HOMILETICS.
MADA YA KWANZA. MAHUBIRI.
Malengo
ya mada.
Baada
ya kumaliza mada hii mwanafunzi ataweza.
§ Kueleza
maana yamahubiri.
§ Kueleza
maana ya kuhubiri.
§ Kueleza
wito wa kuhubiri ulivyo.
§ Kueleza
umuhimu wa kujifunza homiletics.
A. UTANGULIZI
Katika kozi hii tutashughulikia
mojawapo ya kazi kuu ya kanisa.
Mojawapo
ya wajibu mkuu ambao umewekwa mikononi mwa kanisa ni kuhubiri ujumbe wa Mungu yaani Injili. 1Kor 1:21
a) Ni
amri iliyo wazi toka kwa Bwana Yesu kwa wafuasi wake. Mk 16:15.
“Enendeni ulimwenguni mwote
mkaihibiri Injili kwa kila kiumbe”.
b) Kuhubiri
ni mojawapo ya kazi ya thamani sana ambayo
Mungu ametupa. Kuwa msemaji wa Mungu, yaani Mjumbe wa Kristo. 2Kor 5:20.
c) Kuhubiri
ni wajibu mkuu. Rumi 10:14-15.
d) K
wa njia ya mahubiri Mungu alichagua
kujidhihirisha mwenyewe kwa mwanadamu.
B. MAANA YA MAHUBIRI.
Neno mahubiri linatokana na maneno
mawili ya kigiriki ambayo ni homileo na homilia yenye maana ya ‘kuwa pamoja na,
kuongea na kuwasiliana.
a)
Homily pia humaanisha ujumbe au hotuba.
b)
Elimu inayohusu namna ya kuhubiri huitwa
Homileticts.
c)
Homiletics
ni ustadi wa kuhutubia au kuhubiri.
d)
Mtaalamu wa elimu ya kuhuri huitwa Homilist
e) Homiletics
huhusisha kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri au kutunga
hotuba.
f) Mahubiri
huhusu kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri masomo ya
Biblia.
g) Mahubiri
ni ujuzi wa kuhubiri.
h) Ni
elimu au taaluma inayohusu kuhubiri Neno la Mungu.
i)
Ni elimu inayohusu namna ya kuhubiri.{
somo juu ya kila kitu kinachohusiana na kuhubiri}.
j)
Kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu. Mungu hutumia watu wake
aliowachagua kuhubiri ujumbe wake.
k) Ujumbe
unapaswa kuwa ujumbe wa Mungu Kitu kingine chochote na ujum
si mahubiri ila ni maoni na falsafa
za kibinadamu tu.
l)
Kuhubiri ni lazima kuwe ni kutangaza binafsi na si kusoma au kuandika
a) Dr. Martyn Lolyoyd Jones
alisema “ Wahubiri huzaliwa na
hawafanywi kamwe. Kamwe hutamfundisha mtu kuwa mhubiri kama yeye si muhubiri.
Lakini muhubiri wa kuzaliwa unaweza kumsaidia na kumwendeleza akawa mhubiri
bora kwa njia ya mafunzo”
b) -Mhubiri
si chanzo cha ujumbe.Mungu ndiye chanzo cha ujumbe na mhubiri ni bomba au
mfereji ambako Mungu hupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu aliowakusudia.
Ujumbe wa Mugu hutiririka kupitia utu wa
mhubiri.
c) -Ujumbe
unapaswa kutiririka kwa uhuru toka kwenye chanzo chake (Mungu) kwenda kwa wakusudiwa
yaani hadhira au wasikilizaji.
d) Mahubiri
ni zao la mambo mawili ambayo ni Mungu
na mhubiri.Mahubiri mazuri huzaliwa kutokana na ushirikiano mzuri (umoja) na
ushirika mzuri kati ya Mungu na mhubiri.
Hivyo
kuna vipengele viwili vya wazi katika mahubiri S cha kwanza ni kile cha ki
Mungu na cha pili ni kile cha kibinadamu.
Kwa
sababu ya wito wake mkuu mhubiri anapaswa kuwa mwaminifu na awe na ufahamu wa kutosha juu ya Neno la Mungu.
C.
MAANA YA KUHUBIRI.
Mahubiri
yana lengo mahususi katika mpango wa Mungu.
Ni njia mabayo kwayo Mungu
ameamua kuwafikia waliopotea dhambini na kuwaimarisha waamini.Kkwa sababu
mahubiri ni njia ya mungu kuwafikia
wanadamu tutatazama maana ya kuhubiri kwa mitazamo mbalimbali kama ilivyo
ainishwa na wataalamu wa masomo ya homiletics.
1.Kuhubiri ni kuielezea imani.
Mojawapo
ya malengo ya mahubiri ni kuelezea au kutangaza kweli za maandiko matakatifu.
Kila hotuba au ujumbe wapaswa kuwasilisha kweli za maandiko kwa njia
itakayowezesha hadhira kupata uelewa zaidi ju ya maandiko matakatifu.Kuhubiri
husababisha imani kuumbika kwa wasikilizaji wako. Hubiri kwa kukuza imani na
kuielezea imani katika mwana wa Mungu.
II. Kuhubiri ni kuitetea imani.
Haitoshi
kuelezea ukweli wa Mungu bali tunapaswa kuutetea. Shetani, ulimwngu na maadui
wa imani huvamia na kupotosha kweli za neno la Mungu. Hivyo ni lazima kwa
mhubiri yoyote kuwa tayari kuitete imani ya kweli kwa njia ya kuhubiri kweli za
ki-Biblia. Kuna wahubiri wengi wa uongo ambao kazi yao ni kuposha kwali za
maandiko matakatifi. Ni jukumu la kila mhubiri wa kweli kuhakikisha anasimama
imara katika kuitetea imani ya kweli.
III.Kuhubiri ni kuinjilisha.
Wajibu
mkubwa wa Mhubiri ni kuitangaza injili kwa watu waliopotea dhambini. Ni lazima
watu wote waliopotea wapelekewe injili ili wapte kutambua hali yao ya kupotea na kuongozwa kwenye
wokovu wa Yesu Kristo.
IV. Kuhubiri ni kukemea dhambi.
Kama
ukichunguza hotuba za agano jipya utagundua kwaqmba hakuna mubiri hata mmoja
aliyesita kukemea dhambi.mfano Yesu, Yohana, Paulo, Petro n.k wote walikemea
dhambi kwa nguvu zo katika kila mahubiri. Mhubiri nilazima akemee dhambi kila
mara kwani Mhubiri ni kinywa cha Mungu. Kemea dhambi bila kuogopa chochote .
V. Kuhubiri ni kuhamasisha waamini.
Mahubiri
hutakiwa kuwasaidia wakristo kukua katika neema ya Mungu. Pamoja na kuonya na
kukemea dhambi mahubiri hutakiwa kuwahamasisha na kuwawezesha waaamini kukua
kiroho na kufikia kimo cha Kristo.
VI. Kuhubiri ni kufikia mahitaji ya
hadhira.
Mahubiri
yatakuwa yameafanikiwa kama yatakuwa yamepokelewa na kukutana na mahitaji ya
waikilizaji. Mhubiri kwa uangalifu anatakiwa kujiweka katika daraja sawa na
wasikilizaji. Anatakiwa kujitahidi kuhakikisha unapokelewa na makutano na
kukutana na mahitaji yao.
VII.Kuhubiri ni kudhihirisha uweza
wa Mungu. Bwana Yesu aliahidi kuwa na wahubiri kwa kulithibitisha neno kwa
ishara na maajabu. Popote injili inapohubiriwa ni sharti Bwana awepo
akiithibitisha
kwa isharaMk 16:15,20. 1Kor 2:4
D. WITO WA KUHUBIRI
Sehemu ya muhimu sana katika kuhubiri ni
wito. Kimsingi wito ni wa mtu binafsi Mungu huwaita watu katika huduma na watu
hupokea hilo rohoni mwao kisha huja
uthibitisho wa nje kupitia kanisa au watumishi mbalimbali na fursa mbalimbali.
Mungu Huwaita watu wake katika nafasi na huduma mbalimbali. Wengine kuwa
wachungaji, wamishenari, wazee wa kanisani, wainjilisti, au huduma nyinginezo.
Kazi ya kuhubiri si ajira ambayo mtu
anakwenda chuoni kusoma kwa lengo la kupata baada ya kuhitimu masomo yake, bali ni mwito
mtakatifu ambao mtu huitwa na Mungu mwenyewe kuwa muhubiri.
Mtu huenda chuoni ili kupata maarifa yatakayomwezesha na kumsaidia
katika kutimiza mwito wa Mungu uliondani yake. Haendi chuoni kupata mwito bali
wito husababisha mtu kwenda chuoni kama
sehemu ya maandalio.
Hivyo wito usichanganywe na ajira na
maslahi binafsi ya mtu. Ni lazima wito uheshimiwe na kuogopwa. Waamini
hawapaswi kujihusisha na huduma kwa lengo la kujinufaisha na kujipatia mali kwa
njia za ujanja ujanja.
Kimsingi
kila mwamini ni muhubiri kwani agizo kuu linamhusu kila mwamini. Kila mwamini
anapaswa kujihusisha na kupeleka injili kwa watu waliopotea dhambini hili ni
agazo la jumla.
Lakini
kuna watu maalum ambao Bwana ameweka
wito wa muda wote(Full time commitement) ndani yao. Amewachagua kwa kusudi hili
katika maisha yao na muda wao wote. Hawa wanasimama katika zile huduma tano za
uonozi katika kanisa, ambao ni mitume,
manabii, wainjilisti, wachungaji
na waalimu. Hawa ndio Bwana amewaweka kusimama katika kazi ya kuhubiri ya muda
wote, Wao hawapaswi kujihusisha na shughuli zingine bali kazi yao ni
kulihudumia Neno na kuomba yaani Kuhubiri. Bwana ameweka mwito mtakatifu ndani
yao ambao ni wajibu mkuu na wa kuogofyapia{.Mdo6:2,4} hili ni agizo mahususi.
Wito
huu haupatikani kwa njia ya kusoma au kwa njia ya ulaghai bali kwa kuitwa na
Mungu mwenyewe kuwa msemaji wake. Kuna baadhi ya makanisa ambayo yameufanya
wito wa Mungu kuwa ni ajira. Kwani wao huwapeleka watu kwenda chuoni kusomea
huduma fulani mfano uinjilisti, uchungaji nakadharika kwao wito si jambo la
msingi ila elimu ndiyo yenye kupewa
kipaumbele. Wao humpa mtu kushika nafasi
ya huduma baada ya kuhitimu mafunzoya chuo cha Biblia bila kujali kama ana wito
au la.
Matokeo
yake ni kwamba makanisa yamekuwa yakiongozwa na kuhudumiwa na watu wasio na
wito wenye kutegemea elimu ya darasani tu, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo
na uhai wa kanisa.
Elimu
ni jambo la zuri sana lakini elimu haiwezi kuchukua nafasi ya wito katika
kanisa la Mungu ikiwa tunataka kufikia kusudi la Mungu la mwito mtakatifu na
kusimama kiuaminifu mbele zake kupata ushindi mkuu.
Usiwe
mtumwa wa elimu. Elimu hii unayopata
ikusaidie katika kumtumikia Mungu na kufanya huduma lakini isichukue nafasi ya
Roho mtakatifu katika maisha yako na huduma yako. Wala haipaswi kuwa badala ya
Roho mtakatifu.
Usiongozwe
na elimu bali ongozwa na Roho mtkatifu.
Usihubiri
kwa maneno yenye hekima pekee kwa lengo la kushawishi akili za watu bali hubiri Kwa dalili za Roho mtakatifu na nguvu. 1Kor 2:4.
Hakikisha
unautumikia wito ambao Mungu ameweka ndani yako kwa gharama yoyte ile bila
kujali mazingira au kitu kingine chochote.
Kwa
hiyo wito wa kuhubiri hautoki kwa
mwanadamu yoyote Yule bali toka kwa Mungu mwenyewe. Mungu huwafanya watu wake
kuwa wahubiri.
Jiulize
wewe ni mhubiri wa kufanywa na nani ?
Kweli kuu kuhusu
wito wa kuwa mhubiri.
1.
Roho mtakatifu huweka wito ndani ya mtu.
Wito wa Mungu huja juu ya mtu kupitia Roho
mtakatifu. Katika akili ya kawida ni kazi kubwa kuhubiri au kutumika. Wito huja
kwa watu wa aina zote na umri wote wowote. Baahi ya watu husikia wito na
kujitoa wangali wadogo lakini wengine katika umri mkubwa n.k
2. Shauku ya kutimiza wito.
Watu
wanaoitwa kuwa wahubiri waliumbwa na Mungu kwa kusudi hiloYer1:4-10
Hawawezi
kupata utoshelevu kwa kufanya kitu kingine chochote. Hawawezi kupinga
kujihusisha katika huduma au kuchukua fursaza kuhubiri. hHata kama hakuna nafai
za kutumika moja kwa moja bado
watatafuta nafasi katika huduma yoyote inayojitokeza.
3. Mungu huwaandaa wale anaowaita
kwajili ya huduma.
Mungu
hawaiti watu ambao hwana uwezo wa kutimiza mwito wake. Wahubiri wengi
wanakipaji cha kuongea. Watu wenye wito juu ya watoto hupewa hupewa Mungu huwaandaa kwa kuwapa uwezo kwa
kufanya huduma na watoto n na wanaoitwa kuwa wacghungaji huqwezeshwa kuwa
wachungaji. Popotye na kwa namna yoyte Mungu huwaandaa na kutoas nguvu ya
uwezesho juuv yao.
4. Wito wa Mungu wapaswakuwa wazi.
Wito
wa Mungu usifichwe. Wito wa Mungu ulioju yako wapaswa kuwa wazi kwa watu
wangine lakini haupaswi kukimbilia kwenye wito huo mara moja. Hutakuwa na
furaha na mafanikio na wito huo mpaka utakopokuwa umejisalimisha kwa mapenzi
sahihi ya Mungu juu yako.
5.
Wito wa Mungu ni wito wa matayarisho.
Kuna wajibu mwingi na mkubwa ambao huja
pamoja na wito wa kuhubiri .Mungu akisha mwita mtu humuandaa kwanza kabla ya
kumtuma na kumwachilia kwnye huduma aliyomuitia. Mhubiri anapaswa kujiimalisha
kiroho na kimwenendo.Anatakiwa ajiandae kiakili kwa kusoma na kupata mafunzo.
Pia anapaswa kujiandaa kimatendo kwa kunuo vipawa vilivyondani yake na
kuyatisha maisha yake yote kulingana na wito ulio ndani ya
E.Umhuhimu wa kujifunza somo hili la homiletics.
a) Linatusaidia
kujua mbinu mbalimbali za kuhubiri.
b) Linatusaidia
jinsi ya kuhubiri bila kuwachosha watu.
c) Linatufanya
kuwa na ujasiri tunapohubiri.
d) Linatusaidia
kuhubiri kwa usahhi.
e) Linatusaidia
kutambua mahubiri ya uongo.
f) Linatusaidia
kujua nakuheshimu wito tulio nao.
g) Linatusaidia
kujua kusudi la Mungu la mahubiri.
Zoezi.
Jibu
maswali fafuatayo. Wanafunzi waweza kujibu katika makundi au mmoja mmoja kama
kazi ya nyumbani kwa kadri mwalimu atakavyoona inafaa.
1. eleza maana ya mahubi kwa mitazamo mbalimbali.
2.Eleza vile mahubiri yasivyo.
3. Toa tofauti iliyopo
kati ya mahubiri na kuhubiri.
4. Taja faida tano za
kujifunza somo la kuandaa mahubiri.
5. Tathmini misukumo
mbalimbali inayosababisha watu waingie katika huduma tano za uongozi wa kanisa.
na hali hawana wito.
6.Eleza namna gani mtu
aweza kujua kwamba Mungu anamwita kuingia katika huduma.
7.Eleza umuhimu wa
kindicha maandalizi na matayarisho kabla yam tub kuingia katika huduma ambayo
Mungu anamwita kuifanya.
8. Jadili kauli
inayosema wito wa Mungu ni wito wa matayarisho.
9. jadili usemi
unaosema kwamba Mungu humuanda mtu aliyemwita kabla ya kumwachilia katika
huduma.
10. Jadili mabo ya
msingi kuzingatia katika kipindi cha matayarisho kwajili ya huduma na wito ambao Mungu ameweka ndani yako.
MADA YA TATU: MBINU ZA UTAYARISHAJI WA MAHUBIRI.
Utngulizi
Katika
mada hii tutajadili aina mbalimbaliza utayarishaji wa mahubiri, maeno ya
mahubiri na sehumu za mahubiri au hotuba. Tutapitia kwa undani kla kimojawapo
ili kujifunza jinsi vipengele hivyo jinsi vinavyohusiana na amhubiri
tunavyoweza kuvitumia katika huduma ya kuhubiri na kuandaa mahubiri.
Malengo ya mada.
Baada ya kumaliza kujifunza mada
hii mwanafunzi ataweza.
Kutambua njia na mbinu mbalimbaliza
utayarishaji wa ujmbe au hotuba.
Kuandaa mahubiri kwa kutmia mbinu
mbalimbali.
Kutambua sehemu tatu za mahubiri au
hotuba.
A.
Utayarishaji Wa Somo.
Kuna aina nyingi za utayarishaji wa somo
au hotuba, na kila mojawapo ina umuhimu wake. Lakini katika mada hii
tutajifunza aina tatu za utayarishaji wa somo au hotuba.
Kila mwanafunzi anatakiwa kuelewa aina zota
tatu na anapaswa kujizoeza kutumia njia
hizi zote ili aweze kufaidika zaidi.
1.
SOMO LILILOANDIKWA.
Katika aina hii mhubiri hupaswa kuandika
ila kitu anachokusudia kukihubiri. Wakati mwingine somo lote huandikwa. Kilac eneo la asomo
huchambuliwa kwa undani na kuwekwa katika maandishi. Ujumbe au somo lote
huandikwa kikamilifu kabla ya kuhubiri.
Mhubiri huelezea kwa undani somo lake
anapohubiri likiwa katika maandishi. Mhubiri anapohubiri mara nyingi hupitia
kila kitu alichokiweka katika maandishi.
Faida
za aina mbinu hii.
a) Ujumbe
wote huandaliwa kwa uangalifu mkubwa.
b) Ujumbe
huwasilishwa kwa umakini na uhalisia.
c) Ujumbe
huwa ni wa kitaalam.
d) Mhubiri hujikita katika somo.
Hasara ya mbinu hii.
a)
Somo huwa haliwavutii wasikilizaji.
b)
Utoaji wa ujumbe wa namna hii unaweza
kuwa wa kuchosha usipofanywa kwa uangalifu.
c)
Utayarishaji wake huhitaji muda mwingi.
2.SOMO
LISILOANDIKWA.
Hii ni mbinu ya utayarishaji wa somo
bila kuliandika. Mhubiri huosma vifungu vya maandiko na kivitafakari kwa kina
kisha hukariri vitu vya msingi vilivyo katika ujumbe wake na maandiko
yanayohusika.
Aina hii mara nyingi hutumika
katika kutayarisha na kuhubiri ujumbe wenye uvuvio zaidi. Ujumbe hutiririka
toka rohoni na huwa wa kuvutia mno.
Faidaza
mbinu hii.
a)
Ni rahisi kutmia.
b)
Haihitaji muda mwingi wa matayarisho.
c)
Mhubiri huwa huru kutoa kila kinachokuja
ndani yake maadam kinaendana na ujumbe wa somo.
d)
Huwasisimua wasikilizaji na kuwavutia.
Udhaifu wa mbinu hii.
a) Mhubiri
kutoka nje ya ujumbe wake hasa ikifanywa na mhubiri asiye na uzoefu.
b) Wasikilizaji
waweza kulielewa somo vibaya. (waweza
kuelewa vile somo lisichomaanisha).
c) Somo
kutowajenga wasilizaji na kuishia kusisimua tu akili zao.
d) Somo
kutokuwa na maana halisi na hivyo kutowajenga wasikilizaji.
3.MBINU
YA SKELETONI.
Njia hii huhusisha kuandika maelezo ya
somo au ujumbe kwa kifupi kwa lengo la kufanikisha utunzaji wa kumbukumbu
sahihi juu ya ujumbe au somo.
Kwa maana nyingine ni kwamba mhubiri
hutayarisha muhtasari wa ujumbe au somo.Mhutasari huo huwa kama skeleton ya
somo mfano wa fuvu la binadamu.
Mhubiri huhubiri kwa kutumia skeleton
hiyo. Kazi yake hasa ni kuweka nyama katika skeleton hiyo kwa njia ya mahubiri.
Hivyo anapohubiri huweka nyama katika mahubiri yake ili yawze kuwa kitu kamili
. Mhutasari wa somo huwa kama mifupa ya
ujumbe. Ndiyo mifupa mabayo huleta sura na mategemeo kwa kile mhubiri
anachotamani kusema. Anavyosema anaweka nyama
katika mifupa na kuufanya mwili wa somo lake. Hupanua mawazo yake ambayo
maelezo yake mafupi yamekuza.
Faida
za mbinnu hii.
a)
Mbinu hii humpa mhuburi uhuruzaidi.
b)
Utoaji wa somo huwa wa kuvutia sana.
c)
Somo huwajenga wasikilizaji bila
kuwachosha.
d)
Mhubiri huweza kutoa somo kwqa mtiririko
mzuri na sahihi.
Maeneo ya mahubiri.
Kuna maeneo makuu manne ambyo mahubiri
huhusisha. Mhubiri yoyote ni lazima azingatie maeneo hayo ili aweze kufanikisha
mahubiri yake.
I.Wazo
. Hii huhusu namna ya kupokea kichwa cha
somo au ujmbe. Ni ujuzi unaohusu namna ya kupokea ujumbe toka kwa Mungu. Huhusu
namna ya kuptata wazo la awali na kichwa
cha somo.
Mugu hupanda mbeguya wazo kuhusu somo au
ujumbe siku kadhaa kabla ya mahubiri. Mbegu hiyo kukua kwa njia ya kuitafakari
na maombi zaidi. Kutokana na ujuzi mhubiri aweza kuuujenga uwezo wa kumbua mstari.
Muhubiri hupaswa kuliemneleza na
kulikuza wazo lililopandwa ndai yake kwa njia ya maombi, kutafakari na
kuchunguza zaidi juu ya wazo hilo ili aweze kutayarisha ujumbe.
Pata muda wa utulivu utulie uweponi na
omba nuru zaidi ya ufunuo huo.
II.Muundo.
Muundo huhusisha uchambuzi wa wazo ili kuweza kugundua kweli zilizomo
katika wazo hilo.Baada ya kupokea Wazo toka kwa Mungu unapaswa uanze
kulichambua ili kutambua vitu ambavyo
wazo hilo linavyo.
Katika hatua hii inapaswa kuorodhesha
kwa urahisi kila kitu kilichomo kwenye wazo hilo.Mara nyingi unapokuwa katka
hatua hii unahitaji kuandikwa kwa haraka ili kupata kwa kifupi mtririko wa
uvuvio unaokuja. Hakikisha kwamba unaaandika kila kitu. Ili uweze kuchambua
baadae.
Ujenzi.
Huhusiha kukusaya na kuayaweka mawazo
yako uliyoyachambua katika kipengele cha uchambuzi katika mpango mzuri. Kuweka
kila kitu katika mpangilio mzuri kutakusaidia na kukurahisishia katika utoaji
wa somo lako. Kuwasislisha mawazo
yaliyoendelezwa hufanyika msaada sana kwa wasikilizaji wako katika kuelewa na
kufuata mpango wako wa kufikiri.
Somo likiwalimechanganywa itawawia
vigumu wasikilizaji wako katika kulielewa somo hilo.Ujenzi wa osmo hulenga
kulifanya somo rahisi kiasi cha kueleweka vizuiri na wasikilizaji.
Ni muhimu sana kwa mhubiri kuliweka somo
katika namna itakayofanya lieleweke kwa
urahisi.
Mawasiliano.
Hii huhusu namana mhubiri anavyowaislisha somo au ujmbe kwa
hadhira. Mhubiri anatakiwa kuliwasilisha
somo lake kwa njia rahisi na nyepesi kueleweka na waikilizaji wake. Anatak
a)
Kuwasilisha ukweli uliowazi na wenye kueleweka.
b)
Kuota ujumbe kwa njia ya kuteka akili za
hadhira.
c)
Kuendeleza mawazoyako katika mpango
ambao hadhira wataweza kuyafuata kwa urahisi.
d)
Kuwahamasisha hadhira kulitendea kazi somo. Yak 1:22.
B. Sehemmu
Kuu za Mahubiri na Hotuba.
Kwa kawaida
mahubiri au hotuba yoyote ile ni lazima iwe na sehemtu tatu ambazo kwa pamoja
huunda hotuba au mahubiri hayo.
Sehemu tatu hizo ni utangulizi, kiini na
hitimisho.Kila sehemu ni muhimusana na inatikwa kupewa uzito wake.
Sehemu mojawapo
ikipuzwa yawza kuvuruga au kuharibu kabisa ujumbe au hotuba yako.
I. Utangulizi
. Hii ni sehemu ya kwanza ya hotuba.
Utangulizi hutambulisha hotbuba au somo zima na kutoa picha jinsi somo
litakavyokuwa. Utangulizi ni sehemu muhimu ya ujmbe na kama hadhira
hawajakusikilza kwa umakini katika kipindi hiki cha awali yawezekana
kutokuuelewa ujmbe wako au kutokukusikiliza vizuri katika sehemu zinazobaki za
hotuba yako.
Mara nygingi utangulizi huwa kama muhtasari
wa ujumbe.Katika utangulizi mhubiri huwaeleza hadhira kwa kifupi juu ya kile
ulichopanga kuongelea au kuhubiri.
Mambo
ya msingi katika uangulizi.
a)
Kuteka
usikivu. utangulizi wako
unapaswa utawale hamu na mawazo ya wasikilizaji.
b)
Kujenga
masikilizano. Lazima ujenge mawasiliano kati yako na
wasikilizaji.
c)
Kuleta
kukubalika. Ni lazima utangulizi kwako ukujengee kukubalika
kwa wasikilizaji.
a. Unapaswa
kupata usikivu wao, matumaini na heshima.
d)
Kujulisha. Utangulizi wako unapaswa kuwaeleza wasikilizaji
kwamba somo lako lina husu nini hasa, na jinsi utakavyoliwasilisha.
e)
Kusadikisha.
Ni lazima utangulizi uwasadikishe
wasilizaji juu ya umuhimu wa ujumbe na kupata usikivu mzuri wa sehemu iliyobaki
ya hotuba yako.
f)
Usitoe utangulizi kwa kuomba msamaha.
Usiseme “Bahati mbaya sikujiandaa vizuri”
a. Kufanya
hivyo kutapoteza usikivu wa wasikilizaji wako na kukufanya usiaminike kwao.
Sifa
za utangulizi mzuri.
a)
Sio
wa kishindo mno. Utangulizi uwe wa kiasi usiweke hatua ambayo huwezi
kuifikia.
b)
Sio
mrefu mno. Kumbuka kwamba utangulizi si ujumbe wote bali ni
sehemu tu hivyo unapaswa kuwa mfupi.
c)
Utangulizi
uendane na ujumbe. Utangulizi ni sharti ulenge kichwa cha
somo. Waweza kuwa mhtasari wa somo au kisa
ambacho kinaonesha ukweli wakile ulichokusudia kuongelea.
d)
Unapaswa
kuandaliwa kwa uangalifu. Kwa sababu utangulizi wako ni
kitu muhimu katika kuvuta usikivu wa hadhira unapaswa kuandaliwa kwa umakini
sana.
Tayarisha utangulizi wako kwa kujiuliza
maswali yafuatayo
a)
“
Ningekuwa ni msikilizaji ujmbe
huu nini kingenitvuta zaidi ili kuleta usikivu katika yote niliyokusudia
kuyasema?
b)
“ Ni jambo gani hasa ambalo
lngekaata usikivu wangu?
Majibu
yake unayoyapata ndiyo waweza kuyatumiak katika sehemu ya utangulizi wa ujumbe
wako.
Utoe nafasi ya kuptia kwenye kiini cha
ujumbe. Utangulizi unapaswa kutoa njia ya kupitia kwenda kwenye kiini cha
ujumbe. Kusiwe na pengo kati ya utangulizi na kiini cha ujumbe.
2.Kiini.
Hiini sehemu kuu ya
somo au ujmbe ambayo imebeba ukweli wote wa somo. Hatua ya kwaza kwenye kiini
ni kutoa sekeletoni ya kiini na kisha
hatua ya pili ni kuweka nyama katika
skeletoni yako.Waweza kuweka nyama katika sekeletoni yako kwa kufanya yafuatayo:
Kufafanua misamiati mbalimbali inayojitokeza kwenye
kiini na kutoa maelezo ya dondoo ulizoziandaa. Tumia kamusi au itifaki ya
Biblia katika kupata maana ya maneno hayo.
Kutumia vielelezso. Unapaswa kutumia vielelezo
mbalimbali vitakavyosaidia katika kulielezea somo lako au ujmbe wako.
Waweza kutumia vielelezo vifuatavyo
katika kulielezea na kufafanua ujumbe wako.
Vielelezo binafsi.
Wahusika mbalimbali katika Biblia wanaoweza kutumika katika kuelezea dondoo
zako. Ukweli wa kitaalam mfano sayansi,historia, uvumbuzi, Tiba. n.k
Hadithi zenye kufafanua somo lako.Usiwaachie
hadhira kutoa fasili ya bali ifafanue
mwenyewe.
Unapaswa kukigawa kiini katika dondoo
kwa kufuata mtiririko wa mawazo. Hubiri kwa kufuata mtiririko wa mawazo wa
kimantiki.
3.Hitimisho.
Hii ni sehemu ya mwisho ya hotuba au ujmbe
lakini kipengele cha muhumi sana . Kipengele hiki kisipozingatiwa maana na
malengo yote ya kuhubiri huvurugika na kutokuwa na maana. Hivyo ni lazima
kipewe uzito unaostahili.
Mambo ya kuzingatia.
Tunia muda kidogo kwa kuuelezea ujmbe
kwa kifupi. Kazia maeneo ya msingi unayofikiri kwamba hayakueleweka vizuri kwa hadhira wakati ukuhubiri na yale
yanayotakiwa kupewa uzito maalumu.
Pia waweza kurudia kuzitamka kwa
sauti dondoo za ujumbe wako kila moja.
Usiwachushe(bore) kwa kuanza kurudia kuhubiri ujumbe wako wote.
Mwaliko.
Mwaliko ni kipengele muhimu sana katika hitimisho. Kwa sababu mahubiri ni
tofauti na iana nyingine za hotuba hivyo mwaliko huwa ni muhimu sana kwa kuwa mahubiri huhusu kuchukua maamuzi au hatua juu
ya kile kilichohubiriwa. Mahubiri blia mwaliko huwa hayajafikia lengo la
kuhubiri. Mwaliko ni lazima katika mahubiri ya aina yoyote ile.
Mwaliko huwa ni wakati wa kuitikia Kile Mungu amesema kupitia mahubiri. Ni
wakati wa kutendea kazi kile kilichofundishwa au kuhubiriwa.
Mhubiri anapaswa kuufanya mwaliko kuwa
wazi kwa wasikilizaji wote. Lengo la mwaliko si kuwaita watu madhabahuni tu
bali ni kuwahamasisha watu kuweka ujumbe katika matendo.
Pia Mhubiri hutakiwa kuuweka ujumbe wake
katika matendo.
1. Ukihubiri
uponyaji waite watu madhabahuni na waombee uponyaji.
2. Kuhubiri
kutembea katika mamlaka unatakiwa udhihishe mamlaka hiyo.
3. Ukihubiri
utoaji waite watu kumtolea Mungu.
4. Ukihibiri
toba unapaswa kuwaongoza hadhira kwenye maombi ya toba na kuwaita madhabahuni
wale wanohitaji kutengeneza kwa upya mwenendo na mahusiano na Mungu na kuomba nao.
Wapeleke watu kwenye matendo na matumizi
Mt 21:23. Yak 2:22.
Unatakiwa kuwaongoza hadhira kuomba kwaajili ya ujumbe au somo kwa kadri
ya maongozi ya Mungu na kwa kadri Mungu alivyosema na kila mmoja.
Unaweza kuwaongoza watu waimbe wimbo
unaoendana na ujumbe uili kuwaogeza uweponi na kuwapa hamasa.
Toa mwaliko kwa watu ambao wanataka
kuokoka na kama wapo omba pamoja nao.
Baada
ya hapo maliza na mkabiribishe anaehusika na ratiba inayofuata.
Kwa kuhitimisha juu ya sehemu tatu za ujumbe
au hotuba twaweza kuvifupisha vipenele vyote hivyo vitatu kwa sentensi tatu
ambazo ni:
1.
Waambie hadhira kile unachotaka
kuhubiri.(Utangulizi.)
2.
Hubiri kile ulichowaambia (Kiini),
kisha:
3.
Waambie
kile ulichohubiri.(Hitimisho).
AINA MBALIMBALI ZA MAHUBIRI.
I. MAHUBIRI YA KIFUNGU.
Aina hii ya mahubiri hujengwa juu ya kifungu
kimoja kidogo cha maandiko tu.
Huhusisha kuchagua maelezo fulani maalum
ya maandiko na kuyachunguza, kuchambua na kugungua kweli zote zilizomo ndani
yake na kuziwasilisha kwa waikilizaji kwa mtindo rahisi na wenye kueleweka.
A. Faida za mahubiri ya Kifungu.
a)
Huvutia.
b)
Huzuia kutoka nje ya somo.
c)
Hufanya mahubiri kuwa ya ki- Biblia.
d)
Humwongezea mhubiri ujasiri.
e)
Husaidia wasikilizaji kulikumbuka somo.
B.
Jinsi ya kuandaa mahubiri ya
kifungu.Kuna mambo kadha ambayo mhubiri anapaswa
kuyazingatia wakati wa kuandaa mahibiri ya aya badhi ya mambo hayo yamejadiliwa
hapa chini.
1.Soma Biblia mara kwa mara.
Unapaswa kusoma Biblia mara kwa mara ikiwa unataka kuwa mhubiri mqwenye
mafanikio katika huduma yako.
-Tenga muda wa
kusoma biblia kila siku. Beba Biblia ndogo kila mahali unapokwenda ili upatapo
mua uweze kuisoma.
2. Jifunze Biblia. Kujifunza
ni zaidi ya kusoma.Kujifunza kuna husiha kusoma Biblia kwa undani kwa
kuchunguza kikamilifu kila kitu kilicha katika maandiko unayosoma na kutafakari
kwa kina,.Yos1:8.
Unapaswa
kutafakari kwa uangalifu vitu unavyosoma. Viweke kwenye akiliyako na kuvifikiri
tena na tena.
Unapaswa
kujizoesha kuchambua kile ulichojifunza. Baada ya kukichambua kwa umakini
unapaswa kukiweka tena akilini.
2. Kuwa na Daftari la kuandikia. Kila
usomapo Biblia yako jitahidi kuwa na kalamu na daftari la kuandika mambo muhimu
un ayo jifunza.Jenga mazoea ya kuandika kwa ufupikila ufunuo unaoupata.
3. Dumisha hali ya maombi. Unapaswa kuwa katika
hali ya maombi kila usomapo Biblia.Omba Mungu akufunulie upate kulielewa Neno
lake.Pia unapaswa kumwomba Mungu akupe
usikivu juu ya kweli anazokufunulia katika Neno lake.
4. Jenga usikivu.Unapaswa
kuwa katika hali ya utulivu na usikivu katika nyanjazote yaani kimwili, kiroho
na kisaikolojia. Mungu hutoa ufunuo wake
kwa sauti ya kimya ndani ya roho ya mhibiri. Kama hunautulivu na usikivu wa
kutosha ni vigumu kugundua maarifa
hayo..
-
C.Sifa za aya ya mahubiri
Kifungu cha
mahubiri au aya yapasa kuwa :
a. Yenye mamlaka
ya ki-Biblia. Mafundisho anayokusudia kuhubiri toka kifungu
au aya fualni ya
maandiko yapasa ikubaliane na ile biblia nzima inachofundisha.
Katika mahubiri
ya kifungu kuna uwezekano wa kuchukua kimakosamstari nje ya maana yake na
kuutumia kufundishia kitu ambacho Biblia haikubaliani nacho.
Ni Muhimu sana kwa ,uhubiri kujua jinsi mstari
anaoshughulikia jinsi unavyokubaliana na kusudi la sura yote na kitabu chote.
Daima
mhubiri anapaswa kujitahidi kufasili aya yake katika nuru ya yale ambayo Biblia nzima inafundisha.
b.Kamili. Aya yapaswa kuwa katika maandisha ya ukweli
ulio kamilika.
Baadhi ya wahubiri huchukua kifungu
cha maneno katika mstari na kukitumia bila kujali maneno yaliyotangulia au
yanayofuata. Jambo hili si zuri na huzaa mafundsho
ya uongo. Na huku huitwa. “Kulichanganya
neno la Mungu na uongo……..2Kor 4:2.
Ni
lazima uepuke jambo hili kwani litaleta kutokuaminika na maelezo yasiyo ya ki-
Biblia na hatimae utawapotosha wasikilizaji wako.
c. Fupi kiasi. Kifungu
cha mahubiri chapaswa kitolewe kwenye maelezo ya maandiko ambayo ni mafupi nay
a kulizisha.
c. Ya kueleweka.
Aya yapaswa kueleweka na iwe muhtasari wa kutosha wa kile unachotaka
kukishirikisha.
*Unapaswa
ubaki katika mipaka ya kile ambacho aya yako inaelezea.
D. Namna ya kuandaa mahibiri ya aya.
a.
Elewa maneno yake vema.Kipitie kifungu kwa kukisoma mara kadhaa, kitafakari na
kujenga kumbukumbu juu yake na kiseme mwenyewe kwako. Hakikisha unakielewa
vizuri.
b. Elewa lugha yake.Tamabua
lugha yake kama ina maana halisi au kama ni lugha ya mifanotu.
Jiulize
kama mwandishi alikuwa na maana hasaya
kile alichokiandika au maneno yake
yachukuliwe kama mfano wa mahubiri?
c.Changanua ujumbe wake.Chambua
uhjumbe unaoupata na kuutenga katika sehemu kadhaa zenye kulandana ili uweze
kuuwasilisha kwa mtiririko mzuri.
d. Chunguza maneno yake.
Jitahidi kugundua kile maneno hayo yalikusudia kuwasilisha hapo awali. Ikiwa
una kamusi ya kigiriki au Kiebrania unapaswa kulitazama neno hilo kwa lugha ya
zamani au Kigiriki. Jaribi kubaini kama kuna maana maalumu ndani ya mneno
unalolishughulikia.
Kufanya
hivyo kutakusaidia kugundua maaana yoyote maalumu ambayo mwandishi alikusudia
kuiwasilisha.
e. Tathmni mwendelezo wake. Baini
kweli zile mwandishi alitaka
kuzielezea. Tambua jinsi alivyo kamilisha katika kuziwasilisha kweli
hizo.
Jaribu
kufuata mwongozo wake na kuuendeleza
katika mtindo huo.
f. Mkutadha wa kifungu..
i.Maneno ya mbele nay a nyuma ya kifungu.
Angalia jinsi mistari iliyotangulia na inayofuata inachosema. Chunguza aya
kushusiana na sura nzima ambayo umetoka. Chunguza kifungu hicho katika nuru ya
kitabu kizima ambamo kinapatikana.
Jifunze kiini na mazingira yote ya
kitabu.
ii. Hali ya mila. Je mila za wakati ule ziliathiri kile kilichoandikwa?
Je watu walioandikiwa kifungu hicho awali wangekuwa na wazo la kile
kilichoandikwa tofauti na ambalo tungepata katika hali yetu? Kama ndivyo nini
ingekuwa maana inayolingana na sasa?
ii. Hali ya kihistoria.
Je jambo hili liliandikwa lini?je wakati huo ulishawishi kile kilichoandikwa?
Je matukio ya kwakati ule yaliyokuwa yakijulikana wakati ule wa uandishi
yalikuwa na maana maalum ju ya kile
kilichosemwa?
iv.
Hali ya kijiografia.
Mwandishi alikuwa wapi wakati anaandika maneno hayo?je Watu walioandikiwa
walikuwa wapi?Je mazingira yao yana uhusiano wa chochote katika kle
kilichosemwa?
v. Biblia kwa ujumla. Kila sehemu ya maandiko
ifasiliwe kwa uaminifu na kwa umakini ili ikubaliane na maandiko yote. Andiko
lolote lisifasiliwe nje ya mkutadha wake. Maandiko ni lazima yatafsiri
maandiko.
E.Kupanga Maelezo.
Mpanglio
mzuru wa maelezo na kazi kwa ujumla ni
wa faida sana kwa mhubiri. Hakikisha unapnga maelezo yako kimaantiki. Mpangilo
mzuri wa kazi na mawazo humwezesha mhubiri kulielewa vizuri somo na
kulishughulikia somo kikamilifu.
Pia
huwawezesha wasikilizaji kulielwa somo na kulikumbuka somo .
1. Ujumbe uwe katika mpangilio.Panga
ujumbe wako katika mtiririko mzuri ili uweze kuufuata kwa urahisi wakati wa
kuhubiri.
2. Weka ujumbe wako katika hali ya
kueleweka. Jitahidi kukamilisha vipengere vyote unavyohitaji
kuviongelea katika mahubiri yako. Kabla ya kupanda mimbarini.
3. Kazia katika mawazo.
Unapaswa kuyaweka mawazo yakob katika sentensi fupi. Jifunze namna ya
kuyaimarisha mawazo yako kwa pamoja nakuyaelezea katika sentensi fupi
zinazoeleweka kwa urahisi.Jizoeze kupunguza na kulielezea wazo kwa sentensi
moja.
4. Tayarisha maelezo mafupi.Kumbuka
kwamba maelezo yako yako ili kusaidia kumbukumbu yako.unapaswa kuwa na vidokezo
vitakavyosaidia kulikumbuka somolako au ujumbe wako.
5. Ufanye rahisi kuusoma.
Ni vizuri kupiga chapa mahubiri yako ili
uweze kusoma kwa urahisi wakati wa ukihubiri. Pia waweza kutoa vipeperushi na
vijarida kwa wasikilizaji wako ili waweze kufuatilia zaidi ujmbe au somo lako.
Zoezi.
1. Eleza maana ya mahubiri ya aya.
2.Tathmini ubora na udhaifu wa
mahubiri ya aya.
3.Taja mambo mengine muhuimu ya
kuzingatia katika mahubiri ya aya au kifungu licha ya yaliyotajwa katika kitabu
hiki.
4. Andaa hotuba ya mahubiri ya aya
na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako.
II. MAHUBIRI YA KUFAFANUA.
Mhubiri ya kufafanua ni aina ya
mahubiri ambaayo huhusisha kuchagua
sehemu kubwa ya maandiko na kuicghunguza kwa undani na kuifasiri na kugungua
kweli zilizomo katika sehemu hiyo ya maandiko na kushirikisha mkutano au
usharika wako.
Mfano unaweza kuamua kupitia Injili
yote ya Luka sura baada ya sura. Kuanzia sura ya kwanza,
unatafuta kufasili na kuelezea maana na umuhimu wake mstari kwa mstari sura kwa
sura mpaka umeimaliza yote.
Waweza kushughulikia sura moja kila
wiki, na baada ya wiki kadhaa utakuwa umemaliza kitabu chote.Faida ya mahubiri
ya ufafanuzi.
Hufanya
mahubiri kuwa ya ki-Biblia.
1.
Yesu alitumia aina hii ya mahubiri.
Alichukua kifungu cha Agano la kale na kufasili maana yake kwa wasikilizaji
wake.
2.
Petro alitumia njia hii siku ya
Pentekoste.
3.
Stefano alitumia njia hii.
Huwezesha waamini kuwa na msingi na
uelewa mkubwa wa Biblia.Waamini huimalisha na huwa na ufshsmu mzuri na wa kina
wa Neno la Mungu. Kwani kweli zote zilizomo katika kitabu kilichopitiwa tayari
hufahamika vizuri kwa usharika wote.
Huvuta
kuimalishwa na Roho mtakatifu. Roho mtakatifu
hulithibitisha neno lake kwa ishara na miujiza sawasawa na Kweli zote
zilizofunuliwa katika kitabu husika.
Humfanya
mhubiri kuwa wa ki-Biblia. Mahubiri ya kufafanua humfanya
mhubiri kuwa wa ki-Biblia kwani mhubiri huhubiri kile kilicho katika maandiko
ya eneo husika. Mhubiri huwa anajikita katika mkutadha wa aya, sura na kitabu
chote kwa ujumla. Hivyo kiini cha kitabu ndicho ambacho hubeba mahubiri yake
yote.
Mambo
ya kuzingatia katika kutayarisha mahubiri ya kufafanua.
I.
Kwa umakini cuagua kifungu cha maandiko kinachostahili. Hakikishwa
kwamba kifungu hicho kitahudumia uzima na uwezo wa wasikilizajiwao.
1.
Usichague somo kwa sababu linakuvutia au
kukupendeza.
2.
Usichage somo ambalo litazaa machafuko,
mgawanyiko na mashindano.
3.
JItahidi kufanyika njia ili Mungu
akupitie ili Mungu akupitie ili aweze kuongea Neno lake kwa watu wake kwa
kupitia wewe.
4.
HIvyo basi unawajibika kutafuta kujua mawazo ya Mungu kuhusu watu
wake ambao amekupa wajibu juu yao.
5.
Huduma hii ni moja ya heshima kuu
uliopewa lakini pia ni wajibu mkuu unaoogopesha sana. Hivyo basi unapaswa
kuifanya kwa umakini wa hali ya juu.
II.Tafuta
ujumbe unaolingana na hali ya watu ya wakati ule.
1.
Mungu kila mara huwa na ukweli wa sasa ambao hutaka kunena na
watu wake.
2.
Mungu hukusudia jambo maalum kwa kila
kundi la waamini
3.
Jifunze kujua kile Mungu anacho kwaaji
ya kusanyiko kwa kilac wakati.
III.
Jifunze sura ya kitabu kwa umakini.
1.
Soma sura unayo shughulikia mara nyingi
mpaka umeielewa vizuri.
2.
Soma kwa uangalifu mstari hadi mstari.
3.
Kila kunapokuwepo na uhusiano wa wazi
kati ya kifungu hicho na kifungu kingine unapaswa kusoma kifungu hicho ili
uweze kupata maana zaidi. Maandiko hufasiri maandiko.
4.
Jenga usikivu kwa sauti ya Roho
mtakatifu ili kupokea ufunuo toka kwake.
Tunia vitabu vya rejea ili
kupatamsaada zaidi. Mfano. Itifaki ya Biblia, Kamusi ya Biblia, Biblia ya
Tafsiri nyingine.Nk
IV.
Kusanya taarifa muhimu.
Waweza kupata vitu vingine muhimu vya
kuhusisha kwenye somo lako kwa kutumia mbinu ya maswali na majibu kama ifuatavyo.
1.
Nimewahi kusikia au kusoma nini juu ya
somo hili?
2.
Roho mtakatifu amewahi kunionesha nini
juu ya somo hili?
3.
Nimewahi kuona nini chenye uhusiano na
somo hili ?
4.
Nimewahi kuwa na mawazo gani juu ya somo
hili ?
Naweza
kupata habari zaidi ju ya somo hili kwa nani au
wapi ? kueleweka.
5.
V.
Tambua kiini cha somo lako.
1.
Daima tafuta kugundua kiini cha sura
unayoshughulikia.
2.
Tafuta kujua kile Roho mtakatifu
alikusudia kuwasilisha alipoivuvia sura hiyo.
3.
Gundua undani wa somo hilo.
4.
Baini kile Mungu anataka kusema na watu
wake kupitia sura hiyo.
VI.Kuwa
na Lengo kamili.
Lengo lako daima
lapaswa kuendana kikamilifu na lengo la
Mungu.
1.
Hakikisha kwamba Umegundua kile Mungu
anataka kutoa kupitia maadiko hayo na kisha jizamishe katika kile Mungu anataka
kufanya.
2.
Unapaswa kuhisi kile Mungu anachohisi
Mungu humshirikisha mhubiri moyo wake na akili yake ili waweze kufanya kazi
pamoja. Unapaswa kuchangamka.
3.
Fanyika chombo cha Mungu cha kupitishia
ujumbe wake kwenda kwa watu wake.
4.
Kumbuka hukuitwa kushiriki mawazo yako
na watu bali kuwashirikisha watu mawazo ya Mungu.
VII.
Zungumza kulingana na ujuzi wako mwenyewe.
1.
Usitoe nadharia toa uhai. Hubiri kile
ulicho na uzoefu nacho.kile ambacho umekifanyia kazi . wapaswa kuwa mtu kwa
kwanza kula matunda ya kazi yako.
2.
Umeitwa kuwa barua Sio tu kwamba
unataikwa kuuhubiri ukweli bali pia unatakiwa kuufanyia mazoezi na kuuonesha
kwa matendo.
3.
Unapaswa kuwa mfano hai wa yote
unayoyahubiri.
VIII.
Upe maana ujumbe wako.
1. Unawajibika
kwa uwezo wako wote, kuhakikisha kwamba
maana ya kweli na umuhimu wa maandiko unakuwa wazi. Na wakueleweka kwa
wasikilizaji.
2. Daima
jitahidi kuufanya ujumbe wako kuwa rahisi.
3. Hivi
ndivyo Yesu alivyofanya Hii ilisababisha
huduma yake kuwa na nguvu na mafanikio.
4. Alichukua
mambo yaliyokuwa mafumbo na na akayaweka
rahisi sana.
5. Wahubiri
wengine huyachukua masomo rahisi sana na
kuyafanya mafumbo magumu sana kiasi cha kutoeleweka kwa wasikilizaji
wake au kuelewa kidogo.
IX.Fanya
ujumbe wenye kutekelezeka.
1.
Daima unapohubiri jitahidi kuonesha
wazi wasikilizaji wako jinsi wanavyoweza
kuutendea kazi ujumbe wako.
2.
Jitahidi kutoa ushauri wa kimatendo
kuhusu watu wanavyotakiwa kumwitikia Mungu kwa namna ya kufaa.
3.
Husianisha mahubiri yako na maazimio
yako kimatendo ambayo yaweza kuwafanya watu kuwa watendaji wa Neno na si
wasikilizaji tu.
Zoezi
1.Eleza
maana ya mahubiri ya kufafanua.
2.
Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya kufafanua.
3.
Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya kufafanua.
4.
Chagua sura mojawapo ya injili ya Yohana na kisha andaa mahubiri ya kufafanua
kutokana na sura hiyo na kisha hubiri kwa dakika kumi.
III. MAHUBIRI
JUU YA MAISHA YA WATU.
A.Utangulizi
Hii huhusu hadithi ya maisha ya watu. Kwa hiyo
njia hii huhusisha mafunzo juu ya maisha ya watu mbalimbali tunaosoma habari
zao katika Biblia. Kila hadithi ya mtu iliyoandikwa katika Biblia ina umuhimu
kwetu. Maisha ya kila mhusika aliye kwenye Biblia yana mafunzo kadhaa ambayo twaweza kujifunza. Kila habari iliyoandikwa kwenye Biblia ipo
kutufundisha kitu fulani ambacho ni cha thamani sana. 1Kor 10:1-11.
Mhubiri
huchagua mhusika mmojawapo wa wahusika walio katika Biblia na kujifunza kwa
kina kila kitu kilichotoke katika masiha ya mhusika huyo, tangu kuzaliwa kwake
mpaka kufa kwake. Pia mhubiri hutakiwa kujifunza kuhusu nasaba na mbari ya
mhusika huyo ili aweze kufahamu vizuri vitu vilivyomjenga na kumkuza mhusika,
kisha hutayarisha mahubiri juu ya mhusika huyo na kuhubrikatika kusanyiko lake.
Mafundisho
ya wahusika wa Biblia ni ya kushangaza na ya kuvutia.
Katkia
aina hii ya mahubiri, mhubiri hupaswa kuchaqgua mhusika mmoja na kusoma habari
zake zote zilizo kwenye Biblia na kisha huandikia kila wazo analolipata. Hapa
mhubiri anapaswa kusoma kumbukumbuzote za mhusika katika Biblia.
Baada
ya kusoma kumbukumbumbu hizo unapaswa kuanza kuweka pamoja mawazo yote
unayoyapata katika utaratibu wa miaka yaani jinsi matukio yalivyotokea ya
mhusika huyo.
B. Faida za mahubiri juu ya maisha ya watu.
I.Hufunua
ukweli wa maisha. Biblia imeelze wazi maisha ya wahusika kama yalivyokuwa pale kuficha chochote.
Imeeleza mafanikio yao na madhaifu yao. Ukweli wa maisha ya wahusika umewekwa
wazi na kwa uhalisia.
Wengi
wa mashujaa wa biblia wanahitilafu zao za kibinadamu.Twajua kuwa walikuwa
wanadamu kama sisi na walikutana na majaribu kama sisi.
Katika
visa vyote vya historia kuna mtu mmoja mkamirifu ambae ni Yesu kristo pekee.
Hata mashujaa wakubwa wa imani walikuwa na hitilafu zao. Hii inatupa kujua
kwamba wao si tofauti na sisi.
Ni
mifano ya kujifunzia. Ni mifano na msada
kwetu. Tunaweza kujifunza kutokananayo kuliko ujuzi wetu wa uchungu.
C. Mambo ya kuzingatia
a) Jifunze
kuzaliwa kwa huyo mtu.
b) Tafakali
hali na mazingira aliyolelewa.
c) Angalia
uhusiano wake na Mungu katika maisha yake.
d) Angalia
jinsi alivyo wajibika kuhusu uhusiano wake na Mungu.
e) Baini
vitu alivyojifunza kutokana na mahusiano yake na Mungu.
f) Tathimini
mafanikio yake. Jifunze vitu vilivyomfanya afanikiwe.
g) Tazama
maeneo aliyokosea kama yapo. Na jifunze vitu vilivyomfanya akosee.
h) Toa
hitimisho kile tunachoweza kujifunza kutokana
na maisha ya mtu huyo.
Mambo
hayo yote yanavutia na ni yenye vitu vingi vya Kutufundisha ambayo twaweza
kujifunza kutokana na watu hao.
Tunaosoma habari za maisha yao katika Biblia.
D. Hatua za
kufuata katika kuandaa mahubiri juu ya maisha ya watu.
I. Chagua mtu au msusika toka
kwenye Biblia. Unapaswa kuanza na watu mashuhuli katika
biblia ambao habari zao ziko wazi kabisa.kama vile Ibrahimu,Musa,Samweli, Daudi, Yusufu, Debora, Miriamu, Mariamu,
Dorkasi, Paulo, Petro. N.k.
Hawa
ni baadhi ya watu ambao matendo yao yameyanyika kuwa nuru katika historia ya
dushusiano kati ya Mungu na mwanadamu.
Kuna
mambo mengi sana ambayo twaweza kujifunza kutokana na maisha yao. Aina hii ya
mahubiri ni nzuri sana, kujifunza toka kwa wacha Mungu wenzetu waliotutangulia
katiki wito na huduma hii ni jambo la msingi sana. 1Kor 10.1-11.
II. Chunguza maisha yake.
Anza
kwa kusoma hadithi inayoelezea kuzaliwa kwa mtu huyo. Tafuta maana ya jina
lake. Kwani jina lina maana sana ki-Biblia. Angslia kwa umakini kusudi la Mungu
katka maisha yake. Ili uweze kuvumbua vitu vingi unapaswa kujiulza mawsali fafuatayo:
1. Mungu
alitaka kutekeleza nini kupitia mtu huyu ?
2. Je
Mungu alifanya nini ili kusudi lake lijulikane kwa mtu huyu?
3. Mtu
huyu aliitikia vipi Mungu alipomjulisha kusudi lake?
4. Tunaweza
kujifunza nini kutokana na Mungu kuhusika katika maisha yake ?
5. Kuna
tahadhari zozote ambazo tunapaswa kuzichukua ?
6. Je
siri ya mafanikio yake ilikuwa nini ?
7. Je
mwisho wa maisha yake ulikuwaje ?
III. Chambua somo na kisha hubiri.
Baada
ya kujiuliza maswali hayo na kupata
majibu utakuwa umepata vitu vingi ambavyo waweza kuvichambua kwa umakini na
kuandaa somo kisha na kulihubiri somo hilo katika mpanglio na mtiririko Mzuri
wwa mawazo.
Mwombe
Roho mtakatifu akupe ufunuo zaidi unapokuwaukihubiri somo lako na lifanye somo
lako kuwa na uhalisia katika maisha ya sasa ya wasikilizaji.
Zoezi
1.Eleza
maana ya mahubiri ya wahusika au maisha ya watu.
2.
Tengeneza orodha ya watu mashuhuri walio
katika Biblia. Orodha hiyo ihusishe wanawake na wanaume.
3.
Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya wahusika.
4.
Chagua mhusika mmoja wa kike au wa kiume na kisha andaa mahubiri kwa kumtumia
mhusika huyo na kisha hubiri kwa dakika kumi.
IV.
MAHUBIRI YA MIFANO HALISI NA VIVULI.
Huu
ni ujuzi unaohusu kuweka wazi au
kuchimbua na kuwasilisha kweli
uliojificha wa mifano mbalimbali
katika Biblia.
Mfano
ni kitu, mtu au tukio ambalo kinabii ni ishara ya kitu au mtu
fulani.atakaetokea baadae. Inafanana au ni mfano wa Yule mtu au tukio.
Katika
matumizi ya biblia ina maana ya mtu wa bibliaau tukio litakaloonesha kitu
fulani kitakachotokea.
Mfsno
mwanakondoo katika kitabu cha Kutoka ni mfano wa Bwana Yesu.Kila kitu kuhusu kondoo wa pasaka
kiunabii kilkuwa na maana ya ukombozi ya wajibu ambao Bwana yesu Kristo
angetimiza.Yn 1:29.
Mifano
ya biblia mara nyingi inaonekana kama kivuli(type) cha mambo yanayokuja baadae.
Ebr
8:5,10:1.
Siku
takatifu pia katika agano la kale zilikuwa vivuli ju ya mambo ambayo yalikuwa
yanakuja.
Kol
2:17. Hizo siku takatifu hazikukamilika zenyewe sehemu ya kusudi la kutimizwa
kwake ilikuwa ni kutanguliza sura ya
kinabii ya vitu ambavyo vilikuwa bado vinakuja.
Kanuni za kutumia.
a.
Unapojaribu kwa mara ya kwanza
kufundisha kwa kutumia mifano ya kwenye Biblia, zingatia misingi
ifuatayo.
I. Tumia mifano rahisi zaidi.
Anza na mifano rahisi mabayo maana yake iko wazi.
II.Endelea na tafsiri ya wazi. Usijaribu kutafsiri
kila kitu.Elezea ukweli wote kama ulivyo na wala si kutafuta kila kipengele
chake na kukielezea kwa undani.
III. Usitumie maneno makavu.
Usitumie mifano ya kufundishia kama kanuni.
IV.Sisitiza ukweli wa msingi..Usitumie
nafai uliyonayo kwa kutoa mifano ya kufundishia. Mifano itumike kusisitiza
mafundisho na si kutumia kama chanzo cha ukweli.
V. Uwe tayari kusahihishwa. Uwe
tayari kusahihishwa na kukosolewa na wale waliokomaa kuliko wewe ili uweze
kujifunza zaidi.
4. Kuelezea kusudi.
Ni
njia ambayo kwayo mhubiri hupanua maana
ya ukweli ulio katika kifungu maalum cha
maandiko. Unatafuta naman ya kuuweka wazi ukweli ambao umejificha ndani ya
kifungu. Hii njia nzuri sana ya kufundishia kusudi lote la ki-Mungu. Mdo 20:27.
Hapa
mhubiri aweza kuchukua kitabu cha Biblia na kuelezea maana yake sura baada ya sura.
Zoezi
1.
Eleza maana ya vivuli na mifano.(Types).
2.
Taja hatua za kufuata katika kutayarisha na kuhubiri mahubiri ya mifano na
vivuli.s
3.
Tathtmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya mifano na vivuli.
4.
Tayarisha mahubiri ya mifano na vivli na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya
wanafunzi wenzako.
V.
MAHUBIRI YA MADA.
Aina
hii ya mahubiri hukusudiakutoa kiini
maalum kwa hadhira.Mhubiri huchagua somo fulani kisha huchunguza kila
kitu ambacho Biblia inasema juu ya somo hilo. Baada ya kuchunguza na kuchambua
kweli hizo huandikwa katika mapngilo wa somo.Mhubiri hupitia vifungu mbalimbali
vya maandiko vinavyohusu somo hilo.
Aina
hii ya amhubiri huhitaji maandalizi ya muda mrefu na utulivu mwingi. Pia
huwasilishwa katika mfululizo wa vipindi kadhaa na si kimoja, kwa sababu ni
vigumu kupitia kweli zote zilizo katika somo kwa kipindi kimoja tu.
Mfano wa mada za kuhubiri.
1.
Upendo
wa ki-Mungu
2.
Ubatizo
wa Roho mtakatifu
3.
Maombi
ya kufunga.
4.
Nguvu
ya usaidizi.
5.
Vita
vya kiroho.
6.
Kutambua
Ulimwengu wa roho.
7.
Kutembea
katika mamlaka.
8.
Nguvu
ya madhabahu.
9.
Kushughulikia
majira na nyakati.
10. Kutii mamlaka.
Mambo ya kuzingatia katika mahubiri
ya mada.
1. Uwe
na ufahamu kwa kutosha juu ya somo husika.
2. Fanya
maandalizi ya mudamrefu nay a kina
3. Unapaswa
kuwa na lengo mahususi la mahubiri yako.
4. Gawa somo katika vipengele vidogovidogo.
5. Kila
kipengele laima kiwe na maandiko yanayokithibitisha na kukielezea
6. Andiko
liendane na dondoo unayoitoa.
Zoezi.
Somo hili lipo kimatendo zaidi. Kila mwanafunzi
ashiriki katika kufanya mazoezi ya kuandaa mahubiri na ahubiri katika dakika
zilizopendekezwa au mwalimu atakazopanga kulingana na muda uliop.
Mwalimu anatakiwa kusimamia na kusahihisha
kazi za wanafunzi na kutoa marekebisho katika maeneo ambayo wanafunzi
hawajafanya vizuri.
1.Andaa
Ujumbe kwa kutumia aina ya mahubi ya
mada na kisha hubiri mkuano kwa dakikika arabaini. Chagua mada yoyote.
2.Taja
ubora na udhaifu wa mahubiri ya mada.
3.
Taja mambo mengine matano muhumu ya
kuzingati katika kuandaa mahubiri ya mada.
4.
Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri ya
mada na mahubiri ya kufafanua.s
VI.MAHUBIRI YA MATUKIO.
Mahubiri
ya matukio ni kipengele katika mahubiri ya maada, lakini kutokana na umhuhimu
wake tumekitenga na kukielezea peke yake.
Mahubiri
haya ni mahubiri ambayo huandaliwa
kutokana na tukio lilipoau ambalo litafanyika katika kipndi fulani.
Kiini
cha mahubiri haya huwa ni tukio ambalo linafanyika katika ibada hiyo.Mfano wa
matukio hayo ni
Tukio la,
1. Kusimikwa
kwa uongozi wa kanisa.
2. Ndoa
au kumuaga bibi arusi.
3. Kubariki
watoto.
4. Ushirika
mtakatifu
5. Kuweka
wakfu vitu mbalimbali.
6. Kuhitimu
mafunzo.(graduation)
7. Msiba
na mazishi.
8. Sikukuu
mfano Pasaka, mwaka mpya, N.k
Mambo ya
kuzingatia
1.
Mahubiri
haya yanapaswa kuendana na tukio husika.
2.
Mhubiri
anatakiwa kufahamu ratiba nzima ya tukio hilo au shughuli hiyo.
3.
Mhubiri
ahubiri kulingana na tukio husika.
4.
Mhubiri
aepuke kutumia muda mwingi katika mahubiri.
5.
Mhubiri
ahubiri kwa lugha itakayoeleweka na kusanyiko lote na lugha yapaswa kuwa
rahisi.
6.
Mahubiri
yapaswa kugusa kusanyiko lote.
7.
Mhubiri
anapaswa kubiri kwa upendo.
8.
Mhubiri
azingatie ratiba ya tukio.
ZOEZI.
1.
Chagua tukio mojawapo na kisha andaa mahubiri juu ya tukio hilo na hubiri kwa
dakika 10
.2.
Taja mabo mengine kumi ya kuzingatia katika mahubiri ya matukio.
3.Eleza
ubora na udhaifu wa mahubiri ya matukio.
1. MAHITAJI YA
MUHUBIRI:
a.
Anapaswa kuwa ameokoka yaani amezaliwa mara ya pili.
a.
anapaswa kuwa na wito kamili na uliowazi
kwajijli ya kazi hii na sii taaluma tu.
Anapaswa
kuwa amejazwa Roho mtakatifu.
Anapaswakuwa
na wito uliowazi kwake na kwa watu wengine pia.
3. Mhubiri anapaswa
kuboresha utu na wito wake kwa njia
zifuatazo:
I.kuwa
na ushirika wa karibu na Mungu daima.
a) Maombi
na kutafakari Zab 1, Yosh 1:8.
b) Kuishi
maisha matakatifu.
c) Kuwa
mnyenyekevu daima.
II Anatakiwa kujifunza daima.
Neno la
Mungu na vitabu vinginevyo vizuri.
a)
Panga muda wa kusoma (soma kwa bidii).
b)
Pata chakula kwajili yak o mwenyewe.
c)
Pata chakula kwaajili ya watu wengine.
d)
Hudhuria makongamano na semina
mbalimbali.
e)
Jifunze toka kwa wahubiri wengine
wakubwa na wazuri waliokutangulia.
III.Jifunze kutokana na watu
wanaokuzunguka na mazingira yao.
a)
Tazama na soma watu wanavyoishi,
matatizo wanayokutana nayo.
b)
Fungua macho yako kujifunza kila mahali.
IV.. Endeleza vipawa vyako vya asili.
Kil;a mtu anacho
kipaji cha asili. Ni muhimu kuendeleza kipaji ulichonacho kwaajili ya utukufu
wa Mungu. Mfano wa viapji vya asili ni Kuimba, kupiga muziki, kushauri, n.k.
Vipaji vyote vyaweza kuendelezwa kwa njia ya mafuzo na mazoezi. Hivyo hakikisha
unakuza na kuendeleza kipaji chako cha asili.
V..Tunza afya yako.
Ni muhimu kwa muhubiri kutunza afya yake kwanibila kuwa na afya bora muhubiri
hataweza kutimiza wito wake kwa ufanisi.
Pai ni jambo jema kwa muhubiri kufuata ushauri wa kitaalamu yaani
kuchunguza afya yake mara kwa mara ili kushugulikia mapema kama kuna dosari
zozote za kiafya kiwa bado change. Pia ili muhubiri aweze kuwa na afya bora
anatakiwa kufanya yafuatayo:
i.
kula chakula bora.
ii.
Kufanya mazoezi mra kwa mara. Mfano
kukimbia, kuruka, kutembea, N.k
iii.
Kuwa na muda wa kupumzika.( Muhubiri ni lazima awe na muda wa kutulia na familia yake. Pia mhubiri
anapaswa kuwa na likizo.)
VI. Vipaumbele vya muhubiri.
Unapaswa kutambua vipaumbele na uviheshimu ili uweze kuwa na ufanisi katika
huduma na wito wako. Vpaumbele hivyo ni:
a) Mungu.
b) familia.
c) Huduma
d) Watu
wengine.
Kila
kipaumbele kipe nafasi yake. Usipofanya hivyo utumishi wako utatyumba.
VII.
Ni lazima amtegemee kikamilifu Roho mtakatifu.
“
Atatwa katika yaliyo yangu na kuwapa ninyi. Yn 14:26, 16:13-14.
Hivyo
ni lazima mhubiri ajifunze kumtegemea Mungu
kiamilifu;
a)
Katika maisha yake ya kila siku.
b)
Katika masomo yake.
c)
. Katika maandalizi na matayarisho.
-
Katika kuandaa hotuba za kuhubiri.
-
Katika kuandaa matirio ya kutumia katika
kuandaa hotuba zake.
-
Katika kuwasilisha hotuba zake.
a)
Kwa kutumia stadi na ujuzi pekee wa
homiletics na akili yako pekee kusanyiko lako litabaki tupu na ukiwa.
b)
Ni Roho mtakatifu pekee anaewweza kumtia
nguvu mhubiri kuufikia ushindi wa kiroho Mdo 1:8.
c)
Ni Roho mtakatifu pekee anaeweza
kubadilisha na kuhuisha wasikilizaji wako. Yn 16:7-8.
d) Mhibiri unapaswa daima kumtegemea
kikamilifu Roho mtakatifu katika kazi na wito wako wa uhubiri. Hakikisha
unashirikiana nae kikamilifu iliuweze kuwa na ufanisi katika wito na huiduma
yako.
*Roho mtakatifu aweza
kuwa msaada kwa mhubiri lakini yeye ni
kama hua….
MADA
YA PILI.
A.
mhubiri ni mtangaza ujumbe wa Mungu.
-Yeye
ni msemaji wa Mungu. Husimama katika nafasi ya mungu na kuzungumza kwa niaba
yake Mungu.
B.
Biblia ndiyo asili ya ujumbe. Ujumbe wowote uaouhubiri nilazima utokane na
Biblia nje ya Biblia si mahubiri bali ni masimulizi tu.
-Ikiwa
kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu mhubiri anapaswa kwenda mahali Mungu
alipoongea mara nyingi na waziwazi yaani
“Biblia”
Kwa njia nyingine kuhubiri ni kuipa
Biblia sauti.ni kuacha Mungu aongee mwenye koa kwa Neno lake.
Kwa
nini Biblia peke yake? Kwanini si kitu
kingine toka vitabu vizuri vya kikristoau toka magazeti au maelezo na
masimulizi ya mtu maarufu na aliye mkuu.
1.
Biblia ni maoni ya Mungu kwa kila jambololotelililotolewa.
(Mhubiri
aliye kuwa amekosolewa kwaajili ya hotuba yake alisema “hata mimi sikuipenda
pia lakini haikuwa maneno yangu na
nilikuwa sitoi mawazo yangu bali kile Mungu amesema katika Neno lake. Kwahiyo
nilitoa mawazo ya Mungu na si yangu.).
Kuhubiri
hotuba ya ki-Biblia humpa mhubiri ujasiri mkubwa. Kutangaza kwa nguvu;
·
Biblia inasema ………………….
·
Mungu anasema…………………
2.
Neno la Mungu lina nguvu. Wab 4:12.
3.Neno
la Mungu ni kama mbegu.sBiblia hukutana na kila hitajila mwanadamuna matatizo
yake yote yanayomkabili.
5.
Inampendeza Mungu- Neno lake lililovuviwa
amri yake ilikuwa wazi
“Enendeni
mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi na muwafundishe kuyashika yote
niliyowaamuru”
6.
Roho mtakatifu hulithibitisha Neno la Mungu.
C.
jinsi ya kupata maandiko ya Kuhubiri.
Mwombe
Mungu Akupe ujumbe waq kuhubiri.kissha pokea andiko toka kwa Mungu kuhusu
mahubiri hayo kwanini yeye Mungu anajua mahitaji ya watuya sasa yanayotakiwa
kushughulikiwa……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
D.
Namna ya kutumia maandiko kwa usahihi.
Kufasili
na kutumia maandiko matakatifu kwa maana
yake halisi ni kazi moja muhimu na takatifuambayo mhubiri anawajibu wa
kuifanya.
1. Usipindishe wala kugeuza maana
ya andiko ili kulifanya andiko likubaliane na mawazo yako.
2.Usichukue
sehemu ya andiko na kuifanya iseme kitu ambacho hakiendani na mkutadha wake
ambao ambacho mkuadha hauoneshi kuwa ni maana yake halisi.
3. Soma andiko kwa umakni (zingatia
sarufi na misemo iliyomo katika andiko) na ulitafakari katika maana yake
halisi.
- Baini aina ya tungo zilizotumika
na aina za maneno yaliyotumika kuunda tungo hiyo.
-Tazama
maneno maalumu(Key word)yanayotokeza katika andiko unalotafakari.Mfano DAmu, Msalaba, Yerusalemu N.k.
-Kuwa makini kutazama tamathali za
semi zilizotumika au kujitokeza. Mfano. Misemo, nahau,
tashibiha, tashihisi tashititi, tafsida ,methali n.k.
4. Soma andiko katika mkutadha wake
wa sasa. hapa
unatazama mkutadha wa msitari, aya na sura ya andiko.
5.Soma andiko katika mkutadha wake
wote.
Hapa unatazama mkutaqdha wa kitabu. Waweza kutumia mAswali kadha katika
kutazama mkutadha wake mfano Ninin
dhamira ya kitabu au waraka huu wote? Tazama historia, jografia na utamaduni wa
wakati wa Biblia hii daima yaweza kuwa msaada.
* Daima kumbuka kuwa mafundisho ya
Biblia yanapatana na hayapingani kamwe. Hayajipingi yenyewe kwa yenyewe lakini
ufuno wake ni endelevu.
*Mafundisho ya agano la kale ni
lazima yafasiliwe katika nuru ya Agano jipya. Kushindwa kufanya hivyo
kumesababisha kuzaliwa kwa mafundisho mengi ya uongo.(Religious cults).
Mfano. Kutunza sabato, kutokula
baadhi ya wanyama, Kuabudu sanamu, kuoa mitala N.k
D.
mawazo mawili potofu kuhusu mahubiri.
Kuna
dhana mbili potofu ambazo zinajitokeza katika uwanja na taaluma ya mahubiri
mawazo hayo ni:
a. Maaandalizi si lazima.
Wazo la kwanzalenye makosa ni kwamba
maandalizi si lazima na huonesha kukosa imani kwa mhubiri. Watu wenye
kushikilia msimamo huu hufikili kwamba imani ya kweli hutupilia mbali jitihada yoyote inayojaribu kuandaa akili na
hiyvo husimama mimbarini wakiamini
kwamba Mungu atawapa maneno ya kusema.husimamia maawazo haya:
i. Roho mtakatifu atakupa unachohitaji
kuhubiri. Unapopanda mimbarini.
_-
Zab 81:10 “ Fumbua sana kinywa chako name nitakijaza”(Hutumia
andiko hili kutetea msimamo wao.).
Pia
husema kwamba Yesu alisema kwamba “Msifikirifikiri nini cha kusema maana
mtapewa kinywa cha usemi saa ili ilie mnapotakiwa kusema”
Unapoyachunguza kwa umakini maandiko hayo
utagundua kwamba maandiko hayo
wanayafasili nje na mkutadha wake na na kulazimioshwa yaseme kile ambacho
hayamaanishi.
*Mahubiri
ni kamana jengola kiroho ambalo linatakiwa kusanifiwa na kuandaliwa chini ya
uongozi wa Roho Mtakatifu. Roho
mtakatifu ndiye mhandisi mkuu wa mahubiri.
b. Uwezo wa mtu unatosha. Kuweka
mkazo katika matayarisho na kutegemea
uwezo wa kibidanu tu. Wahubri
wanaoshikilia msimamo huu hudai kwamba
maandalizi peke yake yanatosha na
huweka mkazo kwenye matayarisho pekee.Kumtegemea
Roho mtakatifu huwa ni kudogo sana au hakuna kabisa, bali tumaini la mtu
binafsi ambalo ni matokeo ya kujifunza na kuendeleza uwezo wa asili.
Ujumbe
wa namna hii waweza kuwa mzuri kabisa lakini hauwezi kuleta matokeo
yatakikanayo daima. Kwani ni Roho mtakatifu pekee ndiye anaeweza kuleta
badiliko katika maisha ya waikilizaji wako. Bila yeye mahubiri huwa ni maiti na
haiwezi kuleta uhai kwa sababu ni uhai wenye uwezo wa kuzaa uhai.
*Roho
mtakatifu huuhuishaujumbe na kuletaq matokeo yaliyokusudiwa na Mbingu katika
maisha ya wasikilizaji.
Ili
mhubiri aweze kuhubiri sawasawa anapaswa kuwa na maansdalizi ya kutosha katika
kuuandaa ujumbe wake kwa kusoma, kutafakari na kuchambua kweli zote zilizomo
katika ujumbe wake. Lakini hayo yotec anapaswa kuyafanya akiwa katika hali ya
maombi.
Mhubiri
anapaswa kumsikiliza Roho mtakatifu klwa kina na kupata uongozi kwake na kutaka
Roho mtakatifu amshirikishe kile anachotaka kusema na watu wake na kukifanyia
uchambuziyakinifu katika hali ya maombi ili aweze kukiwasilisha kwa ufanisi.
·
Mhubiri anapaswa kutambua kwamba yeye
hana watu wala si Chanzo cha ujumbe. Kwasababu hiyo anatakiwa kumsikiliza
mwenye watu na aliye chanzo cha huo
ujumbe na kusimama katikati kwa uaminifu kuwafikishia watu kwa usahihi kile
mwenye watu anachotaka kiwafikie watu wake.
·
Mhuibiri anapaswa kutambua kwamba kazi ya kuhubiri ni
takatifusana na ni kazi nyeti ambayo yapaswa kufanywa kwa umakini, uaminifu na
unyeyekevu mkuu.
·
Mhubiri mwenye kutegemea juhudi zake na
uwezo wake wa asili atakuwa ni muhubiri kilema na halikadharika mhibiri mweye
kutegemea kupewa ujumbe akiwa mimbarini atakuwa ni kilema.
·
Vyote viwili vyapaswa kwenda pamoja, maombi na matayarisho.Kwa sababu mahubiri ni matokeo ya mawasiliano na
ushirika mzuri kati ya Roho mtakatifu na
mhubiri.
Aina za mahubiri.
Katika kipenele hiki tutaeleza aina saba za
mahubiri. Ni vizuri kwa mhubiri kufahamu aina zote za mahubiri. Hii itamsaidia
kuwa na uhuru waq kutumia ainayoyote
katika huduma yake na kufanya huduma yake kuwa ya kuvutia kwa watu
wanaomsikiliza.
2. Mahubiri ya mada.
Aina
hii ya mahubiri hukusudiakutoa kiini
maalum kwa hadhira.Mhubiri huchagua somo fulani kisha huchunguza kila
kitu ambacho Biblia inasema juu ya somo hilo. Baada ya kuchunguza na kuchambua
kweli hizo huandikwa katika mapngilo wa somo.Mhubiri hupitia vifungu mbalimbali
vya maandiko vinavyohusu somo hilo.
Aina
hii ya amhubiri huhitaji maandalizi ya muda mrefu na utulivu mwingi. Pia
huwasilishwa katika mfululizo wa vipindi kadhaa na si kimoja, kwa sababu ni
vigumu kupitia kweli zote zilizo katika somo kwa kipindi kimoja tu.