo. Kuhubiri kwa kutumia aina mbalimbali za mahubiri huwajenga wasikiliza kwa namna mbalimbali ambapo aina mojaya mahubiri isingeweza kufanya hivyo. Pia husaidia washirika na waamini kuwa na msingi mzuri wa uelewa wa Neno la Mungu. I. Mahubiri ya kifungu. Aina hii ya mahubiri hujengwa juu ya kifungu kimoja kidogo cha maandiko tu. Huhusisha kuchagua maelezo fulani maalum ya maandiko na kuyachunguza, kuchambua na kugundua kweli zote zilizomo ndani yake na kuziwasilisha kwa wasikilizaji kwa mtindo rahisi na wenye kueleweka. A. Faida za mahubiri ya Kifungu. a) Huvutia. b) Huzuia kutoka nje ya somo. c) Hufanya mahubiri kuwa ya ki- Biblia. d) Humwongezea mhubiri ujasiri. e) Husaidia wasikilizaji kulikumbuka somo. B. Jinsi ya kuandaa mahubiri ya kifungu. Kuna mambo kadhaa ambayo mhubiri anapaswa kuyazingatia wakati wa kuandaa mahubiri ya aya, badhi ya mambo hayo yamejadiliwa hapa chini. 1.Soma Biblia mara kwa mara. Unapaswa kusoma Biblia mara kwa mara ikiwa unataka kuwa mhubiri mwenye mafanikio katika huduma yako. -Tenga muda wa kusoma Biblia kila siku. Beba Biblia ndogo kila mahali unapokwenda ili upatapo muda uweze kuisoma. 2. Jifunze Biblia. Kujifunza ni zaidi ya kusoma.Kujifunza kuna husisha kusoma Biblia kwa undani kwa kuchunguza kikamilifu kila kitu kilicho katika maandiko unayosoma na kutafakari kwa kina,.Yos1:8. Unapaswa kutafakari kwa uangalifu vitu unavyosoma. Viweke kwenye akili yako na kuvifikiri tena na tena. Unapaswa kujizoesha kuchambua kile ulichojifunza. Baada ya kukichambua kwa umakini unapaswa kukiweka tena akilini. 2. Kuwa na Daftari la kuandikia. Kila usomapo Biblia yako jitahidi kuwa na kalamu na daftari la kuandika mambo muhimu unayojifunza. Jenga mazoea ya kuandika kwa ufupi kila ufunuo unaoupata. 3. Dumisha hali ya maombi. Unapaswa kuwa katika hali ya maombi kila usomapo Biblia .Omba Mungu akufunulie upate kulielewa Neno lake.Pia unapaswa kumwomba Mungu akupe usikivu juu ya kweli anazokufunulia katika Neno lake. 4. Jenga usikivu.Unapaswa kuwa katika hali ya utulivu na usikivu katika Nyanja zote yaani kimwili, kiroho na kisaikolojia. Mungu hutoa ufunuo wake kwa sauti ya kimya ndani ya roho ya mhubiri. Kama hunautulivu na usikivu wa kutosha ni vigumu kugundua maarifa hayo.. - C.Sifa za aya ya mahubiri Kifungu cha mahubiri au aya yapasa kuwa : a. Yenye mamlaka ya ki-Biblia. Mafundisho unayokusudia kuhubiri toka kifungu au aya fualani ya maandiko yapasa ikubaliane na kile Biblia nzima inachofundisha. Katika mahubiri ya kifungu kuna uwezekano wa kuchukua kimakosa mstari nje ya maana yake na kuutumia kufundishia kitu ambacho Biblia haikubaliani nacho. Ni Muhimu sana kwa ,mhubiri kujua jinsi mstari anaoshughulikia jinsi unavyokubaliana na kusudi la sura yote na kitabu chote. Daima mhubiri anapaswa kujitahidi kufasili aya yake katika nuru ya yale ambayo Biblia nzima inafundisha. b.Kamili. Aya yapaswa kuwa katika maandisha ya ukweli ulio kamilika. Baadhi ya wahubiri huchukua kifungu cha maneno katika mstari na kukitumia bila kujali maneno yaliyotangulia au yanayofuata. Jambo hili si zuri na huzaa mafundsho ya uongo. Na huku huitwa. “Kulichanganya neno la Mungu na uongo……..2Kor 4:2. Ni lazima uepuke jambo hili kwani litaleta kutokuaminika na maelezo yasiyo ya ki- Biblia na hatimae utawapotosha wasikilizaji wako. c. Fupi kiasi. Kifungu cha mahubiri chapaswa kitolewe kwenye maelezo ya maandiko ambayo ni mafupi na ya kulizisha. c. Ya kueleweka. Aya yapaswa kueleweka na iwe muhtasari wa kutosha wa kile unachotaka kukishirikisha. *Unapaswa ubaki katika mipaka ya kile ambacho aya yako inaelezea. D. Namna ya kuandaa mahibiri ya aya. a. Elewa maneno yake vema. Kipitie kifungu kwa kukisoma mara kadhaa, kitafakari na kujenga kumbukumbu juu yake na kiseme mwenyewe kwako. Hakikisha unakielewa vizuri. b. Elewa lugha yake.Tamabua lugha yake kama ina maana halisi au kama ni lugha ya mifano tu. Jiulize kama mwandishi alikuwa na maana hasa ya kile alichokiandika au maneno yake yachukuliwe kama mfano wa mahubiri? c. Changanua ujumbe wake.Chambua ujumbe unaoupata na kuutenga katika sehemu kadhaa zenye kulandana ili uweze kuuwasilisha kwa mtiririko mzuri. d. Chunguza maneno yake. Jitahidi kugundua kile maneno hayo yalikusudia kuwasilisha hapo awali. Ikiwa una kamusi ya kigiriki au Kiebrania unapaswa kulitazama neno hilo. Jaribu kubaini kama kuna maana maalumu ndani ya neno unalolishughulikia. Kufanya hivyo kutakusaidia kugundua maana yoyote maalumu ambayo mwandishi alikusudia kuiwasilisha. e. Tathmni mwendelezo wake. Baini kweli zile mwandishi alitaka kuzielezea. Tambua jinsi alivyo kamilisha katika kuziwasilisha kweli hizo. Jaribu kufuata mwongozo wake na kuuendeleza katika mtindo huo. f. Mkutadha wa kifungu.. i. Maneno ya mbele na ya nyuma ya kifungu. Angalia jinsi mistari iliyotangulia na inayofuata inachosema. Chunguza aya kuhusiana na sura nzima ambayo umetoka. Chunguza kifungu hicho katika nuru ya kitabu kizima ambamo kinapatikana. Jifunze kiini na mazingira yote ya kitabu. ii. Hali ya mila. Je mila za wakati ule ziliathiri kile kilichoandikwa? Je watu walioandikiwa kifungu hicho awali wangekuwa na wazo la kile kilichoandikwa tofauti na ambalo tungepata katika hali yetu? Kama ndivyo nini ingekuwa maana inayolingana na sasa? ii. Hali ya kihistoria. Je jambo hili liliandikwa lini? je wakati huo ulishawishi kile kilichoandikwa? Je matukio ya wakati ule yaliyokuwa yakijulikana wakati ule wa uandishi yalikuwa na maana maalum juu ya kile kilichosemwa? iv. Hali ya kijiografia. Mwandishi alikuwa wapi wakati anaandika maneno hayo? je Watu walioandikiwa walikuwa wapi?Je mazingira yao yana uhusiano wa chochote katika kile kilichosemwa? v. Biblia kwa ujumla. Kila sehemu ya maandiko ifasiliwe kwa uaminifu na kwa umakini ili ikubaliane na maandiko yote. Andiko lolote lisifasiliwe nje ya mkutadha wake. Maandiko ni lazima yafasiri maandiko. E.Kupanga Maelezo. Mpanglio mzuri wa maelezo na kazi kwa ujumla ni wa maana sana kwa mhubiri. Hakikisha unapanga maelezo yako kimaantiki. Mpangilio mzuri wa kazi na mawazo humwezesha mhubiri kulielewa vizuri somo na kulishughulikia somo kikamilifu. Pia huwawezesha wasikilizaji kulielwa somo na kulikumbuka somo . 1. Ujumbe uwe katika mpangilio.Panga ujumbe wako katika mtiririko mzuri ili uweze kuufuata kwa urahisi wakati wa kuhubiri. 2. Weka ujumbe wako katika hali ya kueleweka. Jitahidi kukamilisha vipengele vyote unavyohitaji kuviongelea katika mahubiri yako. Kabla ya kupanda mimbarini. 3. Kazia katika mawazo. Unapaswa kuyaweka mawazo yako katika sentensi fupi. Jifunze namna ya kuyaimarisha mawazo yako kwa pamoja na kuyaelezea katika sentensi fupi zinazoeleweka kwa urahisi.Jizoeze kupunguza na kulielezea wazo kwa sentensi moja. 4. Tayarisha maelezo mafupi.Kumbuka kwamba maelezo yako ili kusaidia kumbukumbu yako.unapaswa kuwa na vidokezo vitakavyosaidia kulikumbuka somo lako au ujumbe wako. 5. Ufanye rahisi kuusoma. Ni vizuri kupiga chapa mahubiri yako ili uweze kusoma kwa urahisi wakati wa kuhubiri. Pia waweza kutoa vipeperushi na vijarida kwa wasikilizaji wako ili waweze kufuatilia zaidi ujmbe au somo lako. Zoezi. 1. Eleza maana ya mahubiri ya aya. 2.Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya aya. 3.Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya aya au kifungu licha ya yaliyotajwa katika kitabu hiki. 4. Andaa hotuba ya mahubiri ya aya na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako. II. MAHUBIRI YA KUFAFANUA. Mahubiri ya kufafanua ni aina ya mahubiri ambayo huhusisha kuchagua sehemu kubwa ya maandiko na kuichunguza kwa undani na kuifasiri na kugungua kweli zilizomo katika sehemu hiyo ya maandiko na kushirikisha mkutano au usharika wako. Mfano unaweza kuamua kupitia Injili yote ya Luka sura baada ya sura. Kuanzia sura ya kwanza, unatafuta kufasili na kuelezea maana na umuhimu wake mstari kwa mstari sura kwa sura mpaka umeimaliza yote. Waweza kushughulikia sura moja kila wiki, na baada ya wiki kadhaa utakuwa umemaliza kitabu chote. A.Faida ya mahubiri ya ufafanuzi. Hufanya mahubiri kuwa ya ki-Biblia. 1. Yesu alitumia aina hii ya mahubiri. Alichukua kifungu cha Agano la kale na kufasili maana yake kwa wasikilizaji wake. 2. Petro alitumia njia hii siku ya Pentekoste. 3. Stefano alitumia njia hii. Huwezesha waamini kuwa na msingi na uelewa mkubwa wa Biblia.Waamini huimalishwa na huwa na ufahamu mzuri na wa kina wa Neno la Mungu. Kwani kweli zote zilizomo katika kitabu kilichopitiwa tayari hufahamika vizuri kwa usharika wote. Huvuta kuimalishwa na Roho mtakatifu. Roho mtakatifu hulithibitisha neno lake kwa ishara na miujiza sawasawa na Kweli zote zilizofunuliwa katika kitabu husika. Humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia. Mahubiri ya kufafanua humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia kwani mhubiri huhubiri kile kilicho katika maandiko ya eneo husika. Mhubiri huwa anajikita katika mkutadha wa aya, sura na kitabu chote kwa ujumla. Hivyo kiini cha kitabu ndicho ambacho hubeba mahubiri yake yote. Mambo ya kuzingatia katika kutayarisha mahubiri ya kufafanua. I. Kwa umakini chagua kifungu cha maandiko kinachostahili. Hakikisha kwamba kifungu hicho kitahudumia uzima na uwezo wa wasikilizaji wako. 1. Usichague somo kwa sababu linakuvutia au kukupendeza. 2. Usichague somo ambalo litazaa machafuko, mgawanyiko na mashindano. 3. Jitahidi kufanyika njia ili Mungu akupitie ili aweze kuongea Neno lake kwa watu wake kwa kupitia wewe. 4. HIvyo basi unawajibika kutafuta kujua mawazo ya Mungu kuhusu watu wake ambao amekupa wajibu juu yao. 5. Huduma hii ni moja ya heshima kuu uliopewa lakini pia ni wajibu mkuu unaoogopesha sana. Hivyo basi unapaswa kuifanya kwa umakini wa hali ya juu. II.Tafuta ujumbe unaolingana na hali ya watu ya wakati ule. 1. Mungu kila mara huwa na ukweli wa sasa ambao hutaka kunena na watu wake. 2. Mungu hukusudia jambo maalum kwa kila kundi la waamini 3. Jifunze kujua kile Mungu anacho kwaajili ya kusanyiko kwa kila wakati. III. Jifunze sura ya kitabu kwa umakini. 1. Soma sura unayoshughulikia mara nyingi mpaka umeielewa vizuri. 2. Soma kwa uangalifu mstari hadi mstari. 3. Kila kunapokuwepo na uhusiano wa wazi kati ya kifungu hicho na kifungu kingine unapaswa kusoma kifungu hicho ili uweze kupata maana zaidi. Maandiko hufasiri maandiko. 4. Jenga usikivu kwa sauti ya Roho mtakatifu ili kupokea ufunuo toka kwake. Tumia vitabu vya rejea ili kupata msaada zaidi. Mfano. Itifaki ya Biblia, Kamusi ya Biblia, Biblia ya Tafsiri nyingine.Nk IV. Kusanya taarifa muhimu. Waweza kupata vitu vingine muhimu vya kuhusisha kwenye somo lako kwa kutumia mbinu ya maswali na majibu kama ifuatavyo. 1. Nimewahi kusikia au kusoma nini juu ya somo hili? 2. Roho mtakatifu amewahi kunionesha nini juu ya somo hili? 3. Nimewahi kuona nini chenye uhusiano na somo hili ? 4. Nimewahi kuwa na mawazo gani juu ya somo hili ? 5. Naweza kupata habari zaidi ju ya somo hili kwa nani au wapi ? 5. V. Tambua kiini cha somo lako. 1. Daima tafuta kugundua kiini cha sura unayoshughulikia. 2. Tafuta kujua kile Roho mtakatifu alikusudia kuwasilisha alipoivuvia sura hiyo. 3. Gundua undani wa somo hilo. 4. Baini kile Mungu anataka kusema na watu wake kupitia sura hiyo. VI.Kuwa na Lengo kamili. Lengo lako daima lapaswa kuendana kikamilifu na lengo la Mungu. 1. Hakikisha kwamba Umegundua kile Mungu anataka kutoa kupitia maadiko hayo na kisha jizamishe katika kile Mungu anataka kufanya. 2. Unapaswa kuhisi kile Mungu anachohisi Mungu humshirikisha mhubiri moyo wake na akili yake ili waweze kufanya kazi pamoja. Unapaswa kuchangamka. 3. Fanyika chombo cha Mungu cha kupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu wake. 4. Kumbuka hukuitwa kushiriki mawazo yako na watu bali kuwashirikisha watu mawazo ya Mungu. VII. Zungumza kulingana na ujuzi wako mwenyewe. 1. Usitoe nadharia toa uhai. Hubiri kile ulicho na uzoefu nacho.kile ambacho umekifanyia kazi . wapaswa kuwa mtu kwa kwanza kula matunda ya kazi yako. 2. Umeitwa kuwa barua Sio tu kwamba unataakiwa kuuhubiri ukweli bali pia unatakiwa kuufanyia mazoezi na kuuonesha kwa matendo. 3. Unapaswa kuwa mfano hai wa yote unayoyahubiri. VIII. Upe maana ujumbe wako. 1. Unawajibika kwa uwezo wako wote, kuhakikisha kwamba maana ya kweli na umuhimu wa maandiko unakuwa wazi na wakueleweka kwa wasikilizaji. 2. Daima jitahidi kuufanya ujumbe wako kuwa rahisi. 3. Hivi ndivyo Yesu alivyofanya Hii ilisababisha huduma yake kuwa na nguvu na mafanikio. 4. Alichukua mambo yaliyokuwa mafumbo na akayaweka rahisi sana. 5. Wahubiri wengine huyachukua masomo rahisi sana na kuyafanya mafumbo magumu sana kiasi cha kutoeleweka kwa wasikilizaji wake au kuelewa kidogo. IX.Fanya ujumbe wenye kutekelezeka. 1. Daima unapohubiri jitahidi kuonesha wazi wasikilizaji wako jinsi wanavyoweza kuutendea kazi ujumbe wako. 2. Jitahidi kutoa ushauri wa kimatendo kuhusu watu wanavyotakiwa kumwitikia Mungu kwa namna ya kufaa. 3. Husianisha mahubiri yako na maazimio yako kimatendo ambayo yaweza kuwafanya watu kuwa watendaji wa Neno na si wasikilizaji tu. Zoezi 1.Eleza maana ya mahubiri ya kufafanua. 2. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya kufafanua. 3. Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya kufafanua. 4. Chagua sura mojawapo ya injili ya Yohana na kisha andaa mahubiri ya kufafanua kutokana na sura hiyo na kisha hubiri kwa dakika kumi. III. MAHUBIRI JUU YA MAISHA YA WATU. A.Utangulizi Hii huhusu hadithi ya maisha ya watu. Kwa hiyo njia hii huhusisha mafunzo juu ya maisha ya watu mbalimbali tunaosoma habari zao katika Biblia. Kila hadithi ya mtu iliyoandikwa katika Biblia ina umuhimu kwetu. Maisha ya kila mhusika aliye kwenye Biblia yana mafunzo kadhaa ambayo twaweza kujifunza. Kila habari iliyoandikwa kwenye Biblia ipo kutufundisha kitu fulani ambacho ni cha thamani sana. 1Kor 10:1-11. Mhubiri huchagua mhusika mmojawapo wa wahusika walio katika Biblia na kujifunza kwa kina kila kitu kilichotoke katika maisha ya mhusika huyo, tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Pia mhubiri hutakiwa kujifunza kuhusu nasaba na mbari ya mhusika huyo ili aweze kufahamu vizuri vitu vilivyomjenga na kumkuza mhusika, kisha hutayarisha mahubiri juu ya mhusika huyo na kuhubri katika kusanyiko lake. Mafundisho ya wahusika wa Biblia ni ya kushangaza na ya kuvutia. Katkia aina hii ya mahubiri, mhubiri hupaswa kuchagua mhusika mmoja na kusoma habari zake zote zilizo kwenye Biblia na kisha huandikia kila wazo analolipata. Hapa mhubiri anapaswa kusoma kumbukumbuzote za mhusika katika Biblia. Baada ya kusoma kumbukumbumbu hizo unapaswa kuanza kuweka pamoja mawazo yote unayoyapata katika utaratibu wa miaka yaani jinsi matukio yalivyotokea ya mhusika huyo. B. Faida za mahubiri juu ya maisha ya watu. I.Hufunua ukweli wa maisha. Biblia imeeleza wazi maisha ya wahusika kama yalivyokuwa bila kuficha chochote. Imeeleza mafanikio yao na madhaifu yao. Ukweli wa maisha ya wahusika umewekwa wazi na kwa uhalisia. Wengi wa mashujaa wa Biblia wanahitilafu zao za kibinadamu.Twajua kuwa walikuwa wanadamu kama sisi na walikutana na majaribu kama sisi. Katika visa vyote vya historia kuna mtu mmoja tu mkamirifu ambae ni Yesu kristo pekee. Hata mashujaa wakubwa wa imani walikuwa na hitilafu zao. Hii inatupa kujua kwamba wao si tofauti na sisi. Ni mifano ya kujifunzia. Ni mifano na msada kwetu. Tunaweza kujifunza kutokana nayo kuliko ujuzi wetu wa uchungu. C. Mambo ya kuzingatia a) Jifunze kuzaliwa kwa huyo mtu. b) Tafakali hali na mazingira aliyolelewa. c) Angalia uhusiano wake na Mungu katika maisha yake. d) Angalia jinsi alivyo wajibika kuhusu uhusiano wake na Mungu. e) Baini vitu alivyojifunza kutokana na mahusiano yake na Mungu. f) Tathimini mafanikio yake. Jifunze vitu vilivyomfanya afanikiwe. g) Tazama maeneo aliyokosea kama yapo. Na jifunze vitu vilivyomfanya akosee. h) Toa hitimisho kile tunachoweza kujifunza kutokana na maisha ya mtu huyo. Mambo hayo yote yanavutia na ni yenye vitu vingi vya Kutufundisha ambayo twaweza kujifunza kutokana na watu hao. Tunaosoma habari za maisha yao katika Biblia. D. Hatua za kufuata katika kuandaa mahubiri juu ya maisha ya watu. I. Chagua mtu au msusika toka kwenye Biblia. Unapaswa kuanza na watu mashuhuri katika Biblia ambao habari zao ziko wazi kabisa, kama vile Ibrahimu,Musa,Samweli, Daudi, Yusufu, Debora, Miriamu, Mariamu, Dorkasi, Paulo, Petro. N.k. Hawa ni baadhi ya watu ambao matendo yao yamefanyika kuwa nuru katika historia ya ushusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Kuna mambo mengi sana ambayo twaweza kujifunza kutokana na maisha yao. Aina hii ya mahubiri ni nzuri sana, kujifunza toka kwa wacha Mungu wenzetu waliotutangulia katiki wito na huduma hii ni jambo la msingi sana. 1Kor 10.1-11. II. Chunguza maisha yake. Anza kwa kusoma hadithi inayoelezea kuzaliwa kwa mtu huyo. Tafuta maana ya jina lake. Kwani jina lina maana sana ki-Biblia. Angalia kwa umakini kusudi la Mungu katka maisha yake. Ili uweze kuvumbua vitu vingi unapaswa kujiuliza maswali yafuatayo: 1. Mungu alitaka kutekeleza nini kupitia mtu huyu ? 2. Je Mungu alifanya nini ili kusudi lake lijulikane kwa mtu huyu? 3. Mtu huyu aliitikia vipi Mungu alipomjulisha kusudi lake? 4. Tunaweza kujifunza nini kutokana na Mungu kuhusika katika maisha yake ? 5. Kuna tahadhari zozote ambazo tunapaswa kuzichukua ? 6. Je siri ya mafanikio yake ilikuwa nini ? 7. Je mwisho wa maisha yake ulikuwaje ? III. Chambua somo na kisha hubiri. Baada ya kujiuliza maswali hayo na kupata majibu utakuwa umepata vitu vingi ambavyo waweza kuvichambua kwa umakini na kuandaa somo kisha na kulihubiri somo hilo katika mpangilio na mtiririko Mzuri wa mawazo. Mwombe Roho mtakatifu akupe ufunuo zaidi unapokuwa ukihubiri somo lako na lifanye somo lako kuwa na uhalisia katika maisha ya sasa ya wasikilizaji. Zoezi 1.Eleza maana ya mahubiri ya wahusika au maisha ya watu. 2. Tengeneza orodha ya watu mashuhuri walio katika Biblia. Orodha hiyo ihusishe wanawake na wanaume. 3. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya wahusika. 4. Chagua mhusika mmoja wa kike au wa kiume na kisha andaa mahubiri kwa kumtumia mhusika huyo na kisha hubiri kwa dakika kumi. IV. MAHUBIRI YA MIFANO HALISI NA VIVULI. Huu ni ujuzi unaohusu kuweka wazi au kuchimbua na kuwasilisha ukweli uliojificha wa mifano mbalimbali katika Biblia. Mfano ni kitu, mtu au tukio ambalo kinabii ni ishara ya kitu au mtu fulani atakaetokea baadae. Inafanana au ni mfano wa Yule mtu au tukio. Katika matumizi ya Biblia ina maana ya mtu wa Bibli au tukio litakaloonesha kitu fulani kitakachotokea. Mfano mwanakondoo katika kitabu cha Kutoka ni mfano wa Bwana Yesu. Kila kitu kuhusu kondoo wa pasaka kiunabii kilikuwa na maana ya ukombozi wa wajibu ambao Bwana Yesu Kristo angetimiza.Yn 1:29. Mifano ya Biblia mara nyingi inaonekana kama kivuli(type) cha mambo yanayokuja baadae. Ebr 8:5,10:1. Siku takatifu pia katika agano la kale zilikuwa vivuli juu ya mambo ambayo yalikuwa yanakuja. Kol 2:17. Hizo siku takatifu hazikukamilika zenyewe sehemu ya kusudi la kutimizwa kwake ilikuwa ni kutanguliza sura ya kinabii ya vitu ambavyo vilikuwa bado vinakuja. Kanuni za kutumia. a. Unapojaribu kwa mara ya kwanza kufundisha kwa kutumia mifano ya kwenye Biblia, zingatia misingi ifuatayo. I. Tumia mifano rahisi zaidi. Anza na mifano rahisi ambayo maana yake iko wazi. II.Endelea na tafsiri ya wazi. Usijaribu kufasiri kila kitu.Elezea ukweli wote kama ulivyo na wala si kutafuta kila kipengele chake na kukielezea kwa undani. III. Usitumie maneno makavu. Usitumie mifano ya kufundishia kama kanuni. IV.Sisitiza ukweli wa msingi. Usitumie nafai uliyonayo kwa kutoa mifano ya kufundishia. Mifano itumike kusisitiza mafundisho na si kutumia kama chanzo cha ukweli. V. Uwe tayari kusahihishwa. Uwe tayari kusahihishwa na kukosolewa na wale waliokomaa kuliko wewe ili uweze kujifunza zaidi. 4. Kuelezea kusudi. Ni njia ambayo kwayo mhubiri hupanua maana ya ukweli ulio katika kifungu maalum cha maandiko. Unatafuta namana ya kuuweka wazi ukweli ambao umejificha ndani ya kifungu. Hii njia nzuri sana ya kufundishia kusudi lote la ki-Mungu. Mdo 20:27. Zoezi 1. Eleza maana ya vivuli na mifano.(Types). 2. Taja hatua za kufuata katika kutayarisha na kuhubiri mahubiri ya mifano na vivuli. 3. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya mifano na vivuli. 4. Tayarisha mahubiri ya mifano na vivuli na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako. V. MAHUBIRI YA MADA. Aina hii ya mahubiri hukusudia kutoa kiini maalum kwa hadhira.Mhubiri huchagua somo fulani kisha huchunguza kila kitu ambacho Biblia inasema juu ya somo hilo. Baada ya kuchunguza na kuchambua, kweli hizo huandikwa katika mapngilio wa somo. Mhubiri hupitia vifungu mbalimbali vya maandiko vinavyohusu somo hilo. Aina hii ya mahubiri huhitaji maandalizi ya muda mrefu na utulivu mwingi. Pia huwasilishwa katika mfululizo wa vipindi kadhaa na si kimoja, kwa sababu ni vigumu kupitia kweli zote zilizo katika somo kwa kipindi kimoja tu. Mfano wa mada za kuhubiri. 1. Upendo wa ki-Mungu 2. Ubatizo wa Roho mtakatifu 3. Maombi ya kufunga. 4. Nguvu ya usaidizi. 5. Vita vya kiroho. 6. Kutambua Ulimwengu wa roho. 7. Kutembea katika mamlaka. 8. Nguvu ya madhabahu. 9. Kushughulikia majira na nyakati. 10. Kutii mamlaka. Mambo ya kuzingatia katika mahubiri ya mada. 1. Uwe na ufahamu wa kutosha juu ya somo husika. 2. Fanya maandalizi ya mudamrefu na ya kina 3. Unapaswa kuwa na lengo mahususi la mahubiri yako. 4. Gawa somo katika vipengele vidogovidogo. 5. Kila kipengele lazima kiwe na maandiko yanayokithibitisha na kukielezea 6. Andiko liendane na dondoo unayoitoa. Zoezi. Somo hili lipo kimatendo zaidi. Kila mwanafunzi ashiriki katika kufanya mazoezi ya kuandaa mahubiri na ahubiri katika dakika zilizopendekezwa au mwalimu atakazopanga kulingana na muda uliopo. Mwalimu anatakiwa kusimamia na kusahihisha kazi za wanafunzi na kutoa marekebisho katika maeneo ambayo wanafunzi hawajafanya vizuri. 1.Andaa Ujumbe kwa kutumia aina ya mahubi ya mada na kisha hubiri mkutano kwa dakikika kumi. Chagua mada yoyote. 2.Taja ubora na udhaifu wa mahubiri ya mada. 3. Taja mambo mengine matano muhimu ya kuzingatia katika kuandaa mahubiri ya mada. 4. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri ya mada na mahubiri ya kufafanua. VI.MAHUBIRI YA MATUKIO. Mahubiri ya matukio ni kipengele katika mahubiri ya maada, lakini kutokana na umhuhimu wake tumekitenga na kukielezea peke yake. Mahubiri haya ni mahubiri ambayo huandaliwa kutokana na tukio lilipo au ambalo litafanyika katika kipndi fulani. Kiini cha mahubiri haya huwa ni tukio ambalo linafanyika katika ibada hiyo.Mfano wa matukio hayo ni Tukio la, 1. Kusimikwa kwa uongozi wa kanisa. 2. Ndoa au kumuaga bnti. 3. Kubariki watoto. 4. Ushirika mtakatifu 5. Ubatizo 6. Kuweka wakfu vitu mbalimbali. 7. Kuhitimu mafunzo.(graduation) 8. Msiba na mazishi. 9. Sikukuu mfano Pasaka, mwaka mpya, N.k Mambo ya kuzingatia 1. Mahubiri haya yanapaswa kuendana na tukio husika. 2. Mhubiri anatakiwa kufahamu ratiba nzima ya tukio hilo au shughuli hiyo. 3. Mhubiri ahubiri kulingana na tukio husika. 4. Mhubiri aepuke kutumia muda mwingi katika mahubiri. 5. Mhubiri ahubiri kwa lugha itakayoeleweka na kusanyiko lote na lugha yapaswa kuwa rahisi. 6. Mahubiri yapaswa kugusa kusanyiko lote. 7. Mhubiri anapaswa kuhubiri kwa upendo. 8. Mhubiri azingatie ratiba ya tukio. ZOEZI. 1. Chagua tukio mojawapo na kisha andaa mahubiri juu ya tukio hilo na hubiri kwa dakika 10 .2. Taja mabo mengine kumi ya kuzingatia katika mahubiri ya matukio. 3.Eleza ubora na udhaifu wa mahubiri ya matukio. MADA YA NNE MHUBIRI. Malengo ya mada. • Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi anataweza. • Kueleza maana ya mhubiri kwa mitazamo mbalimbali. • Kuelza wasifu wa mhubiri. • Kueleza vidokezo mbalimbali kuhusu mhubiri. A. Utangulizi. Mahubiri yana mwanzo wake katika Agano la kale. Wakati manabii walipotangaza neno la Mungu kwa watu wa kale. Manabii walikuwa wahubiri wa kwanza katika agano la kale. Mungu ameamua kuwachagua na kuwatumia watu wa kawaida kulitangaza Neno lake.Amewachagua wanawake na wanaume kuwa vyombo vya kulitangaza neno lake kupitia huduma ya kuhubiri. Ufafanuzi Neno mhubiri (kwa kigiriki kerux) limetumika mara kadhaa katika agano jipya ambapo humaanisha kutangaza. (Rumi 10:14, 1Tim 2:7, 2Tim 1:11, 2Pet 2:5. Unapolitazama neno hili (mhubiri) halijikiti na kuishia kwenye huduma moja au huduma fulani tu bali linahusisha zile huduma zote tano za uongozi wa kanisa. Ikijumuisha mitume, manabii waijilisti,wachungaji na waalimu. Pia linajumuisha kila mtu atangazae neno la Mungu. Hata kama hana mojawapo ya zile huduma tano za uongozi. Ingawa hudma zote hizi zinawasifu wake kila moja lakini zote zaangukia katika neno moja “Mhubiri”. Inavutia kutambua kwamba neno la Kigiriki lililotafsiriwa kama mhubiri linaelezea mtu anaeongea kwa mamlaka , anaewasilisha ujumbe bila kikwazo au kizuizi chochote. Hii hudhihirisha mamlaka iliyo juu ya mhubiri. Mhubiri ni mtu yeyote anayehubiri Injili. • Mhubiri ni mtu anayetumiwa na Roho mtakatifu katika kuwasilisha kweli za ki-Mungu kwa njia ya hotuba. • Mhubiri ni mtangaza ujumbe wa Mungu. • Yeye ni msemaji wa Mungu. Husimama katika nafasi ya Mungu na kuzungumza kwa niaba yake Mungu. Hivyo ni lazima mhubiri awa na sifa zinazostahili ambazo zitamfanya kuwa na mamlaka. B.Sifa za mhubiri. Mhubiri ni lazima awe na sifa stahilifu ambazo zitamfanya awe na mamlaka na thabiti katika wito na huduma yake. Badhi ya sifa hizo zimeorodheshwa hapa chini. 1. Awe ameokoka (Amezaliwa mara ya pili). 2. Awe amejazwa Roho mtakatifu. 3. Awe na wito halisi (Wito ulio wazi na wenye ushahidi). 4. Ajazwe na Neno la Kristo ndani yake Kol 3:16. 5. Awe mtu wa maombi. 6. Awe mwadilifu.( Mkweli na mchaji Mungu na mwenye kuchukia mapatato ya udhalimu ) 7. Awe na nidhamu. 8. Aishi kulingana na wito wake. 9. Asiwe mvivu. 10. Awe na baba wa kiroho. Kuna tofauti kubwa kati ya hotuba na ujumbe.mtu anaweza kujifunza jinsi ya kuandaa hotuba kupitia masomo ya Homiletics lakini Mtu anapaswa kuwa na ushirika na Mungu ili aweze C. Kujihusisha binafsi katika kuhubiri. 1. Unapaswa kuwa kawaida. Unatakiwa kutulia na kuwa vile ulivyo. Mugu hutaka kutumia utu wa kila Mhubiri katika kuwasilisha Neno lake. Unatakiwa kujikubali hivyohivyo ulivyo. Mungu anapendezwa nawe na ndiyo maana amekuita hivyo ulivyo. Usijichambue sana. 2. Kuwa wa kipekee. Unatakiwa kuutayarisha ujumbe wako na kuuwasilisha kwa njia ya kipekee ili uweze kuleta matokeo ya kipekee. Unapasa kutumia utu wako wa kipekee Mungu aliokupa na kumwacha Mungu atumie utu na maisha yako kwa njia maalum ya kipekee anayotaka yeye. 3. Kuwa rahisi. Unapokuwa ndiyo unaanza kuhubiri au kusimama mimbarini kwa mara ya kwanza unatakiwa usijaribu kutumia ufasaha au kuingia ndani mno katika kuhubiri. Huhitaji kuwavuta watu. Upo pale kwa lengo la kuwahudumia na si kuwapendeza. 4. Kuwa huru. Unatakiwa kuwa huru unapohubiri na ujifunze kujizoeza hali mbalimbali. Ufanye mtindo wako wa mawasiliano utiririke kawaida na kwa uhuru. Kila kusanyiko utakalo hubiri linatofautiana na lingine, hivyo unapaswa kujizoeza hali mbalimbali. Mungu huwa na lengo maalumu analotaka kufanikisha katika kila ibada na mhubiri ndiyo ufunguo muhimu katika kutekeleza hili. Kuwa huru na msikivu kwa Roho mtakatifu.Roho mtakatifu anaweza kufanya hali za jinsi mbalimbali katika kila ibada.Wasikilizaji wako wakati mwingine waweza kuwa wachangamfu na wakati mwingine wakimya na wanyenyekevu. 5. Tambua njia ambayo Mungu anapitia na utembee nae. 6. Dhihilisha mamlaka..Hakikisha Kuna madhihirisho ya nguvu za Mungu katika kila ibada unayohubiri. Hakikisha Bwana anakithibitisha kila unachokihubiri kwa ishara na maajabu. Hubiri kwa uthibitisho D. Zana za mhubiri. Kuna vitu kadhaa ambavyo ni muhimu kwa mhubiri yoyote . Bila vitu hivo kazi ya Kuhubiri itakuwa haijafanikiwa au kufika lengo kwani wasikilizaji watakuwa wameachwa njiani. Baadhi ya zana hizo ni: I. Maono. Kila mhubiri nilazima awe na maono katika huduma yake na wito wake. Wazo la kile ambacho huduma yako itafanikisha kwa Mungu. Maono ni picha au taswira juu ya kile unachohitaji kukifikia katika huduma yako. Kumbuka kwamba bila maono watu huangamia Mit 29:18. Ni maono pekee yatakayokuweka salama. Usipokuwa na ufahamu wa kuhusu kusudi la Mungu alilonalo kwaajili yako ,waweza kulemewa na kuishia n jiani na kushindwa kufikia lengo la –ki-Mungu ulilochaguliwa kwalo. II.Msamiati. Msmiati ni jumla ya maneno yaliyo katika lugha fulani. Msamiati wamhubiri hujumuisha maneno yote anayoyajua na kuyazoea kuyatamka. Maneno ni dhana ambayo mhubiri hutumia katika kutimiza wito wake. Muhubiri anatakiwa kuwa mahili wa lugha. Jifunze msamiati mbalimbali na matumizi yake.Silaha yetu kuu ni maneno katika kazi ya kuhubiri. Maneno huundwa na msamiati. Soma vitabu mbalimbali ili uweze kujitajirisha na msamiati. Unapokutana na neno usilolifahamu lichunguze na kutafutamaana yake na matumizi yake. Pia mhubiri anatakiwa afahamu kutumia msamiati mbalimbali katika kazi yake ya kuhubiri. Tambua matumizi ya Lugha kulingana na mahali. Jifunze misimu, Rejesta na misemo mbalimbali inayotumika katika Lugha husika. Hii itakusaidia unapohubiri uweze kuwagusa watu wote waliopo katika eneo hilo. Mhubiri ni lazima ajifunze namna ya kutamka maneno sahihi. Jifunze kutumia lafuzi vizuri na kuepuka athali za lugha mama katika Lugha unayotumia kuhubiri. Kuwa na lafuzi nzuri na kuongea lugha kwa ufasaha hukupa kukubalika kwa wasikilizaji wako na kupewa usikivu. Tumia Lugha inayoeleweka na wasililizaji wako, lakini lugha hiyo yapaswa kuwa sanifu au fasaha III. Sauti. Sauti ndiyo chombo kikuu mhubiri anachotumia katika kuhubiri. Ni lazima mhubiri kujifunza mitindo mbalimbali ya sauti na namna ya kuitumia sauti yake. Jifunze matumizi ya sauti katika mahubiri yako. Sauti yako inapaswa kusikika na wasikilizaji wako lakini haipaswi kuwa kubwa sana kiasi cha kuwaumiza. Fahamu mahali pa kutumia asuti kidogo na mahali pa kuongeza sauti. Hubiri kwa mitindo mbalimbali ya sauti. Zingatia kiimbo, toni na kidatu unapohubiri. E. Kanuni za Kuhubiri Katika kipengere hiki tutaajadili baadhi ya kanuni chache za kuzingaita katika mahubiri ya hadharani. Mhubiri anapswa kufuata na kuzingatia kanuni hizi ili aweze kufanikisha lengo la mahubiri 1. Kuvuta hewa. Kuvutahewa sahihi ni muhimu kwa mhubiri. • Vuta hewa nyingi kiasi cha kufika mapafuni. • Jizoeze kujaza hewa kifuani na kwenye mapafu. • Izuie na kisha itoe nje polepole.Dhibiti utoaji wa hewa. Iache hewa itoke chini ya mapafu kupitia sanduku la sauti na kugusa ukuta wa juu wa mdomo. • Jifunze jinsi ya kupumua ili usiishiwe pumzi wakati wa kuhubiri. 2. Utamkaji mzuri wa maneno. Jitahidi kutamka maneno vizuri na waziwazi. Hakikisha kila neno unalolitamka linasikika vizuri kwa wasikilizaji wako. Usilete kikwazo kwa wasikilizaji wako kwa kutosikika vizuri. 3. Ubadilishaji wa sauti. Hii inahusu kuifanya sauti kuwa nene au nyembamba. Sauti ya kila mwanadamu inahali mbalimbali. Jitahidi kutumia aina mbalimbali za sauti. Ukitumia aina moja ya sauti yaweza kuwachosha wasikilizaji wako. Tambua maeneo unayotakiwa kuongea kwa sauti ya chini na sauti ya juu. Endeleza viwango tofauti vya sauti yako. Ubadilishaji wa ukubwa wa sauti waweza kusisitiza kipengere fulani muhimu. Baadhi ya wahubiri huona ni muhimu sana kuhubiri kwa sauti kubwa sana kiasi chakuumiza masikio ya wasikilizaji . Jaribu kuepuka hili. Iwapo ujumbe wako wote utawasilishwa kwa sauti kubwa au ya juu itakuwa vigumu kusisitiza jambo maalum katika zile sehemu ambazo ni za maana zaidi. 4. Kasi ya kuongea. Kasi unayotumia kuongea ni muhimu sana katika mahubiri. Baadhi ya wahubiri huhubiri kwa kasi moja tu . hii si nzuri, pia yaweza kuwachosha wasikilizaji. Sehemu kubwa ya ujumbe wako yapaswa kuwasilishwa kwa mwendo na kasi ya kawaida ya mazungumzo. Katika maeneo mbalimbali ni lazima kuongeza au kupunguza mwendo ilikuleta tofauti na msisitizo zaidi katika mahubiri yako. 5. Kupumzika kidogo. Usiongee mfululizo bila kuwa na vituo. Kupumzika kidogo wakati wa kuongea au kuhubiri ni muhimu pia kwaweza kuongeza msisitizo kwenye maeneo ya muhimu. Kuongea mfululizo kwaweza kusababisha wasikilizaji washindwe kusharabu mambo ya muhimu katika akili zao. Usipitie ujumbe kwa kukimbia na kuongea kwa haraka bila kuvuta pumzi. Hadhira wanahitaji muda wa kufikiri na kuchambua kile ulichosema, Hii inasaidia sana kusharabu ukweli wa ujumbe wako. Unahitaji kuzifahamisha akili pamoja na kuzichangamsha hisia za hadhira. Kama ukihubiri kwa haraka tu bila kupumzika utawaacha hadhira wako nyuma. 6. Kurudia. Kurudia sehemu za msingi wakati unahubiri ni jambo la msingi sana. Inasaidia kusisitiza vipengere na kushindilia kwenye akili za wasikilizaji. Unatakiwa kukielezea kipengere kwa njia mbalimbali. Usisite kurudia eneo unalohisi wasikilizaji wako hawajakuelewa vizuri. F.Vidokezo muhimu kwa mhubiri. 1. Uwe vile ulivyo.Usijaribu kutokeza sura ambayo si ya kweli. Kuwa vile ulivyo ndiyo njia pekee inayoweza kukufanya utulie.usijaribu kumwiga mhubiri mwingine yeyote ukifanya hivi itakusababishia kutoaminika kwa hadhira wako.Jitahidi kuwa mhubiri bora na si kuwa mhubiri mkuu. 2. Usijenge sauti ya kidini. Baadhi ya wahubiri wamejiundia sauti za mimbarini ambazo ni tofauti na sauti zao za kawaida.Hii huleta kutokuaminika na kuonesha kana kwamba unamwiga mtu mwingine. Jizoeze kuhubiri kwa kutumia sauti ya kawaida na unayotumia katika mawasiliano katika maisha ya kila siku. Hii huonesha ukweli na uaminifu katika mahubiri. 3. Usiongee kwa sauti ndogo mno. Hakikisha kwamba kila mmoja katika mkutano wako anakusikiliza vema. Usifanye wachoke kwa sababu ya kutokukusikia vizuri. Ikibidi uliza je kila mmoja ananisikia vizuri ? Si vizuri kuendelea kuhubiri na hali kuna baadhi ya watu hawakusikilizi. 4. Usipige kelele. Jitahidi kuongea kwa sauti ya kawaida ya maongezi ambayo inaweza kuongezwa kiasi kufuatana na wingi wa makutano na kama huna au una vyombo vya kupazia sauti. Sauti iongezwa kulingana wingi wa hadhira. 5. Kumbuka kubadili kasi na upeo wa sauti ya mahubiri kukwepa kuchosha hadhira. 6. Ufanye mkutano ukukubali. Pata matumaini ya hadhira.Hakikisha mkutano wako unakukubali.. Kama mkutano wako hawakukubali nidhahiri kabisa kwamba hawataupokea ujumbe wako. 7. Vaa vizuri. Ni jambo la maana sana kwa mhubiri kuvaa mavazi ya heshima na safi. Namna ulivyo vaa yaweza kuharibu ujumbe wako.Hakikisha uvaaji wako hauvurugi ujumbe wako. Vaa kulingana na tamaduni za taifa husika. 8. Jifunze kusimama vizuri. Ni vizuri sana kusimama wakati unazungumza au kuhubiri. Simama vizuri kwa miguu yote miwili.. Simama wima ukitazamana na hadhira wako. Usipende kuegemea kitu chochote. Kama kuna mimbari itumie kuwekea Biblia na zana zako za kuhubiria. Kusimama wima kutakusadia katika kuvuta hewa. Watazame hadhira wako wakati wote unapohubiri. Hubiri kwa kumgusa kila mtu. Kila mtu ajione kwamba unaongea na yeye binafsi. 9. Jifunze kutembea wakati unahubiri. Usisimame mahali pamoja kana kwamba umefungwa.Jizoeze kutembeatembea wakati unahubiri. Mwili wako unaleta ujumbe sawaswa na sauti yako.Tumia ishara wakati unahubiri lakini epuka ishara sisizo na umuhimu. Kama unaeleza juu ya kitu fulani ni kawaida kuelezea jambo hilo kwa mikono yako. Ishara za namna hiyo zinapaswa kutokea zenyewe kiasili bila kuzilazimisha. 10. Endeleza uhuisano na hadhira. Macho ya mhubiri huelezea ujumbe pia. Usiangalie hewani au juu ya vichwa vya watu. Waangalie watu unaowahubiri moja kwa moja. Kila mmoja atambue kwamba unamwangalia yeye binafsi. 11. Jifunze kutawala mkutano. Hakikisha unatawala kusanyiko. Watu wote wako pale kukusikiliza wewe hakikisha kila mmoja anakusikia. Zungukia watu wako nakuwashitua wanao lala au kusinzia. Tafuta namna itakayosababisha watu wote kukusiliza kwa makini. 12. Omba upako wa Roho mtakatifu. Mwombe Mungu akupake mafuta daima. Hakikisha utendaji wa Roho mtakatifu upo katika mahubiri yako. F. Matumizi ya muda katika mahubiri. Ni lazima mhubiri ajifunze matumizi sahihi ya muda katika mahubiri. Jambo hili ni la muhimu sana na lisipozingatiwa huweza kuvuruga kazi nzima ya kuhubiri. Ni lazima kuamua muda utako tumia kuhubiri kabla ya kupanda mimbarini. Utafiti kule Marekani umeonesha kwamba watu huanza kupoteza usikivu wao baada ya dakika ishirini tu za mahubiri. Waweza usikubaliane na matokeo ya utafiti huo lakini unatakiwa kukumbuka kwamba akili ya mwanadamu inakiwango cha kuelwa na muda wa kuelewa. Muda ukizidi kila kinachoongelewa au kuhubiriwa huwa hakisharabiwi kwani akili hufikia upeo wa kuelewa na kushika mambo. Upako wa Roho Mtakatifu huhuisha akili za wasikilizaji kwa kiwango fulani lakini mhubiri aepuke kuwachosha wasikilizaji. Ni vizuri sana kumaliza ujumbe wako wakati watu wanatamani uendelee na ni vibaya sana kumaliza ujumbe wako wakati watu wanataka umalize. Jitahidi kuzingatia muda katika kazi yako ya kuhubiri. Kwa kawaida ujumbe unapaswa kutumia dakika arobaini na tano. Utangulizi uwe na dakika tatu hadi tano, Kiini kiwe na dakika ishirini na tanno hadi therathini. Hitimisho liwe na kakika tatu hadi tano. Ujumbe wote usizidi dakika arobaini Vinginevyo utawaacha wasikilizaji wako. Ukitaka kuhubiri kwa muda mrefu hakikisha ujumbe wako unauvuvio mwingi. Spurgeon alisema” tumia muda mwingi katika matayarisho ili uweze kutumia muda mchache katika kuhubiri” Kutumia muda mrefu katika kuhubiri hakukufanyi ueleweke zaidi wala hakufanikishi zaidi lengo la kuhubiri. Tambua cha kusema. Kiseme na kisha maliza. Unapokuwa umealikwa na mhubiri mwingine kuhubiri unapaswa kumuuliza muda ambao yeye hutumia katika kuhubiri na muda wa kumaliza mahubiri. Unapokuwa unahubiri zingati muda ulioelekezwa na mwenyeji wako na uwezo wa kuelewa wa wasikilizaji wako. Mgeni akija kanisani kwako kama hukumwandaa kuhubiri kabla si vizuri kumpa madhabahu ili ahubiri. Kwani kuhubiri ni kazi nyeti sana na inahitaji maandalizi ya kutosha. Maelezo haya hayazuii mwongozo na maelekezo ya Roho mtakatifu. Lakini ni vizuri kumwandaa mhubiri mapema ili awe na muda wa kuafanya maandalizi. Usiwashitukize watu kuhubiri. Ni lazima uwe na heshima kwa kazi hii kwani Mungu mwenyewe anaiheshimu sana. Usihubiri ujmube au somo ambalo mwenyeji wako hakubaliani nalo. Kama kuna ulazima fanya nae mazungumzo kabla ya kuhubiri au tafuta namna utakayotumia kuhubiri na kufanya akubaliane na kile unachohubiri. Jambo hili ni muhimu sana na linapaswa kuzingatiwa. Mahubiri na mazingira. Mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyopatikana na kuzunguka eneo fulani. Mazingira ni muhimu sana katika kufanikisha kazi ya kuhubiri. Ni lazima mazingira yawe safi hasa ikiwa mahubri yatafanywa katika eneo fulani maalum. Mfano kanisani, uanjani au eneo lolote rasmi. Kuna baadhi ya mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa. Baadhi ya mambo hayo yameorodheshwa hapa chini. 1. Watu wanaokuja kwa kuchelewa wakae katika viti vya nyuma. 2. Mimbari inapaswa kuwekwa mahali sahihi panapoonekana na watu wote bila shida. 3. Lango la kuingilia lapaswa kuwa mahali sahihi. 4. Akina mamawenye watoto wadogo wakae eno maalumu. 5. Watoto wanapaswakutengewa sehemu yao ya kukaa kama hakuna kanisa la watoto. 6. Mwanga na hewa ya kutosha ni kitu muhimu sana katka eneo lolote. G. Jaribu kuu la Mhubiri. Wahubiri wengi hujisulisha na kutafuta chakula kwajili ya watu wengine na kujisahau wenyewe. Huu ni mtego mkubwa katika kazi ya kuhubiri na ni moja ya hatari za huduma. Wakati mwingine mhubiri aweza kujishughulisha sana na kutafuta haki za kiroho za kundi lake na kwa masikitiko makubwa anasahau zile za kwake mwenyewe. Hii ni moja ya sababu kuu zinazomfanya mhubiri kushindwa. Sulemani anasema katika kitabu cha Wimbo ulio bora “”’ Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu bali shamba langu mwenyewe sikulilinda” Mhubiri ni lazima ajali kwanzai maisha yake mwenyewe ya kiroho. Mhubiri anapaswa kulipa neno la Mungu nafasi ya kuchipua ndani ya moyo na roho yake. Aliache likue kwa nguvu katika maisha na ujuzi wake. Halafu atakapohubiri atahudumu kutokana na ujuzi. Hataongea kamwe kama mwenye nadharia bali atashirikisha vitu ambavyo yeye mwenyewe anavielewa kikamilifu na ana ujuzi navyo. Paulo anasema hivi. “Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza kupata fungu la matunda”. ( 2Tim 2:6 ). Hii inatufundisha kwamba unachopanda na kuvuna ( kiroho) yapasa ule (ujuzi)- kabla ya kulisha wengine. Huwezi kulisha wengine kile ambacho wewe mweyewe hujakila kwanza. Huwezi kujaribu kuongoza wengine katika njia na mapito ambayo wewe mwenyewe hujapitia. Jinsi Neno la Mungu linavyokuwa dhahiri katika maneno yako ndivyo wewe unafanyika ujumbe toka kwa Mungu. Hutakuwa mtu anaye kariri somo tu bali mtu ambaye uhai wake binafsi na mtindo wake wa maisha huhudumia uhai, Baraka na nguvu kwa wale wanaomfahamu na kumsikia. I.Hitimisho. Mahubiri mazuri hayaji kirahisi wala hayatokei tu. Ni matokeo ya vitu vingi. Kama tulivyotazama huko nyuma kwamba mahubiri huanza na wito wa mhubiri na wasifu wake.Pia huhusisha maandalizi ya kutosha kwa kuomba na kusoma kwa bidii. Kilele cha mahubiri ni katika kuwasilisha ujumbe. Ujumbe hauwi ujumbe mpaka umewasilishwa. Ujumbe ulioandaliwa vema utakuwa ujumbe wa kiungu pale Roho mtakatifu atakpoupaka mafuta. Mahubi mazuri daima yataleta matokeo mazuri. Mahubiri mazuri dama yatamtukuza Mungu na si mhubiri au mtu mwingine yeyote. Yatawaongozawatu msalabani na kuwafanya kuwa wanafunzi. Angalizo.Mhubiri hapaswi kutwaa utukufu kwa namna yoyote ile katika kila inachotokea katika kazi yake ya kuhubiri. Daima anapaswa kumpa Mungu heshima na utukufu kwa kila kinachotokea. HOMILETICS. MADA YA KWANZA. MAHUBIRI. Malengo ya mada. Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi aweze.  Kueleza maana yamahubiri.  Kueleza maana ya kuhubiri.  Kueleza wito wa kuhubiri ulivyo.  Kueleza umuhimu wa kujifunza homiletics. A. UTANGULIZI Katika kozi hii tutashughulikia mojawapo ya kazi kuu ya kanisa. Mojawapo ya wajibu mkuu ambao umewekwa mikononi mwa kanisa ni kuhubiri ujumbe wa Mungu yaani Injili. 1Kor 1:21 a) Ni amri iliyo wazi toka kwa Bwana Yesu kwa wafuasi wake. Mk 16:15. “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe”. b) Kuhubiri ni mojawapo ya kazi ya thamani sana ambayo Mungu ametupa. Kuwa msemaji wa Mungu, yaani Mjumbe wa Kristo. 2Kor 5:20. c) Kuhubiri ni wajibu mkuu. Rumi 10:14-15. d) K wa njia ya mahubiri Mungu alichagua kujidhihirisha mwenyewe kwa mwanadamu. B. MAANA YA MAHUBIRI. Neno mahubiri linatokana na maneno mawili ya kigiriki ambayo ni homileo na homilia yenye maana ya ‘kuwa pamoja na, kuongea na kuwasiliana. a) Homily pia humaanisha ujumbe au hotuba. b) Elimu inayohusu namna ya kuhubiri huitwa Homileticts. c) Homiletics ni ustadi wa kuhutubia au kuhubiri. d) Mtaalamu wa elimu ya kuhubiri huitwa Homilist e) Homiletics huhusisha kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri au kutunga hotuba. f) Mahubiri huhusu kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri masomo ya Biblia. g) Mahubiri ni ujuzi wa kuhubiri. h) Ni elimu au taaluma inayohusu kuhubiri Neno la Mungu. i) Ni elimu inayohusu namna ya kuhubiri.{ somo juu ya kila kitu kinachohusiana na kuhubiri}. j) Kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu. Mungu hutumia watu wake aliowachagua kuhubiri ujumbe wake. k) Ujumbe unapaswa kuwa ujumbe wa Mungu Kitu kingine chochote si mahubiri ila ni maoni na falsafa za kibinadamu tu. l) Kuhubiri ni lazima kuwe ni kutangaza binafsi na si kusoma au kuandika Dr. Martyn Lolyoyd Jones alisema “ Wahubiri huzaliwa na hawafanywi kamwe. Kamwe hutamfundisha mtu kuwa mhubiri kama yeye si muhubiri. Lakini mhubiri wa kuzaliwa unaweza kumsaidia na kumwendeleza akawa mhubiri bora kwa njia ya mafunzo” 1. -Mhubiri si chanzo cha ujumbe.Mungu ndiye chanzo cha ujumbe na mhubiri ni bomba au mfereji ambako Mungu hupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu aliowakusudia. Ujumbe wa Mugu hutiririka kupitia utu wa mhubiri. 2. -Ujumbe unapaswa kutiririka kwa uhuru toka kwenye chanzo chake (Mungu) kwenda kwa wakusudiwa yaani hadhira au wasikilizaji. 3. Mahubiri ni zao la mambo mawili ambayo ni Mungu na mhubiri. Mahubiri mazuri huzaliwa kutokana na ushirikiano mzuri (umoja) na ushirika mzuri kati ya Mungu na mhubiri. Hivyo kuna vipengele viwili vya wazi katika mahubiri cha kwanza ni kile cha ki Mungu na cha pili ni kile cha kibinadamu. Kwa sababu ya wito wake mkuu mhubiri anapaswa kuwa mwaminifu na awe na ufahamu wa kutosha juu ya Neno la Mungu. 4. Biblia ndiyo asili ya ujumbe. • Ujumbe wowote unaohubiri nilazima utokane na Biblia nje ya Biblia si mahubiri bali ni masimulizi tu. • Kwa nini Biblia peke yake? Kwanini si kitu kingine toka vitabu vizuri vya kikristoau toka magazeti au maelezo na masimulizi ya mtu maarufu na aliye mkuu. • Biblia ni maoni ya Mungu kwa kila jambo lolote lililotolewa. Mhubiri aliye kuwa amekosolewa kwaajili ya hotuba yake alisema “hata mimi sikuipenda pia lakini haikuwa maneno yangu na nilikuwa sitoi mawazo yangu bali kile Mungu amesema katika Neno lake. Kwahiyo nilitoa mawazo ya Mungu na si yangu. • Kuhubiri hotuba ya ki-Biblia humpa mhubiri ujasiri mkubwa. Kutangaza kwa nguvu; Biblia inasema …………………. Mungu anasema………………… • Neno la Mungu lina nguvu. Wab 4:12. • Neno la Mungu ni kama mbegu.sBiblia hukutana na kila hitajila mwanadamuna matatizo yake yote yanayomkabili. • Inampendeza Mungu- Neno lake lililovuviwa amri yake ilikuwa wazi • “Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi na muwafundishe kuyashika yote niliyowaamuru” • Roho mtakatifu hulithibitisha Neno la Mungu. C. MAANA YA KUHUBIRI. Mahubiri yana lengo mahususi katika mpango wa Mungu. Ni njia ambayo kwayo Mungu ameamua kuwafikia waliopotea dhambini na kuwaimarisha waamini.Kkwa sababu mahubiri ni njia ya Mungu kuwafikia wanadamu, tutatazama maana ya kuhubiri kwa mitazamo mbalimbali kama ilivyo ainishwa na wataalamu wa masomo ya homiletics. 1.Kuhubiri ni kuielezea imani. Mojawapo ya malengo ya mahubiri ni kuelezea au kutangaza kweli za maandiko matakatifu. Kila hotuba au ujumbe wapaswa kuwasilisha kweli za maandiko kwa njia itakayowezesha hadhira kupata uelewa zaidi juu ya maandiko matakatifu. Kuhubiri husababisha imani kuumbika kwa wasikilizaji wako. Hubiri kwa kukuza imani na kuielezea imani katika mwana wa Mungu Yesu Kristo. II. Kuhubiri ni kuitetea imani. Haitoshi kuelezea ukweli wa Mungu bali tunapaswa kuutetea. Shetani, ulimwengu na maadui wa imani huvamia na kupotosha kweli za neno la Mungu. Hivyo ni lazima kwa mhubiri yoyote kuwa tayari kuitete imani ya kweli kwa njia ya kuhubiri kweli za ki-Biblia. Kuna wahubiri wengi wa uongo ambao kazi yao ni kuposha kweli za maandiko matakatifi. Ni jukumu la kila mhubiri wa kweli kuhakikisha anasimama imara katika kuitetea imani ya kweli. III.Kuhubiri ni kuinjilisha. Wajibu mkubwa wa Mhubiri ni kuitangaza injili kwa watu waliopotea dhambini. Ni lazima watu wote waliopotea wapelekewe injili ili wapte kutambua hali yao ya kupotea na kuongozwa kwenye wokovu wa Yesu Kristo.Kila mhubiri ahakikishe anatimiza Agizo kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Ahakikishe anawafikia watu wote wasiofikiwa na injili na kuwaleta kwa Bwana Yesu. IV. Kuhubiri ni kukemea dhambi. Kama ukichunguza hotuba za agano jipya utagundua kwamba hakuna mhubiri hata mmoja aliyesita kukemea dhambi.mfano Yesu, Yohana, Paulo, Petro n.k wote walikemea dhambi kwa nguvu zo katika kila mahubiri. Mhubiri nilazima akemee dhambi kila mara kwani Mhubiri ni kinywa cha Mungu. Kemea dhambi bila kuogopa chochote .Mhubiri ni lazima afunue ubaya wa dhambi na kuwahamasisha waamini kuishi maisha matakatifu yenye kumpendeza Bwana Yesu na kujiepusha na uovu. V. Kuhubiri ni kuhamasisha waamini Mahubiri hutakiwa kuwasaidia wakristo kukua katika neema ya Mungu. Pamoja na kuonya na kukemea dhambi mahubiri hutakiwa kuwahamasisha na kuwawezesha waaamini kukua kiroho na kufikia kimo cha Kristo. Hili ni moja wapo wa lengo kuu la mhubiri. Hatuhubiri ili kupisha muda au kwa sababu ya mazoea bali kwa sababu Mungu anakitu anataka tukipeleke kwa watu wake. Lengo la mahubiri ni kuwabadilisha waamini kuwakuza na kuwawezesha kufikia kimo cha Kristo Yesu., Tunapohubiri tunaumba sura ya Kristo ndani ya wale tunaowahubiri. Hakikisha wale unaowahubiri wanakua kiroho na kufanana na kristo VI. Kuhubiri ni kufikia mahitaji ya hadhira. Mahubiri yatakuwa yameafanikiwa kama yatakuwa yamepokelewa na kukutana na mahitaji ya wasikilizaji. Mhubiri kwa uangalifu anatakiwa kujiweka katika daraja sawa na wasikilizaji. Anatakiwa kujitahidi kuhakikisha anapokelewa na makutano na kukutana na mahitaji yao. Mhubiri anapaswa kuhubiri kwa mguso. Hakikisha unagusa mahitaji ya watu unapohubiri. Mahubiri ni uhai hivyo ni lazima yalete majawabu kwa wale tunaowahubiri. Gusa mahitaji halisi ya watu ambayo Mungu anakusukuma kuyashughulikia. Hubiri kwa ufanisi na kwa mguso. VII.Kuhubiri ni kudhihirisha uweza wa Mungu. • Bwana Yesu aliahidi kuwa na wahubiri kwa kulithibitisha neno kwa ishara na maajabu. Popote injili inapohubiriwa ni sharti Bwana awepo akiithibitisha kwa isharaMk 16:15,20. 1Kor 2:4. Hakikisha nguvu ya Mungu iko juu yako unapohubiri. Unapaswa kupakwa mafuta kikamilifu a Roho mtakatifu unapokwenda kwenye huduma ya kuhubiri kwa sababu kuhubiri ni vita. Omba Mungu Roho mtakatifu afanye uthibitisho kwa kila utakachohubiri. Ishara na maajabu ziambatane nawe kokote unakohubiri. -Ikiwa kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu mhubiri anapaswa kwenda mahali Mungu alipoongea mara nyingi na waziwazi yaani “Biblia” • Kwa njia nyingine kuhubiri ni kuipa Biblia sauti.ni kuacha Mungu aongee mwenye toka kwa Neno l D. WITO WA KUHUBIRI Sehemu ya muhimu sana katika kuhubiri ni wito. Kimsingi wito ni wa mtu binafsi Mungu huwaita watu katika huduma na watu hupokea hilo rohoni mwao kisha huja uthibitisho wa nje kupitia kanisa au watumishi mbalimbali na fursa mbalimbali. Mungu Huwaita watu wake katika nafasi na huduma mbalimbali. Wengine kuwa wachungaji, wamishenari, wazee wa kanisani, wainjilisti, au huduma nyinginezo. Kazi ya kuhubiri si ajira ambayo mtu anakwenda chuoni kusoma kwa lengo la kupata baada ya kuhitimu masomo yake, bali ni mwito mtakatifu ambao mtu huitwa na Mungu mwenyewe kuwa muhubiri. Mtu huenda chuoni ili kupata maarifa yatakayomwezesha na kumsaidia katika kutimiza mwito wa Mungu uliondani yake. Haendi chuoni kupata mwito bali wito husababisha mtu kwenda chuoni kama sehemu ya maandalio. Hivyo wito usichanganywe na ajira na maslahi binafsi ya mtu. Ni lazima wito uheshimiwe na kuogopwa. Waamini hawapaswi kujihusisha na huduma kwa lengo la kujinufaisha na kujipatia mali kwa njia za ujanja ujanja. Kimsingi kila mwamini ni muhubiri kwani agizo kuu linamhusu kila mwamini. Kila mwamini anapaswa kujihusisha na kupeleka injili kwa watu waliopotea dhambini hili ni agazo la jumla. Lakini kuna watu maalumu ambao Bwana ameweka wito wa muda wote(Full time commitement) ndani yao. Amewachagua kwa kusudi hili katika maisha yao na muda wao wote. Hawa wanasimama katika zile huduma tano za uongozi katika kanisa, ambao ni mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu. Hawa ndio Bwana amewaweka kusimama katika kazi ya kuhubiri ya muda wote, Wao hawapaswi kujihusisha na shughuli zingine bali kazi yao ni kulihudumia Neno na kuomba yaani Kuhubiri. Bwana ameweka mwito mtakatifu ndani yao ambao ni wajibu mkuu na wa kuogofyapia{.Mdo6:2,4} hili ni agizo mahususi. Wito huu haupatikani kwa njia ya kusoma au kwa njia ya ulaghai bali kwa kuitwa na Mungu mwenyewe kuwa msemaji wake. Kuna baadhi ya makanisa ambayo yameufanya wito wa Mungu kuwa ni ajira. Kwani wao huwapeleka watu kwenda chuoni kusomea huduma fulani mfano uinjilisti, uchungaji nakadharika kwao wito si jambo la msingi kwao ila elimu ndiyo yenye kupewa kipaumbele. Wao humpa mtu kushika nafasi ya huduma baada ya kuhitimu mafunzo ya chuo cha Biblia bila kujali kama ana wito au la. Matokeo yake ni kwamba makanisa yamekuwa yakiongozwa na kuhudumiwa na watu wasio na wito wenye kutegemea elimu ya darasani tu, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo na uhai wa kanisa. Elimu ni jambo la zuri sana lakini elimu haiwezi kuchukua nafasi ya wito katika kanisa la Mungu ikiwa tunataka kufikia kusudi la Mungu la mwito mtakatifu na kusimama kiuaminifu mbele zake kupata ushindi mkuu. Usiwe mtumwa wa elimu. Elimu hii unayopata ikusaidie katika kumtumikia Mungu na kufanya huduma lakini isichukue nafasi ya Roho mtakatifu katika maisha yako na huduma yako. Wala haipaswi kuwa badala ya Roho mtakatifu. E. MAANDALIO KWAJILI YA HUDUMA. Ni muhimu mara mtu atambuapo kwamba Mungu anamwita katika huduma kufanya mambo kadhaa. Mojawapo ni kuanza kumngojea Bwana kwa njia ya maombi, Kujihusisha na huduma mbalimbali zinazojitokeza kanisani au sehemu nyingine yeyote . Pia ni muhimu kwenda shule kwajili ya mafunzo zaidi ya maandalio ya huduma. Kuwa na mlezi. Ni lazima kuwa na mlezi wa huduma ambae atakusaidia katika kutimiza mwito ulio ndani yako. Mlezi wa kwanza wa huduma na wito wako ni mchungaji wako. Mweleze mchungaji kuhusu wito ulio ndani yako na mwombe akusaidie katika kuulea wito huo. Kuwa mtii na mnyenyekevu kwa mcungaji wako. Shirikiana na watu wenye wito kama wako ili uweze kujifunza zaidi. Fanya kazi na huduma mbalimbali unazopewa na mchungaji au viongozi wa kanisa. Jifunze kwa watu wenye wito kama wako walifanikiwa katika utumishi wao. Kupata mafunzo zaidi. Ni vizuri mara unapogudua kwamba Mungu amekuita katika utumishi au mojawapo ya zile huduma tano kwenda chuo cha Biblia kwaajili ya mafunzo na matayarisho kwaajili ya huduma Mungu anayokuitia. Namna ya kuchagua Chuo cha Biblia 1. Omba Uongozi wa Mungu juu ya jambo hili. 2. Angalia chuo kitakachokidhi mahitaji yako ya kuandaliwa. 3. Angalia maswala ya usajili wa chuo.(Vyuo vingi vya Biblia havina usajili wa serikali kwani haviko kitaaluma zaidi bali kihuduma). 4. Chunguza misingi ya imani ya chuo. 5. Tathmini uwezekano wa kuingizwa katika huduma baada ya mafunzo. 1. Mambo ya kuzingatia unapokuwa katika Chuo cha Biblia. 2. Jikite katika masomo kabisa kwa miguu yako yote miwili. 3. Jihusishe kikamilifu na ratiba nzima ya Chuo. 4. Tia bidii katika masomo. 5. Tumia muda kuwa na waalimu na wanafunzi wenzako na jifunze vitu vyema toka kwao. 6. Epuka kuwa mjuaji (arogant). 7. Kuwa mtumishi. 8. Jitahidi kuonekana na si kusikika. 9. Shirikisha baadhi ya watu maono na wito ulio ndani yako. 10. Baki kuwa mwanafunzi daima hata baada ya kuhutimu mafunzo. 11. Kwa mtii kwa amri, shria, kanuni na taratibu za Chuo. • Usiongozwe na elimu bali ongozwa na Roho mtkatifu. • Usihubiri kwa maneno yenye hekima pekee kwa lengo la kushawishi akili za watu bali hubiri Kwa dalili za Roho mtakatifu na nguvu. 1Kor 2:4. • Hakikisha unautumikia wito ambao Mungu ameweka ndani yako kwa gharama yoyte ile bila kujali mazingira au kitu kingine chochote. • Kwa hiyo wito wa kuhubiri hautoki kwa mwanadamu yoyote Yule bali toka kwa Mungu mwenyewe. Mungu huwafanya watu wake kuwa wahubiri. • Jiulize wewe ni mhubiri wa kufanywa na nani ? F. Kweli kuu kuhusu wito wa kuwa mhubiri. 1. Roho mtakatifu huweka wito ndani ya mtu. Wito wa Mungu huja juu ya mtu kupitia Roho mtakatifu. Katika akili ya kawida ni kazi kubwa kuhubiri au kutumika. Wito huja kwa watu wa aina zote na umri wote wowote. Baahi ya watu husikia wito na kujitoa wangali wadogo lakini wengine katika umri mkubwa n.k 2. Shauku ya kutimiza wito. Watu wanaoitwa kuwa wahubiri waliumbwa na Mungu kwa kusudi hiloYer1:4-10 Hawawezi kupata utoshelevu kwa kufanya kitu kingine chochote. Hawawezi kupinga kujihusisha katika huduma au kuchukua fursa za kuhubiri. Hata kama hakuna nafasi za kutumika moja kwa moja bado watatafuta nafasi katika huduma yoyote inayojitokeza. 3. Mungu huwaandaa wale anaowaita kwajili ya huduma. Mungu hawaiti watu ambao hwana uwezo wa kutimiza mwito wake. Wahubiri wengi wanakipaji cha kuongea. Watu wenye wito juu ya watoto Mungu huwaandaa kwa kuwapa uwezo kwa kufanya huduma na watoto n na wanaoitwa kuwa wacghungaji huwezeshwa kuwa wachungaji. Kwa namna yoyte Mungu huwaandaa na kutoa nguvu ya uwezesho juuv yao. 4. Wito wa Mungu wapaswakuwa wazi. Wito wa Mungu usifichwe. Wito wa Mungu ulioju yako wapaswa kuwa wazi kwa watu wangine lakini haupaswi kukimbilia kwenye wito huo mara moja. Hutakuwa na furaha na mafanikio na wito huo mpaka utakopokuwa umejisalimisha kwa mapenzi sahihi ya Mungu juu yako.Wito ambao Mungu amekuita kuutimiza unapaswa kuuweka wazi. Shirikisha watu ambo watafanyika msaada katiki kuulea wito wako. Fanya kazi na watu. Tumika na watu wenye wito kama wako. Kaa chini ya mtu mwenye neema kama ya wito ulionao ili uweze kujifunza zaidi. 5. Wito wa Mungu ni wito wa matayarisho. Kuna wajibu mwingi na mkubwa ambao huja pamoja na wito wa kuhubiri. Mungu akisha mwita mtu humuandaa kwanza kabla ya kumtuma na kumwachilia kwnye huduma aliyomuitia. Mhubiri anapaswa kujiimalisha kiroho na kimwenendo.Anatakiwa ajiandae kiakili kwa kusoma na kupata mafunzo. Pia anapaswa kujiandaa kimatendo kwa kunoa vipawa vilivyo ndani yake na kuyatisha maisha yake yote kulingana na wito ulio ndani ya yake. Mungu akisha weka wito wake ndani ya mtu huanza kumwandaa kwajili ya wito huo. Humpitisha katika majaribu mbalimbali yanayoendana na wito wake, humpeleka kwenye shule yake ijulikanayo kama shule ya moto na baada ya kufuzu huko Mungu humwachilia mtu katika huduma. Musa aliandaliwa kwa zaidi ya miaka arobaini, Yusufu kwa muda wa zaidi ya miaka kumi, Paulo kwa muda wa miaka kadhaa.Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba Mungu huwa hana haraka. Ukipata wito wa Mungu ndani yako usifanye haraka kuutimiza Bwana anatenda kwa wakati. Unapaswa kusubiri wakati wa Bwana na ufanye kwa wakati wake na si nje ya wakati wa Mungu. G. Mawazo mawili potofu kuhusu mahubiri. Kuna dhana mbili potofu ambazo zinajitokeza katika uwanja na taaluma ya mahubiri mawazo hayo ni: a. Maaandalizi si lazima. Wazo la kwanzalenye makosa ni kwamba maandalizi si lazima na huonesha kukosa imani kwa mhubiri. Watu wenye kushikilia msimamo huu hufikili kwamba imani ya kweli hutupilia mbali jitihada yoyote inayojaribu kuandaa akili na hiyvo husimama mimbarini wakiamini kwamba Mungu atawapa maneno ya kusema.husimamia maawazo haya: i. Roho mtakatifu atakupa unachohitaji kuhubiri. Unapopanda mimbarini. _- Zab 81:10 “ Fumbua sana kinywa chako name nitakijaza”(Hutumia andiko hili kutetea msimamo wao.). Pia husema kwamba Yesu alisema kwamba “Msifikirifikiri nini cha kusema maana mtapewa kinywa cha usemi saa ili ilie mnapotakiwa kusema” Unapoyachunguza kwa umakini maandiko hayo utagundua kwamba maandiko hayo wanayafasili nje na mkutadha wake na na kulazimioshwa yaseme kile ambacho hayamaanishi. *Mahubiri ni kamana jengola kiroho ambalo linatakiwa kusanifiwa na kuandaliwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Roho mtakatifu ndiye mhandisi mkuu wa mahubiri. b. Uwezo wa mtu unatosha. Kuweka mkazo katika matayarisho na kutegemea uwezo wa kibidanu tu. Wahubri wanaoshikilia msimamo huu hudai kwamba maandalizi peke yake yanatosha na huweka mkazo kwenye matayarisho pekee.Kumtegemea Roho mtakatifu huwa ni kudogo sana au hakuna kabisa, bali tumaini la mtu binafsi ambalo ni matokeo ya kujifunza na kuendeleza uwezo wa asili. Ujumbe wa namna hii waweza kuwa mzuri kabisa lakini hauwezi kuleta matokeo yatakikanayo daima. Kwani ni Roho mtakatifu pekee ndiye anaeweza kuleta badiliko katika maisha ya waikilizaji wako. Bila yeye mahubiri huwa ni maiti na haiwezi kuleta uhai kwa sababu ni uhai wenye uwezo wa kuzaa uhai. *Roho mtakatifu huuhuishaujumbe na kuletaq matokeo yaliyokusudiwa na Mbingu katika maisha ya wasikilizaji. Ili mhubiri aweze kuhubiri sawasawa anapaswa kuwa na maansdalizi ya kutosha katika kuuandaa ujumbe wake kwa kusoma, kutafakari na kuchambua kweli zote zilizomo katika ujumbe wake. Lakini hayo yotec anapaswa kuyafanya akiwa katika hali ya maombi. Mhubiri anapaswa kumsikiliza Roho mtakatifu klwa kina na kupata uongozi kwake na kutaka Roho mtakatifu amshirikishe kile anachotaka kusema na watu wake na kukifanyia uchambuziyakinifu katika hali ya maombi ili aweze kukiwasilisha kwa ufanisi. • Mhubiri anapaswa kutambua kwamba yeye hana watu wala si Chanzo cha ujumbe. Kwasababu hiyo anatakiwa kumsikiliza mwenye watu na aliye chanzo cha huo ujumbe na kusimama katikati kwa uaminifu kuwafikishia watu kwa usahihi kile mwenye watu anachotaka kiwafikie watu wake. • Mhuibiri anapaswa kutambua kwamba kazi ya kuhubiri ni takatifusana na ni kazi nyeti ambayo yapaswa kufanywa kwa umakini, uaminifu na unyeyekevu mkuu. • Mhubiri mwenye kutegemea juhudi zake na uwezo wake wa asili atakuwa ni muhubiri kilema na halikadharika mhibiri mweye kutegemea kupewa ujumbe akiwa mimbarini atakuwa ni kilema. • Vyote viwili vyapaswa kwenda pamoja, maombi na matayarisho.Kwa sababu mahubiri ni matokeo ya mawasiliano na ushirika mzuri kati ya Roho mtakatifu na mhubiri. H. Umhuhimu wa kujifunza homiletics. a) Linatusaidia kujua mbinu mbalimbali za kuhubiri. b) Linatusaidia jinsi ya kuhubiri bila kuwachosha watu. c) Linatufanya kuwa na ujasiri tunapohubiri. d) Linatusaidia kuhubiri kwa usahhi. e) Linatusaidia kutambua mahubiri ya uongo. f) Linatusaidia kujua na kuheshimu wito tulio nao. g) Linatusaidia kujua kusudi la Mungu la mahubiri. h) Linatusaidia katika kuheshimu wito wa watu wengine. Zoezi. Jibu maswali fafuatayo. Wanafunzi waweza kujibu katika makundi au mmoja mmoja kama kazi ya nyumbani kwa kadri mwalimu atakavyoona inafaa. 1. eleza maana ya mahubiri kwa mitazamo mbalimbali. 2. Eleza vile mahubiri yasivyo. 3. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri na kuhubiri. 4. Taja faida tano za kujifunza somo la kuandaa mahubiri. 5. Tathmini misukumo mbalimbali inayosababisha watu waingie katika huduma tano za uongozi wa kanisa. na hali hawana wito. 6. Eleza namna gani mtu aweza kujua kwamba Mungu anamwita kuingia katika huduma. 7. Eleza umuhimu wa kipindi cha maandalizi na matayarisho kabla ya mtu kuingia katika huduma ambayo Mungu anamwita kuifanya. MADA YA PILI: MBINU ZA UTAYARISHAJI WA MAHUBIRI Utangulizi Katika mada hii tutajadili aina mbalimbali za utayarishaji wa mahubiri, maeno ya mahubiri na sehumu za mahubiri au hotuba. Tutapitia kwa undani kila kimojawapo ya vipengele hivi ili kujifunza jinsi vipengele hivyo vinavyohusiana na mahubiri na tunavyoweza kuvitumia katika huduma ya kuhubiri na kuandaa mahubiri. Malengo ya mada. Baada ya kumaliza kujifunza mada hii mwanafunzi ataweza. • Kutaja na kueleza mbinu mbalimbali zinazotumika katika utayarishaji wa mahubiri au hotuba. • Kutathmini kila mbinu kwa kueleza ubora na udhaifu wake. • Kuandaa jumbe za mahubiri kwa kutumia mbinu mbalimbali. • Kutambua maeneo muhimu katika mahubiri. • Kutambua sehemu muhimu katika jumbe na hotuba. • Kutayarisha jumbe na hotuba za ki-Biblia kwa kuzingatia sehemu muhumi katika • jumbe na hotuba. A. Mbinu za Utayarishaji wa jumbe na hotuba. Kuna aina nyingi za utayarishaji wa somo au hotuba, na kila mojawapo ina umuhimu wake. Lakini katika mada hii tutajifunza aina tatu za utayarishaji wa somo au hotuba. Kila mwanafunzi anatakiwa kuelewa aina zote tatu na anapaswa kujizoeza kutumia njia hizi zote ili aweze kufaidika zaidi. Mbinu hizi za utayarishaji wa somo pia zaweza kutumika kama mbinu za kuhubri. Kwa hiyo tutakapokuwa tunajadili zitaangaliwa katika maeneo haya mawili. ( Kama mbinu za utayarishaji na kuhubiri.) 1. Somo Lililoandikwa. Katika aina hii mhubiri hupaswa kuandika kila kitu anachokusudia kukihubiri. Wakati mwingine somo lote huandikwa. Kila eneo la somo huchambuliwa kwa undani na kuwekwa katika maandishi. Ujumbe au somo lote huandikwa kikamilifu kabla ya kuhubiri. Mhubiri huelezea kwa undani somo lake anapohubiri likiwa katika maandishi. Mhubiri anapohubiri mara nyingi hupitia kila kitu alichokiweka katika maandishi. Faida za aina mbinu hii. a) Ujumbe wote huandaliwa kwa uangalifu mkubwa. b) Ujumbe huwasilishwa kwa umakini na uhalisia. c) Ujumbe huwa ni wa kitaalam. d) Mhubiri hujikita katika somo. Hasara ya mbinu hii. a) Somo huwa haliwavutii wasikilizaji. b) Utoaji wa ujumbe wa namna hii unaweza kuwa wa kuchosha usipofanywa kwa uangalifu c) Utayarishaji wake huhitaji muda mwingi. ZOEZI. 1. Eleza maana ya somo lililoandikwa. 2. Taja vitu muhimu vilivyo katika somo lililoandikwa. 3. Taja ubora na udhaifu wa njia hii licha ya zilizotolewa katika kitabu hiki. 4. .Andaa ujumbe kwa kutumia mbinu ya somo lililoandikwa na kisha huburi kwa dakika kumi. 2.Somo Lisiloandikwa. Hii ni mbinu ya utayarishaji wa somo bila kuliandika. Mhubiri husoma vifungu vya maandiko na kivitafakari kwa kina kisha hukariri vitu vya msingi vilivyo katika ujumbe wake na maandiko yanayohusika. Aina hii mara nyingi hutumika katika kutayarisha na kuhubiri ujumbe wenye uvuvio zaidi. Njia hii ni nzuri sana katika kuhubiri ujumbe wa kiinjilisti. Ujumbe hutiririka toka rohoni na huwa wa kuvutia mno. Faidaza mbinu hii. a) Ni rahisi kutumia. b) Haihitaji muda mwingi wa matayarisho. c) Mhubiri huwa huru kutoa kila kinachokuja ndani yake maadam kinaendana na ujumbe wa somo. d) Huwasisimua wasikilizaji na kuwavutia. Udhaifu wa mbinu hii. a) Mhubiri kutoka nje ya ujumbe wake hasa ikifanywa na mhubiri asiye na uzoefu. b) Wasikilizaji waweza kulielewa somo vibaya. (waweza kuelewa vile somo lisicho maanisha). c) Somo kutowajenga wasikilizaji na kuishia kusisimua tu akili zao. d) Somo kutokuwa na maana halisi na hivyo kutowajenga wasikilizaji. ZOEZI. 1.Eleza maana ya somo lisiloandikwa. 2. Taja mabo matano ya kuzingatia katika utayarishaji wa ujumbe kwa kutumia njia ya somo sililoandikwa. 3.Toa tofauti iliyopo kati ya somo lililoandikwa na somo lisiloandikwa. 4. Andaa ujumbe kwa kutumia mbinu ya somo lisiloandikwa na kisha hubiri kwa dakika kumi 3.Mbinu Ya Skeletoni. Njia hii huhusisha kuandika maelezo ya somo au ujumbe kwa kifupi kwa lengo la kufanikisha utunzaji wa kumbukumbu sahihi juu ya ujumbe au somo. Kwa maana nyingine ni kwamba mhubiri hutayarisha muhtasari wa ujumbe au somo.Mhutasari huo huwa kama skeletoni ya somo, Skeletoni maana yake ni fuvu. Mfano wa fuvu la binadamu. . Mhubiri huhubiri kwa kutumia skeleton hiyo. Kazi yake hasa ni kuweka nyama katika skeletoni hiyo kwa njia ya mahubiri. Hivyo anapohubiri huweka nyama katika mahubiri yake ili yawze kuwa kitu kamili . Mhutasari wa somo huwa kama mifupa ya ujumbe. Ndiyo mifupa ambayo huleta sura na mategemeo kwa kile mhubiri anachotamani kusema. Anavyosema anaweka nyama katika mifupa na kuufanya mwili wa somo lake. Hupanua mawazo yake ambayo maelezo yake mafupi yamekuza. Faida za mbinu hii. a) Mbinu hii humpa mhubiri uhuru zaidi. b) Utoaji wa somo huwa wa kuvutia sana. c) Somo huwajenga wasikilizaji bila kuwachosha. d) Mhubiri huweza kutoa somo kwa mtiririko mzuri na sahihi. Zoezi 1. Eleza maana ya skeletoni. 2. Eleza maana ya mbinu ya skeletoni. 3. Linganua kati ya minu ya somo lisiloandikwa na mbinu ya skeleton. 4. Eleza kati ya mbinu tatu ulizosoma, ipi ni bora kuliko zote na toa sababu ya jibu lako B. Maeneo ya Mahubiri. Kuna maeneo makuu manne ambyo mahubiri huhusisha. Mhubiri yoyote ni lazima azingatie maeneo hayo ili aweze kufanikisha mahubiri yake. I.Wazo . Hii huhusu namna ya kupokea kichwa cha somo au ujmbe. Ni ujuzi unaohusu namna ya kupokea ujumbe toka kwa Mungu. Huhusu namna ya kupata wazo la awali na kichwa cha somo. Mungu hupanda mbegu ya wazo kuhusu somo au ujumbe siku kadhaa kabla ya mahubiri. Mbegu hiyo hukua kwa njia ya kuitafakari na maombi zaidi. Kutokana na ujuzi mhubiri aweza kuujenga uwezo wa kutambua mstari unaohusika. Mhubiri hupaswa kuliendeleza na kulikuza wazo lililopandwa ndani yake kwa njia ya maombi, kutafakari na kuchunguza zaidi juu ya wazo hilo ili aweze kutayarisha ujumbe. Pata muda wa utulivu utulie uweponi na omba nuru zaidi ya ufunuo huo. Kuna tofauti kubwa kati ya hotuba na ujumbe.mtu anaweza kujifunza jinsi ya kuandaa hotuba kupitia masomo ya Homiletics lakini Mtu anapaswa kuwa na ushirika na Mungu ili aweze kupata ujumbe. Kupata ujumbe ni jambo la kiroho zaidi kuliko taaluma. Wale wanaofanikiwa kupokea ujmbe wa kuhubiri toka kwa Mungu ndio wanaoweza kufanikisha lengo la kuhubiri. Mambo ya kusaidia kupata ujumbe. Tambua mahitaji ya watu.(Mahitaji ya kiroho na kimwili). Kujazwa na Neno la Mungu. Kujiweka katika viatu vya wengine (Soma Hotuba na sikiliza mahubiri ya watu wengine. Kutokana na uzoefu wa mhubiri. Kutambua kalenda ya Kikristo. Kutokana na mafundisho ya msingi ya Biblia. Kutokana na matukio mbalimbali. II.Muundo. Muundo huhusisha uchambuzi wa wazo ili kuweza kugundua kweli zilizomo katika wazo hilo.Baada ya kupokea Wazo toka kwa Mungu unapaswa uanze kulichambua ili kutambua vitu ambavyo wazo hilo linavyo. Katika hatua hii unapaswa kuorodhesha kwa urahisi kila kitu kilichomo kwenye wazo hilo.Mara nyingi unapokuwa katka hatua hii unahitaji kuandika kwa haraka ili kupata kwa kifupi mtiririko wa uvuvio unaokuja. Hakikisha kwamba unaandika kila kitu ili uweze kuchambua baadae. III. Ujenzi. Huhusisha kukusanya na kuyaweka mawazo yako uliyoyachambua katika kipengele cha uchambuzi katika mpango mzuri. Kuweka kila kitu katika mpangilio mzuri kutakusaidia na kukurahisishia katika utoaji wa somo lako. Kuwasislisha mawazo yaliyoendelezwa hufanyika msaada sana kwa wasikilizaji wako katika kuelewa na kufuata mpango wako wa kufikiri. Somo likiwalimechanganywa itawawia vigumu wasikilizaji wako katika kulielewa somo hilo.Ujenzi wa somo hulenga kulifanya somo rahisi kiasi cha kueleweka vizuri na wasikilizaji. Ni muhimu sana kwa mhubiri kuliweka somo katika namna itakayofanya lieleweke kwa urahisi. IV. Mawasiliano. Hii huhusu namana mhubiri anavyowasilisha somo au ujumbe kwa hadhira. Mhubiri anatakiwa kuliwasilisha somo lake kwa njia rahisi na nyepesi kueleweka na wasikilizaji wake. Anatakiwa: a) Kuwasilisha ukweli uliowazi na wenye kueleweka. b) Kutoa ujumbe kwa njia ya kuteka akili za hadhira. c) Kuendeleza mawazo yake katika mpango ambao hadhira wataweza kuyafuata kwa urahisi. d) Kuwahamasisha hadhira kulitendea kazi somo. Yak 1:22. C.Sehemu Kuu za ujumbe na Hotuba. Kwa kawaida mahubiri au hotuba yoyote ile ni lazima iwe na sehemtu tatu ambazo kwa pamoja huunda hotuba au mahubiri hayo. Sehemu tatu hizo ni utangulizi, kiini na hitimisho.Kila sehemu ni muhimusana na inatakiwa kupewa uzito wake. Sehemu mojawapo ikipuzwa yaweza kuvuruga au kuharibu kabisa ujumbe au hotuba yako. I.Utangulizi. I. Hii ni sehemu ya kwanza ya hotuba. Utangulizi hutambulisha hotuba au somo zima na kutoa picha jinsi somo litakavyokuwa. Utangulizi ni sehemu muhimu ya ujumbe na kama hadhira hawajakusikiliza kwa umakini katika kipindi hiki cha awali yawezekana kutokuuelewa ujumbe wako au kutokukusikiliza vizuri katika sehemu zinazobaki za hotuba yako. Mara nygingi utangulizi huwa kama muhtasari wa ujumbe.Katika utangulizi mhubiri huwaeleza hadhira kwa kifupi juu ya kile ulichopanga kuongelea au kuhubiri. Utangulizi ni kama mlango wa nyumba katika ujumbe na hotuba.Uangulizi huwa na lengo mahususi la kuwajulisha hadhira ujumbe ambao unawasislishwa kwao. Waamni wengi huja kanisani wakiwa na matatizo mbalimbali ya kifamilia , kikazi N.k .Utangulizi unatakiwa kuwavuta ili waweze kujikita kwenye ujumbe na kuwasahaulisha matatizo waliokuja nayo. Uangulizi ni silaha ya kuwateka wasikilizaji. Kuna namna mbalimbali za kuanza utangulizi. Mhubiri anapaswa kujifunza namna mbalimbali za kuanza utangulizi na ajizoeze kuanza utangulizi wa mahubiri yake kwa njia tofauti tofauti. Baadhi ya njia za kuanza utagulizi zimeorodheshwa hapa chini. II.Namana ya kuanza Utangulizi 1. Kuanza kwa kuuliza swali. 2. Kuanza na maelezo ya kuchanganya(Yenye kuhamasisha watu kusikia kw2a makini swehemu ya ujumbe inayobaki ). 3. Anza kwa andiko 4. Anza kwa mkutadha 5. Anza na habari au kielelezo. 6. Anza na tukio la sasa. 7. Anza na nukuu III. Mambo ya msingi katika utangulizi. Kuteka usikivu. utangulizi wako unapaswa utawale hamu na mawazo ya wasikilizaji. Kujenga masikilizano. Lazima ujenge mawasiliano kati yako na wasikilizaji. Kuleta kukubalika. Ni lazima utangulizi kwako ukujengee kukubalika kwa wasikilizaji. Unapaswa kupata usikivu wao, matumaini na heshima. Kujulisha. Utangulizi wako unapaswa kuwaeleza wasikilizaji kwamba somo lako lina husu nini hasa, na jinsi utakavyoliwasilisha. Kusadikisha. Ni lazima utangulizi uwasadikishe wasilizaji juu ya umuhimu wa ujumbe na kupata usikivu mzuri wa sehemu iliyobaki ya hotuba yako. Usitoe utangulizi kwa kuomba msamaha. Usiseme “Bahati mbaya sikujiandaa vizuri” Kufanya hivyo kutapoteza usikivu wa wasikilizaji wako na kukufanya usiaminike kwao. Sifa za utangulizi mzuri. 1.Sio wa kishindo mno. Utangulizi uwe wa kiasi usiweke hatua ambayo huwezi kuifikia. 2.Sio mrefu mno. Kumbuka kwamba utangulizi si ujumbe wote bali ni sehemu tu hivyo unapaswa kuwa mfupi. 3.Utangulizi uendane na ujumbe. Utangulizi ni sharti ulenge kichwa cha somo. Waweza kuwa muhtasari wa somo au kisa ambacho kinaonesha ukweli wa kile ulichokusudia kuongelea. 4.Unapaswa kuandaliwa kwa uangalifu. Kwa sababu utangulizi wako ni kitu muhimu katika kuvuta usikivu wa hadhira unapaswa kuandaliwa kwa umakini sana. 5.Tayarisha utangulizi wako kwa kujiuliza maswali yafuatayo a.“ Ningekuwa ni msikilizaji wa ujumbe huu nini kingenivuta zaidi ili kuleta usikivu katika yote niliyokusudia kuyasema? 1. “ Ni jambo gani hasa ambalo lingekamata usikivu wangu? b.Majibu yake unayoyapata ndiyo waweza kuyatumia katika sehemu ya utangulizi wa ujumbe wako. 6. Utoe nafasi ya kupitia kwenye kiini cha ujumbe. Utangulizi unapaswa kutoa njia ya kupitia kwenda kwenye kiini cha ujumbe. Kusiwe na pengo kati ya utangulizi na kiini cha ujumbe. II. Kiini. Hii ni sehemu kuu ya somo au ujumbe ambayo imebeba ukweli wote wa somo. Hatua ya kwaza kwenye kiini ni kutoa skeletoni ya kiini na kisha hatua ya pili ni kuweka nyama katika skeletoni yako.Waweza kuweka nyama katika sekeletoni yako kwa kufanya yafuatayo: Kufafanua msamiati mbalimbali inayojitokeza kwenye kiini na kutoa maelezo ya dondoo ulizoziandaa. Tumia kamusi au itifaki ya Biblia katika kupata maana ya maneno hayo. Kiini. Kiini cha ujumbe ni lazima kieleze, kisimulie, kijadili na kutoa kweli yote inayokusudiwa kuwasilishwa. Ni lazima kueleza maana ya andiko au habari. Ni lazima kutoa ushahidi wa kweli inayohubiriwa. Neno la Mungu linajieleza lenyewe. Jambo lingine la kutumia kuthibitisha ni ushuhuda binafsi. Mfano kama unahubiri uponyaji toa uthibitisho kwa kutumia wewe binafsi jinsi Mungu alivyokuponya au alivyowaponya watu wengine. Unapounda kiini unapaswa kujiuliza maswali kadhaa 1. NIini nataka kusema ? 2. Kwanini ninataka kusema hiki ? 3. Ni vipi nitakisema ? 4. Ninachotaka kukisema kitafanikisha nini ? Unaposhughulikia andiko au mada ni lazima kujiuliza kwanini? Namna gani ?, Lini?, Wapi ?, Nini kilitokea kabla na baada ?, Mazingira yalikuwaje?, Matokeo yake yalikuwa nini ?, Nani walikuwa pale ?, na kwanini walikuwepo pale? Walifanya nini?, Hii huhusikaje leo ? na inamaanisha nini leo ?. Kujua majibu ya maswali haya kutakusaidia kutengeneza mhutasari wa somo au andiko. Mfano Luka 16:19 Matumizi ya vielelezo. Moja wapo ya vipengele muhimu katika ujmube au kiini ni vielelezo.Vielelezo ni mifano mbalimbali inayotumika kufafanua na kuelezea ujumbe au somo. Watu wengi huweza kukumbuka vielelezo kuliko ujumbe na hivyo basi vielelezo husadia watu kukumbuka ujumbe. Bwana Yesu amekuwa kielelzo na mwalimu wa vielelezo. Watu hufurahia kusikia vielelezo. Wahubiri wenye ujuzi wa kutumia vielelezo katika jmube na hotuba zao hufanikiwaq kuvuta usikivu wa wasikilizaji wao. Vielelezo ni sawa na madirisha katika nyumba. Vielelzo ni madirisha ya jumbe na hotuba. Jumbe nyingi zinazohubiriwa na wahubiri wengi ni kama nyumba zisizo na madirisha. Nhyumba hizo zaweza kuwa na msingi imara na kuta imara lakini zitashindwa kuingiza mwanga na hewa ya Oksijeni ambayo ni muhimu kwa mwanadamu ili aweze kuishi. Vielelezo hutimiza lengo la kuleta nuru na hewa ya oksijeni ya ki-Biblia katika ujumbe. Vielelezo havipaswi kuwa mwisho vyenyewe lakini vyapaswa kufafanua kweli zinazoawsislishwa. Lengo la vielelezo. Kuleta nuru kwenye somo. Kuvuta usikivu. Kuelezea na kufafanua ujumbe. Kuthibitsha kweli (dondoo). Kanuni za kutumia vielelezo. Kuna kanuni kadha ambazo ni muhimu kuzizingatia wakati wa kutumia vielelezo . Baadhi ya kanuni hizo zimejadiliwa hapa chini. 1. Urahisi. Vielelezo vinapaswa kuwa rahisi kiasi cha kueleweka na kila msikilizaji. Havipaswi kuwa vigumu kiasi cha kuwachanganya wasikilizaji na kuhitaji vielelezo zaidi ili kufafanua vielelezo. Kuna baadhi ya vielelezo ambavyo huhitaji vielelzo vingine . Epuka kutumia vielelezo vya namna hiyo. Yesu alipotumia vielelezo vilikuwa rahisi na wazi Mifano aliyotoa ilkuwa wazi na rahis kueleweka na waikilizaji wa aina zot. Wasomi(mafarisayo na masadukayo) na wasio wasomi (wakulima na wavuvi). Kumbuka kwamba watu wengi utakaokuwa unawahubiria watakuwa ni wenye elimu ya kawaida au wasio na elimu. 2.Ukweli. Hadithi na vilelelzovinavyotumiaka katika amhubiri view wazi. Kama ni hadhi za kutunga usiwaambie watu kwamba ni matukio halisi yaliyotokea. Usilazimishe mfano na kuelelzo kuwa kitu halisi. 3.Kiasi. Vielelzo visizidi na wala visigeuke kuwa ujumbe. Kuna baadhi ya wahjubiri ambao ni mabigwa wa kutoa vielelezona watu huvutiwa sana na vielelezo hivyo. Wanatumia muda mwingi kusimulia vielelzo badala ya kuhubiri. Jambo hili ni hatari sana. Vielelezo vinatakiwa kutumika kuelezea kweli za kiroho na na visigeuke kuwa jumbe.Yesu hakututuma kusimulia hadithi na vielelzo alitutuma kuhubiri. Kwa kawaida kila dondoo kuu inapaswa kuwa na kielelezo kimoja na si vinginevyo. 4. Lengo. Unapaswa kukumbuka kwamba lengo la vielelezo ni kuelezea na kufafanua ujumbe wako. Kweli zipo kumsaidia mhubiri kufikia lengo lake la mahubiri. Lengo la mhubiri linapaswa kubaki kuwa ujumbe na si vielelezo. 5. Uhalisia. Vielelezo viendane na dondoo unayoielezea. Kama hakuna uhusiano hakuna umhuhiu wa kutumia kielelezo hicho. Hakikisha vinahusiana na kwendana. Vyanzo vya vielelezo. Bwana wetu Yesu Kristo alitmia vielelezo na mifano kutoka katika mazingira ya kawaida yaliyomzunguka. Alitumia mifano rahisi kama vile nuru, chumvi mbegu. Mzabibu, kondoo. N.k. Alitumia mifano iliyokuwaikitumika katika maisha ya kawaida. Alizielezea na kuzifafanuana kuzifundisha kweli za kiroho kwa kutumia vielelezo vilivyokuwa katika ulimwengu uliomzunguka. Hivyo basi kila mhubiri anatakiwa kujifunza kutumia vitu mbalimbali vilivyo katka mazingira yake kama vielelezo. Soma vitabu, magazeti ,vijarida na vipeperushi. Sikiliza natutzama vyombo vya habari. Katika mabo yote hayo kua vielelezo vingi ambavyo waweza kuvipata na kuvitumia. Kabla ya kuanza kuitumia kielelezo hakikisha unatihafamu vizuri. Kielelezo kiwasaidie watu kujisikia, kusikia na kuona kile unachokielezea. Ni lazima wewe mwenyewe uguswe na kuvutiwa na kielelezo hicho. Kama hakikuvuti wewe bila shaka hata watu wengine hakita wavutia. Jifunze kwa mwalimu mkuu Yesu Kristo. Vichekesho. . Vichekesho ni muhimu katika mahubiri kutegemeana na ujumbe unaohubriwa. Vichekesho vyapaswa kuendana na somo au ujumbe. Tumia vichekesho kuamsha akili za watu na kuvuta usikivu wao. Vichekesho havipaswi kuzidi kiasi cha kupunguza uzito wa somo. Pia Ujumbe usitawaliwa na vichekesho. Kumbuka kwamba mahubiri si vichekezo ni kitu muhimu na nyeti sana. Usifanye mahubiri kuwa komedi. Wala usiwe mwanakomedi. III. Hitimisho. Hii ni sehemu ya mwisho ya hotuba au ujmbe lakini kipengele cha muhumi sana . Kipengele hiki kisipozingatiwa maana na malengo yote ya kuhubiri huvurugika na kutokuwa na maana. Hivyo ni lazima kipewe uzito unaostahili. Mambo ya kuzingatia. Tunia muda kidogo kwa kuuelezea ujumbe kwa kifupi. Kazia maeneo ya msingi unayofikiri kwamba hayakueleweka vizuri kwa hadhira wakati ukihubiri na yale yanayotakiwa kupewa uzito maalumu. Pia waweza kurudia kuzitamka kwa sauti dondoo za ujumbe wako kila moja. Usiwachushe (bore) kwa kuanza kurudia kuhubiri ujumbe wako wote. Mwaliko. Mwaliko ni kipengele muhimu sana katika hitimisho. Kwa sababu mahubiri ni tofauti na aina nyingine za hotuba hivyo mwaliko huwa ni muhimu sana kwa kuwa mahubiri huhusu kuchukua maamuzi au hatua juu ya kile kilichohubiriwa. Mahubiri bila mwaliko huwa hayajafikia lengo la kuhubiri. Mwaliko ni lazima katika mahubiri ya aina yoyote ile. Mwaliko huwa ni wakati wa kuitikia Kile Mungu amesema kupitia mahubiri. Ni wakati wa kutendea kazi kile kilichofundishwa au kuhubiriwa. Mhubiri anapaswa kuufanya mwaliko kuwa wazi kwa wasikilizaji wote. Lengo la mwaliko si kuwaita watu madhabahuni tu bali ni kuwahamasisha watu kuweka ujumbe katika matendo. Pia Mhubiri hutakiwa kuuweka ujumbe wake katika matendo. • Ukihubiri uponyaji waite watu madhabahuni na waombee uponyaji. • Ukihubiri kutembea katika mamlaka unatakiwa udhihishe mamlaka hiyo. • Ukihubiri utoaji waite watu kumtolea Mungu. • Ukihibiri toba unapaswa kuwaongoza hadhira kwenye maombi ya toba na kuwaita madhabahuni wale wanohitaji kutengeneza kwa upya mwenendo na mahusiano na Mungu na kuomba nao. • Wapeleke watu kwenye matendo na matumizi Mt 21:23. Yak 2:22. • Unatakiwa kuwaongoza hadhira kuomba kwaajili ya ujumbe au somo kwa kadri ya maongozi ya Mungu na kwa kadri Mungu alivyosema na kila mmoja. • Unaweza kuwaongoza watu waimbe wimbo unaoendana na ujumbe uili kuwaogoza uweponi na kuwapa hamasa. • Toa mwaliko kwa watu ambao wanataka kuokoka na kama wapo omba nao. Baada ya hapo maliza na mkabiribishe anaehusika na ratiba inayofuata. Kwa kuhitimisha juu ya sehemu tatu za ujumbe au hotuba twaweza kuvifupisha vipenele vyote hivyo vitatu kwa sentensi tatu ambazo ni: 1. Waambie hadhira kile unachotaka kuhubiri.(Utangulizi.) 2. Hubiri kile ulichowaambia (Kiini), kisha: 3. Waambie kile ulichohubiri.(Hitimisho). ZOEZI. Katika makundi ya watu watatu watatu jadilini maswali yafuatayo: 1. Jadili umuhimu wa vipengele vinne vya maeneo ya mahubiri kila kimoja. 2. Nini kitatokea kama mhubiri atatayarisha ujumbe wa mahubiri bila kuzingatia maeneo hayo. 3. Eleza umuhimu wa sehemu tatu za ujumbe wa mahubiri. 4. Mhubiri bora ni lazima azingatie sehemu tatu za ujumbe. Jadili kauli hii kwa mifano dhahiri. Kuhubiri si kazi rahisi. Kubali usemi huu kwa hoja kumi madhubuti. MADA YA TATU: AINA MBALIMBALI ZA MAHUBIRI. Kuna aina mbalimbali za mahubiri na kila aina ya mahubiri ina nafasi yake katika kuujenga na kuimarisha mwili wa Kristo na kuwaleta waliopotea dhambini. Mhubiri analazimika kufahamu aina mbalimbali za mahubiri ili aweze kuwa na ujuzi mwingi wa kuhubiri na ili aweze kuhubiri kwa kuyafanya mahubiri kuwa mapya kila ahubiripo. Kuhubiri kwa kutumia aina mbalimbali za mahubiri huwajenga wasikiliza kwa namna mbalimbali ambapo aina mojaya mahubiri isingeweza kufanya hivyo. Pia husaidia washirika na waamini kuwa na msingi mzuri wa uelewa wa Neno la Mungu. I. Mahubiri ya kifungu. Aina hii ya mahubiri hujengwa juu ya kifungu kimoja kidogo cha maandiko tu. Huhusisha kuchagua maelezo fulani maalum ya maandiko na kuyachunguza, kuchambua na kugundua kweli zote zilizomo ndani yake na kuziwasilisha kwa wasikilizaji kwa mtindo rahisi na wenye kueleweka. A. Faida za mahubiri ya Kifungu. a) Huvutia. b) Huzuia kutoka nje ya somo. c) Hufanya mahubiri kuwa ya ki- Biblia. d) Humwongezea mhubiri ujasiri. e) Husaidia wasikilizaji kulikumbuka somo. B. Jinsi ya kuandaa mahubiri ya kifungu. Kuna mambo kadhaa ambayo mhubiri anapaswa kuyazingatia wakati wa kuandaa mahubiri ya aya, badhi ya mambo hayo yamejadiliwa hapa chini. 1.Soma Biblia mara kwa mara. Unapaswa kusoma Biblia mara kwa mara ikiwa unataka kuwa mhubiri mwenye mafanikio katika huduma yako. -Tenga muda wa kusoma Biblia kila siku. Beba Biblia ndogo kila mahali unapokwenda ili upatapo muda uweze kuisoma. 2. Jifunze Biblia. Kujifunza ni zaidi ya kusoma.Kujifunza kuna husisha kusoma Biblia kwa undani kwa kuchunguza kikamilifu kila kitu kilicho katika maandiko unayosoma na kutafakari kwa kina,.Yos1:8. Unapaswa kutafakari kwa uangalifu vitu unavyosoma. Viweke kwenye akili yako na kuvifikiri tena na tena. Unapaswa kujizoesha kuchambua kile ulichojifunza. Baada ya kukichambua kwa umakini unapaswa kukiweka tena akilini. 2. Kuwa na Daftari la kuandikia. Kila usomapo Biblia yako jitahidi kuwa na kalamu na daftari la kuandika mambo muhimu unayojifunza. Jenga mazoea ya kuandika kwa ufupi kila ufunuo unaoupata. 3. Dumisha hali ya maombi. Unapaswa kuwa katika hali ya maombi kila usomapo Biblia .Omba Mungu akufunulie upate kulielewa Neno lake.Pia unapaswa kumwomba Mungu akupe usikivu juu ya kweli anazokufunulia katika Neno lake. 4. Jenga usikivu.Unapaswa kuwa katika hali ya utulivu na usikivu katika Nyanja zote yaani kimwili, kiroho na kisaikolojia. Mungu hutoa ufunuo wake kwa sauti ya kimya ndani ya roho ya mhubiri. Kama hunautulivu na usikivu wa kutosha ni vigumu kugundua maarifa hayo.. - C.Sifa za aya ya mahubiri Kifungu cha mahubiri au aya yapasa kuwa : a. Yenye mamlaka ya ki-Biblia. Mafundisho unayokusudia kuhubiri toka kifungu au aya fualani ya maandiko yapasa ikubaliane na kile Biblia nzima inachofundisha. Katika mahubiri ya kifungu kuna uwezekano wa kuchukua kimakosa mstari nje ya maana yake na kuutumia kufundishia kitu ambacho Biblia haikubaliani nacho. Ni Muhimu sana kwa ,mhubiri kujua jinsi mstari anaoshughulikia jinsi unavyokubaliana na kusudi la sura yote na kitabu chote. Daima mhubiri anapaswa kujitahidi kufasili aya yake katika nuru ya yale ambayo Biblia nzima inafundisha. b.Kamili. Aya yapaswa kuwa katika maandisha ya ukweli ulio kamilika. Baadhi ya wahubiri huchukua kifungu cha maneno katika mstari na kukitumia bila kujali maneno yaliyotangulia au yanayofuata. Jambo hili si zuri na huzaa mafundsho ya uongo. Na huku huitwa. “Kulichanganya neno la Mungu na uongo……..2Kor 4:2. Ni lazima uepuke jambo hili kwani litaleta kutokuaminika na maelezo yasiyo ya ki- Biblia na hatimae utawapotosha wasikilizaji wako. c. Fupi kiasi. Kifungu cha mahubiri chapaswa kitolewe kwenye maelezo ya maandiko ambayo ni mafupi na ya kulizisha. c. Ya kueleweka. Aya yapaswa kueleweka na iwe muhtasari wa kutosha wa kile unachotaka kukishirikisha. *Unapaswa ubaki katika mipaka ya kile ambacho aya yako inaelezea. D. Namna ya kuandaa mahibiri ya aya. a. Elewa maneno yake vema. Kipitie kifungu kwa kukisoma mara kadhaa, kitafakari na kujenga kumbukumbu juu yake na kiseme mwenyewe kwako. Hakikisha unakielewa vizuri. b. Elewa lugha yake.Tamabua lugha yake kama ina maana halisi au kama ni lugha ya mifano tu. Jiulize kama mwandishi alikuwa na maana hasa ya kile alichokiandika au maneno yake yachukuliwe kama mfano wa mahubiri? c. Changanua ujumbe wake.Chambua ujumbe unaoupata na kuutenga katika sehemu kadhaa zenye kulandana ili uweze kuuwasilisha kwa mtiririko mzuri. d. Chunguza maneno yake. Jitahidi kugundua kile maneno hayo yalikusudia kuwasilisha hapo awali. Ikiwa una kamusi ya kigiriki au Kiebrania unapaswa kulitazama neno hilo. Jaribu kubaini kama kuna maana maalumu ndani ya neno unalolishughulikia. Kufanya hivyo kutakusaidia kugundua maana yoyote maalumu ambayo mwandishi alikusudia kuiwasilisha. e. Tathmni mwendelezo wake. Baini kweli zile mwandishi alitaka kuzielezea. Tambua jinsi alivyo kamilisha katika kuziwasilisha kweli hizo. Jaribu kufuata mwongozo wake na kuuendeleza katika mtindo huo. f. Mkutadha wa kifungu.. i. Maneno ya mbele na ya nyuma ya kifungu. Angalia jinsi mistari iliyotangulia na inayofuata inachosema. Chunguza aya kuhusiana na sura nzima ambayo umetoka. Chunguza kifungu hicho katika nuru ya kitabu kizima ambamo kinapatikana. Jifunze kiini na mazingira yote ya kitabu. ii. Hali ya mila. Je mila za wakati ule ziliathiri kile kilichoandikwa? Je watu walioandikiwa kifungu hicho awali wangekuwa na wazo la kile kilichoandikwa tofauti na ambalo tungepata katika hali yetu? Kama ndivyo nini ingekuwa maana inayolingana na sasa? ii. Hali ya kihistoria. Je jambo hili liliandikwa lini? je wakati huo ulishawishi kile kilichoandikwa? Je matukio ya wakati ule yaliyokuwa yakijulikana wakati ule wa uandishi yalikuwa na maana maalum juu ya kile kilichosemwa? iv. Hali ya kijiografia. Mwandishi alikuwa wapi wakati anaandika maneno hayo? je Watu walioandikiwa walikuwa wapi?Je mazingira yao yana uhusiano wa chochote katika kile kilichosemwa? v. Biblia kwa ujumla. Kila sehemu ya maandiko ifasiliwe kwa uaminifu na kwa umakini ili ikubaliane na maandiko yote. Andiko lolote lisifasiliwe nje ya mkutadha wake. Maandiko ni lazima yafasiri maandiko. E.Kupanga Maelezo. Mpanglio mzuri wa maelezo na kazi kwa ujumla ni wa maana sana kwa mhubiri. Hakikisha unapanga maelezo yako kimaantiki. Mpangilio mzuri wa kazi na mawazo humwezesha mhubiri kulielewa vizuri somo na kulishughulikia somo kikamilifu. Pia huwawezesha wasikilizaji kulielwa somo na kulikumbuka somo . 1. Ujumbe uwe katika mpangilio.Panga ujumbe wako katika mtiririko mzuri ili uweze kuufuata kwa urahisi wakati wa kuhubiri. 2. Weka ujumbe wako katika hali ya kueleweka. Jitahidi kukamilisha vipengele vyote unavyohitaji kuviongelea katika mahubiri yako. Kabla ya kupanda mimbarini. 3. Kazia katika mawazo. Unapaswa kuyaweka mawazo yako katika sentensi fupi. Jifunze namna ya kuyaimarisha mawazo yako kwa pamoja na kuyaelezea katika sentensi fupi zinazoeleweka kwa urahisi.Jizoeze kupunguza na kulielezea wazo kwa sentensi moja. 4. Tayarisha maelezo mafupi.Kumbuka kwamba maelezo yako ili kusaidia kumbukumbu yako.unapaswa kuwa na vidokezo vitakavyosaidia kulikumbuka somo lako au ujumbe wako. 5. Ufanye rahisi kuusoma. Ni vizuri kupiga chapa mahubiri yako ili uweze kusoma kwa urahisi wakati wa kuhubiri. Pia waweza kutoa vipeperushi na vijarida kwa wasikilizaji wako ili waweze kufuatilia zaidi ujmbe au somo lako. Zoezi. 1. Eleza maana ya mahubiri ya aya. 2.Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya aya. 3.Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya aya au kifungu licha ya yaliyotajwa katika kitabu hiki. 4. Andaa hotuba ya mahubiri ya aya na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako. II. MAHUBIRI YA KUFAFANUA. Mahubiri ya kufafanua ni aina ya mahubiri ambayo huhusisha kuchagua sehemu kubwa ya maandiko na kuichunguza kwa undani na kuifasiri na kugungua kweli zilizomo katika sehemu hiyo ya maandiko na kushirikisha mkutano au usharika wako. Mfano unaweza kuamua kupitia Injili yote ya Luka sura baada ya sura. Kuanzia sura ya kwanza, unatafuta kufasili na kuelezea maana na umuhimu wake mstari kwa mstari sura kwa sura mpaka umeimaliza yote. Waweza kushughulikia sura moja kila wiki, na baada ya wiki kadhaa utakuwa umemaliza kitabu chote. A.Faida ya mahubiri ya ufafanuzi. Hufanya mahubiri kuwa ya ki-Biblia. 1. Yesu alitumia aina hii ya mahubiri. Alichukua kifungu cha Agano la kale na kufasili maana yake kwa wasikilizaji wake. 2. Petro alitumia njia hii siku ya Pentekoste. 3. Stefano alitumia njia hii. Huwezesha waamini kuwa na msingi na uelewa mkubwa wa Biblia.Waamini huimalishwa na huwa na ufahamu mzuri na wa kina wa Neno la Mungu. Kwani kweli zote zilizomo katika kitabu kilichopitiwa tayari hufahamika vizuri kwa usharika wote. Huvuta kuimalishwa na Roho mtakatifu. Roho mtakatifu hulithibitisha neno lake kwa ishara na miujiza sawasawa na Kweli zote zilizofunuliwa katika kitabu husika. Humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia. Mahubiri ya kufafanua humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia kwani mhubiri huhubiri kile kilicho katika maandiko ya eneo husika. Mhubiri huwa anajikita katika mkutadha wa aya, sura na kitabu chote kwa ujumla. Hivyo kiini cha kitabu ndicho ambacho hubeba mahubiri yake yote. Mambo ya kuzingatia katika kutayarisha mahubiri ya kufafanua. I. Kwa umakini chagua kifungu cha maandiko kinachostahili. Hakikisha kwamba kifungu hicho kitahudumia uzima na uwezo wa wasikilizaji wako. 1. Usichague somo kwa sababu linakuvutia au kukupendeza. 2. Usichague somo ambalo litazaa machafuko, mgawanyiko na mashindano. 3. Jitahidi kufanyika njia ili Mungu akupitie ili aweze kuongea Neno lake kwa watu wake kwa kupitia wewe. 4. HIvyo basi unawajibika kutafuta kujua mawazo ya Mungu kuhusu watu wake ambao amekupa wajibu juu yao. 5. Huduma hii ni moja ya heshima kuu uliopewa lakini pia ni wajibu mkuu unaoogopesha sana. Hivyo basi unapaswa kuifanya kwa umakini wa hali ya juu. II.Tafuta ujumbe unaolingana na hali ya watu ya wakati ule. 1. Mungu kila mara huwa na ukweli wa sasa ambao hutaka kunena na watu wake. 2. Mungu hukusudia jambo maalum kwa kila kundi la waamini 3. Jifunze kujua kile Mungu anacho kwaajili ya kusanyiko kwa kila wakati. III. Jifunze sura ya kitabu kwa umakini. 1. Soma sura unayoshughulikia mara nyingi mpaka umeielewa vizuri. 2. Soma kwa uangalifu mstari hadi mstari. 3. Kila kunapokuwepo na uhusiano wa wazi kati ya kifungu hicho na kifungu kingine unapaswa kusoma kifungu hicho ili uweze kupata maana zaidi. Maandiko hufasiri maandiko. 4. Jenga usikivu kwa sauti ya Roho mtakatifu ili kupokea ufunuo toka kwake. Tumia vitabu vya rejea ili kupata msaada zaidi. Mfano. Itifaki ya Biblia, Kamusi ya Biblia, Biblia ya Tafsiri nyingine.Nk IV. Kusanya taarifa muhimu. Waweza kupata vitu vingine muhimu vya kuhusisha kwenye somo lako kwa kutumia mbinu ya maswali na majibu kama ifuatavyo. 1. Nimewahi kusikia au kusoma nini juu ya somo hili? 2. Roho mtakatifu amewahi kunionesha nini juu ya somo hili? 3. Nimewahi kuona nini chenye uhusiano na somo hili ? 4. Nimewahi kuwa na mawazo gani juu ya somo hili ? 5. Naweza kupata habari zaidi ju ya somo hili kwa nani au wapi ? 5. V. Tambua kiini cha somo lako. 1. Daima tafuta kugundua kiini cha sura unayoshughulikia. 2. Tafuta kujua kile Roho mtakatifu alikusudia kuwasilisha alipoivuvia sura hiyo. 3. Gundua undani wa somo hilo. 4. Baini kile Mungu anataka kusema na watu wake kupitia sura hiyo. VI.Kuwa na Lengo kamili. Lengo lako daima lapaswa kuendana kikamilifu na lengo la Mungu. 1. Hakikisha kwamba Umegundua kile Mungu anataka kutoa kupitia maadiko hayo na kisha jizamishe katika kile Mungu anataka kufanya. 2. Unapaswa kuhisi kile Mungu anachohisi Mungu humshirikisha mhubiri moyo wake na akili yake ili waweze kufanya kazi pamoja. Unapaswa kuchangamka. 3. Fanyika chombo cha Mungu cha kupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu wake. 4. Kumbuka hukuitwa kushiriki mawazo yako na watu bali kuwashirikisha watu mawazo ya Mungu. VII. Zungumza kulingana na ujuzi wako mwenyewe. 1. Usitoe nadharia toa uhai. Hubiri kile ulicho na uzoefu nacho.kile ambacho umekifanyia kazi . wapaswa kuwa mtu kwa kwanza kula matunda ya kazi yako. 2. Umeitwa kuwa barua Sio tu kwamba unataakiwa kuuhubiri ukweli bali pia unatakiwa kuufanyia mazoezi na kuuonesha kwa matendo. 3. Unapaswa kuwa mfano hai wa yote unayoyahubiri. VIII. Upe maana ujumbe wako. 1. Unawajibika kwa uwezo wako wote, kuhakikisha kwamba maana ya kweli na umuhimu wa maandiko unakuwa wazi na wakueleweka kwa wasikilizaji. 2. Daima jitahidi kuufanya ujumbe wako kuwa rahisi. 3. Hivi ndivyo Yesu alivyofanya Hii ilisababisha huduma yake kuwa na nguvu na mafanikio. 4. Alichukua mambo yaliyokuwa mafumbo na akayaweka rahisi sana. 5. Wahubiri wengine huyachukua masomo rahisi sana na kuyafanya mafumbo magumu sana kiasi cha kutoeleweka kwa wasikilizaji wake au kuelewa kidogo. IX.Fanya ujumbe wenye kutekelezeka. 1. Daima unapohubiri jitahidi kuonesha wazi wasikilizaji wako jinsi wanavyoweza kuutendea kazi ujumbe wako. 2. Jitahidi kutoa ushauri wa kimatendo kuhusu watu wanavyotakiwa kumwitikia Mungu kwa namna ya kufaa. 3. Husianisha mahubiri yako na maazimio yako kimatendo ambayo yaweza kuwafanya watu kuwa watendaji wa Neno na si wasikilizaji tu. Zoezi 1.Eleza maana ya mahubiri ya kufafanua. 2. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya kufafanua. 3. Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya kufafanua. 4. Chagua sura mojawapo ya injili ya Yohana na kisha andaa mahubiri ya kufafanua kutokana na sura hiyo na kisha hubiri kwa dakika kumi. III. MAHUBIRI JUU YA MAISHA YA WATU. A.Utangulizi Hii huhusu hadithi ya maisha ya watu. Kwa hiyo njia hii huhusisha mafunzo juu ya maisha ya watu mbalimbali tunaosoma habari zao katika Biblia. Kila hadithi ya mtu iliyoandikwa katika Biblia ina umuhimu kwetu. Maisha ya kila mhusika aliye kwenye Biblia yana mafunzo kadhaa ambayo twaweza kujifunza. Kila habari iliyoandikwa kwenye Biblia ipo kutufundisha kitu fulani ambacho ni cha thamani sana. 1Kor 10:1-11. Mhubiri huchagua mhusika mmojawapo wa wahusika walio katika Biblia na kujifunza kwa kina kila kitu kilichotoke katika maisha ya mhusika huyo, tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Pia mhubiri hutakiwa kujifunza kuhusu nasaba na mbari ya mhusika huyo ili aweze kufahamu vizuri vitu vilivyomjenga na kumkuza mhusika, kisha hutayarisha mahubiri juu ya mhusika huyo na kuhubri katika kusanyiko lake. Mafundisho ya wahusika wa Biblia ni ya kushangaza na ya kuvutia. Katkia aina hii ya mahubiri, mhubiri hupaswa kuchagua mhusika mmoja na kusoma habari zake zote zilizo kwenye Biblia na kisha huandikia kila wazo analolipata. Hapa mhubiri anapaswa kusoma kumbukumbuzote za mhusika katika Biblia. Baada ya kusoma kumbukumbumbu hizo unapaswa kuanza kuweka pamoja mawazo yote unayoyapata katika utaratibu wa miaka yaani jinsi matukio yalivyotokea ya mhusika huyo. B. Faida za mahubiri juu ya maisha ya watu. I.Hufunua ukweli wa maisha. Biblia imeeleza wazi maisha ya wahusika kama yalivyokuwa bila kuficha chochote. Imeeleza mafanikio yao na madhaifu yao. Ukweli wa maisha ya wahusika umewekwa wazi na kwa uhalisia. Wengi wa mashujaa wa Biblia wanahitilafu zao za kibinadamu.Twajua kuwa walikuwa wanadamu kama sisi na walikutana na majaribu kama sisi. Katika visa vyote vya historia kuna mtu mmoja tu mkamirifu ambae ni Yesu kristo pekee. Hata mashujaa wakubwa wa imani walikuwa na hitilafu zao. Hii inatupa kujua kwamba wao si tofauti na sisi. Ni mifano ya kujifunzia. Ni mifano na msada kwetu. Tunaweza kujifunza kutokana nayo kuliko ujuzi wetu wa uchungu. C. Mambo ya kuzingatia a) Jifunze kuzaliwa kwa huyo mtu. b) Tafakali hali na mazingira aliyolelewa. c) Angalia uhusiano wake na Mungu katika maisha yake. d) Angalia jinsi alivyo wajibika kuhusu uhusiano wake na Mungu. e) Baini vitu alivyojifunza kutokana na mahusiano yake na Mungu. f) Tathimini mafanikio yake. Jifunze vitu vilivyomfanya afanikiwe. g) Tazama maeneo aliyokosea kama yapo. Na jifunze vitu vilivyomfanya akosee. h) Toa hitimisho kile tunachoweza kujifunza kutokana na maisha ya mtu huyo. Mambo hayo yote yanavutia na ni yenye vitu vingi vya Kutufundisha ambayo twaweza kujifunza kutokana na watu hao. Tunaosoma habari za maisha yao katika Biblia. D. Hatua za kufuata katika kuandaa mahubiri juu ya maisha ya watu. I. Chagua mtu au msusika toka kwenye Biblia. Unapaswa kuanza na watu mashuhuri katika Biblia ambao habari zao ziko wazi kabisa, kama vile Ibrahimu,Musa,Samweli, Daudi, Yusufu, Debora, Miriamu, Mariamu, Dorkasi, Paulo, Petro. N.k. Hawa ni baadhi ya watu ambao matendo yao yamefanyika kuwa nuru katika historia ya ushusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Kuna mambo mengi sana ambayo twaweza kujifunza kutokana na maisha yao. Aina hii ya mahubiri ni nzuri sana, kujifunza toka kwa wacha Mungu wenzetu waliotutangulia katiki wito na huduma hii ni jambo la msingi sana. 1Kor 10.1-11. II. Chunguza maisha yake. Anza kwa kusoma hadithi inayoelezea kuzaliwa kwa mtu huyo. Tafuta maana ya jina lake. Kwani jina lina maana sana ki-Biblia. Angalia kwa umakini kusudi la Mungu katka maisha yake. Ili uweze kuvumbua vitu vingi unapaswa kujiuliza maswali yafuatayo: 1. Mungu alitaka kutekeleza nini kupitia mtu huyu ? 2. Je Mungu alifanya nini ili kusudi lake lijulikane kwa mtu huyu? 3. Mtu huyu aliitikia vipi Mungu alipomjulisha kusudi lake? 4. Tunaweza kujifunza nini kutokana na Mungu kuhusika katika maisha yake ? 5. Kuna tahadhari zozote ambazo tunapaswa kuzichukua ? 6. Je siri ya mafanikio yake ilikuwa nini ? 7. Je mwisho wa maisha yake ulikuwaje ? III. Chambua somo na kisha hubiri. Baada ya kujiuliza maswali hayo na kupata majibu utakuwa umepata vitu vingi ambavyo waweza kuvichambua kwa umakini na kuandaa somo kisha na kulihubiri somo hilo katika mpangilio na mtiririko Mzuri wa mawazo. Mwombe Roho mtakatifu akupe ufunuo zaidi unapokuwa ukihubiri somo lako na lifanye somo lako kuwa na uhalisia katika maisha ya sasa ya wasikilizaji. Zoezi 1.Eleza maana ya mahubiri ya wahusika au maisha ya watu. 2. Tengeneza orodha ya watu mashuhuri walio katika Biblia. Orodha hiyo ihusishe wanawake na wanaume. 3. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya wahusika. 4. Chagua mhusika mmoja wa kike au wa kiume na kisha andaa mahubiri kwa kumtumia mhusika huyo na kisha hubiri kwa dakika kumi. IV. MAHUBIRI YA MIFANO HALISI NA VIVULI. Huu ni ujuzi unaohusu kuweka wazi au kuchimbua na kuwasilisha ukweli uliojificha wa mifano mbalimbali katika Biblia. Mfano ni kitu, mtu au tukio ambalo kinabii ni ishara ya kitu au mtu fulani atakaetokea baadae. Inafanana au ni mfano wa Yule mtu au tukio. Katika matumizi ya Biblia ina maana ya mtu wa Bibli au tukio litakaloonesha kitu fulani kitakachotokea. Mfano mwanakondoo katika kitabu cha Kutoka ni mfano wa Bwana Yesu. Kila kitu kuhusu kondoo wa pasaka kiunabii kilikuwa na maana ya ukombozi wa wajibu ambao Bwana Yesu Kristo angetimiza.Yn 1:29. Mifano ya Biblia mara nyingi inaonekana kama kivuli(type) cha mambo yanayokuja baadae. Ebr 8:5,10:1. Siku takatifu pia katika agano la kale zilikuwa vivuli juu ya mambo ambayo yalikuwa yanakuja. Kol 2:17. Hizo siku takatifu hazikukamilika zenyewe sehemu ya kusudi la kutimizwa kwake ilikuwa ni kutanguliza sura ya kinabii ya vitu ambavyo vilikuwa bado vinakuja. Kanuni za kutumia. a. Unapojaribu kwa mara ya kwanza kufundisha kwa kutumia mifano ya kwenye Biblia, zingatia misingi ifuatayo. I. Tumia mifano rahisi zaidi. Anza na mifano rahisi ambayo maana yake iko wazi. II.Endelea na tafsiri ya wazi. Usijaribu kufasiri kila kitu.Elezea ukweli wote kama ulivyo na wala si kutafuta kila kipengele chake na kukielezea kwa undani. III. Usitumie maneno makavu. Usitumie mifano ya kufundishia kama kanuni. IV.Sisitiza ukweli wa msingi. Usitumie nafai uliyonayo kwa kutoa mifano ya kufundishia. Mifano itumike kusisitiza mafundisho na si kutumia kama chanzo cha ukweli. V. Uwe tayari kusahihishwa. Uwe tayari kusahihishwa na kukosolewa na wale waliokomaa kuliko wewe ili uweze kujifunza zaidi. 4. Kuelezea kusudi. Ni njia ambayo kwayo mhubiri hupanua maana ya ukweli ulio katika kifungu maalum cha maandiko. Unatafuta namana ya kuuweka wazi ukweli ambao umejificha ndani ya kifungu. Hii njia nzuri sana ya kufundishia kusudi lote la ki-Mungu. Mdo 20:27. Zoezi 1. Eleza maana ya vivuli na mifano.(Types). 2. Taja hatua za kufuata katika kutayarisha na kuhubiri mahubiri ya mifano na vivuli. 3. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya mifano na vivuli. 4. Tayarisha mahubiri ya mifano na vivuli na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako. V. MAHUBIRI YA MADA. Aina hii ya mahubiri hukusudia kutoa kiini maalum kwa hadhira.Mhubiri huchagua somo fulani kisha huchunguza kila kitu ambacho Biblia inasema juu ya somo hilo. Baada ya kuchunguza na kuchambua, kweli hizo huandikwa katika mapngilio wa somo. Mhubiri hupitia vifungu mbalimbali vya maandiko vinavyohusu somo hilo. Aina hii ya mahubiri huhitaji maandalizi ya muda mrefu na utulivu mwingi. Pia huwasilishwa katika mfululizo wa vipindi kadhaa na si kimoja, kwa sababu ni vigumu kupitia kweli zote zilizo katika somo kwa kipindi kimoja tu. Mfano wa mada za kuhubiri. 1. Upendo wa ki-Mungu 2. Ubatizo wa Roho mtakatifu 3. Maombi ya kufunga. 4. Nguvu ya usaidizi. 5. Vita vya kiroho. 6. Kutambua Ulimwengu wa roho. 7. Kutembea katika mamlaka. 8. Nguvu ya madhabahu. 9. Kushughulikia majira na nyakati. 10. Kutii mamlaka. Mambo ya kuzingatia katika mahubiri ya mada. 1. Uwe na ufahamu wa kutosha juu ya somo husika. 2. Fanya maandalizi ya mudamrefu na ya kina 3. Unapaswa kuwa na lengo mahususi la mahubiri yako. 4. Gawa somo katika vipengele vidogovidogo. 5. Kila kipengele lazima kiwe na maandiko yanayokithibitisha na kukielezea 6. Andiko liendane na dondoo unayoitoa. Zoezi. Somo hili lipo kimatendo zaidi. Kila mwanafunzi ashiriki katika kufanya mazoezi ya kuandaa mahubiri na ahubiri katika dakika zilizopendekezwa au mwalimu atakazopanga kulingana na muda uliopo. Mwalimu anatakiwa kusimamia na kusahihisha kazi za wanafunzi na kutoa marekebisho katika maeneo ambayo wanafunzi hawajafanya vizuri. 1.Andaa Ujumbe kwa kutumia aina ya mahubi ya mada na kisha hubiri mkutano kwa dakikika kumi. Chagua mada yoyote. 2.Taja ubora na udhaifu wa mahubiri ya mada. 3. Taja mambo mengine matano muhimu ya kuzingatia katika kuandaa mahubiri ya mada. 4. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri ya mada na mahubiri ya kufafanua. VI.MAHUBIRI YA MATUKIO. Mahubiri ya matukio ni kipengele katika mahubiri ya maada, lakini kutokana na umhuhimu wake tumekitenga na kukielezea peke yake. Mahubiri haya ni mahubiri ambayo huandaliwa kutokana na tukio lilipo au ambalo litafanyika katika kipndi fulani. Kiini cha mahubiri haya huwa ni tukio ambalo linafanyika katika ibada hiyo.Mfano wa matukio hayo ni Tukio la, 1. Kusimikwa kwa uongozi wa kanisa. 2. Ndoa au kumuaga bnti. 3. Kubariki watoto. 4. Ushirika mtakatifu 5. Ubatizo 6. Kuweka wakfu vitu mbalimbali. 7. Kuhitimu mafunzo.(graduation) 8. Msiba na mazishi. 9. Sikukuu mfano Pasaka, mwaka mpya, N.k Mambo ya kuzingatia 1. Mahubiri haya yanapaswa kuendana na tukio husika. 2. Mhubiri anatakiwa kufahamu ratiba nzima ya tukio hilo au shughuli hiyo. 3. Mhubiri ahubiri kulingana na tukio husika. 4. Mhubiri aepuke kutumia muda mwingi katika mahubiri. 5. Mhubiri ahubiri kwa lugha itakayoeleweka na kusanyiko lote na lugha yapaswa kuwa rahisi. 6. Mahubiri yapaswa kugusa kusanyiko lote. 7. Mhubiri anapaswa kuhubiri kwa upendo. 8. Mhubiri azingatie ratiba ya tukio. ZOEZI. 1. Chagua tukio mojawapo na kisha andaa mahubiri juu ya tukio hilo na hubiri kwa dakika 10 .2. Taja mabo mengine kumi ya kuzingatia katika mahubiri ya matukio. 3.Eleza ubora na udhaifu wa mahubiri ya matukio. MADA YA NNE MHUBIRI. Malengo ya mada. • Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi anataweza. • Kueleza maana ya mhubiri kwa mitazamo mbalimbali. • Kuelza wasifu wa mhubiri. • Kueleza vidokezo mbalimbali kuhusu mhubiri. A. Utangulizi. Mahubiri yana mwanzo wake katika Agano la kale. Wakati manabii walipotangaza neno la Mungu kwa watu wa kale. Manabii walikuwa wahubiri wa kwanza katika agano la kale. Mungu ameamua kuwachagua na kuwatumia watu wa kawaida kulitangaza Neno lake.Amewachagua wanawake na wanaume kuwa vyombo vya kulitangaza neno lake kupitia huduma ya kuhubiri. Ufafanuzi Neno mhubiri (kwa kigiriki kerux) limetumika mara kadhaa katika agano jipya ambapo humaanisha kutangaza. (Rumi 10:14, 1Tim 2:7, 2Tim 1:11, 2Pet 2:5. Unapolitazama neno hili (mhubiri) halijikiti na kuishia kwenye huduma moja au huduma fulani tu bali linahusisha zile huduma zote tano za uongozi wa kanisa. Ikijumuisha mitume, manabii waijilisti,wachungaji na waalimu. Pia linajumuisha kila mtu atangazae neno la Mungu. Hata kama hana mojawapo ya zile huduma tano za uongozi. Ingawa hudma zote hizi zinawasifu wake kila moja lakini zote zaangukia katika neno moja “Mhubiri”. Inavutia kutambua kwamba neno la Kigiriki lililotafsiriwa kama mhubiri linaelezea mtu anaeongea kwa mamlaka , anaewasilisha ujumbe bila kikwazo au kizuizi chochote. Hii hudhihirisha mamlaka iliyo juu ya mhubiri. Mhubiri ni mtu yeyote anayehubiri Injili. • Mhubiri ni mtu anayetumiwa na Roho mtakatifu katika kuwasilisha kweli za ki-Mungu kwa njia ya hotuba. • Mhubiri ni mtangaza ujumbe wa Mungu. • Yeye ni msemaji wa Mungu. Husimama katika nafasi ya Mungu na kuzungumza kwa niaba yake Mungu. Hivyo ni lazima mhubiri awa na sifa zinazostahili ambazo zitamfanya kuwa na mamlaka. B.Sifa za mhubiri. Mhubiri ni lazima awe na sifa stahilifu ambazo zitamfanya awe na mamlaka na thabiti katika wito na huduma yake. Badhi ya sifa hizo zimeorodheshwa hapa chini. 1. Awe ameokoka (Amezaliwa mara ya pili). 2. Awe amejazwa Roho mtakatifu. 3. Awe na wito halisi (Wito ulio wazi na wenye ushahidi). 4. Ajazwe na Neno la Kristo ndani yake Kol 3:16. 5. Awe mtu wa maombi. 6. Awe mwadilifu.( Mkweli na mchaji Mungu na mwenye kuchukia mapatato ya udhalimu ) 7. Awe na nidhamu. 8. Aishi kulingana na wito wake. 9. Asiwe mvivu. 10. Awe na baba wa kiroho. Kuna tofauti kubwa kati ya hotuba na ujumbe.mtu anaweza kujifunza jinsi ya kuandaa hotuba kupitia masomo ya Homiletics lakini Mtu anapaswa kuwa na ushirika na Mungu ili aweze C. Kujihusisha binafsi katika kuhubiri. 1. Unapaswa kuwa kawaida. Unatakiwa kutulia na kuwa vile ulivyo. Mugu hutaka kutumia utu wa kila Mhubiri katika kuwasilisha Neno lake. Unatakiwa kujikubali hivyohivyo ulivyo. Mungu anapendezwa nawe na ndiyo maana amekuita hivyo ulivyo. Usijichambue sana. 2. Kuwa wa kipekee. Unatakiwa kuutayarisha ujumbe wako na kuuwasilisha kwa njia ya kipekee ili uweze kuleta matokeo ya kipekee. Unapasa kutumia utu wako wa kipekee Mungu aliokupa na kumwacha Mungu atumie utu na maisha yako kwa njia maalum ya kipekee anayotaka yeye. 3. Kuwa rahisi. Unapokuwa ndiyo unaanza kuhubiri au kusimama mimbarini kwa mara ya kwanza unatakiwa usijaribu kutumia ufasaha au kuingia ndani mno katika kuhubiri. Huhitaji kuwavuta watu. Upo pale kwa lengo la kuwahudumia na si kuwapendeza. 4. Kuwa huru. Unatakiwa kuwa huru unapohubiri na ujifunze kujizoeza hali mbalimbali. Ufanye mtindo wako wa mawasiliano utiririke kawaida na kwa uhuru. Kila kusanyiko utakalo hubiri linatofautiana na lingine, hivyo unapaswa kujizoeza hali mbalimbali. Mungu huwa na lengo maalumu analotaka kufanikisha katika kila ibada na mhubiri ndiyo ufunguo muhimu katika kutekeleza hili. Kuwa huru na msikivu kwa Roho mtakatifu.Roho mtakatifu anaweza kufanya hali za jinsi mbalimbali katika kila ibada.Wasikilizaji wako wakati mwingine waweza kuwa wachangamfu na wakati mwingine wakimya na wanyenyekevu. 5. Tambua njia ambayo Mungu anapitia na utembee nae. 6. Dhihilisha mamlaka..Hakikisha Kuna madhihirisho ya nguvu za Mungu katika kila ibada unayohubiri. Hakikisha Bwana anakithibitisha kila unachokihubiri kwa ishara na maajabu. Hubiri kwa uthibitisho D. Zana za mhubiri. Kuna vitu kadhaa ambavyo ni muhimu kwa mhubiri yoyote . Bila vitu hivo kazi ya Kuhubiri itakuwa haijafanikiwa au kufika lengo kwani wasikilizaji watakuwa wameachwa njiani. Baadhi ya zana hizo ni: I. Maono. Kila mhubiri nilazima awe na maono katika huduma yake na wito wake. Wazo la kile ambacho huduma yako itafanikisha kwa Mungu. Maono ni picha au taswira juu ya kile unachohitaji kukifikia katika huduma yako. Kumbuka kwamba bila maono watu huangamia Mit 29:18. Ni maono pekee yatakayokuweka salama. Usipokuwa na ufahamu wa kuhusu kusudi la Mungu alilonalo kwaajili yako ,waweza kulemewa na kuishia n jiani na kushindwa kufikia lengo la –ki-Mungu ulilochaguliwa kwalo. II.Msamiati. Msmiati ni jumla ya maneno yaliyo katika lugha fulani. Msamiati wamhubiri hujumuisha maneno yote anayoyajua na kuyazoea kuyatamka. Maneno ni dhana ambayo mhubiri hutumia katika kutimiza wito wake. Muhubiri anatakiwa kuwa mahili wa lugha. Jifunze msamiati mbalimbali na matumizi yake.Silaha yetu kuu ni maneno katika kazi ya kuhubiri. Maneno huundwa na msamiati. Soma vitabu mbalimbali ili uweze kujitajirisha na msamiati. Unapokutana na neno usilolifahamu lichunguze na kutafutamaana yake na matumizi yake. Pia mhubiri anatakiwa afahamu kutumia msamiati mbalimbali katika kazi yake ya kuhubiri. Tambua matumizi ya Lugha kulingana na mahali. Jifunze misimu, Rejesta na misemo mbalimbali inayotumika katika Lugha husika. Hii itakusaidia unapohubiri uweze kuwagusa watu wote waliopo katika eneo hilo. Mhubiri ni lazima ajifunze namna ya kutamka maneno sahihi. Jifunze kutumia lafuzi vizuri na kuepuka athali za lugha mama katika Lugha unayotumia kuhubiri. Kuwa na lafuzi nzuri na kuongea lugha kwa ufasaha hukupa kukubalika kwa wasikilizaji wako na kupewa usikivu. Tumia Lugha inayoeleweka na wasililizaji wako, lakini lugha hiyo yapaswa kuwa sanifu au fasaha III. Sauti. Sauti ndiyo chombo kikuu mhubiri anachotumia katika kuhubiri. Ni lazima mhubiri kujifunza mitindo mbalimbali ya sauti na namna ya kuitumia sauti yake. Jifunze matumizi ya sauti katika mahubiri yako. Sauti yako inapaswa kusikika na wasikilizaji wako lakini haipaswi kuwa kubwa sana kiasi cha kuwaumiza. Fahamu mahali pa kutumia asuti kidogo na mahali pa kuongeza sauti. Hubiri kwa mitindo mbalimbali ya sauti. Zingatia kiimbo, toni na kidatu unapohubiri. E. Kanuni za Kuhubiri Katika kipengere hiki tutaajadili baadhi ya kanuni chache za kuzingaita katika mahubiri ya hadharani. Mhubiri anapswa kufuata na kuzingatia kanuni hizi ili aweze kufanikisha lengo la mahubiri 1. Kuvuta hewa. Kuvutahewa sahihi ni muhimu kwa mhubiri. • Vuta hewa nyingi kiasi cha kufika mapafuni. • Jizoeze kujaza hewa kifuani na kwenye mapafu. • Izuie na kisha itoe nje polepole.Dhibiti utoaji wa hewa. Iache hewa itoke chini ya mapafu kupitia sanduku la sauti na kugusa ukuta wa juu wa mdomo. • Jifunze jinsi ya kupumua ili usiishiwe pumzi wakati wa kuhubiri. 2. Utamkaji mzuri wa maneno. Jitahidi kutamka maneno vizuri na waziwazi. Hakikisha kila neno unalolitamka linasikika vizuri kwa wasikilizaji wako. Usilete kikwazo kwa wasikilizaji wako kwa kutosikika vizuri. 3. Ubadilishaji wa sauti. Hii inahusu kuifanya sauti kuwa nene au nyembamba. Sauti ya kila mwanadamu inahali mbalimbali. Jitahidi kutumia aina mbalimbali za sauti. Ukitumia aina moja ya sauti yaweza kuwachosha wasikilizaji wako. Tambua maeneo unayotakiwa kuongea kwa sauti ya chini na sauti ya juu. Endeleza viwango tofauti vya sauti yako. Ubadilishaji wa ukubwa wa sauti waweza kusisitiza kipengere fulani muhimu. Baadhi ya wahubiri huona ni muhimu sana kuhubiri kwa sauti kubwa sana kiasi chakuumiza masikio ya wasikilizaji . Jaribu kuepuka hili. Iwapo ujumbe wako wote utawasilishwa kwa sauti kubwa au ya juu itakuwa vigumu kusisitiza jambo maalum katika zile sehemu ambazo ni za maana zaidi. 4. Kasi ya kuongea. Kasi unayotumia kuongea ni muhimu sana katika mahubiri. Baadhi ya wahubiri huhubiri kwa kasi moja tu . hii si nzuri, pia yaweza kuwachosha wasikilizaji. Sehemu kubwa ya ujumbe wako yapaswa kuwasilishwa kwa mwendo na kasi ya kawaida ya mazungumzo. Katika maeneo mbalimbali ni lazima kuongeza au kupunguza mwendo ilikuleta tofauti na msisitizo zaidi katika mahubiri yako. 5. Kupumzika kidogo. Usiongee mfululizo bila kuwa na vituo. Kupumzika kidogo wakati wa kuongea au kuhubiri ni muhimu pia kwaweza kuongeza msisitizo kwenye maeneo ya muhimu. Kuongea mfululizo kwaweza kusababisha wasikilizaji washindwe kusharabu mambo ya muhimu katika akili zao. Usipitie ujumbe kwa kukimbia na kuongea kwa haraka bila kuvuta pumzi. Hadhira wanahitaji muda wa kufikiri na kuchambua kile ulichosema, Hii inasaidia sana kusharabu ukweli wa ujumbe wako. Unahitaji kuzifahamisha akili pamoja na kuzichangamsha hisia za hadhira. Kama ukihubiri kwa haraka tu bila kupumzika utawaacha hadhira wako nyuma. 6. Kurudia. Kurudia sehemu za msingi wakati unahubiri ni jambo la msingi sana. Inasaidia kusisitiza vipengere na kushindilia kwenye akili za wasikilizaji. Unatakiwa kukielezea kipengere kwa njia mbalimbali. Usisite kurudia eneo unalohisi wasikilizaji wako hawajakuelewa vizuri. F.Vidokezo muhimu kwa mhubiri. 1. Uwe vile ulivyo.Usijaribu kutokeza sura ambayo si ya kweli. Kuwa vile ulivyo ndiyo njia pekee inayoweza kukufanya utulie.usijaribu kumwiga mhubiri mwingine yeyote ukifanya hivi itakusababishia kutoaminika kwa hadhira wako.Jitahidi kuwa mhubiri bora na si kuwa mhubiri mkuu. 2. Usijenge sauti ya kidini. Baadhi ya wahubiri wamejiundia sauti za mimbarini ambazo ni tofauti na sauti zao za kawaida.Hii huleta kutokuaminika na kuonesha kana kwamba unamwiga mtu mwingine. Jizoeze kuhubiri kwa kutumia sauti ya kawaida na unayotumia katika mawasiliano katika maisha ya kila siku. Hii huonesha ukweli na uaminifu katika mahubiri. 3. Usiongee kwa sauti ndogo mno. Hakikisha kwamba kila mmoja katika mkutano wako anakusikiliza vema. Usifanye wachoke kwa sababu ya kutokukusikia vizuri. Ikibidi uliza je kila mmoja ananisikia vizuri ? Si vizuri kuendelea kuhubiri na hali kuna baadhi ya watu hawakusikilizi. 4. Usipige kelele. Jitahidi kuongea kwa sauti ya kawaida ya maongezi ambayo inaweza kuongezwa kiasi kufuatana na wingi wa makutano na kama huna au una vyombo vya kupazia sauti. Sauti iongezwa kulingana wingi wa hadhira. 5. Kumbuka kubadili kasi na upeo wa sauti ya mahubiri kukwepa kuchosha hadhira. 6. Ufanye mkutano ukukubali. Pata matumaini ya hadhira.Hakikisha mkutano wako unakukubali.. Kama mkutano wako hawakukubali nidhahiri kabisa kwamba hawataupokea ujumbe wako. 7. Vaa vizuri. Ni jambo la maana sana kwa mhubiri kuvaa mavazi ya heshima na safi. Namna ulivyo vaa yaweza kuharibu ujumbe wako.Hakikisha uvaaji wako hauvurugi ujumbe wako. Vaa kulingana na tamaduni za taifa husika. 8. Jifunze kusimama vizuri. Ni vizuri sana kusimama wakati unazungumza au kuhubiri. Simama vizuri kwa miguu yote miwili.. Simama wima ukitazamana na hadhira wako. Usipende kuegemea kitu chochote. Kama kuna mimbari itumie kuwekea Biblia na zana zako za kuhubiria. Kusimama wima kutakusadia katika kuvuta hewa. Watazame hadhira wako wakati wote unapohubiri. Hubiri kwa kumgusa kila mtu. Kila mtu ajione kwamba unaongea na yeye binafsi. 9. Jifunze kutembea wakati unahubiri. Usisimame mahali pamoja kana kwamba umefungwa.Jizoeze kutembeatembea wakati unahubiri. Mwili wako unaleta ujumbe sawaswa na sauti yako.Tumia ishara wakati unahubiri lakini epuka ishara sisizo na umuhimu. Kama unaeleza juu ya kitu fulani ni kawaida kuelezea jambo hilo kwa mikono yako. Ishara za namna hiyo zinapaswa kutokea zenyewe kiasili bila kuzilazimisha. 10. Endeleza uhuisano na hadhira. Macho ya mhubiri huelezea ujumbe pia. Usiangalie hewani au juu ya vichwa vya watu. Waangalie watu unaowahubiri moja kwa moja. Kila mmoja atambue kwamba unamwangalia yeye binafsi. 11. Jifunze kutawala mkutano. Hakikisha unatawala kusanyiko. Watu wote wako pale kukusikiliza wewe hakikisha kila mmoja anakusikia. Zungukia watu wako nakuwashitua wanao lala au kusinzia. Tafuta namna itakayosababisha watu wote kukusiliza kwa makini. 12. Omba upako wa Roho mtakatifu. Mwombe Mungu akupake mafuta daima. Hakikisha utendaji wa Roho mtakatifu upo katika mahubiri yako. F. Matumizi ya muda katika mahubiri. Ni lazima mhubiri ajifunze matumizi sahihi ya muda katika mahubiri. Jambo hili ni la muhimu sana na lisipozingatiwa huweza kuvuruga kazi nzima ya kuhubiri. Ni lazima kuamua muda utako tumia kuhubiri kabla ya kupanda mimbarini. Utafiti kule Marekani umeonesha kwamba watu huanza kupoteza usikivu wao baada ya dakika ishirini tu za mahubiri. Waweza usikubaliane na matokeo ya utafiti huo lakini unatakiwa kukumbuka kwamba akili ya mwanadamu inakiwango cha kuelwa na muda wa kuelewa. Muda ukizidi kila kinachoongelewa au kuhubiriwa huwa hakisharabiwi kwani akili hufikia upeo wa kuelewa na kushika mambo. Upako wa Roho Mtakatifu huhuisha akili za wasikilizaji kwa kiwango fulani lakini mhubiri aepuke kuwachosha wasikilizaji. Ni vizuri sana kumaliza ujumbe wako wakati watu wanatamani uendelee na ni vibaya sana kumaliza ujumbe wako wakati watu wanataka umalize. Jitahidi kuzingatia muda katika kazi yako ya kuhubiri. Kwa kawaida ujumbe unapaswa kutumia dakika arobaini na tano. Utangulizi uwe na dakika tatu hadi tano, Kiini kiwe na dakika ishirini na tanno hadi therathini. Hitimisho liwe na kakika tatu hadi tano. Ujumbe wote usizidi dakika arobaini Vinginevyo utawaacha wasikilizaji wako. Ukitaka kuhubiri kwa muda mrefu hakikisha ujumbe wako unauvuvio mwingi. Spurgeon alisema” tumia muda mwingi katika matayarisho ili uweze kutumia muda mchache katika kuhubiri” Kutumia muda mrefu katika kuhubiri hakukufanyi ueleweke zaidi wala hakufanikishi zaidi lengo la kuhubiri. Tambua cha kusema. Kiseme na kisha maliza. Unapokuwa umealikwa na mhubiri mwingine kuhubiri unapaswa kumuuliza muda ambao yeye hutumia katika kuhubiri na muda wa kumaliza mahubiri. Unapokuwa unahubiri zingati muda ulioelekezwa na mwenyeji wako na uwezo wa kuelewa wa wasikilizaji wako. Mgeni akija kanisani kwako kama hukumwandaa kuhubiri kabla si vizuri kumpa madhabahu ili ahubiri. Kwani kuhubiri ni kazi nyeti sana na inahitaji maandalizi ya kutosha. Maelezo haya hayazuii mwongozo na maelekezo ya Roho mtakatifu. Lakini ni vizuri kumwandaa mhubiri mapema ili awe na muda wa kuafanya maandalizi. Usiwashitukize watu kuhubiri. Ni lazima uwe na heshima kwa kazi hii kwani Mungu mwenyewe anaiheshimu sana. Usihubiri ujmube au somo ambalo mwenyeji wako hakubaliani nalo. Kama kuna ulazima fanya nae mazungumzo kabla ya kuhubiri au tafuta namna utakayotumia kuhubiri na kufanya akubaliane na kile unachohubiri. Jambo hili ni muhimu sana na linapaswa kuzingatiwa. Mahubiri na mazingira. Mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyopatikana na kuzunguka eneo fulani. Mazingira ni muhimu sana katika kufanikisha kazi ya kuhubiri. Ni lazima mazingira yawe safi hasa ikiwa mahubri yatafanywa katika eneo fulani maalum. Mfano kanisani, uanjani au eneo lolote rasmi. Kuna baadhi ya mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa. Baadhi ya mambo hayo yameorodheshwa hapa chini. 1. Watu wanaokuja kwa kuchelewa wakae katika viti vya nyuma. 2. Mimbari inapaswa kuwekwa mahali sahihi panapoonekana na watu wote bila shida. 3. Lango la kuingilia lapaswa kuwa mahali sahihi. 4. Akina mamawenye watoto wadogo wakae eno maalumu. 5. Watoto wanapaswakutengewa sehemu yao ya kukaa kama hakuna kanisa la watoto. 6. Mwanga na hewa ya kutosha ni kitu muhimu sana katka eneo lolote. G. Jaribu kuu la Mhubiri. Wahubiri wengi hujisulisha na kutafuta chakula kwajili ya watu wengine na kujisahau wenyewe. Huu ni mtego mkubwa katika kazi ya kuhubiri na ni moja ya hatari za huduma. Wakati mwingine mhubiri aweza kujishughulisha sana na kutafuta haki za kiroho za kundi lake na kwa masikitiko makubwa anasahau zile za kwake mwenyewe. Hii ni moja ya sababu kuu zinazomfanya mhubiri kushindwa. Sulemani anasema katika kitabu cha Wimbo ulio bora “”’ Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu bali shamba langu mwenyewe sikulilinda” Mhubiri ni lazima ajali kwanzai maisha yake mwenyewe ya kiroho. Mhubiri anapaswa kulipa neno la Mungu nafasi ya kuchipua ndani ya moyo na roho yake. Aliache likue kwa nguvu katika maisha na ujuzi wake. Halafu atakapohubiri atahudumu kutokana na ujuzi. Hataongea kamwe kama mwenye nadharia bali atashirikisha vitu ambavyo yeye mwenyewe anavielewa kikamilifu na ana ujuzi navyo. Paulo anasema hivi. “Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza kupata fungu la matunda”. ( 2Tim 2:6 ). Hii inatufundisha kwamba unachopanda na kuvuna ( kiroho) yapasa ule (ujuzi)- kabla ya kulisha wengine. Huwezi kulisha wengine kile ambacho wewe mweyewe hujakila kwanza. Huwezi kujaribu kuongoza wengine katika njia na mapito ambayo wewe mwenyewe hujapitia. Jinsi Neno la Mungu linavyokuwa dhahiri katika maneno yako ndivyo wewe unafanyika ujumbe toka kwa Mungu. Hutakuwa mtu anaye kariri somo tu bali mtu ambaye uhai wake binafsi na mtindo wake wa maisha huhudumia uhai, Baraka na nguvu kwa wale wanaomfahamu na kumsikia. I.Hitimisho. Mahubiri mazuri hayaji kirahisi wala hayatokei tu. Ni matokeo ya vitu vingi. Kama tulivyotazama huko nyuma kwamba mahubiri huanza na wito wa mhubiri na wasifu wake.Pia huhusisha maandalizi ya kutosha kwa kuomba na kusoma kwa bidii. Kilele cha mahubiri ni katika kuwasilisha ujumbe. Ujumbe hauwi ujumbe mpaka umewasilishwa. Ujumbe ulioandaliwa vema utakuwa ujumbe wa kiungu pale Roho mtakatifu atakpoupaka mafuta. Mahubi mazuri daima yataleta matokeo mazuri. Mahubiri mazuri dama yatamtukuza Mungu na si mhubiri au mtu mwingine yeyote. Yatawaongozawatu msalabani na kuwafanya kuwa wanafunzi. Angalizo.Mhubiri hapaswi kutwaa utukufu kwa namna yoyote ile katika kila inachotokea katika kazi yake ya kuhubiri. Daima anapaswa kumpa Mungu heshima na utukufu kwa kila kinachotokea. HOMILETICS. MADA YA KWANZA. MAHUBIRI. Malengo ya mada. Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi aweze.  Kueleza maana yamahubiri.  Kueleza maana ya kuhubiri.  Kueleza wito wa kuhubiri ulivyo.  Kueleza umuhimu wa kujifunza homiletics. A. UTANGULIZI Katika kozi hii tutashughulikia mojawapo ya kazi kuu ya kanisa. Mojawapo ya wajibu mkuu ambao umewekwa mikononi mwa kanisa ni kuhubiri ujumbe wa Mungu yaani Injili. 1Kor 1:21 a) Ni amri iliyo wazi toka kwa Bwana Yesu kwa wafuasi wake. Mk 16:15. “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe”. b) Kuhubiri ni mojawapo ya kazi ya thamani sana ambayo Mungu ametupa. Kuwa msemaji wa Mungu, yaani Mjumbe wa Kristo. 2Kor 5:20. c) Kuhubiri ni wajibu mkuu. Rumi 10:14-15. d) K wa njia ya mahubiri Mungu alichagua kujidhihirisha mwenyewe kwa mwanadamu. B. MAANA YA MAHUBIRI. Neno mahubiri linatokana na maneno mawili ya kigiriki ambayo ni homileo na homilia yenye maana ya ‘kuwa pamoja na, kuongea na kuwasiliana. a) Homily pia humaanisha ujumbe au hotuba. b) Elimu inayohusu namna ya kuhubiri huitwa Homileticts. c) Homiletics ni ustadi wa kuhutubia au kuhubiri. d) Mtaalamu wa elimu ya kuhubiri huitwa Homilist e) Homiletics huhusisha kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri au kutunga hotuba. f) Mahubiri huhusu kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri masomo ya Biblia. g) Mahubiri ni ujuzi wa kuhubiri. h) Ni elimu au taaluma inayohusu kuhubiri Neno la Mungu. i) Ni elimu inayohusu namna ya kuhubiri.{ somo juu ya kila kitu kinachohusiana na kuhubiri}. j) Kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu. Mungu hutumia watu wake aliowachagua kuhubiri ujumbe wake. k) Ujumbe unapaswa kuwa ujumbe wa Mungu Kitu kingine chochote si mahubiri ila ni maoni na falsafa za kibinadamu tu. l) Kuhubiri ni lazima kuwe ni kutangaza binafsi na si kusoma au kuandika Dr. Martyn Lolyoyd Jones alisema “ Wahubiri huzaliwa na hawafanywi kamwe. Kamwe hutamfundisha mtu kuwa mhubiri kama yeye si muhubiri. Lakini mhubiri wa kuzaliwa unaweza kumsaidia na kumwendeleza akawa mhubiri bora kwa njia ya mafunzo” 1. -Mhubiri si chanzo cha ujumbe.Mungu ndiye chanzo cha ujumbe na mhubiri ni bomba au mfereji ambako Mungu hupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu aliowakusudia. Ujumbe wa Mugu hutiririka kupitia utu wa mhubiri. 2. -Ujumbe unapaswa kutiririka kwa uhuru toka kwenye chanzo chake (Mungu) kwenda kwa wakusudiwa yaani hadhira au wasikilizaji. 3. Mahubiri ni zao la mambo mawili ambayo ni Mungu na mhubiri. Mahubiri mazuri huzaliwa kutokana na ushirikiano mzuri (umoja) na ushirika mzuri kati ya Mungu na mhubiri. Hivyo kuna vipengele viwili vya wazi katika mahubiri cha kwanza ni kile cha ki Mungu na cha pili ni kile cha kibinadamu. Kwa sababu ya wito wake mkuu mhubiri anapaswa kuwa mwaminifu na awe na ufahamu wa kutosha juu ya Neno la Mungu. 4. Biblia ndiyo asili ya ujumbe. • Ujumbe wowote unaohubiri nilazima utokane na Biblia nje ya Biblia si mahubiri bali ni masimulizi tu. • Kwa nini Biblia peke yake? Kwanini si kitu kingine toka vitabu vizuri vya kikristoau toka magazeti au maelezo na masimulizi ya mtu maarufu na aliye mkuu. • Biblia ni maoni ya Mungu kwa kila jambo lolote lililotolewa. Mhubiri aliye kuwa amekosolewa kwaajili ya hotuba yake alisema “hata mimi sikuipenda pia lakini haikuwa maneno yangu na nilikuwa sitoi mawazo yangu bali kile Mungu amesema katika Neno lake. Kwahiyo nilitoa mawazo ya Mungu na si yangu. • Kuhubiri hotuba ya ki-Biblia humpa mhubiri ujasiri mkubwa. Kutangaza kwa nguvu; Biblia inasema …………………. Mungu anasema………………… • Neno la Mungu lina nguvu. Wab 4:12. • Neno la Mungu ni kama mbegu.sBiblia hukutana na kila hitajila mwanadamuna matatizo yake yote yanayomkabili. • Inampendeza Mungu- Neno lake lililovuviwa amri yake ilikuwa wazi • “Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi na muwafundishe kuyashika yote niliyowaamuru” • Roho mtakatifu hulithibitisha Neno la Mungu. C. MAANA YA KUHUBIRI. Mahubiri yana lengo mahususi katika mpango wa Mungu. Ni njia ambayo kwayo Mungu ameamua kuwafikia waliopotea dhambini na kuwaimarisha waamini.Kkwa sababu mahubiri ni njia ya Mungu kuwafikia wanadamu, tutatazama maana ya kuhubiri kwa mitazamo mbalimbali kama ilivyo ainishwa na wataalamu wa masomo ya homiletics. 1.Kuhubiri ni kuielezea imani. Mojawapo ya malengo ya mahubiri ni kuelezea au kutangaza kweli za maandiko matakatifu. Kila hotuba au ujumbe wapaswa kuwasilisha kweli za maandiko kwa njia itakayowezesha hadhira kupata uelewa zaidi juu ya maandiko matakatifu. Kuhubiri husababisha imani kuumbika kwa wasikilizaji wako. Hubiri kwa kukuza imani na kuielezea imani katika mwana wa Mungu Yesu Kristo. II. Kuhubiri ni kuitetea imani. Haitoshi kuelezea ukweli wa Mungu bali tunapaswa kuutetea. Shetani, ulimwengu na maadui wa imani huvamia na kupotosha kweli za neno la Mungu. Hivyo ni lazima kwa mhubiri yoyote kuwa tayari kuitete imani ya kweli kwa njia ya kuhubiri kweli za ki-Biblia. Kuna wahubiri wengi wa uongo ambao kazi yao ni kuposha kweli za maandiko matakatifi. Ni jukumu la kila mhubiri wa kweli kuhakikisha anasimama imara katika kuitetea imani ya kweli. III.Kuhubiri ni kuinjilisha. Wajibu mkubwa wa Mhubiri ni kuitangaza injili kwa watu waliopotea dhambini. Ni lazima watu wote waliopotea wapelekewe injili ili wapte kutambua hali yao ya kupotea na kuongozwa kwenye wokovu wa Yesu Kristo.Kila mhubiri ahakikishe anatimiza Agizo kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Ahakikishe anawafikia watu wote wasiofikiwa na injili na kuwaleta kwa Bwana Yesu. IV. Kuhubiri ni kukemea dhambi. Kama ukichunguza hotuba za agano jipya utagundua kwamba hakuna mhubiri hata mmoja aliyesita kukemea dhambi.mfano Yesu, Yohana, Paulo, Petro n.k wote walikemea dhambi kwa nguvu zo katika kila mahubiri. Mhubiri nilazima akemee dhambi kila mara kwani Mhubiri ni kinywa cha Mungu. Kemea dhambi bila kuogopa chochote .Mhubiri ni lazima afunue ubaya wa dhambi na kuwahamasisha waamini kuishi maisha matakatifu yenye kumpendeza Bwana Yesu na kujiepusha na uovu. V. Kuhubiri ni kuhamasisha waamini Mahubiri hutakiwa kuwasaidia wakristo kukua katika neema ya Mungu. Pamoja na kuonya na kukemea dhambi mahubiri hutakiwa kuwahamasisha na kuwawezesha waaamini kukua kiroho na kufikia kimo cha Kristo. Hili ni moja wapo wa lengo kuu la mhubiri. Hatuhubiri ili kupisha muda au kwa sababu ya mazoea bali kwa sababu Mungu anakitu anataka tukipeleke kwa watu wake. Lengo la mahubiri ni kuwabadilisha waamini kuwakuza na kuwawezesha kufikia kimo cha Kristo Yesu., Tunapohubiri tunaumba sura ya Kristo ndani ya wale tunaowahubiri. Hakikisha wale unaowahubiri wanakua kiroho na kufanana na kristo VI. Kuhubiri ni kufikia mahitaji ya hadhira. Mahubiri yatakuwa yameafanikiwa kama yatakuwa yamepokelewa na kukutana na mahitaji ya wasikilizaji. Mhubiri kwa uangalifu anatakiwa kujiweka katika daraja sawa na wasikilizaji. Anatakiwa kujitahidi kuhakikisha anapokelewa na makutano na kukutana na mahitaji yao. Mhubiri anapaswa kuhubiri kwa mguso. Hakikisha unagusa mahitaji ya watu unapohubiri. Mahubiri ni uhai hivyo ni lazima yalete majawabu kwa wale tunaowahubiri. Gusa mahitaji halisi ya watu ambayo Mungu anakusukuma kuyashughulikia. Hubiri kwa ufanisi na kwa mguso. VII.Kuhubiri ni kudhihirisha uweza wa Mungu. • Bwana Yesu aliahidi kuwa na wahubiri kwa kulithibitisha neno kwa ishara na maajabu. Popote injili inapohubiriwa ni sharti Bwana awepo akiithibitisha kwa isharaMk 16:15,20. 1Kor 2:4. Hakikisha nguvu ya Mungu iko juu yako unapohubiri. Unapaswa kupakwa mafuta kikamilifu a Roho mtakatifu unapokwenda kwenye huduma ya kuhubiri kwa sababu kuhubiri ni vita. Omba Mungu Roho mtakatifu afanye uthibitisho kwa kila utakachohubiri. Ishara na maajabu ziambatane nawe kokote unakohubiri. -Ikiwa kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu mhubiri anapaswa kwenda mahali Mungu alipoongea mara nyingi na waziwazi yaani “Biblia” • Kwa njia nyingine kuhubiri ni kuipa Biblia sauti.ni kuacha Mungu aongee mwenye toka kwa Neno l D. WITO WA KUHUBIRI Sehemu ya muhimu sana katika kuhubiri ni wito. Kimsingi wito ni wa mtu binafsi Mungu huwaita watu katika huduma na watu hupokea hilo rohoni mwao kisha huja uthibitisho wa nje kupitia kanisa au watumishi mbalimbali na fursa mbalimbali. Mungu Huwaita watu wake katika nafasi na huduma mbalimbali. Wengine kuwa wachungaji, wamishenari, wazee wa kanisani, wainjilisti, au huduma nyinginezo. Kazi ya kuhubiri si ajira ambayo mtu anakwenda chuoni kusoma kwa lengo la kupata baada ya kuhitimu masomo yake, bali ni mwito mtakatifu ambao mtu huitwa na Mungu mwenyewe kuwa muhubiri. Mtu huenda chuoni ili kupata maarifa yatakayomwezesha na kumsaidia katika kutimiza mwito wa Mungu uliondani yake. Haendi chuoni kupata mwito bali wito husababisha mtu kwenda chuoni kama sehemu ya maandalio. Hivyo wito usichanganywe na ajira na maslahi binafsi ya mtu. Ni lazima wito uheshimiwe na kuogopwa. Waamini hawapaswi kujihusisha na huduma kwa lengo la kujinufaisha na kujipatia mali kwa njia za ujanja ujanja. Kimsingi kila mwamini ni muhubiri kwani agizo kuu linamhusu kila mwamini. Kila mwamini anapaswa kujihusisha na kupeleka injili kwa watu waliopotea dhambini hili ni agazo la jumla. Lakini kuna watu maalumu ambao Bwana ameweka wito wa muda wote(Full time commitement) ndani yao. Amewachagua kwa kusudi hili katika maisha yao na muda wao wote. Hawa wanasimama katika zile huduma tano za uongozi katika kanisa, ambao ni mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu. Hawa ndio Bwana amewaweka kusimama katika kazi ya kuhubiri ya muda wote, Wao hawapaswi kujihusisha na shughuli zingine bali kazi yao ni kulihudumia Neno na kuomba yaani Kuhubiri. Bwana ameweka mwito mtakatifu ndani yao ambao ni wajibu mkuu na wa kuogofyapia{.Mdo6:2,4} hili ni agizo mahususi. Wito huu haupatikani kwa njia ya kusoma au kwa njia ya ulaghai bali kwa kuitwa na Mungu mwenyewe kuwa msemaji wake. Kuna baadhi ya makanisa ambayo yameufanya wito wa Mungu kuwa ni ajira. Kwani wao huwapeleka watu kwenda chuoni kusomea huduma fulani mfano uinjilisti, uchungaji nakadharika kwao wito si jambo la msingi kwao ila elimu ndiyo yenye kupewa kipaumbele. Wao humpa mtu kushika nafasi ya huduma baada ya kuhitimu mafunzo ya chuo cha Biblia bila kujali kama ana wito au la. Matokeo yake ni kwamba makanisa yamekuwa yakiongozwa na kuhudumiwa na watu wasio na wito wenye kutegemea elimu ya darasani tu, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo na uhai wa kanisa. Elimu ni jambo la zuri sana lakini elimu haiwezi kuchukua nafasi ya wito katika kanisa la Mungu ikiwa tunataka kufikia kusudi la Mungu la mwito mtakatifu na kusimama kiuaminifu mbele zake kupata ushindi mkuu. Usiwe mtumwa wa elimu. Elimu hii unayopata ikusaidie katika kumtumikia Mungu na kufanya huduma lakini isichukue nafasi ya Roho mtakatifu katika maisha yako na huduma yako. Wala haipaswi kuwa badala ya Roho mtakatifu. E. MAANDALIO KWAJILI YA HUDUMA. Ni muhimu mara mtu atambuapo kwamba Mungu anamwita katika huduma kufanya mambo kadhaa. Mojawapo ni kuanza kumngojea Bwana kwa njia ya maombi, Kujihusisha na huduma mbalimbali zinazojitokeza kanisani au sehemu nyingine yeyote . Pia ni muhimu kwenda shule kwajili ya mafunzo zaidi ya maandalio ya huduma. Kuwa na mlezi. Ni lazima kuwa na mlezi wa huduma ambae atakusaidia katika kutimiza mwito ulio ndani yako. Mlezi wa kwanza wa huduma na wito wako ni mchungaji wako. Mweleze mchungaji kuhusu wito ulio ndani yako na mwombe akusaidie katika kuulea wito huo. Kuwa mtii na mnyenyekevu kwa mcungaji wako. Shirikiana na watu wenye wito kama wako ili uweze kujifunza zaidi. Fanya kazi na huduma mbalimbali unazopewa na mchungaji au viongozi wa kanisa. Jifunze kwa watu wenye wito kama wako walifanikiwa katika utumishi wao. Kupata mafunzo zaidi. Ni vizuri mara unapogudua kwamba Mungu amekuita katika utumishi au mojawapo ya zile huduma tano kwenda chuo cha Biblia kwaajili ya mafunzo na matayarisho kwaajili ya huduma Mungu anayokuitia. Namna ya kuchagua Chuo cha Biblia 1. Omba Uongozi wa Mungu juu ya jambo hili. 2. Angalia chuo kitakachokidhi mahitaji yako ya kuandaliwa. 3. Angalia maswala ya usajili wa chuo.(Vyuo vingi vya Biblia havina usajili wa serikali kwani haviko kitaaluma zaidi bali kihuduma). 4. Chunguza misingi ya imani ya chuo. 5. Tathmini uwezekano wa kuingizwa katika huduma baada ya mafunzo. 1. Mambo ya kuzingatia unapokuwa katika Chuo cha Biblia. 2. Jikite katika masomo kabisa kwa miguu yako yote miwili. 3. Jihusishe kikamilifu na ratiba nzima ya Chuo. 4. Tia bidii katika masomo. 5. Tumia muda kuwa na waalimu na wanafunzi wenzako na jifunze vitu vyema toka kwao. 6. Epuka kuwa mjuaji (arogant). 7. Kuwa mtumishi. 8. Jitahidi kuonekana na si kusikika. 9. Shirikisha baadhi ya watu maono na wito ulio ndani yako. 10. Baki kuwa mwanafunzi daima hata baada ya kuhutimu mafunzo. 11. Kwa mtii kwa amri, shria, kanuni na taratibu za Chuo. • Usiongozwe na elimu bali ongozwa na Roho mtkatifu. • Usihubiri kwa maneno yenye hekima pekee kwa lengo la kushawishi akili za watu bali hubiri Kwa dalili za Roho mtakatifu na nguvu. 1Kor 2:4. • Hakikisha unautumikia wito ambao Mungu ameweka ndani yako kwa gharama yoyte ile bila kujali mazingira au kitu kingine chochote. • Kwa hiyo wito wa kuhubiri hautoki kwa mwanadamu yoyote Yule bali toka kwa Mungu mwenyewe. Mungu huwafanya watu wake kuwa wahubiri. • Jiulize wewe ni mhubiri wa kufanywa na nani ? F. Kweli kuu kuhusu wito wa kuwa mhubiri. 1. Roho mtakatifu huweka wito ndani ya mtu. Wito wa Mungu huja juu ya mtu kupitia Roho mtakatifu. Katika akili ya kawida ni kazi kubwa kuhubiri au kutumika. Wito huja kwa watu wa aina zote na umri wote wowote. Baahi ya watu husikia wito na kujitoa wangali wadogo lakini wengine katika umri mkubwa n.k 2. Shauku ya kutimiza wito. Watu wanaoitwa kuwa wahubiri waliumbwa na Mungu kwa kusudi hiloYer1:4-10 Hawawezi kupata utoshelevu kwa kufanya kitu kingine chochote. Hawawezi kupinga kujihusisha katika huduma au kuchukua fursa za kuhubiri. Hata kama hakuna nafasi za kutumika moja kwa moja bado watatafuta nafasi katika huduma yoyote inayojitokeza. 3. Mungu huwaandaa wale anaowaita kwajili ya huduma. Mungu hawaiti watu ambao hwana uwezo wa kutimiza mwito wake. Wahubiri wengi wanakipaji cha kuongea. Watu wenye wito juu ya watoto Mungu huwaandaa kwa kuwapa uwezo kwa kufanya huduma na watoto n na wanaoitwa kuwa wacghungaji huwezeshwa kuwa wachungaji. Kwa namna yoyte Mungu huwaandaa na kutoa nguvu ya uwezesho juuv yao. 4. Wito wa Mungu wapaswakuwa wazi. Wito wa Mungu usifichwe. Wito wa Mungu ulioju yako wapaswa kuwa wazi kwa watu wangine lakini haupaswi kukimbilia kwenye wito huo mara moja. Hutakuwa na furaha na mafanikio na wito huo mpaka utakopokuwa umejisalimisha kwa mapenzi sahihi ya Mungu juu yako.Wito ambao Mungu amekuita kuutimiza unapaswa kuuweka wazi. Shirikisha watu ambo watafanyika msaada katiki kuulea wito wako. Fanya kazi na watu. Tumika na watu wenye wito kama wako. Kaa chini ya mtu mwenye neema kama ya wito ulionao ili uweze kujifunza zaidi. 5. Wito wa Mungu ni wito wa matayarisho. Kuna wajibu mwingi na mkubwa ambao huja pamoja na wito wa kuhubiri. Mungu akisha mwita mtu humuandaa kwanza kabla ya kumtuma na kumwachilia kwnye huduma aliyomuitia. Mhubiri anapaswa kujiimalisha kiroho na kimwenendo.Anatakiwa ajiandae kiakili kwa kusoma na kupata mafunzo. Pia anapaswa kujiandaa kimatendo kwa kunoa vipawa vilivyo ndani yake na kuyatisha maisha yake yote kulingana na wito ulio ndani ya yake. Mungu akisha weka wito wake ndani ya mtu huanza kumwandaa kwajili ya wito huo. Humpitisha katika majaribu mbalimbali yanayoendana na wito wake, humpeleka kwenye shule yake ijulikanayo kama shule ya moto na baada ya kufuzu huko Mungu humwachilia mtu katika huduma. Musa aliandaliwa kwa zaidi ya miaka arobaini, Yusufu kwa muda wa zaidi ya miaka kumi, Paulo kwa muda wa miaka kadhaa.Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba Mungu huwa hana haraka. Ukipata wito wa Mungu ndani yako usifanye haraka kuutimiza Bwana anatenda kwa wakati. Unapaswa kusubiri wakati wa Bwana na ufanye kwa wakati wake na si nje ya wakati wa Mungu. G. Mawazo mawili potofu kuhusu mahubiri. Kuna dhana mbili potofu ambazo zinajitokeza katika uwanja na taaluma ya mahubiri mawazo hayo ni: a. Maaandalizi si lazima. Wazo la kwanzalenye makosa ni kwamba maandalizi si lazima na huonesha kukosa imani kwa mhubiri. Watu wenye kushikilia msimamo huu hufikili kwamba imani ya kweli hutupilia mbali jitihada yoyote inayojaribu kuandaa akili na hiyvo husimama mimbarini wakiamini kwamba Mungu atawapa maneno ya kusema.husimamia maawazo haya: i. Roho mtakatifu atakupa unachohitaji kuhubiri. Unapopanda mimbarini. _- Zab 81:10 “ Fumbua sana kinywa chako name nitakijaza”(Hutumia andiko hili kutetea msimamo wao.). Pia husema kwamba Yesu alisema kwamba “Msifikirifikiri nini cha kusema maana mtapewa kinywa cha usemi saa ili ilie mnapotakiwa kusema” Unapoyachunguza kwa umakini maandiko hayo utagundua kwamba maandiko hayo wanayafasili nje na mkutadha wake na na kulazimioshwa yaseme kile ambacho hayamaanishi. *Mahubiri ni kamana jengola kiroho ambalo linatakiwa kusanifiwa na kuandaliwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Roho mtakatifu ndiye mhandisi mkuu wa mahubiri. b. Uwezo wa mtu unatosha. Kuweka mkazo katika matayarisho na kutegemea uwezo wa kibidanu tu. Wahubri wanaoshikilia msimamo huu hudai kwamba maandalizi peke yake yanatosha na huweka mkazo kwenye matayarisho pekee.Kumtegemea Roho mtakatifu huwa ni kudogo sana au hakuna kabisa, bali tumaini la mtu binafsi ambalo ni matokeo ya kujifunza na kuendeleza uwezo wa asili. Ujumbe wa namna hii waweza kuwa mzuri kabisa lakini hauwezi kuleta matokeo yatakikanayo daima. Kwani ni Roho mtakatifu pekee ndiye anaeweza kuleta badiliko katika maisha ya waikilizaji wako. Bila yeye mahubiri huwa ni maiti na haiwezi kuleta uhai kwa sababu ni uhai wenye uwezo wa kuzaa uhai. *Roho mtakatifu huuhuishaujumbe na kuletaq matokeo yaliyokusudiwa na Mbingu katika maisha ya wasikilizaji. Ili mhubiri aweze kuhubiri sawasawa anapaswa kuwa na maansdalizi ya kutosha katika kuuandaa ujumbe wake kwa kusoma, kutafakari na kuchambua kweli zote zilizomo katika ujumbe wake. Lakini hayo yotec anapaswa kuyafanya akiwa katika hali ya maombi. Mhubiri anapaswa kumsikiliza Roho mtakatifu klwa kina na kupata uongozi kwake na kutaka Roho mtakatifu amshirikishe kile anachotaka kusema na watu wake na kukifanyia uchambuziyakinifu katika hali ya maombi ili aweze kukiwasilisha kwa ufanisi. • Mhubiri anapaswa kutambua kwamba yeye hana watu wala si Chanzo cha ujumbe. Kwasababu hiyo anatakiwa kumsikiliza mwenye watu na aliye chanzo cha huo ujumbe na kusimama katikati kwa uaminifu kuwafikishia watu kwa usahihi kile mwenye watu anachotaka kiwafikie watu wake. • Mhuibiri anapaswa kutambua kwamba kazi ya kuhubiri ni takatifusana na ni kazi nyeti ambayo yapaswa kufanywa kwa umakini, uaminifu na unyeyekevu mkuu. • Mhubiri mwenye kutegemea juhudi zake na uwezo wake wa asili atakuwa ni muhubiri kilema na halikadharika mhibiri mweye kutegemea kupewa ujumbe akiwa mimbarini atakuwa ni kilema. • Vyote viwili vyapaswa kwenda pamoja, maombi na matayarisho.Kwa sababu mahubiri ni matokeo ya mawasiliano na ushirika mzuri kati ya Roho mtakatifu na mhubiri. H. Umhuhimu wa kujifunza homiletics. a) Linatusaidia kujua mbinu mbalimbali za kuhubiri. b) Linatusaidia jinsi ya kuhubiri bila kuwachosha watu. c) Linatufanya kuwa na ujasiri tunapohubiri. d) Linatusaidia kuhubiri kwa usahhi. e) Linatusaidia kutambua mahubiri ya uongo. f) Linatusaidia kujua na kuheshimu wito tulio nao. g) Linatusaidia kujua kusudi la Mungu la mahubiri. h) Linatusaidia katika kuheshimu wito wa watu wengine. Zoezi. Jibu maswali fafuatayo. Wanafunzi waweza kujibu katika makundi au mmoja mmoja kama kazi ya nyumbani kwa kadri mwalimu atakavyoona inafaa. 1. eleza maana ya mahubiri kwa mitazamo mbalimbali. 2. Eleza vile mahubiri yasivyo. 3. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri na kuhubiri. 4. Taja faida tano za kujifunza somo la kuandaa mahubiri. 5. Tathmini misukumo mbalimbali inayosababisha watu waingie katika huduma tano za uongozi wa kanisa. na hali hawana wito. 6. Eleza namna gani mtu aweza kujua kwamba Mungu anamwita kuingia katika huduma. 7. Eleza umuhimu wa kipindi cha maandalizi na matayarisho kabla ya mtu kuingia katika huduma ambayo Mungu anamwita kuifanya. MADA YA PILI: MBINU ZA UTAYARISHAJI WA MAHUBIRI Utangulizi Katika mada hii tutajadili aina mbalimbali za utayarishaji wa mahubiri, maeno ya mahubiri na sehumu za mahubiri au hotuba. Tutapitia kwa undani kila kimojawapo ya vipengele hivi ili kujifunza jinsi vipengele hivyo vinavyohusiana na mahubiri na tunavyoweza kuvitumia katika huduma ya kuhubiri na kuandaa mahubiri. Malengo ya mada. Baada ya kumaliza kujifunza mada hii mwanafunzi ataweza. • Kutaja na kueleza mbinu mbalimbali zinazotumika katika utayarishaji wa mahubiri au hotuba. • Kutathmini kila mbinu kwa kueleza ubora na udhaifu wake. • Kuandaa jumbe za mahubiri kwa kutumia mbinu mbalimbali. • Kutambua maeneo muhimu katika mahubiri. • Kutambua sehemu muhimu katika jumbe na hotuba. • Kutayarisha jumbe na hotuba za ki-Biblia kwa kuzingatia sehemu muhumi katika • jumbe na hotuba. A. Mbinu za Utayarishaji wa jumbe na hotuba. Kuna aina nyingi za utayarishaji wa somo au hotuba, na kila mojawapo ina umuhimu wake. Lakini katika mada hii tutajifunza aina tatu za utayarishaji wa somo au hotuba. Kila mwanafunzi anatakiwa kuelewa aina zote tatu na anapaswa kujizoeza kutumia njia hizi zote ili aweze kufaidika zaidi. Mbinu hizi za utayarishaji wa somo pia zaweza kutumika kama mbinu za kuhubri. Kwa hiyo tutakapokuwa tunajadili zitaangaliwa katika maeneo haya mawili. ( Kama mbinu za utayarishaji na kuhubiri.) 1. Somo Lililoandikwa. Katika aina hii mhubiri hupaswa kuandika kila kitu anachokusudia kukihubiri. Wakati mwingine somo lote huandikwa. Kila eneo la somo huchambuliwa kwa undani na kuwekwa katika maandishi. Ujumbe au somo lote huandikwa kikamilifu kabla ya kuhubiri. Mhubiri huelezea kwa undani somo lake anapohubiri likiwa katika maandishi. Mhubiri anapohubiri mara nyingi hupitia kila kitu alichokiweka katika maandishi. Faida za aina mbinu hii. a) Ujumbe wote huandaliwa kwa uangalifu mkubwa. b) Ujumbe huwasilishwa kwa umakini na uhalisia. c) Ujumbe huwa ni wa kitaalam. d) Mhubiri hujikita katika somo. Hasara ya mbinu hii. a) Somo huwa haliwavutii wasikilizaji. b) Utoaji wa ujumbe wa namna hii unaweza kuwa wa kuchosha usipofanywa kwa uangalifu c) Utayarishaji wake huhitaji muda mwingi. ZOEZI. 1. Eleza maana ya somo lililoandikwa. 2. Taja vitu muhimu vilivyo katika somo lililoandikwa. 3. Taja ubora na udhaifu wa njia hii licha ya zilizotolewa katika kitabu hiki. 4. .Andaa ujumbe kwa kutumia mbinu ya somo lililoandikwa na kisha huburi kwa dakika kumi. 2.Somo Lisiloandikwa. Hii ni mbinu ya utayarishaji wa somo bila kuliandika. Mhubiri husoma vifungu vya maandiko na kivitafakari kwa kina kisha hukariri vitu vya msingi vilivyo katika ujumbe wake na maandiko yanayohusika. Aina hii mara nyingi hutumika katika kutayarisha na kuhubiri ujumbe wenye uvuvio zaidi. Njia hii ni nzuri sana katika kuhubiri ujumbe wa kiinjilisti. Ujumbe hutiririka toka rohoni na huwa wa kuvutia mno. Faidaza mbinu hii. a) Ni rahisi kutumia. b) Haihitaji muda mwingi wa matayarisho. c) Mhubiri huwa huru kutoa kila kinachokuja ndani yake maadam kinaendana na ujumbe wa somo. d) Huwasisimua wasikilizaji na kuwavutia. Udhaifu wa mbinu hii. a) Mhubiri kutoka nje ya ujumbe wake hasa ikifanywa na mhubiri asiye na uzoefu. b) Wasikilizaji waweza kulielewa somo vibaya. (waweza kuelewa vile somo lisicho maanisha). c) Somo kutowajenga wasikilizaji na kuishia kusisimua tu akili zao. d) Somo kutokuwa na maana halisi na hivyo kutowajenga wasikilizaji. ZOEZI. 1.Eleza maana ya somo lisiloandikwa. 2. Taja mabo matano ya kuzingatia katika utayarishaji wa ujumbe kwa kutumia njia ya somo sililoandikwa. 3.Toa tofauti iliyopo kati ya somo lililoandikwa na somo lisiloandikwa. 4. Andaa ujumbe kwa kutumia mbinu ya somo lisiloandikwa na kisha hubiri kwa dakika kumi 3.Mbinu Ya Skeletoni. Njia hii huhusisha kuandika maelezo ya somo au ujumbe kwa kifupi kwa lengo la kufanikisha utunzaji wa kumbukumbu sahihi juu ya ujumbe au somo. Kwa maana nyingine ni kwamba mhubiri hutayarisha muhtasari wa ujumbe au somo.Mhutasari huo huwa kama skeletoni ya somo, Skeletoni maana yake ni fuvu. Mfano wa fuvu la binadamu. . Mhubiri huhubiri kwa kutumia skeleton hiyo. Kazi yake hasa ni kuweka nyama katika skeletoni hiyo kwa njia ya mahubiri. Hivyo anapohubiri huweka nyama katika mahubiri yake ili yawze kuwa kitu kamili . Mhutasari wa somo huwa kama mifupa ya ujumbe. Ndiyo mifupa ambayo huleta sura na mategemeo kwa kile mhubiri anachotamani kusema. Anavyosema anaweka nyama katika mifupa na kuufanya mwili wa somo lake. Hupanua mawazo yake ambayo maelezo yake mafupi yamekuza. Faida za mbinu hii. a) Mbinu hii humpa mhubiri uhuru zaidi. b) Utoaji wa somo huwa wa kuvutia sana. c) Somo huwajenga wasikilizaji bila kuwachosha. d) Mhubiri huweza kutoa somo kwa mtiririko mzuri na sahihi. Zoezi 1. Eleza maana ya skeletoni. 2. Eleza maana ya mbinu ya skeletoni. 3. Linganua kati ya minu ya somo lisiloandikwa na mbinu ya skeleton. 4. Eleza kati ya mbinu tatu ulizosoma, ipi ni bora kuliko zote na toa sababu ya jibu lako B. Maeneo ya Mahubiri. Kuna maeneo makuu manne ambyo mahubiri huhusisha. Mhubiri yoyote ni lazima azingatie maeneo hayo ili aweze kufanikisha mahubiri yake. I.Wazo . Hii huhusu namna ya kupokea kichwa cha somo au ujmbe. Ni ujuzi unaohusu namna ya kupokea ujumbe toka kwa Mungu. Huhusu namna ya kupata wazo la awali na kichwa cha somo. Mungu hupanda mbegu ya wazo kuhusu somo au ujumbe siku kadhaa kabla ya mahubiri. Mbegu hiyo hukua kwa njia ya kuitafakari na maombi zaidi. Kutokana na ujuzi mhubiri aweza kuujenga uwezo wa kutambua mstari unaohusika. Mhubiri hupaswa kuliendeleza na kulikuza wazo lililopandwa ndani yake kwa njia ya maombi, kutafakari na kuchunguza zaidi juu ya wazo hilo ili aweze kutayarisha ujumbe. Pata muda wa utulivu utulie uweponi na omba nuru zaidi ya ufunuo huo. Kuna tofauti kubwa kati ya hotuba na ujumbe.mtu anaweza kujifunza jinsi ya kuandaa hotuba kupitia masomo ya Homiletics lakini Mtu anapaswa kuwa na ushirika na Mungu ili aweze kupata ujumbe. Kupata ujumbe ni jambo la kiroho zaidi kuliko taaluma. Wale wanaofanikiwa kupokea ujmbe wa kuhubiri toka kwa Mungu ndio wanaoweza kufanikisha lengo la kuhubiri. Mambo ya kusaidia kupata ujumbe. Tambua mahitaji ya watu.(Mahitaji ya kiroho na kimwili). Kujazwa na Neno la Mungu. Kujiweka katika viatu vya wengine (Soma Hotuba na sikiliza mahubiri ya watu wengine. Kutokana na uzoefu wa mhubiri. Kutambua kalenda ya Kikristo. Kutokana na mafundisho ya msingi ya Biblia. Kutokana na matukio mbalimbali. II.Muundo. Muundo huhusisha uchambuzi wa wazo ili kuweza kugundua kweli zilizomo katika wazo hilo.Baada ya kupokea Wazo toka kwa Mungu unapaswa uanze kulichambua ili kutambua vitu ambavyo wazo hilo linavyo. Katika hatua hii unapaswa kuorodhesha kwa urahisi kila kitu kilichomo kwenye wazo hilo.Mara nyingi unapokuwa katka hatua hii unahitaji kuandika kwa haraka ili kupata kwa kifupi mtiririko wa uvuvio unaokuja. Hakikisha kwamba unaandika kila kitu ili uweze kuchambua baadae. III. Ujenzi. Huhusisha kukusanya na kuyaweka mawazo yako uliyoyachambua katika kipengele cha uchambuzi katika mpango mzuri. Kuweka kila kitu katika mpangilio mzuri kutakusaidia na kukurahisishia katika utoaji wa somo lako. Kuwasislisha mawazo yaliyoendelezwa hufanyika msaada sana kwa wasikilizaji wako katika kuelewa na kufuata mpango wako wa kufikiri. Somo likiwalimechanganywa itawawia vigumu wasikilizaji wako katika kulielewa somo hilo.Ujenzi wa somo hulenga kulifanya somo rahisi kiasi cha kueleweka vizuri na wasikilizaji. Ni muhimu sana kwa mhubiri kuliweka somo katika namna itakayofanya lieleweke kwa urahisi. IV. Mawasiliano. Hii huhusu namana mhubiri anavyowasilisha somo au ujumbe kwa hadhira. Mhubiri anatakiwa kuliwasilisha somo lake kwa njia rahisi na nyepesi kueleweka na wasikilizaji wake. Anatakiwa: a) Kuwasilisha ukweli uliowazi na wenye kueleweka. b) Kutoa ujumbe kwa njia ya kuteka akili za hadhira. c) Kuendeleza mawazo yake katika mpango ambao hadhira wataweza kuyafuata kwa urahisi. d) Kuwahamasisha hadhira kulitendea kazi somo. Yak 1:22. C.Sehemu Kuu za ujumbe na Hotuba. Kwa kawaida mahubiri au hotuba yoyote ile ni lazima iwe na sehemtu tatu ambazo kwa pamoja huunda hotuba au mahubiri hayo. Sehemu tatu hizo ni utangulizi, kiini na hitimisho.Kila sehemu ni muhimusana na inatakiwa kupewa uzito wake. Sehemu mojawapo ikipuzwa yaweza kuvuruga au kuharibu kabisa ujumbe au hotuba yako. I.Utangulizi. I. Hii ni sehemu ya kwanza ya hotuba. Utangulizi hutambulisha hotuba au somo zima na kutoa picha jinsi somo litakavyokuwa. Utangulizi ni sehemu muhimu ya ujumbe na kama hadhira hawajakusikiliza kwa umakini katika kipindi hiki cha awali yawezekana kutokuuelewa ujumbe wako au kutokukusikiliza vizuri katika sehemu zinazobaki za hotuba yako. Mara nygingi utangulizi huwa kama muhtasari wa ujumbe.Katika utangulizi mhubiri huwaeleza hadhira kwa kifupi juu ya kile ulichopanga kuongelea au kuhubiri. Utangulizi ni kama mlango wa nyumba katika ujumbe na hotuba.Uangulizi huwa na lengo mahususi la kuwajulisha hadhira ujumbe ambao unawasislishwa kwao. Waamni wengi huja kanisani wakiwa na matatizo mbalimbali ya kifamilia , kikazi N.k .Utangulizi unatakiwa kuwavuta ili waweze kujikita kwenye ujumbe na kuwasahaulisha matatizo waliokuja nayo. Uangulizi ni silaha ya kuwateka wasikilizaji. Kuna namna mbalimbali za kuanza utangulizi. Mhubiri anapaswa kujifunza namna mbalimbali za kuanza utangulizi na ajizoeze kuanza utangulizi wa mahubiri yake kwa njia tofauti tofauti. Baadhi ya njia za kuanza utagulizi zimeorodheshwa hapa chini. II.Namana ya kuanza Utangulizi 1. Kuanza kwa kuuliza swali. 2. Kuanza na maelezo ya kuchanganya(Yenye kuhamasisha watu kusikia kw2a makini swehemu ya ujumbe inayobaki ). 3. Anza kwa andiko 4. Anza kwa mkutadha 5. Anza na habari au kielelezo. 6. Anza na tukio la sasa. 7. Anza na nukuu III. Mambo ya msingi katika utangulizi. Kuteka usikivu. utangulizi wako unapaswa utawale hamu na mawazo ya wasikilizaji. Kujenga masikilizano. Lazima ujenge mawasiliano kati yako na wasikilizaji. Kuleta kukubalika. Ni lazima utangulizi kwako ukujengee kukubalika kwa wasikilizaji. Unapaswa kupata usikivu wao, matumaini na heshima. Kujulisha. Utangulizi wako unapaswa kuwaeleza wasikilizaji kwamba somo lako lina husu nini hasa, na jinsi utakavyoliwasilisha. Kusadikisha. Ni lazima utangulizi uwasadikishe wasilizaji juu ya umuhimu wa ujumbe na kupata usikivu mzuri wa sehemu iliyobaki ya hotuba yako. Usitoe utangulizi kwa kuomba msamaha. Usiseme “Bahati mbaya sikujiandaa vizuri” Kufanya hivyo kutapoteza usikivu wa wasikilizaji wako na kukufanya usiaminike kwao. Sifa za utangulizi mzuri. 1.Sio wa kishindo mno. Utangulizi uwe wa kiasi usiweke hatua ambayo huwezi kuifikia. 2.Sio mrefu mno. Kumbuka kwamba utangulizi si ujumbe wote bali ni sehemu tu hivyo unapaswa kuwa mfupi. 3.Utangulizi uendane na ujumbe. Utangulizi ni sharti ulenge kichwa cha somo. Waweza kuwa muhtasari wa somo au kisa ambacho kinaonesha ukweli wa kile ulichokusudia kuongelea. 4.Unapaswa kuandaliwa kwa uangalifu. Kwa sababu utangulizi wako ni kitu muhimu katika kuvuta usikivu wa hadhira unapaswa kuandaliwa kwa umakini sana. 5.Tayarisha utangulizi wako kwa kujiuliza maswali yafuatayo a.“ Ningekuwa ni msikilizaji wa ujumbe huu nini kingenivuta zaidi ili kuleta usikivu katika yote niliyokusudia kuyasema? 1. “ Ni jambo gani hasa ambalo lingekamata usikivu wangu? b.Majibu yake unayoyapata ndiyo waweza kuyatumia katika sehemu ya utangulizi wa ujumbe wako. 6. Utoe nafasi ya kupitia kwenye kiini cha ujumbe. Utangulizi unapaswa kutoa njia ya kupitia kwenda kwenye kiini cha ujumbe. Kusiwe na pengo kati ya utangulizi na kiini cha ujumbe. II. Kiini. Hii ni sehemu kuu ya somo au ujumbe ambayo imebeba ukweli wote wa somo. Hatua ya kwaza kwenye kiini ni kutoa skeletoni ya kiini na kisha hatua ya pili ni kuweka nyama katika skeletoni yako.Waweza kuweka nyama katika sekeletoni yako kwa kufanya yafuatayo: Kufafanua msamiati mbalimbali inayojitokeza kwenye kiini na kutoa maelezo ya dondoo ulizoziandaa. Tumia kamusi au itifaki ya Biblia katika kupata maana ya maneno hayo. Kiini. Kiini cha ujumbe ni lazima kieleze, kisimulie, kijadili na kutoa kweli yote inayokusudiwa kuwasilishwa. Ni lazima kueleza maana ya andiko au habari. Ni lazima kutoa ushahidi wa kweli inayohubiriwa. Neno la Mungu linajieleza lenyewe. Jambo lingine la kutumia kuthibitisha ni ushuhuda binafsi. Mfano kama unahubiri uponyaji toa uthibitisho kwa kutumia wewe binafsi jinsi Mungu alivyokuponya au alivyowaponya watu wengine. Unapounda kiini unapaswa kujiuliza maswali kadhaa 1. NIini nataka kusema ? 2. Kwanini ninataka kusema hiki ? 3. Ni vipi nitakisema ? 4. Ninachotaka kukisema kitafanikisha nini ? Unaposhughulikia andiko au mada ni lazima kujiuliza kwanini? Namna gani ?, Lini?, Wapi ?, Nini kilitokea kabla na baada ?, Mazingira yalikuwaje?, Matokeo yake yalikuwa nini ?, Nani walikuwa pale ?, na kwanini walikuwepo pale? Walifanya nini?, Hii huhusikaje leo ? na inamaanisha nini leo ?. Kujua majibu ya maswali haya kutakusaidia kutengeneza mhutasari wa somo au andiko. Mfano Luka 16:19 Matumizi ya vielelezo. Moja wapo ya vipengele muhimu katika ujmube au kiini ni vielelezo.Vielelezo ni mifano mbalimbali inayotumika kufafanua na kuelezea ujumbe au somo. Watu wengi huweza kukumbuka vielelezo kuliko ujumbe na hivyo basi vielelezo husadia watu kukumbuka ujumbe. Bwana Yesu amekuwa kielelzo na mwalimu wa vielelezo. Watu hufurahia kusikia vielelezo. Wahubiri wenye ujuzi wa kutumia vielelezo katika jmube na hotuba zao hufanikiwaq kuvuta usikivu wa wasikilizaji wao. Vielelezo ni sawa na madirisha katika nyumba. Vielelzo ni madirisha ya jumbe na hotuba. Jumbe nyingi zinazohubiriwa na wahubiri wengi ni kama nyumba zisizo na madirisha. Nhyumba hizo zaweza kuwa na msingi imara na kuta imara lakini zitashindwa kuingiza mwanga na hewa ya Oksijeni ambayo ni muhimu kwa mwanadamu ili aweze kuishi. Vielelezo hutimiza lengo la kuleta nuru na hewa ya oksijeni ya ki-Biblia katika ujumbe. Vielelezo havipaswi kuwa mwisho vyenyewe lakini vyapaswa kufafanua kweli zinazoawsislishwa. Lengo la vielelezo. Kuleta nuru kwenye somo. Kuvuta usikivu. Kuelezea na kufafanua ujumbe. Kuthibitsha kweli (dondoo). Kanuni za kutumia vielelezo. Kuna kanuni kadha ambazo ni muhimu kuzizingatia wakati wa kutumia vielelezo . Baadhi ya kanuni hizo zimejadiliwa hapa chini. 1. Urahisi. Vielelezo vinapaswa kuwa rahisi kiasi cha kueleweka na kila msikilizaji. Havipaswi kuwa vigumu kiasi cha kuwachanganya wasikilizaji na kuhitaji vielelezo zaidi ili kufafanua vielelezo. Kuna baadhi ya vielelezo ambavyo huhitaji vielelzo vingine . Epuka kutumia vielelezo vya namna hiyo. Yesu alipotumia vielelezo vilikuwa rahisi na wazi Mifano aliyotoa ilkuwa wazi na rahis kueleweka na waikilizaji wa aina zot. Wasomi(mafarisayo na masadukayo) na wasio wasomi (wakulima na wavuvi). Kumbuka kwamba watu wengi utakaokuwa unawahubiria watakuwa ni wenye elimu ya kawaida au wasio na elimu. 2.Ukweli. Hadithi na vilelelzovinavyotumiaka katika amhubiri view wazi. Kama ni hadhi za kutunga usiwaambie watu kwamba ni matukio halisi yaliyotokea. Usilazimishe mfano na kuelelzo kuwa kitu halisi. 3.Kiasi. Vielelzo visizidi na wala visigeuke kuwa ujumbe. Kuna baadhi ya wahjubiri ambao ni mabigwa wa kutoa vielelezona watu huvutiwa sana na vielelezo hivyo. Wanatumia muda mwingi kusimulia vielelzo badala ya kuhubiri. Jambo hili ni hatari sana. Vielelezo vinatakiwa kutumika kuelezea kweli za kiroho na na visigeuke kuwa jumbe.Yesu hakututuma kusimulia hadithi na vielelzo alitutuma kuhubiri. Kwa kawaida kila dondoo kuu inapaswa kuwa na kielelezo kimoja na si vinginevyo. 4. Lengo. Unapaswa kukumbuka kwamba lengo la vielelezo ni kuelezea na kufafanua ujumbe wako. Kweli zipo kumsaidia mhubiri kufikia lengo lake la mahubiri. Lengo la mhubiri linapaswa kubaki kuwa ujumbe na si vielelezo. 5. Uhalisia. Vielelezo viendane na dondoo unayoielezea. Kama hakuna uhusiano hakuna umhuhiu wa kutumia kielelezo hicho. Hakikisha vinahusiana na kwendana. Vyanzo vya vielelezo. Bwana wetu Yesu Kristo alitmia vielelezo na mifano kutoka katika mazingira ya kawaida yaliyomzunguka. Alitumia mifano rahisi kama vile nuru, chumvi mbegu. Mzabibu, kondoo. N.k. Alitumia mifano iliyokuwaikitumika katika maisha ya kawaida. Alizielezea na kuzifafanuana kuzifundisha kweli za kiroho kwa kutumia vielelezo vilivyokuwa katika ulimwengu uliomzunguka. Hivyo basi kila mhubiri anatakiwa kujifunza kutumia vitu mbalimbali vilivyo katka mazingira yake kama vielelezo. Soma vitabu, magazeti ,vijarida na vipeperushi. Sikiliza natutzama vyombo vya habari. Katika mabo yote hayo kua vielelezo vingi ambavyo waweza kuvipata na kuvitumia. Kabla ya kuanza kuitumia kielelezo hakikisha unatihafamu vizuri. Kielelezo kiwasaidie watu kujisikia, kusikia na kuona kile unachokielezea. Ni lazima wewe mwenyewe uguswe na kuvutiwa na kielelezo hicho. Kama hakikuvuti wewe bila shaka hata watu wengine hakita wavutia. Jifunze kwa mwalimu mkuu Yesu Kristo. Vichekesho. . Vichekesho ni muhimu katika mahubiri kutegemeana na ujumbe unaohubriwa. Vichekesho vyapaswa kuendana na somo au ujumbe. Tumia vichekesho kuamsha akili za watu na kuvuta usikivu wao. Vichekesho havipaswi kuzidi kiasi cha kupunguza uzito wa somo. Pia Ujumbe usitawaliwa na vichekesho. Kumbuka kwamba mahubiri si vichekezo ni kitu muhimu na nyeti sana. Usifanye mahubiri kuwa komedi. Wala usiwe mwanakomedi. III. Hitimisho. Hii ni sehemu ya mwisho ya hotuba au ujmbe lakini kipengele cha muhumi sana . Kipengele hiki kisipozingatiwa maana na malengo yote ya kuhubiri huvurugika na kutokuwa na maana. Hivyo ni lazima kipewe uzito unaostahili. Mambo ya kuzingatia. Tunia muda kidogo kwa kuuelezea ujumbe kwa kifupi. Kazia maeneo ya msingi unayofikiri kwamba hayakueleweka vizuri kwa hadhira wakati ukihubiri na yale yanayotakiwa kupewa uzito maalumu. Pia waweza kurudia kuzitamka kwa sauti dondoo za ujumbe wako kila moja. Usiwachushe (bore) kwa kuanza kurudia kuhubiri ujumbe wako wote. Mwaliko. Mwaliko ni kipengele muhimu sana katika hitimisho. Kwa sababu mahubiri ni tofauti na aina nyingine za hotuba hivyo mwaliko huwa ni muhimu sana kwa kuwa mahubiri huhusu kuchukua maamuzi au hatua juu ya kile kilichohubiriwa. Mahubiri bila mwaliko huwa hayajafikia lengo la kuhubiri. Mwaliko ni lazima katika mahubiri ya aina yoyote ile. Mwaliko huwa ni wakati wa kuitikia Kile Mungu amesema kupitia mahubiri. Ni wakati wa kutendea kazi kile kilichofundishwa au kuhubiriwa. Mhubiri anapaswa kuufanya mwaliko kuwa wazi kwa wasikilizaji wote. Lengo la mwaliko si kuwaita watu madhabahuni tu bali ni kuwahamasisha watu kuweka ujumbe katika matendo. Pia Mhubiri hutakiwa kuuweka ujumbe wake katika matendo. • Ukihubiri uponyaji waite watu madhabahuni na waombee uponyaji. • Ukihubiri kutembea katika mamlaka unatakiwa udhihishe mamlaka hiyo. • Ukihubiri utoaji waite watu kumtolea Mungu. • Ukihibiri toba unapaswa kuwaongoza hadhira kwenye maombi ya toba na kuwaita madhabahuni wale wanohitaji kutengeneza kwa upya mwenendo na mahusiano na Mungu na kuomba nao. • Wapeleke watu kwenye matendo na matumizi Mt 21:23. Yak 2:22. • Unatakiwa kuwaongoza hadhira kuomba kwaajili ya ujumbe au somo kwa kadri ya maongozi ya Mungu na kwa kadri Mungu alivyosema na kila mmoja. • Unaweza kuwaongoza watu waimbe wimbo unaoendana na ujumbe uili kuwaogoza uweponi na kuwapa hamasa. • Toa mwaliko kwa watu ambao wanataka kuokoka na kama wapo omba nao. Baada ya hapo maliza na mkabiribishe anaehusika na ratiba inayofuata. Kwa kuhitimisha juu ya sehemu tatu za ujumbe au hotuba twaweza kuvifupisha vipenele vyote hivyo vitatu kwa sentensi tatu ambazo ni: 1. Waambie hadhira kile unachotaka kuhubiri.(Utangulizi.) 2. Hubiri kile ulichowaambia (Kiini), kisha: 3. Waambie kile ulichohubiri.(Hitimisho). ZOEZI. Katika makundi ya watu watatu watatu jadilini maswali yafuatayo: 1. Jadili umuhimu wa vipengele vinne vya maeneo ya mahubiri kila kimoja. 2. Nini kitatokea kama mhubiri atatayarisha ujumbe wa mahubiri bila kuzingatia maeneo hayo. 3. Eleza umuhimu wa sehemu tatu za ujumbe wa mahubiri. 4. Mhubiri bora ni lazima azingatie sehemu tatu za ujumbe. Jadili kauli hii kwa mifano dhahiri. Kuhubiri si kazi rahisi. Kubali usemi huu kwa hoja kumi madhubuti. MADA YA TATU: AINA MBALIMBALI ZA MAHUBIRI. Kuna aina mbalimbali za mahubiri na kila aina ya mahubiri ina nafasi yake katika kuujenga na kuimarisha mwili wa Kristo na kuwaleta waliopotea dhambini. Mhubiri analazimika kufahamu aina mbalimbali za mahubiri ili aweze kuwa na ujuzi mwingi wa kuhubiri na ili aweze kuhubiri kwa kuyafanya mahubiri kuwa mapya kila ahubiripo. Kuhubiri kwa kutumia aina mbalimbali za mahubiri huwajenga wasikiliza kwa namna mbalimbali ambapo aina mojaya mahubiri isingeweza kufanya hivyo. Pia husaidia washirika na waamini kuwa na msingi mzuri wa uelewa wa Neno la Mungu. I. Mahubiri ya kifungu. Aina hii ya mahubiri hujengwa juu ya kifungu kimoja kidogo cha maandiko tu. Huhusisha kuchagua maelezo fulani maalum ya maandiko na kuyachunguza, kuchambua na kugundua kweli zote zilizomo ndani yake na kuziwasilisha kwa wasikilizaji kwa mtindo rahisi na wenye kueleweka. A. Faida za mahubiri ya Kifungu. a) Huvutia. b) Huzuia kutoka nje ya somo. c) Hufanya mahubiri kuwa ya ki- Biblia. d) Humwongezea mhubiri ujasiri. e) Husaidia wasikilizaji kulikumbuka somo. B. Jinsi ya kuandaa mahubiri ya kifungu. Kuna mambo kadhaa ambayo mhubiri anapaswa kuyazingatia wakati wa kuandaa mahubiri ya aya, badhi ya mambo hayo yamejadiliwa hapa chini. 1.Soma Biblia mara kwa mara. Unapaswa kusoma Biblia mara kwa mara ikiwa unataka kuwa mhubiri mwenye mafanikio katika huduma yako. -Tenga muda wa kusoma Biblia kila siku. Beba Biblia ndogo kila mahali unapokwenda ili upatapo muda uweze kuisoma. 2. Jifunze Biblia. Kujifunza ni zaidi ya kusoma.Kujifunza kuna husisha kusoma Biblia kwa undani kwa kuchunguza kikamilifu kila kitu kilicho katika maandiko unayosoma na kutafakari kwa kina,.Yos1:8. Unapaswa kutafakari kwa uangalifu vitu unavyosoma. Viweke kwenye akili yako na kuvifikiri tena na tena. Unapaswa kujizoesha kuchambua kile ulichojifunza. Baada ya kukichambua kwa umakini unapaswa kukiweka tena akilini. 2. Kuwa na Daftari la kuandikia. Kila usomapo Biblia yako jitahidi kuwa na kalamu na daftari la kuandika mambo muhimu unayojifunza. Jenga mazoea ya kuandika kwa ufupi kila ufunuo unaoupata. 3. Dumisha hali ya maombi. Unapaswa kuwa katika hali ya maombi kila usomapo Biblia .Omba Mungu akufunulie upate kulielewa Neno lake.Pia unapaswa kumwomba Mungu akupe usikivu juu ya kweli anazokufunulia katika Neno lake. 4. Jenga usikivu.Unapaswa kuwa katika hali ya utulivu na usikivu katika Nyanja zote yaani kimwili, kiroho na kisaikolojia. Mungu hutoa ufunuo wake kwa sauti ya kimya ndani ya roho ya mhubiri. Kama hunautulivu na usikivu wa kutosha ni vigumu kugundua maarifa hayo.. - C.Sifa za aya ya mahubiri Kifungu cha mahubiri au aya yapasa kuwa : a. Yenye mamlaka ya ki-Biblia. Mafundisho unayokusudia kuhubiri toka kifungu au aya fualani ya maandiko yapasa ikubaliane na kile Biblia nzima inachofundisha. Katika mahubiri ya kifungu kuna uwezekano wa kuchukua kimakosa mstari nje ya maana yake na kuutumia kufundishia kitu ambacho Biblia haikubaliani nacho. Ni Muhimu sana kwa ,mhubiri kujua jinsi mstari anaoshughulikia jinsi unavyokubaliana na kusudi la sura yote na kitabu chote. Daima mhubiri anapaswa kujitahidi kufasili aya yake katika nuru ya yale ambayo Biblia nzima inafundisha. b.Kamili. Aya yapaswa kuwa katika maandisha ya ukweli ulio kamilika. Baadhi ya wahubiri huchukua kifungu cha maneno katika mstari na kukitumia bila kujali maneno yaliyotangulia au yanayofuata. Jambo hili si zuri na huzaa mafundsho ya uongo. Na huku huitwa. “Kulichanganya neno la Mungu na uongo……..2Kor 4:2. Ni lazima uepuke jambo hili kwani litaleta kutokuaminika na maelezo yasiyo ya ki- Biblia na hatimae utawapotosha wasikilizaji wako. c. Fupi kiasi. Kifungu cha mahubiri chapaswa kitolewe kwenye maelezo ya maandiko ambayo ni mafupi na ya kulizisha. c. Ya kueleweka. Aya yapaswa kueleweka na iwe muhtasari wa kutosha wa kile unachotaka kukishirikisha. *Unapaswa ubaki katika mipaka ya kile ambacho aya yako inaelezea. D. Namna ya kuandaa mahibiri ya aya. a. Elewa maneno yake vema. Kipitie kifungu kwa kukisoma mara kadhaa, kitafakari na kujenga kumbukumbu juu yake na kiseme mwenyewe kwako. Hakikisha unakielewa vizuri. b. Elewa lugha yake.Tamabua lugha yake kama ina maana halisi au kama ni lugha ya mifano tu. Jiulize kama mwandishi alikuwa na maana hasa ya kile alichokiandika au maneno yake yachukuliwe kama mfano wa mahubiri? c. Changanua ujumbe wake.Chambua ujumbe unaoupata na kuutenga katika sehemu kadhaa zenye kulandana ili uweze kuuwasilisha kwa mtiririko mzuri. d. Chunguza maneno yake. Jitahidi kugundua kile maneno hayo yalikusudia kuwasilisha hapo awali. Ikiwa una kamusi ya kigiriki au Kiebrania unapaswa kulitazama neno hilo. Jaribu kubaini kama kuna maana maalumu ndani ya neno unalolishughulikia. Kufanya hivyo kutakusaidia kugundua maana yoyote maalumu ambayo mwandishi alikusudia kuiwasilisha. e. Tathmni mwendelezo wake. Baini kweli zile mwandishi alitaka kuzielezea. Tambua jinsi alivyo kamilisha katika kuziwasilisha kweli hizo. Jaribu kufuata mwongozo wake na kuuendeleza katika mtindo huo. f. Mkutadha wa kifungu.. i. Maneno ya mbele na ya nyuma ya kifungu. Angalia jinsi mistari iliyotangulia na inayofuata inachosema. Chunguza aya kuhusiana na sura nzima ambayo umetoka. Chunguza kifungu hicho katika nuru ya kitabu kizima ambamo kinapatikana. Jifunze kiini na mazingira yote ya kitabu. ii. Hali ya mila. Je mila za wakati ule ziliathiri kile kilichoandikwa? Je watu walioandikiwa kifungu hicho awali wangekuwa na wazo la kile kilichoandikwa tofauti na ambalo tungepata katika hali yetu? Kama ndivyo nini ingekuwa maana inayolingana na sasa? ii. Hali ya kihistoria. Je jambo hili liliandikwa lini? je wakati huo ulishawishi kile kilichoandikwa? Je matukio ya wakati ule yaliyokuwa yakijulikana wakati ule wa uandishi yalikuwa na maana maalum juu ya kile kilichosemwa? iv. Hali ya kijiografia. Mwandishi alikuwa wapi wakati anaandika maneno hayo? je Watu walioandikiwa walikuwa wapi?Je mazingira yao yana uhusiano wa chochote katika kile kilichosemwa? v. Biblia kwa ujumla. Kila sehemu ya maandiko ifasiliwe kwa uaminifu na kwa umakini ili ikubaliane na maandiko yote. Andiko lolote lisifasiliwe nje ya mkutadha wake. Maandiko ni lazima yafasiri maandiko. E.Kupanga Maelezo. Mpanglio mzuri wa maelezo na kazi kwa ujumla ni wa maana sana kwa mhubiri. Hakikisha unapanga maelezo yako kimaantiki. Mpangilio mzuri wa kazi na mawazo humwezesha mhubiri kulielewa vizuri somo na kulishughulikia somo kikamilifu. Pia huwawezesha wasikilizaji kulielwa somo na kulikumbuka somo . 1. Ujumbe uwe katika mpangilio.Panga ujumbe wako katika mtiririko mzuri ili uweze kuufuata kwa urahisi wakati wa kuhubiri. 2. Weka ujumbe wako katika hali ya kueleweka. Jitahidi kukamilisha vipengele vyote unavyohitaji kuviongelea katika mahubiri yako. Kabla ya kupanda mimbarini. 3. Kazia katika mawazo. Unapaswa kuyaweka mawazo yako katika sentensi fupi. Jifunze namna ya kuyaimarisha mawazo yako kwa pamoja na kuyaelezea katika sentensi fupi zinazoeleweka kwa urahisi.Jizoeze kupunguza na kulielezea wazo kwa sentensi moja. 4. Tayarisha maelezo mafupi.Kumbuka kwamba maelezo yako ili kusaidia kumbukumbu yako.unapaswa kuwa na vidokezo vitakavyosaidia kulikumbuka somo lako au ujumbe wako. 5. Ufanye rahisi kuusoma. Ni vizuri kupiga chapa mahubiri yako ili uweze kusoma kwa urahisi wakati wa kuhubiri. Pia waweza kutoa vipeperushi na vijarida kwa wasikilizaji wako ili waweze kufuatilia zaidi ujmbe au somo lako. Zoezi. 1. Eleza maana ya mahubiri ya aya. 2.Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya aya. 3.Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya aya au kifungu licha ya yaliyotajwa katika kitabu hiki. 4. Andaa hotuba ya mahubiri ya aya na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako. II. MAHUBIRI YA KUFAFANUA. Mahubiri ya kufafanua ni aina ya mahubiri ambayo huhusisha kuchagua sehemu kubwa ya maandiko na kuichunguza kwa undani na kuifasiri na kugungua kweli zilizomo katika sehemu hiyo ya maandiko na kushirikisha mkutano au usharika wako. Mfano unaweza kuamua kupitia Injili yote ya Luka sura baada ya sura. Kuanzia sura ya kwanza, unatafuta kufasili na kuelezea maana na umuhimu wake mstari kwa mstari sura kwa sura mpaka umeimaliza yote. Waweza kushughulikia sura moja kila wiki, na baada ya wiki kadhaa utakuwa umemaliza kitabu chote. A.Faida ya mahubiri ya ufafanuzi. Hufanya mahubiri kuwa ya ki-Biblia. 1. Yesu alitumia aina hii ya mahubiri. Alichukua kifungu cha Agano la kale na kufasili maana yake kwa wasikilizaji wake. 2. Petro alitumia njia hii siku ya Pentekoste. 3. Stefano alitumia njia hii. Huwezesha waamini kuwa na msingi na uelewa mkubwa wa Biblia.Waamini huimalishwa na huwa na ufahamu mzuri na wa kina wa Neno la Mungu. Kwani kweli zote zilizomo katika kitabu kilichopitiwa tayari hufahamika vizuri kwa usharika wote. Huvuta kuimalishwa na Roho mtakatifu. Roho mtakatifu hulithibitisha neno lake kwa ishara na miujiza sawasawa na Kweli zote zilizofunuliwa katika kitabu husika. Humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia. Mahubiri ya kufafanua humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia kwani mhubiri huhubiri kile kilicho katika maandiko ya eneo husika. Mhubiri huwa anajikita katika mkutadha wa aya, sura na kitabu chote kwa ujumla. Hivyo kiini cha kitabu ndicho ambacho hubeba mahubiri yake yote. Mambo ya kuzingatia katika kutayarisha mahubiri ya kufafanua. I. Kwa umakini chagua kifungu cha maandiko kinachostahili. Hakikisha kwamba kifungu hicho kitahudumia uzima na uwezo wa wasikilizaji wako. 1. Usichague somo kwa sababu linakuvutia au kukupendeza. 2. Usichague somo ambalo litazaa machafuko, mgawanyiko na mashindano. 3. Jitahidi kufanyika njia ili Mungu akupitie ili aweze kuongea Neno lake kwa watu wake kwa kupitia wewe. 4. HIvyo basi unawajibika kutafuta kujua mawazo ya Mungu kuhusu watu wake ambao amekupa wajibu juu yao. 5. Huduma hii ni moja ya heshima kuu uliopewa lakini pia ni wajibu mkuu unaoogopesha sana. Hivyo basi unapaswa kuifanya kwa umakini wa hali ya juu. II.Tafuta ujumbe unaolingana na hali ya watu ya wakati ule. 1. Mungu kila mara huwa na ukweli wa sasa ambao hutaka kunena na watu wake. 2. Mungu hukusudia jambo maalum kwa kila kundi la waamini 3. Jifunze kujua kile Mungu anacho kwaajili ya kusanyiko kwa kila wakati. III. Jifunze sura ya kitabu kwa umakini. 1. Soma sura unayoshughulikia mara nyingi mpaka umeielewa vizuri. 2. Soma kwa uangalifu mstari hadi mstari. 3. Kila kunapokuwepo na uhusiano wa wazi kati ya kifungu hicho na kifungu kingine unapaswa kusoma kifungu hicho ili uweze kupata maana zaidi. Maandiko hufasiri maandiko. 4. Jenga usikivu kwa sauti ya Roho mtakatifu ili kupokea ufunuo toka kwake. Tumia vitabu vya rejea ili kupata msaada zaidi. Mfano. Itifaki ya Biblia, Kamusi ya Biblia, Biblia ya Tafsiri nyingine.Nk IV. Kusanya taarifa muhimu. Waweza kupata vitu vingine muhimu vya kuhusisha kwenye somo lako kwa kutumia mbinu ya maswali na majibu kama ifuatavyo. 1. Nimewahi kusikia au kusoma nini juu ya somo hili? 2. Roho mtakatifu amewahi kunionesha nini juu ya somo hili? 3. Nimewahi kuona nini chenye uhusiano na somo hili ? 4. Nimewahi kuwa na mawazo gani juu ya somo hili ? 5. Naweza kupata habari zaidi ju ya somo hili kwa nani au wapi ? 5. V. Tambua kiini cha somo lako. 1. Daima tafuta kugundua kiini cha sura unayoshughulikia. 2. Tafuta kujua kile Roho mtakatifu alikusudia kuwasilisha alipoivuvia sura hiyo. 3. Gundua undani wa somo hilo. 4. Baini kile Mungu anataka kusema na watu wake kupitia sura hiyo. VI.Kuwa na Lengo kamili. Lengo lako daima lapaswa kuendana kikamilifu na lengo la Mungu. 1. Hakikisha kwamba Umegundua kile Mungu anataka kutoa kupitia maadiko hayo na kisha jizamishe katika kile Mungu anataka kufanya. 2. Unapaswa kuhisi kile Mungu anachohisi Mungu humshirikisha mhubiri moyo wake na akili yake ili waweze kufanya kazi pamoja. Unapaswa kuchangamka. 3. Fanyika chombo cha Mungu cha kupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu wake. 4. Kumbuka hukuitwa kushiriki mawazo yako na watu bali kuwashirikisha watu mawazo ya Mungu. VII. Zungumza kulingana na ujuzi wako mwenyewe. 1. Usitoe nadharia toa uhai. Hubiri kile ulicho na uzoefu nacho.kile ambacho umekifanyia kazi . wapaswa kuwa mtu kwa kwanza kula matunda ya kazi yako. 2. Umeitwa kuwa barua Sio tu kwamba unataakiwa kuuhubiri ukweli bali pia unatakiwa kuufanyia mazoezi na kuuonesha kwa matendo. 3. Unapaswa kuwa mfano hai wa yote unayoyahubiri. VIII. Upe maana ujumbe wako. 1. Unawajibika kwa uwezo wako wote, kuhakikisha kwamba maana ya kweli na umuhimu wa maandiko unakuwa wazi na wakueleweka kwa wasikilizaji. 2. Daima jitahidi kuufanya ujumbe wako kuwa rahisi. 3. Hivi ndivyo Yesu alivyofanya Hii ilisababisha huduma yake kuwa na nguvu na mafanikio. 4. Alichukua mambo yaliyokuwa mafumbo na akayaweka rahisi sana. 5. Wahubiri wengine huyachukua masomo rahisi sana na kuyafanya mafumbo magumu sana kiasi cha kutoeleweka kwa wasikilizaji wake au kuelewa kidogo. IX.Fanya ujumbe wenye kutekelezeka. 1. Daima unapohubiri jitahidi kuonesha wazi wasikilizaji wako jinsi wanavyoweza kuutendea kazi ujumbe wako. 2. Jitahidi kutoa ushauri wa kimatendo kuhusu watu wanavyotakiwa kumwitikia Mungu kwa namna ya kufaa. 3. Husianisha mahubiri yako na maazimio yako kimatendo ambayo yaweza kuwafanya watu kuwa watendaji wa Neno na si wasikilizaji tu. Zoezi 1.Eleza maana ya mahubiri ya kufafanua. 2. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya kufafanua. 3. Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya kufafanua. 4. Chagua sura mojawapo ya injili ya Yohana na kisha andaa mahubiri ya kufafanua kutokana na sura hiyo na kisha hubiri kwa dakika kumi. III. MAHUBIRI JUU YA MAISHA YA WATU. A.Utangulizi Hii huhusu hadithi ya maisha ya watu. Kwa hiyo njia hii huhusisha mafunzo juu ya maisha ya watu mbalimbali tunaosoma habari zao katika Biblia. Kila hadithi ya mtu iliyoandikwa katika Biblia ina umuhimu kwetu. Maisha ya kila mhusika aliye kwenye Biblia yana mafunzo kadhaa ambayo twaweza kujifunza. Kila habari iliyoandikwa kwenye Biblia ipo kutufundisha kitu fulani ambacho ni cha thamani sana. 1Kor 10:1-11. Mhubiri huchagua mhusika mmojawapo wa wahusika walio katika Biblia na kujifunza kwa kina kila kitu kilichotoke katika maisha ya mhusika huyo, tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Pia mhubiri hutakiwa kujifunza kuhusu nasaba na mbari ya mhusika huyo ili aweze kufahamu vizuri vitu vilivyomjenga na kumkuza mhusika, kisha hutayarisha mahubiri juu ya mhusika huyo na kuhubri katika kusanyiko lake. Mafundisho ya wahusika wa Biblia ni ya kushangaza na ya kuvutia. Katkia aina hii ya mahubiri, mhubiri hupaswa kuchagua mhusika mmoja na kusoma habari zake zote zilizo kwenye Biblia na kisha huandikia kila wazo analolipata. Hapa mhubiri anapaswa kusoma kumbukumbuzote za mhusika katika Biblia. Baada ya kusoma kumbukumbumbu hizo unapaswa kuanza kuweka pamoja mawazo yote unayoyapata katika utaratibu wa miaka yaani jinsi matukio yalivyotokea ya mhusika huyo. B. Faida za mahubiri juu ya maisha ya watu. I.Hufunua ukweli wa maisha. Biblia imeeleza wazi maisha ya wahusika kama yalivyokuwa bila kuficha chochote. Imeeleza mafanikio yao na madhaifu yao. Ukweli wa maisha ya wahusika umewekwa wazi na kwa uhalisia. Wengi wa mashujaa wa Biblia wanahitilafu zao za kibinadamu.Twajua kuwa walikuwa wanadamu kama sisi na walikutana na majaribu kama sisi. Katika visa vyote vya historia kuna mtu mmoja tu mkamirifu ambae ni Yesu kristo pekee. Hata mashujaa wakubwa wa imani walikuwa na hitilafu zao. Hii inatupa kujua kwamba wao si tofauti na sisi. Ni mifano ya kujifunzia. Ni mifano na msada kwetu. Tunaweza kujifunza kutokana nayo kuliko ujuzi wetu wa uchungu. C. Mambo ya kuzingatia a) Jifunze kuzaliwa kwa huyo mtu. b) Tafakali hali na mazingira aliyolelewa. c) Angalia uhusiano wake na Mungu katika maisha yake. d) Angalia jinsi alivyo wajibika kuhusu uhusiano wake na Mungu. e) Baini vitu alivyojifunza kutokana na mahusiano yake na Mungu. f) Tathimini mafanikio yake. Jifunze vitu vilivyomfanya afanikiwe. g) Tazama maeneo aliyokosea kama yapo. Na jifunze vitu vilivyomfanya akosee. h) Toa hitimisho kile tunachoweza kujifunza kutokana na maisha ya mtu huyo. Mambo hayo yote yanavutia na ni yenye vitu vingi vya Kutufundisha ambayo twaweza kujifunza kutokana na watu hao. Tunaosoma habari za maisha yao katika Biblia. D. Hatua za kufuata katika kuandaa mahubiri juu ya maisha ya watu. I. Chagua mtu au msusika toka kwenye Biblia. Unapaswa kuanza na watu mashuhuri katika Biblia ambao habari zao ziko wazi kabisa, kama vile Ibrahimu,Musa,Samweli, Daudi, Yusufu, Debora, Miriamu, Mariamu, Dorkasi, Paulo, Petro. N.k. Hawa ni baadhi ya watu ambao matendo yao yamefanyika kuwa nuru katika historia ya ushusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Kuna mambo mengi sana ambayo twaweza kujifunza kutokana na maisha yao. Aina hii ya mahubiri ni nzuri sana, kujifunza toka kwa wacha Mungu wenzetu waliotutangulia katiki wito na huduma hii ni jambo la msingi sana. 1Kor 10.1-11. II. Chunguza maisha yake. Anza kwa kusoma hadithi inayoelezea kuzaliwa kwa mtu huyo. Tafuta maana ya jina lake. Kwani jina lina maana sana ki-Biblia. Angalia kwa umakini kusudi la Mungu katka maisha yake. Ili uweze kuvumbua vitu vingi unapaswa kujiuliza maswali yafuatayo: 1. Mungu alitaka kutekeleza nini kupitia mtu huyu ? 2. Je Mungu alifanya nini ili kusudi lake lijulikane kwa mtu huyu? 3. Mtu huyu aliitikia vipi Mungu alipomjulisha kusudi lake? 4. Tunaweza kujifunza nini kutokana na Mungu kuhusika katika maisha yake ? 5. Kuna tahadhari zozote ambazo tunapaswa kuzichukua ? 6. Je siri ya mafanikio yake ilikuwa nini ? 7. Je mwisho wa maisha yake ulikuwaje ? III. Chambua somo na kisha hubiri. Baada ya kujiuliza maswali hayo na kupata majibu utakuwa umepata vitu vingi ambavyo waweza kuvichambua kwa umakini na kuandaa somo kisha na kulihubiri somo hilo katika mpangilio na mtiririko Mzuri wa mawazo. Mwombe Roho mtakatifu akupe ufunuo zaidi unapokuwa ukihubiri somo lako na lifanye somo lako kuwa na uhalisia katika maisha ya sasa ya wasikilizaji. Zoezi 1.Eleza maana ya mahubiri ya wahusika au maisha ya watu. 2. Tengeneza orodha ya watu mashuhuri walio katika Biblia. Orodha hiyo ihusishe wanawake na wanaume. 3. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya wahusika. 4. Chagua mhusika mmoja wa kike au wa kiume na kisha andaa mahubiri kwa kumtumia mhusika huyo na kisha hubiri kwa dakika kumi. IV. MAHUBIRI YA MIFANO HALISI NA VIVULI. Huu ni ujuzi unaohusu kuweka wazi au kuchimbua na kuwasilisha ukweli uliojificha wa mifano mbalimbali katika Biblia. Mfano ni kitu, mtu au tukio ambalo kinabii ni ishara ya kitu au mtu fulani atakaetokea baadae. Inafanana au ni mfano wa Yule mtu au tukio. Katika matumizi ya Biblia ina maana ya mtu wa Bibli au tukio litakaloonesha kitu fulani kitakachotokea. Mfano mwanakondoo katika kitabu cha Kutoka ni mfano wa Bwana Yesu. Kila kitu kuhusu kondoo wa pasaka kiunabii kilikuwa na maana ya ukombozi wa wajibu ambao Bwana Yesu Kristo angetimiza.Yn 1:29. Mifano ya Biblia mara nyingi inaonekana kama kivuli(type) cha mambo yanayokuja baadae. Ebr 8:5,10:1. Siku takatifu pia katika agano la kale zilikuwa vivuli juu ya mambo ambayo yalikuwa yanakuja. Kol 2:17. Hizo siku takatifu hazikukamilika zenyewe sehemu ya kusudi la kutimizwa kwake ilikuwa ni kutanguliza sura ya kinabii ya vitu ambavyo vilikuwa bado vinakuja. Kanuni za kutumia. a. Unapojaribu kwa mara ya kwanza kufundisha kwa kutumia mifano ya kwenye Biblia, zingatia misingi ifuatayo. I. Tumia mifano rahisi zaidi. Anza na mifano rahisi ambayo maana yake iko wazi. II.Endelea na tafsiri ya wazi. Usijaribu kufasiri kila kitu.Elezea ukweli wote kama ulivyo na wala si kutafuta kila kipengele chake na kukielezea kwa undani. III. Usitumie maneno makavu. Usitumie mifano ya kufundishia kama kanuni. IV.Sisitiza ukweli wa msingi. Usitumie nafai uliyonayo kwa kutoa mifano ya kufundishia. Mifano itumike kusisitiza mafundisho na si kutumia kama chanzo cha ukweli. V. Uwe tayari kusahihishwa. Uwe tayari kusahihishwa na kukosolewa na wale waliokomaa kuliko wewe ili uweze kujifunza zaidi. 4. Kuelezea kusudi. Ni njia ambayo kwayo mhubiri hupanua maana ya ukweli ulio katika kifungu maalum cha maandiko. Unatafuta namana ya kuuweka wazi ukweli ambao umejificha ndani ya kifungu. Hii njia nzuri sana ya kufundishia kusudi lote la ki-Mungu. Mdo 20:27. Zoezi 1. Eleza maana ya vivuli na mifano.(Types). 2. Taja hatua za kufuata katika kutayarisha na kuhubiri mahubiri ya mifano na vivuli. 3. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya mifano na vivuli. 4. Tayarisha mahubiri ya mifano na vivuli na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako. V. MAHUBIRI YA MADA. Aina hii ya mahubiri hukusudia kutoa kiini maalum kwa hadhira.Mhubiri huchagua somo fulani kisha huchunguza kila kitu ambacho Biblia inasema juu ya somo hilo. Baada ya kuchunguza na kuchambua, kweli hizo huandikwa katika mapngilio wa somo. Mhubiri hupitia vifungu mbalimbali vya maandiko vinavyohusu somo hilo. Aina hii ya mahubiri huhitaji maandalizi ya muda mrefu na utulivu mwingi. Pia huwasilishwa katika mfululizo wa vipindi kadhaa na si kimoja, kwa sababu ni vigumu kupitia kweli zote zilizo katika somo kwa kipindi kimoja tu. Mfano wa mada za kuhubiri. 1. Upendo wa ki-Mungu 2. Ubatizo wa Roho mtakatifu 3. Maombi ya kufunga. 4. Nguvu ya usaidizi. 5. Vita vya kiroho. 6. Kutambua Ulimwengu wa roho. 7. Kutembea katika mamlaka. 8. Nguvu ya madhabahu. 9. Kushughulikia majira na nyakati. 10. Kutii mamlaka. Mambo ya kuzingatia katika mahubiri ya mada. 1. Uwe na ufahamu wa kutosha juu ya somo husika. 2. Fanya maandalizi ya mudamrefu na ya kina 3. Unapaswa kuwa na lengo mahususi la mahubiri yako. 4. Gawa somo katika vipengele vidogovidogo. 5. Kila kipengele lazima kiwe na maandiko yanayokithibitisha na kukielezea 6. Andiko liendane na dondoo unayoitoa. Zoezi. Somo hili lipo kimatendo zaidi. Kila mwanafunzi ashiriki katika kufanya mazoezi ya kuandaa mahubiri na ahubiri katika dakika zilizopendekezwa au mwalimu atakazopanga kulingana na muda uliopo. Mwalimu anatakiwa kusimamia na kusahihisha kazi za wanafunzi na kutoa marekebisho katika maeneo ambayo wanafunzi hawajafanya vizuri. 1.Andaa Ujumbe kwa kutumia aina ya mahubi ya mada na kisha hubiri mkutano kwa dakikika kumi. Chagua mada yoyote. 2.Taja ubora na udhaifu wa mahubiri ya mada. 3. Taja mambo mengine matano muhimu ya kuzingatia katika kuandaa mahubiri ya mada. 4. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri ya mada na mahubiri ya kufafanua. VI.MAHUBIRI YA MATUKIO. Mahubiri ya matukio ni kipengele katika mahubiri ya maada, lakini kutokana na umhuhimu wake tumekitenga na kukielezea peke yake. Mahubiri haya ni mahubiri ambayo huandaliwa kutokana na tukio lilipo au ambalo litafanyika katika kipndi fulani. Kiini cha mahubiri haya huwa ni tukio ambalo linafanyika katika ibada hiyo.Mfano wa matukio hayo ni Tukio la, 1. Kusimikwa kwa uongozi wa kanisa. 2. Ndoa au kumuaga bnti. 3. Kubariki watoto. 4. Ushirika mtakatifu 5. Ubatizo 6. Kuweka wakfu vitu mbalimbali. 7. Kuhitimu mafunzo.(graduation) 8. Msiba na mazishi. 9. Sikukuu mfano Pasaka, mwaka mpya, N.k Mambo ya kuzingatia 1. Mahubiri haya yanapaswa kuendana na tukio husika. 2. Mhubiri anatakiwa kufahamu ratiba nzima ya tukio hilo au shughuli hiyo. 3. Mhubiri ahubiri kulingana na tukio husika. 4. Mhubiri aepuke kutumia muda mwingi katika mahubiri. 5. Mhubiri ahubiri kwa lugha itakayoeleweka na kusanyiko lote na lugha yapaswa kuwa rahisi. 6. Mahubiri yapaswa kugusa kusanyiko lote. 7. Mhubiri anapaswa kuhubiri kwa upendo. 8. Mhubiri azingatie ratiba ya tukio. ZOEZI. 1. Chagua tukio mojawapo na kisha andaa mahubiri juu ya tukio hilo na hubiri kwa dakika 10 .2. Taja mabo mengine kumi ya kuzingatia katika mahubiri ya matukio. 3.Eleza ubora na udhaifu wa mahubiri ya matukio. MADA YA NNE MHUBIRI. Malengo ya mada. • Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi anataweza. • Kueleza maana ya mhubiri kwa mitazamo mbalimbali. • Kuelza wasifu wa mhubiri. • Kueleza vidokezo mbalimbali kuhusu mhubiri. A. Utangulizi. Mahubiri yana mwanzo wake katika Agano la kale. Wakati manabii walipotangaza neno la Mungu kwa watu wa kale. Manabii walikuwa wahubiri wa kwanza katika agano la kale. Mungu ameamua kuwachagua na kuwatumia watu wa kawaida kulitangaza Neno lake.Amewachagua wanawake na wanaume kuwa vyombo vya kulitangaza neno lake kupitia huduma ya kuhubiri. Ufafanuzi Neno mhubiri (kwa kigiriki kerux) limetumika mara kadhaa katika agano jipya ambapo humaanisha kutangaza. (Rumi 10:14, 1Tim 2:7, 2Tim 1:11, 2Pet 2:5. Unapolitazama neno hili (mhubiri) halijikiti na kuishia kwenye huduma moja au huduma fulani tu bali linahusisha zile huduma zote tano za uongozi wa kanisa. Ikijumuisha mitume, manabii waijilisti,wachungaji na waalimu. Pia linajumuisha kila mtu atangazae neno la Mungu. Hata kama hana mojawapo ya zile huduma tano za uongozi. Ingawa hudma zote hizi zinawasifu wake kila moja lakini zote zaangukia katika neno moja “Mhubiri”. Inavutia kutambua kwamba neno la Kigiriki lililotafsiriwa kama mhubiri linaelezea mtu anaeongea kwa mamlaka , anaewasilisha ujumbe bila kikwazo au kizuizi chochote. Hii hudhihirisha mamlaka iliyo juu ya mhubiri. Mhubiri ni mtu yeyote anayehubiri Injili. • Mhubiri ni mtu anayetumiwa na Roho mtakatifu katika kuwasilisha kweli za ki-Mungu kwa njia ya hotuba. • Mhubiri ni mtangaza ujumbe wa Mungu. • Yeye ni msemaji wa Mungu. Husimama katika nafasi ya Mungu na kuzungumza kwa niaba yake Mungu. Hivyo ni lazima mhubiri awa na sifa zinazostahili ambazo zitamfanya kuwa na mamlaka. B.Sifa za mhubiri. Mhubiri ni lazima awe na sifa stahilifu ambazo zitamfanya awe na mamlaka na thabiti katika wito na huduma yake. Badhi ya sifa hizo zimeorodheshwa hapa chini. 1. Awe ameokoka (Amezaliwa mara ya pili). 2. Awe amejazwa Roho mtakatifu. 3. Awe na wito halisi (Wito ulio wazi na wenye ushahidi). 4. Ajazwe na Neno la Kristo ndani yake Kol 3:16. 5. Awe mtu wa maombi. 6. Awe mwadilifu.( Mkweli na mchaji Mungu na mwenye kuchukia mapatato ya udhalimu ) 7. Awe na nidhamu. 8. Aishi kulingana na wito wake. 9. Asiwe mvivu. 10. Awe na baba wa kiroho. Kuna tofauti kubwa kati ya hotuba na ujumbe.mtu anaweza kujifunza jinsi ya kuandaa hotuba kupitia masomo ya Homiletics lakini Mtu anapaswa kuwa na ushirika na Mungu ili aweze C. Kujihusisha binafsi katika kuhubiri. 1. Unapaswa kuwa kawaida. Unatakiwa kutulia na kuwa vile ulivyo. Mugu hutaka kutumia utu wa kila Mhubiri katika kuwasilisha Neno lake. Unatakiwa kujikubali hivyohivyo ulivyo. Mungu anapendezwa nawe na ndiyo maana amekuita hivyo ulivyo. Usijichambue sana. 2. Kuwa wa kipekee. Unatakiwa kuutayarisha ujumbe wako na kuuwasilisha kwa njia ya kipekee ili uweze kuleta matokeo ya kipekee. Unapasa kutumia utu wako wa kipekee Mungu aliokupa na kumwacha Mungu atumie utu na maisha yako kwa njia maalum ya kipekee anayotaka yeye. 3. Kuwa rahisi. Unapokuwa ndiyo unaanza kuhubiri au kusimama mimbarini kwa mara ya kwanza unatakiwa usijaribu kutumia ufasaha au kuingia ndani mno katika kuhubiri. Huhitaji kuwavuta watu. Upo pale kwa lengo la kuwahudumia na si kuwapendeza. 4. Kuwa huru. Unatakiwa kuwa huru unapohubiri na ujifunze kujizoeza hali mbalimbali. Ufanye mtindo wako wa mawasiliano utiririke kawaida na kwa uhuru. Kila kusanyiko utakalo hubiri linatofautiana na lingine, hivyo unapaswa kujizoeza hali mbalimbali. Mungu huwa na lengo maalumu analotaka kufanikisha katika kila ibada na mhubiri ndiyo ufunguo muhimu katika kutekeleza hili. Kuwa huru na msikivu kwa Roho mtakatifu.Roho mtakatifu anaweza kufanya hali za jinsi mbalimbali katika kila ibada.Wasikilizaji wako wakati mwingine waweza kuwa wachangamfu na wakati mwingine wakimya na wanyenyekevu. 5. Tambua njia ambayo Mungu anapitia na utembee nae. 6. Dhihilisha mamlaka..Hakikisha Kuna madhihirisho ya nguvu za Mungu katika kila ibada unayohubiri. Hakikisha Bwana anakithibitisha kila unachokihubiri kwa ishara na maajabu. Hubiri kwa uthibitisho D. Zana za mhubiri. Kuna vitu kadhaa ambavyo ni muhimu kwa mhubiri yoyote . Bila vitu hivo kazi ya Kuhubiri itakuwa haijafanikiwa au kufika lengo kwani wasikilizaji watakuwa wameachwa njiani. Baadhi ya zana hizo ni: I. Maono. Kila mhubiri nilazima awe na maono katika huduma yake na wito wake. Wazo la kile ambacho huduma yako itafanikisha kwa Mungu. Maono ni picha au taswira juu ya kile unachohitaji kukifikia katika huduma yako. Kumbuka kwamba bila maono watu huangamia Mit 29:18. Ni maono pekee yatakayokuweka salama. Usipokuwa na ufahamu wa kuhusu kusudi la Mungu alilonalo kwaajili yako ,waweza kulemewa na kuishia n jiani na kushindwa kufikia lengo la –ki-Mungu ulilochaguliwa kwalo. II.Msamiati. Msmiati ni jumla ya maneno yaliyo katika lugha fulani. Msamiati wamhubiri hujumuisha maneno yote anayoyajua na kuyazoea kuyatamka. Maneno ni dhana ambayo mhubiri hutumia katika kutimiza wito wake. Muhubiri anatakiwa kuwa mahili wa lugha. Jifunze msamiati mbalimbali na matumizi yake.Silaha yetu kuu ni maneno katika kazi ya kuhubiri. Maneno huundwa na msamiati. Soma vitabu mbalimbali ili uweze kujitajirisha na msamiati. Unapokutana na neno usilolifahamu lichunguze na kutafutamaana yake na matumizi yake. Pia mhubiri anatakiwa afahamu kutumia msamiati mbalimbali katika kazi yake ya kuhubiri. Tambua matumizi ya Lugha kulingana na mahali. Jifunze misimu, Rejesta na misemo mbalimbali inayotumika katika Lugha husika. Hii itakusaidia unapohubiri uweze kuwagusa watu wote waliopo katika eneo hilo. Mhubiri ni lazima ajifunze namna ya kutamka maneno sahihi. Jifunze kutumia lafuzi vizuri na kuepuka athali za lugha mama katika Lugha unayotumia kuhubiri. Kuwa na lafuzi nzuri na kuongea lugha kwa ufasaha hukupa kukubalika kwa wasikilizaji wako na kupewa usikivu. Tumia Lugha inayoeleweka na wasililizaji wako, lakini lugha hiyo yapaswa kuwa sanifu au fasaha III. Sauti. Sauti ndiyo chombo kikuu mhubiri anachotumia katika kuhubiri. Ni lazima mhubiri kujifunza mitindo mbalimbali ya sauti na namna ya kuitumia sauti yake. Jifunze matumizi ya sauti katika mahubiri yako. Sauti yako inapaswa kusikika na wasikilizaji wako lakini haipaswi kuwa kubwa sana kiasi cha kuwaumiza. Fahamu mahali pa kutumia asuti kidogo na mahali pa kuongeza sauti. Hubiri kwa mitindo mbalimbali ya sauti. Zingatia kiimbo, toni na kidatu unapohubiri. E. Kanuni za Kuhubiri Katika kipengere hiki tutaajadili baadhi ya kanuni chache za kuzingaita katika mahubiri ya hadharani. Mhubiri anapswa kufuata na kuzingatia kanuni hizi ili aweze kufanikisha lengo la mahubiri 1. Kuvuta hewa. Kuvutahewa sahihi ni muhimu kwa mhubiri. • Vuta hewa nyingi kiasi cha kufika mapafuni. • Jizoeze kujaza hewa kifuani na kwenye mapafu. • Izuie na kisha itoe nje polepole.Dhibiti utoaji wa hewa. Iache hewa itoke chini ya mapafu kupitia sanduku la sauti na kugusa ukuta wa juu wa mdomo. • Jifunze jinsi ya kupumua ili usiishiwe pumzi wakati wa kuhubiri. 2. Utamkaji mzuri wa maneno. Jitahidi kutamka maneno vizuri na waziwazi. Hakikisha kila neno unalolitamka linasikika vizuri kwa wasikilizaji wako. Usilete kikwazo kwa wasikilizaji wako kwa kutosikika vizuri. 3. Ubadilishaji wa sauti. Hii inahusu kuifanya sauti kuwa nene au nyembamba. Sauti ya kila mwanadamu inahali mbalimbali. Jitahidi kutumia aina mbalimbali za sauti. Ukitumia aina moja ya sauti yaweza kuwachosha wasikilizaji wako. Tambua maeneo unayotakiwa kuongea kwa sauti ya chini na sauti ya juu. Endeleza viwango tofauti vya sauti yako. Ubadilishaji wa ukubwa wa sauti waweza kusisitiza kipengere fulani muhimu. Baadhi ya wahubiri huona ni muhimu sana kuhubiri kwa sauti kubwa sana kiasi chakuumiza masikio ya wasikilizaji . Jaribu kuepuka hili. Iwapo ujumbe wako wote utawasilishwa kwa sauti kubwa au ya juu itakuwa vigumu kusisitiza jambo maalum katika zile sehemu ambazo ni za maana zaidi. 4. Kasi ya kuongea. Kasi unayotumia kuongea ni muhimu sana katika mahubiri. Baadhi ya wahubiri huhubiri kwa kasi moja tu . hii si nzuri, pia yaweza kuwachosha wasikilizaji. Sehemu kubwa ya ujumbe wako yapaswa kuwasilishwa kwa mwendo na kasi ya kawaida ya mazungumzo. Katika maeneo mbalimbali ni lazima kuongeza au kupunguza mwendo ilikuleta tofauti na msisitizo zaidi katika mahubiri yako. 5. Kupumzika kidogo. Usiongee mfululizo bila kuwa na vituo. Kupumzika kidogo wakati wa kuongea au kuhubiri ni muhimu pia kwaweza kuongeza msisitizo kwenye maeneo ya muhimu. Kuongea mfululizo kwaweza kusababisha wasikilizaji washindwe kusharabu mambo ya muhimu katika akili zao. Usipitie ujumbe kwa kukimbia na kuongea kwa haraka bila kuvuta pumzi. Hadhira wanahitaji muda wa kufikiri na kuchambua kile ulichosema, Hii inasaidia sana kusharabu ukweli wa ujumbe wako. Unahitaji kuzifahamisha akili pamoja na kuzichangamsha hisia za hadhira. Kama ukihubiri kwa haraka tu bila kupumzika utawaacha hadhira wako nyuma. 6. Kurudia. Kurudia sehemu za msingi wakati unahubiri ni jambo la msingi sana. Inasaidia kusisitiza vipengere na kushindilia kwenye akili za wasikilizaji. Unatakiwa kukielezea kipengere kwa njia mbalimbali. Usisite kurudia eneo unalohisi wasikilizaji wako hawajakuelewa vizuri. F.Vidokezo muhimu kwa mhubiri. 1. Uwe vile ulivyo.Usijaribu kutokeza sura ambayo si ya kweli. Kuwa vile ulivyo ndiyo njia pekee inayoweza kukufanya utulie.usijaribu kumwiga mhubiri mwingine yeyote ukifanya hivi itakusababishia kutoaminika kwa hadhira wako.Jitahidi kuwa mhubiri bora na si kuwa mhubiri mkuu. 2. Usijenge sauti ya kidini. Baadhi ya wahubiri wamejiundia sauti za mimbarini ambazo ni tofauti na sauti zao za kawaida.Hii huleta kutokuaminika na kuonesha kana kwamba unamwiga mtu mwingine. Jizoeze kuhubiri kwa kutumia sauti ya kawaida na unayotumia katika mawasiliano katika maisha ya kila siku. Hii huonesha ukweli na uaminifu katika mahubiri. 3. Usiongee kwa sauti ndogo mno. Hakikisha kwamba kila mmoja katika mkutano wako anakusikiliza vema. Usifanye wachoke kwa sababu ya kutokukusikia vizuri. Ikibidi uliza je kila mmoja ananisikia vizuri ? Si vizuri kuendelea kuhubiri na hali kuna baadhi ya watu hawakusikilizi. 4. Usipige kelele. Jitahidi kuongea kwa sauti ya kawaida ya maongezi ambayo inaweza kuongezwa kiasi kufuatana na wingi wa makutano na kama huna au una vyombo vya kupazia sauti. Sauti iongezwa kulingana wingi wa hadhira. 5. Kumbuka kubadili kasi na upeo wa sauti ya mahubiri kukwepa kuchosha hadhira. 6. Ufanye mkutano ukukubali. Pata matumaini ya hadhira.Hakikisha mkutano wako unakukubali.. Kama mkutano wako hawakukubali nidhahiri kabisa kwamba hawataupokea ujumbe wako. 7. Vaa vizuri. Ni jambo la maana sana kwa mhubiri kuvaa mavazi ya heshima na safi. Namna ulivyo vaa yaweza kuharibu ujumbe wako.Hakikisha uvaaji wako hauvurugi ujumbe wako. Vaa kulingana na tamaduni za taifa husika. 8. Jifunze kusimama vizuri. Ni vizuri sana kusimama wakati unazungumza au kuhubiri. Simama vizuri kwa miguu yote miwili.. Simama wima ukitazamana na hadhira wako. Usipende kuegemea kitu chochote. Kama kuna mimbari itumie kuwekea Biblia na zana zako za kuhubiria. Kusimama wima kutakusadia katika kuvuta hewa. Watazame hadhira wako wakati wote unapohubiri. Hubiri kwa kumgusa kila mtu. Kila mtu ajione kwamba unaongea na yeye binafsi. 9. Jifunze kutembea wakati unahubiri. Usisimame mahali pamoja kana kwamba umefungwa.Jizoeze kutembeatembea wakati unahubiri. Mwili wako unaleta ujumbe sawaswa na sauti yako.Tumia ishara wakati unahubiri lakini epuka ishara sisizo na umuhimu. Kama unaeleza juu ya kitu fulani ni kawaida kuelezea jambo hilo kwa mikono yako. Ishara za namna hiyo zinapaswa kutokea zenyewe kiasili bila kuzilazimisha. 10. Endeleza uhuisano na hadhira. Macho ya mhubiri huelezea ujumbe pia. Usiangalie hewani au juu ya vichwa vya watu. Waangalie watu unaowahubiri moja kwa moja. Kila mmoja atambue kwamba unamwangalia yeye binafsi. 11. Jifunze kutawala mkutano. Hakikisha unatawala kusanyiko. Watu wote wako pale kukusikiliza wewe hakikisha kila mmoja anakusikia. Zungukia watu wako nakuwashitua wanao lala au kusinzia. Tafuta namna itakayosababisha watu wote kukusiliza kwa makini. 12. Omba upako wa Roho mtakatifu. Mwombe Mungu akupake mafuta daima. Hakikisha utendaji wa Roho mtakatifu upo katika mahubiri yako. F. Matumizi ya muda katika mahubiri. Ni lazima mhubiri ajifunze matumizi sahihi ya muda katika mahubiri. Jambo hili ni la muhimu sana na lisipozingatiwa huweza kuvuruga kazi nzima ya kuhubiri. Ni lazima kuamua muda utako tumia kuhubiri kabla ya kupanda mimbarini. Utafiti kule Marekani umeonesha kwamba watu huanza kupoteza usikivu wao baada ya dakika ishirini tu za mahubiri. Waweza usikubaliane na matokeo ya utafiti huo lakini unatakiwa kukumbuka kwamba akili ya mwanadamu inakiwango cha kuelwa na muda wa kuelewa. Muda ukizidi kila kinachoongelewa au kuhubiriwa huwa hakisharabiwi kwani akili hufikia upeo wa kuelewa na kushika mambo. Upako wa Roho Mtakatifu huhuisha akili za wasikilizaji kwa kiwango fulani lakini mhubiri aepuke kuwachosha wasikilizaji. Ni vizuri sana kumaliza ujumbe wako wakati watu wanatamani uendelee na ni vibaya sana kumaliza ujumbe wako wakati watu wanataka umalize. Jitahidi kuzingatia muda katika kazi yako ya kuhubiri. Kwa kawaida ujumbe unapaswa kutumia dakika arobaini na tano. Utangulizi uwe na dakika tatu hadi tano, Kiini kiwe na dakika ishirini na tanno hadi therathini. Hitimisho liwe na kakika tatu hadi tano. Ujumbe wote usizidi dakika arobaini Vinginevyo utawaacha wasikilizaji wako. Ukitaka kuhubiri kwa muda mrefu hakikisha ujumbe wako unauvuvio mwingi. Spurgeon alisema” tumia muda mwingi katika matayarisho ili uweze kutumia muda mchache katika kuhubiri” Kutumia muda mrefu katika kuhubiri hakukufanyi ueleweke zaidi wala hakufanikishi zaidi lengo la kuhubiri. Tambua cha kusema. Kiseme na kisha maliza. Unapokuwa umealikwa na mhubiri mwingine kuhubiri unapaswa kumuuliza muda ambao yeye hutumia katika kuhubiri na muda wa kumaliza mahubiri. Unapokuwa unahubiri zingati muda ulioelekezwa na mwenyeji wako na uwezo wa kuelewa wa wasikilizaji wako. Mgeni akija kanisani kwako kama hukumwandaa kuhubiri kabla si vizuri kumpa madhabahu ili ahubiri. Kwani kuhubiri ni kazi nyeti sana na inahitaji maandalizi ya kutosha. Maelezo haya hayazuii mwongozo na maelekezo ya Roho mtakatifu. Lakini ni vizuri kumwandaa mhubiri mapema ili awe na muda wa kuafanya maandalizi. Usiwashitukize watu kuhubiri. Ni lazima uwe na heshima kwa kazi hii kwani Mungu mwenyewe anaiheshimu sana. Usihubiri ujmube au somo ambalo mwenyeji wako hakubaliani nalo. Kama kuna ulazima fanya nae mazungumzo kabla ya kuhubiri au tafuta namna utakayotumia kuhubiri na kufanya akubaliane na kile unachohubiri. Jambo hili ni muhimu sana na linapaswa kuzingatiwa. Mahubiri na mazingira. Mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyopatikana na kuzunguka eneo fulani. Mazingira ni muhimu sana katika kufanikisha kazi ya kuhubiri. Ni lazima mazingira yawe safi hasa ikiwa mahubri yatafanywa katika eneo fulani maalum. Mfano kanisani, uanjani au eneo lolote rasmi. Kuna baadhi ya mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa. Baadhi ya mambo hayo yameorodheshwa hapa chini. 1. Watu wanaokuja kwa kuchelewa wakae katika viti vya nyuma. 2. Mimbari inapaswa kuwekwa mahali sahihi panapoonekana na watu wote bila shida. 3. Lango la kuingilia lapaswa kuwa mahali sahihi. 4. Akina mamawenye watoto wadogo wakae eno maalumu. 5. Watoto wanapaswakutengewa sehemu yao ya kukaa kama hakuna kanisa la watoto. 6. Mwanga na hewa ya kutosha ni kitu muhimu sana katka eneo lolote. G. Jaribu kuu la Mhubiri. Wahubiri wengi hujisulisha na kutafuta chakula kwajili ya watu wengine na kujisahau wenyewe. Huu ni mtego mkubwa katika kazi ya kuhubiri na ni moja ya hatari za huduma. Wakati mwingine mhubiri aweza kujishughulisha sana na kutafuta haki za kiroho za kundi lake na kwa masikitiko makubwa anasahau zile za kwake mwenyewe. Hii ni moja ya sababu kuu zinazomfanya mhubiri kushindwa. Sulemani anasema katika kitabu cha Wimbo ulio bora “”’ Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu bali shamba langu mwenyewe sikulilinda” Mhubiri ni lazima ajali kwanzai maisha yake mwenyewe ya kiroho. Mhubiri anapaswa kulipa neno la Mungu nafasi ya kuchipua ndani ya moyo na roho yake. Aliache likue kwa nguvu katika maisha na ujuzi wake. Halafu atakapohubiri atahudumu kutokana na ujuzi. Hataongea kamwe kama mwenye nadharia bali atashirikisha vitu ambavyo yeye mwenyewe anavielewa kikamilifu na ana ujuzi navyo. Paulo anasema hivi. “Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza kupata fungu la matunda”. ( 2Tim 2:6 ). Hii inatufundisha kwamba unachopanda na kuvuna ( kiroho) yapasa ule (ujuzi)- kabla ya kulisha wengine. Huwezi kulisha wengine kile ambacho wewe mweyewe hujakila kwanza. Huwezi kujaribu kuongoza wengine katika njia na mapito ambayo wewe mwenyewe hujapitia. Jinsi Neno la Mungu linavyokuwa dhahiri katika maneno yako ndivyo wewe unafanyika ujumbe toka kwa Mungu. Hutakuwa mtu anaye kariri somo tu bali mtu ambaye uhai wake binafsi na mtindo wake wa maisha huhudumia uhai, Baraka na nguvu kwa wale wanaomfahamu na kumsikia. I.Hitimisho. Mahubiri mazuri hayaji kirahisi wala hayatokei tu. Ni matokeo ya vitu vingi. Kama tulivyotazama huko nyuma kwamba mahubiri huanza na wito wa mhubiri na wasifu wake.Pia huhusisha maandalizi ya kutosha kwa kuomba na kusoma kwa bidii. Kilele cha mahubiri ni katika kuwasilisha ujumbe. Ujumbe hauwi ujumbe mpaka umewasilishwa. Ujumbe ulioandaliwa vema utakuwa ujumbe wa kiungu pale Roho mtakatifu atakpoupaka mafuta. Mahubi mazuri daima yataleta matokeo mazuri. Mahubiri mazuri dama yatamtukuza Mungu na si mhubiri au mtu mwingine yeyote. Yatawaongozawatu msalabani na kuwafanya kuwa wanafunzi. Angalizo.Mhubiri hapaswi kutwaa utukufu kwa namna yoyote ile katika kila inachotokea katika kazi yake ya kuhubiri. Daima anapaswa kumpa Mungu heshima na utukufu kwa kila kinachotokea.